Punguza gharama za kutumia mafuta kwenye gari lako. Sasa unaweza kutembea kilomita 180 kwa gharama ya Tsh.15,000 tu

Punguza gharama za kutumia mafuta kwenye gari lako. Sasa unaweza kutembea kilomita 180 kwa gharama ya Tsh.15,000 tu

Gesi kwenye IST inakupa uroda wa 200km with full ac kwa Tsh.17,000 tu! Kwa petrol ungetumia takriban Tsh.45,000 for the same joy ride. Wacha watu waweke gas tu aisee its meaningful than it might sound!
Mkuu gari ya V6 Kwa gesi unaenda umbali gani say 1,000 Kms?
 
Upatikanaji wa gesi ya kujazia kwenye gari

Mpaka sasa kuna vituo 2 vinavyojaza mafuta ambavyo vipo ubungo maziwa na kingine kipo tazara.. Na kuna vituo vingine 3 hapa jijini dar es salaam vipo kwenye hatua za mwisho kupitishwa kwa ajili ya utoaji wa huduma ya kujazia gesi .
Mpaka mwisho wa mwaka huu vitakuwa vimekamilika
Tulioko nje ya Dar tunanufaikaje na hii huduma?
 
Nimeeleza hapo mkuu...kwa sasa kuna vituo 2 tu vinavyojaza gesi dar ambavyo ni ubungo na tazara...vingine vitatu vipp hatua ya mwsho... Kukamilika ila vyote vipo dar..

Mikoani ni ngumu kwa sasa
Hilo neno lako la mwisho ndio dharau yenyewe, yaani mikoani ngumu kuwekwa au ngumu kufikika ?
 
Ni rahisi kwa waishio Dar mkuu. Kwa sisi wa Dodoma haitufai
Nimeeleza hapo mkuu...kwa sasa kuna vituo 2 tu vinavyojaza gesi dar ambavyo ni ubungo na tazara...vingine vitatu vipp hatua ya mwsho... Kukamilika ila vyote vipo dar..

Mikoani ni ngumu kwa sasa
 
Kwa jamaa yangu alieweka kwenye IST yeye full tank ni Tshs.17,000 tukienda kwa hesabu kuigawa hii kwa 1,550 itatupa 10.9 ambayo hii ni Kg’s.

So approximately ni kilo 11 ambazo anasema kwa wastani zinakupigisha 200km before taa ya gas haijawaka then unaweza kupiga extra 40km taa ikiwa still on! Ameshafanya hii trial and it works like charm!

Ili uzipate 200km kwa Petrol itakubidi utumie 13 ltr kwa gari inayokwenda kwa wastani wa 15km/l ambayo itakugharimu kama Tshs.32,000 kulingania na bei ya sasa ya Tsh.2429
Vp kuhusu uwezo wa gari,nasikia gari uwa inapungua nguvu.... ni sawa au story tu.
 
Mtungi kwenye gari ndogo ni kilo 11 na hii kilo 11 itakupeleka umbali mara 2 zaidi ya ule wa lita 11 za Petrol.

Wakijitahidi kupeleka hizi huduma mikoani watasanya wateja wengi sana.
Yaani kama unaenda Dodoma kutoka Dar ina maana hutajaza gesi tena hadi urudi Dar! Mimi naoma TPDC hawajiandaa vizuri kwenye huu mradi, ingepasa angalau kila makao makuu ya mkoa kungekuwa na kituo cha kujazia gesi.

Vv
 
Kwa wale wamiliki wa magari ikiwa umekuwa ukiwaza ni namna gani utapunguza gharama za matumizi ya mafuta kwenye gari lako BASI UJUMBE HUU UNAKUHUSU.

Tumekuwa tukilalamikia juu ya gharama za mafuta katika kuhudumia magari yetu ila kwa sasa mkombozi amewasili.

Gharama za maisha zinapanda kila siku na katika sekta muhimu ya maisha ambayo hatuwezi kuikwepa mi usafiri.

Watu wengi tunapenda kuwa na usafiri binafsi mzuri na wa uhakika ila kuna wakati unataka kuchagua gari zuri ila unahofia juu ya gharama ya mafuta na kujikuta ukichagua gari ambalo moyo haujaliridhia ila tu mfuko wako wa pesa ndio umeridhia kwa kuwa utamudu matumizi ya kila siku ya mafuta.

