Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Maxence Melo!, this is shocking news to me, taarifa hii sikupaswa kusomea JF, nilipaswa kuipata in box!.Wakuu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024.
Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, SimbaNet na makampuni mengine, pia alikuwa Mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi na Mjumbe wa Bodi na taasisi kadhaa za umma na binafsi. Alipenda sana sanaa.
Ndg. Mtsimbe alikuwa ni Mwanazuoni mzuri, mbobezi, mbunifu na Mzalendo wa kweli kwa nchi yetu.
Kwa mujibu wa familia, Msiba upo nyumbani kwake Tabata Segerea, Mtaa wa Meja.
Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani ndugu yetu
Sanctus alikuwa patner wangu kwenye baadhi ya projects zake.
Huyu ndie aliongoza ile kampeni ya Kumuenzi Regia Mtema. Huyu ndie alimbeba Le Le Mutuz pale ofisinini kwake!, ni mtu wa pili kunipandisha Range Rover Sport baada ya ile ya Range Rover Autobiography ya Wakili Beredy ambayo ni custom made na kuwa delivered by BA Cargo, ile 2005, Range Sport ya Sanctus Mtsimbe ya 2007 ndio ya pili mimi kuipanda.
Kuna baadhi ya vitu tulifanana na vingine tulitofautiana, tulifanana kupenda totoz bomba, ofisini kwake akawajaza, wasanii wa kike ndio usiseme!, tofauti yetu yeye mwenzangu aliwaheshimu, ilikuwa ni mahusiano ya kikazi tuu, wakati mimi ilikuwa ni "Kazi na Dawa". Wekeza inalipa Movie Launch.
RIP Comred Santus Mtsimbe.
Tribute: Usichokijua Kumhusu Sanctus Mtsimbe, Sio Smart, Mawazo, Maneno, kwa Mavazi, na Muonekano Tuu, He was Very Smart Upstairs!.
Wanabodi Leo asubuhi nimeianza siku vibaya, kwa bandiko la Mkuu Maxence Melo kuhusu msiba huu. Wakuu, Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yetu na mwanachama wa JamiiForums, Sanctus Mtsimbe, mchana wa tarehe 13 Machi 2024. Sanctus alikuwa Rais wa kwanza wa...