Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Japo nimechelewa ila huu ni uzi bora niliosoma kwakufungua mwaka huu 2023Na Jumaa Kilumbi,
31.10.2022
Punyeto ni nini?
ni kitendo cha kujiridhisha kingono kwa kujichua sehemu za siri.
Lakini ieleweke kuwa Punyeto ni kitendo cha kiasili kibailojia na hufanywa na watu wengi sana.
Japokuwa ukiuliza watu wengi hawasemi ukweli ila kila mtu anajua anachokifanya anapokuwa peke yake.
Kuna maneno husemwa kuwa “99% ya watu hupiga punyeto, iliyobaki wanadanganya”
Huo ni utani ila takwimu za kitafiti zinaonesha wazi kuwa zaidi ya asilimia 95% ya Wanaume hupiga punyeto au waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani cha maisha yao.
View attachment 2403300
Na ni 80% ya Wanawake hupiga punyeto au waliwahi fanya hivyo kipindi fulani cha maisha yao.
View attachment 2403302
Tatizo kubwa kuhusu punyeto ni kwamba ‘it is addictive’ yani inapelekea mfanyaji kuwa mraibu wa tendo hilo.
Na hufanywa kwa mitindo mbalimbali maana wanaadamu ni wabunifu sana.
Zamani ilikuwa inadhaniwa kuwa punyeto husababisha upofu lakini imegundulika kumbe ni uzushi mtupu na hakuna ukweli wowote wa madai hayo.
Punyeto ikikolea huleta madhara mengi sana kwa mfanyaji ila hilo limeshaandikwa sana hivyo sitalijadili hapa, katika madhara hayo majuto pia huwa ni miongoni mwao.
SABABU ZA WATU KUPIGA PUNYETO
Punyeto hufanywa kwa sababu mbalimbali zikiwemo swala zima la ‘Libido/Sex drive’ au mihemko (naam tunatofautiana viwango, wengine sex drive yao iko juu sana), na sababu nyingine ni muaniko (exposure) tuliyonayo kwenye maudhui ya kingono.
Pigia mfano zile post za Malkia nyuki kule twitter, Post za Kim kardashian huko Instagram, nyimbo za Bongo Fleva huko Youtube, Story za kula tunda kimasikhara za rikiboy na story za Sexual Fantasy za Count Capone hapa JamiiForums vyote hivi vinashambulia akili zetu ku-focus na maudhui haya.
ATHARI YA KUBWA YA PUNYETO
Katika watu niliozungumza nao kuhusu swala hili walisema huwa wanajilaumu na muda mwingine kujichukia baada ya kufanya kitendo hiko.
Sasa haya majuto ndiyo kitu kilichonisukuma kulitazama hili kwa undani kabisa maana ndiyo tatizo kubwa linalowakabili watu.
Majuto haya hupelekea kutojiamini mbele za watu, stress, kujichukia, kutilia mashaka imani zao kwa Mungu n.k
JE, PUNYETO NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU?
Ndiyo, tuangalie kwenye vitabu vitakatifu Quran na Biblia Je, Mungu kakataza Punyeto au tunajishtukia?
Tuanze na kitabu kitakatifu cha Biblia
Katika Biblia nzima hakuna mstari au aya iliyotoa katazo kuhusu punyeto.
Kwenye biblia Kitabu cha mwanzo 38: 3-10 Mungu anatueleza hadithi ya Judah na wanawe Er na Onan.
“1 Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
2 Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.
3 Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.
4 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.
5 Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.
6 Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.
7 Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua.
8 Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.
9 Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao.
10 Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.”
Kwahiyo Mungu akamuua Onani kwa kosa la kumwaga nje, hii ndiyo maelezo pekee kwenye biblia yanayokaribiana na suala la Punyeto.
Lakini hapa Mungu alimuua Onani kwa kosa la kutokumpatia kaka yake mrithi maana Onani alimwaga nje kusudi ili kaka yake asipate mrithi na sio Nyeto. Case closed!
