Putin anaonya nchi za Magharibi: Urusi itaibuka kama taifa lenye nguvu zaidi

Putin alisema hakujawa na mbadala wa kile Urusi inachokiita operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kwamba Urusi sio nchi ambayo inaweza kukubali kuathiri uhuru wake kwa aina fulani ya faida za kiuchumi za muda mfupi.
Haya ni maneno ya Putin ya kijamaaa, lakini katika dunia ya SASA yanaitajika kweli uache kutumia bidhaaa za Western Union kisa Putin

Sent from my Nokia 1 Plus using JamiiForums mobile app
 
nchi nyingi sana ambazo ni marafiki na USA ni nchi ambazo haziko stable kiuchumi na nyingi kisiri lazima zinatafuta namna ya kujitoa kwenye mkono wa hili beberu la west. ila nchi nyingi sana ambazo ziko stable kiuchumi ni zile ambazo wako na uhuru wao bila kutazama west wanafanya nini mwangalie mchini, Russia mwenyewe mwangalie mkolea, mwanagalie libya enzi yuko Raisi wao pendwa angalia na wakati alipo pingwa tukio ni wakati sasa nchi za west ziondoe vikwazo vyao kwa kutishia kuporomoka kwa uchumi lakini kwa mda mfupi alafu uchumi wa kila mmoja duniani utakua sawaa kulingana na matakwa ya nchi husika na uongozi uliopo madarakani
 
Kwisha habari yake alijua ataingusha Ukraine siku 2 tu, sasa leo anaongea hivi mara vile., si alisema yeye hatatetereka kwa vikwazo mbona sasa anaviita haramu maana yake ni kwamba anakiri anaumia na kudhoofika, kama ataibuka kuwa taifa lenye nguvu maana yake kwamba sasa hali ni ngumu sana na anahitaji muda na hajuwi pia kwa baadae hali itakuwaje, majenerali wake 2 wamepata kibano ukraine, amepata pigo nadhan moyoni anajuta
 
Vikwazo alivyowekewa russia ni kifo., haijawahi tokea kama hivi kwa nchi yoyte, ngoja kwanza watu wajipigie ngawira meli za makampuni ya russia zinashikwa uko ufaransa watu wanakula ngawira
 
Asant mkuu mshana Jr
Putin alisema hakujawa na mbadala wa kile Urusi inachokiita operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kwamba Urusi sio nchi ambayo inaweza kukubali kuathiri uhuru wake kwa aina fulani ya faida za kiuchumi za muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…