Wengi hatuhofii kuingia gharama za kumiliki magari wakatibwa kununua mtu unaweza kujipinda na kutenga milioni 15 au 20 au hata 30 na kuagiza gari zuri tu ila kinachokuja kupasua kichwa ni gharama za kila siku za kulihudumia hilo gari kuanzia mafuta hadi kwenye services

Tunawaletea huduma ya kuongeza mfumo wa kutumia gesi kwenye magari.mfumo huu utapunguza gharama ya kutumia mafuta kwa 50%

View attachment 1909482

Nini maana ya kupunguza gharama kwa 50%?
CNG(compressed natural gas) ni gesi asilia ambayo inaweza kutumika katika kuendeshea injini za magari.. Ni tofauti na gesi ya kupikia majumbani..

Gesi hii ni salama zaidi na haishiki moto kwa haraka ukilinganisha na mafuta...
Kilo 1 ya gesi inaweza kuzalisha nguvu ambayo ni sawa na 1.8 litre ya petrol ... Hapo utaona kabisa gesi inaweza kukupeleka umbali mrefu zaidi kuliko petrol

Cha kufurahusha zaidi bei ya kilo moja ya gesi ni ndogo kuliko klita 1 ya petrol..

Kilo 1 ya gesi ni 1,550
View attachment 1909479

Hiyo unayoiona hapo kwenye lorry la kampuni ya dangote ni mitungi ya gesi

Maana yake kama ulikuwa unatumia mafuta ya 45,000 kwa safari ya km 180.kwa sasa utatumia gesi ya 15,000 kwa safari hiyo hiyo bila kuathiri uwezo/perfomance ya gari.
View attachment 1909484

Jambo muhimu ya kufahamu ni kuwa unapofunga mfumo huu wa kutumia gesi hauondoi mfumo wa mafuta bali unaongezea tu mfumo wa gesi na unaweza ku switch muda wowote ukihitaji kubadili nishati unayotaka kutumia kama ni mafuta au gesi

View attachment 1909481
Hapo utaona kuna valve ya gesi na kuna mfuniko wa mafuta ya kawaida

View attachment 1909483

Ubora na uthabiti wa huduma hii
kama unajiuliza na kuhofia juu ya usalama wa gari lako au wewe mwenyewe basi ondoa shaka huduma hii inatolewa namtaalamu aliyeithinishwa kimataifa juu ya uwekaji wa huduma hii katika magari.. Wataalamu hawa wapo 3 tu tanzania walioidhinishwa na mamlaka za kimataifa juu ya matumizi ya gesi katika vyombo vya moto.hauwezi kwenda kujaziwa gesi kwenye gari lako bila miongoni mwa wataalamu hawa kukupa kibali cha uthibiti wa mfumo wako wa gesi kwenye gari lako.

Upatikanaji wa gesi ya kujazia kwenye gari

Mpaka sasa kuna vituo 2 vinavyojaza mafuta ambavyo vipo ubungo maziwa na kingine kipo tazara.. Na kuna vituo vingine 3 hapa jijini dar es salaam vipo kwenye hatua za mwisho kupitishwa kwa ajili ya utoaji wa huduma ya kujazia gesi .
Mpaka mwisho wa mwaka huu vitakuwa vimekamilika

Gharama zikoje?
Gharama za kuweka mfumo huu zinategemea na aina ya injine kama ni cylinder 4 au 6 au 8

Gari yenye injini ya cylinder 4 kuwekewa mfumo huu inagharimu milioni 1.8M, cylinder 6 ni milioni 2 na cylinder 8 ni milioni 2.4

Gharama ni nafuu sana kwakuwa ndani ya miezi 3 mpaka 4 utakuwa umeokoa kiasi hicho ambacho ulikitumia kuweka mfumo ( nina uhakika na hili)... Baada ya miezi hiyo maisha yako ya usafiri yatakuwa nafuu mnooo.

Wamiliki wa magari hasa yale ya biashara madogo kwa makubwa hufuma hii itawapunguzia gharama za mafuta na itaweza kurudishwa kwa kipindi cha miezi 3 tu

Kwanini uendelee kuwa na msongo wa mawazo kutokana na gharama kubwa za mafuta na wakati mkombozi yupo .wahi sasa huduma hii

Ni ndani ya siku 1 mpaka 2 tu gari yako inakuwa tayari kwa matumizi yako
Tumia gesi asilia kwa unafuu wa maisha
Weka mawasiliano yako.
 
Nikampe mtu 2M ili achokonoe hili VQ35DE langu?

Tafuteni pengine pa kufanyia experiments

And by the way hii inafaa kwa mnaozunguka dar tu wale wa road trips kila wiki za 1000+km haisaidii kitu.
Pamoja na kwamba unaongea kwa majigambo na kejeli lakini naona una point mkuu
 
Back
Top Bottom