Tuje kwenye Quran tukufu na hadithi sahih:
Kwenye Uislam tuna vyanzo vikuu vinne vya elimu tuna
1. Quran
2. Hadithi za mtume
3. Fatwa za Wanazuoni
4. Qias
Pia kwenye Quran suala hili halikutajwa moja kwa moja ila aya pekee iliyo karibu na maelezo kuhusu Punyeto ni ile Quran 23:5-7.
“5. Na ambao wanazilinda tupu zao,
6. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.
7. Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.”
Pia hakuna hadithi sahih ya Mtume (SAW) inayokataza Punyeto.
Dr. Zakir Naik ambaye ni Daktari na mhubiri mashuhuri wa kiislamu anajibu uhalali au uharamu wa nyeto kama ifuatavyo.
Quran na hadithi havijaeleza kuhusu Punyeto, katika vile vyanzo vya elimu tunalazimika kufuata chanzo kinachofuata ambacho ni Fatwa za wanazuoni. Wao wanasemaje?
Hapa Wanazuoni kama ilivyo kwenye mambo mengine wamekhitilafiana (tofautiana). Tuna makundi matatu
- Wanaosema Punyeto ni haramu na mbaya
- Wanaosema Punyeto ni Muba’a (hiyari, optional)
- Wanaosema Punyeto ni Makrooh (yaani si haramu ila haipendezi, kama ilivyo kwa uvutaji wa sigara)
Kwakuwa hili suala ni zito ila japo kwa juu juu tuwatazame hawa wanazuoni wana hoja gani juu ya hili.
1. Wanaosema Punyeto ni haramu na mbaya
Wasomi wengi wa Madhehebu ya Imam shafi na Malik wanasema Punyeto ni haramu na wananukuu aya za Quran 23:5-7 kama nilivyozieleza hapo juu.
Kundi hili la wanazuoni Wanasema kuwa aya ipo wazi na kwamba kujiridhisha kingono (sexual satisfaction) ni halali baina ya mke na mume tu na si vinginevyo.
Kujiridhisha kingono kwa namna nyingine yeyote ni haram.
Hivyo kwao Punyeto ni kinyume na maelekezo ya aya hii.
2. Wanaosema Punyeto ni halali (Muba’a - Halali ila ni hiyari)
Katika aya hizo hizo Quran 23:5-7 kuna kundi la pili la wanazuoni, wao wanaifasiri suala la kujiridhisha kingono kuwa Mungu alimaanisha kufanya mapenzi ambapo ni baina ya watu wawili (ni tofauti na Punyeto ambapo anayehusika ni mmoja na nyeti zake tu) ni halali kwa mume na mke tu ila hakusema kuhusu kujiridhisha mwenyewe (yaani Punyeto) ambapo hauhitaji mtu wa pili.
Kwahiyo wanazuoni hawa wanadai kuwa Punyeto haijakatazwa kilichokatazwa kwenye aya hizo ni kufanya mapenzi na mtu asiye mume au mke wa mhusika tu na haihusiani na kujiridhisha mwenyewe.
Na sababu yao ni kuwa katika Quran na hadith hakuna mahali suala hili limekatazwa na kwakuwa halijakatazwa basi halali na ni muba’a kwa maana ni hiyari kwa mtu mwenyewe.
3. Wanaosema ni makrooh (ni halali la haipendezi)
Kundi hili tunawakuta wanafunzi wa Ibn Abbas ambao wao kwa maoni yao walieleza kuwa Punyeto ni halali ila haipendezi kuwa sifa ya watu wema.
Na kundi hili hutilia uzito suala la punyeto katika mazingira fulani maalum.
Mathalan mtu kapandwa hamu ya kushiriki tendo hapo anakuwa na chaguzi (options) mbili;
Wanazuoni hawa wanasema kuliko mtu azini ni bora afanye Punyeto.
- Atafute mtu azini nae
- Afanye nyeto hamu imuishe
Katika hali hii wanazuoni hawa wanasema kuwa
Ndoa ni bora kuliko Nyeto,
Nyeto ni bora kuliko zinaa,
Zinaa ni mama wa madhambi.
