Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu,Mkuu nataka kujua hii saikolojia ya kuacha pombe. Mtaani kuna perception nyingi sana, Mungu anisamehe lakini pia hata makanisani huku kuna kitu hakijakaa sawa. Je, wewe binafsi ulifanyaje mpaka umeweza huu mwaka haugausa kabisa kinywaji ? Nitashukuru sana kwa jibu makini
Mimi nina saikolojia kwamba mimi ni mtawala. Pombe hainitawali mimi, mimi naitawala pombe.
Saikolojia hii huwa nai test kila mara, hii wala si mara ya kwanza kuacha kunywa pombe, kuna wakati nilikaa miaka miwili bila kunywa pombe.
Yani kila mara nataka kuji test kwamba nikiamua kuacha kunywa pombe kwa mwaka mmoja au miwili, naweza kufanya hivyo.
Na kila nikiacha kunywa pombe hivyo, ni lazima niwe na pombe nyumbani. Kwa mfano sasa hivi nina Scotch, nina Tequila, nina Vodka, nina wine, nina mpaka beer kwenye friji la garage kila nikifungua friji la garage naziona beer za baridi, lakini sijanywa, nimeziweka kama atatokea mgeni mnywa bia anywe na pia kujihakikishia kwamba nimeacha kunywa pombe kwa kuamua, si kwa sababu nyumbani nimeishiwa pombe.
Ni uamuzi wa mtu tu. Mpaka watu wa kazini tukitoka out wanajua Kiranga hanywi pombe siku hizi. Wananiwekea mazingira ya kunywa vinywaji vingine. Mpaka watu wangu wa karibu ni hivyo hivyo.
Najisikia nishakunywa pombe kama zote ma Bourbon, Whisky, Sake, Tequila,Vodka, wine, beer Champagne.
Sina cha kunywa zaidi.