TANZIA Pumzika kwa amani Sanctus Mtsimbe

Ni katika mwezi mmoja February -march nimefiwa na watu 2 mmoja ndg wa damu kabisa mwingine ni binamu, najiona kama kupooza mwaka umeanza vibaya, ooh kifo hakina huruma, kisikieni tu utatamani umfufue mpendwa wako walau apate kuendelea kuishi,,,

wapumzike kwa amani tutaonana badae😭😭😭😭
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Umeshau pia kwamba alikuwa member mzuri wa Jamiiforums kwa siku nyingi. Alikuwa akianzisha njuzi mbalimbali humu. RIP Sanctus
 
Kuna jina la kikatoliki?? Ni sawa na majina ya kiarabu kusema ni ya kiislam, jisomee kidogo vitabu utaelewa.
Utakuwa huelewi! Unafikri majina ya Kikristo yanaenda enda tu? Kawaulize Wasabato watakuambia! Protestants wana majina yao na Catholics wana majina yao! Wala mfano wako hata hauendani! Ulisikia wapi Wasabato wana ushirika na Latin?
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
R.i.p
 
Pole sana Max na wana JF.

Sanctus alikuwa mzalendo na mwenye nidhamu kama mwanadiplomasia mbobezi, kuanzia mavazi mpaka anavyoongea. Akivaa suti zake na viatu vyake maarufu vya "wanchoma kumoyo" kwenye joto la Dar, nikimtania kwamba anatimiza msemo wa Waingereza "A gentleman has no weather".

Akijibizana nawe, huwezi kujua kwamba huyu mtu anaweza kukasirika, sauti au maandishi yake yakijaa tabasamu, ucheshi, na hata alipokuwa serious, alionekana mtu serious mwenye matumaini mazuri. Kamwe si serious ya frustration. Hii ni alama ya ukomavu mkubwa kabisa wa kisaikolojia.

Alikuwa mtu wa kujenga ushawishi kwa hoja, si wa kusema kwa papara. Sanctus alichukua muda kumsikiliza mtu, kumsikiliza kweli, si kungojea umalize kusema akupinge, alikuwa anasikiliza kweli, na kupenda kujifunza kwa dhati kutoka kusikiliza kwake, mara nyingi akijibu na kuelezea masomo aliyojifunza ambayo wengine tuliyakosa.

Sanctus alikuwa na moyo wa kutatua matatizo, bila kujali ugumu.Iwe kwenye biashara za mitandao au hata majibizano ya hapa JF tu.

Nimesikitika sana kwa msiba huu, alikuwa bado anahitajika sana kwenye kazi zake nyingi alizoanza ambazo hazijakamilika.
Nimefurahi hapo kwenye wanchoma kumoyo..

Asante brother kiranga kwa kutupa wasifu wa marehemu japo kwa ufupi..

Apumzike kwa amani
 
Wakuu,

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.

Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.

Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.

Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Rest in Eternal Peace Sanctus.
 
Rip Mwana Jamii forum mwenzetu.

Mkuu japo sio mhala pake hili jambo ila ni kwanini mnapuuzia kuhusu notification na picha kutoonekana kwenye app yenu na kila tukiwaambia hamjali wala nini?

Maxence Melo
 
Back
Top Bottom