UHARAMU WA PUNYETO
Dr. Zakir Naik ameeleza kuwa Punyeto inakuwa haramu bila shaka pale inaposindikizwa na kutazama picha au video chafu za utupu.
JINSI YA KUACHA PUNYETO
Njia hutajwa kwa wingi sana ila hapa nitaeleza mbili.
Dr. Zakir Naik amependekeza njia mbili kuepukana na Punyeto.
Mhusika aingie ndoani ili badala ya kupiga Punyeto kujiridhisha ajiridhishe kwa mwenza wake.
- Ndoa
2. Kufunga swaum
Swaum inafahamika kwa kupunguza hamu ya kufanya Mapenzi, kama mtu anashikwa sana na hamu ya kufanya tendo basi afunge kupunguza.
MAONI YANGU
Maoni yangu binafsi ni kwamba nakubaliana na Dr. Zakir Naik kuwa Punyeto ni Makrooh, yaani ni halali ila haipendezi.
Kuhusu madhara ukweli usemwe kuwa “an excess of anything is harmful” (Chochote kikizidi huwa na madhara)
Soda ni tamu ila ukinywa sana kisukari kitakushika.
‘Fast food’ tunazipenda lakini tukila sana Presha na kuzidi uzito kutatushika.
Kila unapogusa kuna uzuri na ubaya, na ubaya huwepo pale tu tunapozidisha.
Ukifanya Punyeto kama mara 5-10 kwa siku bila shaka utapata athari mbaya kabisa.
Ushauri wangu kuhusu kila kitu maishani ni “Fanya kistaarabu”
Hii tafsiri yako sijui ni doctrine ya dhehebu gani??Waache uvivu wakasome Biblia:
Biblia inasema wafiraji na wazinzi hawatauona ufalme wa mbinguni. .
Soma: 1 Wakorinto 6:9
Msidanganyike waasherati hawatourithi ufalme wa Mungu, Wala waabudi sanamu, Wala wazinzi, Wala wafiraji, Wala walawiti, Wala watamanio, Wala wevi, Wala walevi, Wala watukanaji, Wala wanyang'anyi.
1. Waasherati - Hawa ndio wale wapiga nyeto, wawaza sex, wasagaji, wanaoshiriki tendo nje ya ndoa etc
2. Waabudu sanamu - Hawa ndio wale watumiao sex toys na kusema oh my god.
3. Wazinzi - Hawa wanandoa wanaofanya nyeto, mapenzi nje ya ndoa, orgy, threesome. ..
4. Wafiraji - Hawa Wala Tigo, kikunyeo, nyonya puru...
5. Walawiti - Hawa wasagaji, mashoga, wapenda puru.
6. Wevi - wapiga chabo, kuiba wake za watu, kutamani, sex plays ...
7. Watamanio - wapiga chabo, kuota wake waume za watu, sex toys, penda penda
8. Walevi - Hawa wanaongoza kwa ngono zembe
9. Watukanaji- Hawa wanafanya dirt sex like I wanna JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala you infront of your mommy
10. Wanyang'anyi - Hawa wabakaji washenzi wakubwa nao watabakwa motoni, mfano demu kala Hela zako unapanga kumkomoa unahusika. .
Nakunywa juice hapa nikimaliza nitautupia dhambi nyingine wapendwa wa Mungu wazitambue. .
Nini dhambi mkuu?Ni dhambi immorality,kutokuwa safi
Yani unataka kusemaje? Tafsiri au imeandikwa kwenye Biblia?Hii tafsiri yako sijui ni doctrine ya dhehebu gani??
Yani unataka kusemaje? Tafsiri au imeandikwa kwenye Biblia?Hii tafsiri yako sijui ni doctrine ya dhehebu gani??
This is good brother na iman ukiendelea hv utakua OK. anza mazoez mdgo mdgo you gonna be OK.Nmepunguza kuangalia porno, nmejiepusha kukaa chumban pekeangu na mda nkiwa pekeangu bas ntakuwa naangalia movie au kucheza game
Pia nlfkria sana itakuaje sku na mm ikantokea ile hali ya watu wanayosema kimoja tu chali mtu hawez kuendlea na ndo limenfanya pia nichukue hatua ya kuacha kupiga
Nmefuta channel zote za porno, mfano za huko telegram, Twitter ili kuepusha kuangalia vdeo ztakazonfanya npige
Hayo ni baadh tu.
