Putin alimheshimu sana Trump, ubabe wake aliufanya kabla Trump hajaingia madarakani na baada ya Trump kutoka madarakani

Putin alimheshimu sana Trump, ubabe wake aliufanya kabla Trump hajaingia madarakani na baada ya Trump kutoka madarakani

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Siwezi kusema Putin alimuogopa Trump lakini ni wazi alimpa heshima yake kwa kutojaribu kufurukuta kama alivyozoea.

Putin aliitwanga Georgia kipindi cha Bush, aliichukua Crimea kipindi cha Obama, Ahakufanya vurugu kwa Trump, kaivamia Ukraine kipindi cha Biden.

katika historia nzima ya marekani ni kipindi cha Trump jeshi lilikuwa bora zaidi na liligharamiwa sana kufanikisha peace through strength.

magaidi watukutu wa ISIS waliovuma sana kipindi cha obama walisambatishwa bila huruma wala kulemba ndani ya mwaka moja tu Trump akiwa madarakani.

uchumi wa marekani ulifufuliwa ukawa juu sana, mfano mdogo tatizo la kukosa ajira lilipungua kwa viwango vilivyovunja rekodi kwa wamarekani weusi, walatino, wa asia, mavererani, wenye ulemavu na wenye elimu ya chini.. haya yalikuwa ni matamanio hata kwa Putin.

jenerali Solemni wa Iran alikuwa akiongea sana akidhani Trump ni kama wengine, Alijibiwa kwa vitendo na kilichomkuta ni history.

Trump aliweza kwenda hadi kwa kiduku Kim jong un wa Korea Kaskazini katika makubaliano endelevu, makubaliano yalileta ahueni na hili ni jambo la kihistoria, kwa sasa kiduku kashaanza vituo cyake chini ya Biden.

Mataifa ya Nato ya ulaya yalikuwa yanachangia kidogo kwenye bdget ya ulinzi lakini Trump aliwapa makavu kuwachana live waanze kuchangia fair share yao, na kweli ikawa hivyo mataifa ya ulaya yaliongeza michango yao.

Ni mengi sana aliyafanya Trump kuiheshimisha Marekani lakini ni kazi sana kuvisikia kwasababu mambo ya Marekani watu wengi walio nje hutegemea vyombo vya habari maarufu kama Cnn ambao wapo left wing kusapoti itikadi za chama pinzani cha Democrats, Ndio waliopika na kutrendisha kwamba Russia walidukua matokeo kumweka Trump kwa lengo la kumchafua, uchunguzi ulifanyika kwa bilioni 70 chini na kubaini hakuna ushahidi lakini vyombo hivvo mpaka leo wamepiga kimya.
 
Hata mi naona kadodges kidogo kipindi cha Trump ilikuwa ni USA na IRAN,KOREA KASKAZINI
 
... huyo fashisti wamepita marais wangapi wa US lenyewe lipo tu; is Russia led by a monarch? That hobgoblin has to go hakuna kuendelea kucheka na that monaster ambalo limefikia hatua kujiona kama mungu wa Urusi.
 
Putin na Trump ni Swahiba. USA ina laani hadi leo kuwa PUTIN ndie alikumuweka Trump madarakani USA kwa kuingilia mfumo wa kura.
Thread zingine zifutwe humu.
 
Unafahamu Marekani kila jimbo linapiga kura kivyake na hakuna mfumo mmoja wa kura??!
Putin na Trump ni Swahiba. USA ina laani hadi leo kuwa PUTIN ndie alikumuweka Trump madarakani USA kwa kuingilia mfumo wa kura.
Thread zingine zifutwe humu.
 
Putin na Trump ni Swahiba. USA ina laani hadi leo kuwa PUTIN ndie alikumuweka Trump madarakani USA kwa kuingilia mfumo wa kura.
Thread zingine zifutwe humu.
ni Media za left za chama pinzani cha Democrats ndio ziliibua hayo mambo, Trump kafanya mengi mazuri tu lakini huwezi kuja kusikia hizo media zikitangaza,,,, hasa Cnn
 
Trump alikuwa anafanikisha mengi ambayo yalikuwa ni matamanio ya Putin hivyo Putin hakuwa na haja ya kufanya vimbwanga vyake wakati kuna mtu alikuwa anamsaidia.

Angalia yafuatayao
1.Trump alitaka kuipeleka NATO kaburini kabisa kwa kupunguza bajeti ya US na wanajeshi na pia kutoa tuhuma kwa wanachama wengine kiholela sana.

2.Trump alitaka Zelenskyy amfanyie Rushwa ya kumchafua Biden ndio ampe msaada wa silaha.

3.Trump alikuwa anadharau hadharani taarifa za vyombo vyake vya intelejensia kuhusu Russia na alifikia hatua ya kuvikejeli akiwa na Putin
 
Trump alikuwa anafanikisha mengi ambayo yalikuwa ni matamanio ya Putin hivyo Putin hakuwa na haja ya kufanya vimbwanga vyake wakati kuna mtu alikuwa anamsaidia...
Hizo habari zote zilipikwa na CNN chombo kinachomilikiwa na chama pinzani, wabongo kama wewe mkisikia habari yoyote cnn wala hamchunguzi mnaiamini kama ilivyo, ni cnn hawa wasioweza kuripoti matatizo kibao ya kiafya ya biden watatoa vipi habari za kiweledi?

Trump alishawapiga biti hao Nato walikuwa wanachangia bajeti kidogo sana na wakaanza kuchangia kiasi kikubwa na kuifanya budget ya Nato iwe imenonona, ni vipi hapa Nato ilikuwa inaenda kaburini?

Jibu ni kwamba vyanzo vyako vya habari ni vile vinavyomilikuwa na vyama pinzani vya kupika stori kumfanya Trump aonekane dhaifu
 
Hizo habari zote zilipikwa na CNN chombo kinachomilikiwa na chama pinzani, wabongo kama wewe mkisikia habari yoyote cnn wala hamchunguzi mnaiamini kama ilivyo, ni cnn hawa wasioweza kuripoti matatizo kibao ya kiafya ya biden watatoa vipi habari za kiweledi ??

Trump alishawapiga biti hao Nato walikuwa wanachangia bajeti kidogo sana na wakaanza kuchangia kiasi kikubwa na kuifanya budget ya Nato iwe imenonona, ni vipi hapa Nato ilikuwa inaenda kaburini ? Jibu ni kwamba vyanzo vyako vya habari ni vile vinavyomilikuwa na vyama pinzani vya kupika stori kumfanya Trump aonekane dhaifu
Screenshot_20221001-214522_Twitter.jpg
 
Ona kichekesho,walolianzisha ISIS hao hao ndo walilidhibiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
hata Tanzania inaweza kuwa moja lakini watu wapo tofauti, huyo Obama na Biden wana sera ya kuruhusu maharamia waingie nchini bila vibali lakini Trump aliwafungia, hapo unaweza kuona kirahisi yupi mwenye akili
 
Trump ndiye alikuwa raisi anayehitajika Marekani kwa sasa ila bahati mbaya kizuri huwa hakithaminiki na wapuuzi. Watamkumbuka sana Trump.
 
Trump ndiye alikuwa raisi anayehitajika Marekani kwa sasa ila bahati mbaya kizuri huwa hakithaminiki na wapuuzi. Watamkumbuka sana Trump.
Watu mnaandika as if mlipiga kura. Wamarekani wenyewe wanasemaje?

Ya kwao waachieni wao.
 
Back
Top Bottom