The more you do the more you became more female, yaan kadri unavyopiga nyeto ndio unavyozidi kua na tabia za kike (feminine) ukiacha na kuzuia mbegu tabia inahama unaanza kua na tabia za kiume (masculine), sasa chagua unataka kua mwanamke au unataka kua mwanaume?Punyeto ni nini
Nukuu ni sawa ila huo ufafanuzi ndo unanishangazaYani unataka kusemaje? Tafsiri au imeandikwa kwenye Biblia?
Haya madai unayatoa wapi mkuu?The more you do the more you became more female, yaan kadri unavyopiga nyeto ndio unavyozidi kua na tabia za kike (feminine) ukiacha na kuzuia mbegu tabia inahama unaanza kua na tabia za kiume (masculine), sasa chagua unataka kua mwanamke au unataka kua mwanaume?
Haujaelewa ipo hivi kuna energy mbili kila moja ipo upande wake na inafanya kazi yake
Feminine energy & Masculine energy
Feminine energy = female.
Masculine energy = male
Daoist / Taoist wanaiita Yin & Yang.
Sasa ipo hivi ukipiga puli au nyeto unapoteza masculine energy Ila unapokea feminine energy.
Ukiacha puli au nyeto unapoteza feminine energy unapokea masculine energy.
Sasa chagua unataka kua mwanamke au unataka kua mwanaume?
Future is female maana wanaume wengi wanapiga puli wanapiga nyeto idadi ya wanaume inazidi kupungua kadri wanaume wanavyopiga puli.
Mkuu kila kitu nimeandika hapo ubaya wa karne hii ni kwamba dunia na maarifa vipo kiganjani kwako, ukitaka kua mwanaume hakikisha unahifadhi testosterone hormones zako kadri uwezavyo, ukizipoteza ovyo ovyo utaanza kujiremba uwe km mwanamke ili upendwe ili upewe ili upokeeHaya madai unayatoa wapi mkuu?
Kuna msomi yeyote alifanya tafiti au ni mawazo yako mkuu?
Tupe Rejea tafadhali.
Rejea iko wapi mkuu?Mkuu kila kitu nimeandika hapo ubaya wa karne hii ni kwamba dunia na maarifa vipo kiganjani kwako, ukitaka kua mwanaume hakikisha unahifadhi testosterone hormones zako kadri uwezavyo, ukizipoteza ovyo ovyo utaanza kujiremba uwe km mwanamke ili upendwe ili upewe ili upokee
Emu jaribu kupitia hapa mkuu maana naona mimi hunielewiRejea iko wapi mkuu?
Au hayo maarifa umeyatoa wapi? Kuna mwanasayansi aliyafanyia utafiti akaandika kitabu?
Kama ndiyo, tuwekee rejea zako hapa.
Kuna mtaalam wa kiroho amesema?
Kama ndiyo, weka rejea hapa.
Kwenye andiko langu nimesema madai nilipoyatoa, yako umetoa wapi?
Kama ni mawazo yako tu hakuna ubaya pia tuambie, maana kila mmoja anao uhuru kutoa mawazo yake, lakini hatukubali maoni yako kuyafanya yaonekane kana kwamba ni ‘fact’.
Kwahiyo hiyo ndiyo rejea yako?Emu jaribu kupitia hapa mkuu maana naona mimi hunielewi
Ukitaka usimkinai mwanamke, usiwe unapiga bao!
Saikolojia ya mwanaume iko hivi... Mwanaume rijali always huwa anatamani kulala (kufanya mapenzi) na mwanamke ambaye hajawahi kulala nae kabla. Si unasikiaga wanasema eti, wanaume ni watu wa tamaa, wao kila mwanamke anamtamani tu. Hiyo ndio sababu sasa. Yani iko hivi, mwanaume akishamgonga...www.jamiiforums.com
Mkuu nimejaribu kukuelezea kwa summary fupi haujanielewa nimejaribu kukupa maelezo haujanielewa sasa hata nikikupa rejea 700 najua hautanielewa, tusijaze server za JF kwa kitu cha kawaida ambacho kipo wazi fanya hivi wewe baki na kile unachokiamini nami nibaki na kile ninachokiamini na kukielewa, hapo unaonaje au unahitaji mjadala uendelee nikuletee hizo rejea unazozihitaji?Kwahiyo hiyo ndiyo rejea yako?
Mkuu mimi sina shida, niko tayari kujifunza.Mkuu nimejaribu kukuelezea kwa summary fupi haujanielewa nimejaribu kukupa maelezo haujanielewa sasa hata nikikupa rejea 700 najua hautanielewa, tusijaze server za JF kwa kitu cha kawaida ambacho kipo wazi fanya hivi wewe baki na kile unachokiamini nami nibaki na kile ninachokiamini na kukielewa, hapo unaonaje au unahitaji mjadala uendelee nikuletee hizo rejea unazozihitaji?
Ni ngumu kunielewa mkuu nikitulia nitafungua uzi ikiwezekana nitaku-tag kabisa maana nikiandika hapa hapawezi kutosha na pia inahitaji mtu mwenye akili pana kuelewa hili jambo ukiwa na akili za kushikiwa ni ngumu kuelewa,Mkuu mimi sina shida, niko tayari kujifunza.
Madai uliyoleta ni ‘very serious’ na ndiyo maana ninataka rejea kujiridhisha kuwa ni kweli au vinginevyo ifahamike kuwa ni maoni yako.
Yaani madai ya kuwa wanaume wakipiga nyeto wanakuwa na tabia za kike hivyo inatishia uwepo wa wanaume huko mbeleni.
Haya madai ni mazito sana kiasi yanaweza zua taharuki, na ndiyo maana nikaomba rejea maana nimeshtuka sana ukiangalia karibia 95% ya ME wanapiga au waliwahi piga nyeto wakati fulani.
Sasa rejea uliyonipa ni ‘post’ ya mdau mmoja hapa JF ambayo nayo sijaona ikiwa na ushahidi wa kisayansi.
Sasa kama una rejea 700 tafadhali ishushe moja tu kuliweka hili sawa, na kama huna basi iweke wazi kuwa yale ni maoni yako mkuu.
Na usijali kunieleza kwa ‘summary’ nina muda wa kutosha kuzisoma zote 700 mkuu, zilete tu.
Mkuu wewe haupo kwenye nafasi ya kuamua kama itakuwa ngumu kwangu kukuelewa ama la, wewe weka rejea zako hapa tutazipitia na tuone kama kuna mashiko.Ni ngumu kunielewa mkuu nikitulia nitafungua uzi ikiwezekana nitaku-tag kabisa maana nikiandika hapa hapawezi kutosha na pia inahitaji mtu mwenye akili pana kuelewa hili jambo ukiwa na akili za kushikiwa ni ngumu kuelewa,
Hapo mwanzoni kipindi cha ujana wangu nilipokua nasikia habari za nguvu za kiume nilikua sielewi hawa wanamaanisha nini maana wanasema tu nguvu za kiume Ila hawaendi deep kuelezea nguvu za kiume ni nini haswa? Au mwanaume nguvu zake haswa zilipo ni wapi? Wamefanya Siri
Madaktari na wengineo hua wanasema juu juu tu kujichua sijui punyeto inasababisha unapoteza nguvu za kiume Ila hawaelezi kinaganaga kwamba anazipotezaje hizo nguvu zinapopotea hua zinaenda wapi?
Inakubidi ujue nguvu za kiume au nguvu za mwanaume zipo kwenye mbegu zake yaan ukipoteza mbegu zako ukazimwaga aidha kwa kupiga punyeto au vinginevyo, wewe una-shift kutoka kwenye upande wa mwanaume unahamia upande wa mwanamke, umeielewa hio concept kidogo lakini au bado nakuumiza kichwa hapo?
Ngumu kuelewa, basi emu endelea kutafakari.