Putin anaonya nchi za Magharibi: Urusi itaibuka kama taifa lenye nguvu zaidi

Putin anaonya nchi za Magharibi: Urusi itaibuka kama taifa lenye nguvu zaidi

Watu wa JF munajitahid kuzungumzia uchumi lakin hamna kitu ,wengi wa humu wanadhani uchumi ni thamani ya pesa tu. Utakuta mtu anasema Uchumi wa Russia hamna kitu au wa Iran hamna kitu hata hawaz hivyo vikwazo vilikuwepo toka mwaka gani na kufatilia maendeleo ya hizo nchi kwa sasa zilipo. Mfano mdogo Iran toka wafanye mapinduzi kumtoa kibaraka wa marekan mpaka wanadumu na vikwazo lakin Muiran huyo huyo kapeleka mafuta kwa Maduro meli 3 baada ya marekan kuiwekea vikwazo Venezuela na hamna alichomfanya unadhan bira ya kua na power unaweza fanya hivi mbele ya marekan hebu mda mwengine tujaribu japo kulinganisha nchi yetu isiewekewa vikwazo na inayopewa misaada yote na hizo nchi zilizowekewa vikwazo je tunazikaribia kwa uchumi ,labda hapo mtu utaweza kuandika point inayoeleweka kidogo.
Watu wa JF ukiwafuatilia sana utazani wana uchumi kumzidi Russia, wakati wenzetu wanajitegemea kwa kila kitu. Leo sis ndio tuwe na ufaham mwingi kuwazidi wao hahahaha.
 
Yaani kichwa cha habari hakiendani na content.
Inabidi tuwe wapenzi wasomaji wa comment tu hapa,lakini uhalisia wenyewe anaujua Putin na wanaomzunguka ndiyo maana kageuka kuwa motivational Speakaer kujaribu kuwaondolea hofu wananchi wake kwa kile kinachokuja mbele yao.Vita na iishe hata kesho,Putin aikalie Ukraine ikiwezekana halafu sasa tutarudi kwenye uhalisia tuone nani atakuwa mshindi wa hii vita.
 
Inabidi tuwe wapenzi wasomaji wa comment tu hapa,lakini uhalisia wenyewe anaujua Putin na wanaomzunguka ndiyo maana kageuka kuwa motivational Speakaer kujaribu kuwaondolea hofu wananchi wake kwa kile kinachokuja mbele yao.Vita na iishe hata kesho,Putin aikalie Ukraine ikiwezekana halafu sasa tutarudi kwenye uhalisia tuone nani atakuwa mshindi wa hii vita.
Kweli.
 
Hali ilishakuwa mbaya huko!!na wananchi wake wameshaanza kumkataa!!na zamu hii atapata shida sana
Halafu watu tuko hapa tunadharau vikwazo utadhani waliovibuni viwepo walikuwa wajinga.Tungekuwa na uwezo kama tunaouonyesha katika hii mijadala wa kudharau waliotuzidi Tanzania ingekuwa Ulimwengu wa kwanza ki uchumi na katika nyanja mbali mbali,lakini kwakuwa tumejaliwa midomo tu ya kuongea basi tutaendela kuwa hivi hivi tulivyo kizazi hadi kizazi.
 
Naona ndo anawapa moyo watendaji wake wasikate tamaa.
Hata yeye anajua hofu kuu waliyonayo lakini pia deep down hana amani,huwezi watawala watu waliojawa na hofu ya nini hatma yao ya kesho na hasa watu wenyewe ni kama hao ambao tayari walishaonja matunda ya kuishi na kula bata kibepari.Mtu kazoe kwenda kushop kwa LV,GUCCI,PRADA and the likes leo hii anaona hakuna tena maduka kama hayo achilia mbali wenye maisha ya kawaida ambao ni wengi zaidi wataumia
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Watu wa JF ukiwafuatilia sana utazani wana uchumi kumzidi Russia, wakati wenzetu wanajitegemea kwa kila kitu. Leo sis ndio tuwe na ufaham mwingi kuwazidi wao hahahaha.
Na wale wanaodharau Upande wa pili je?
 
Pro Russia
Screenshot_20220312-000129~3.jpg
status_me_status_IMG-20220312-WA0000.jpg
 
Rais wa Russia Comrade Vladmir Putin Amesema Nchi hiyo inakwenda kuwa Nchi Imara na yenye Uchumi Mzito kuliko ilivyo Leo kinyume na Maadui zake wanavyojidanganya.

Putin aliyasema hayo Alhamis alipokuta na Baraza la Uongozi la Russia kwenye Kikao ambacho kilikuwa Live kwenye Radio na TV, na kuonyeshwa Live na TV na Radio zaidi ya 420, kwenye Mataifa Mbali mbali yenye Uhuru wa kuonyesha Habari kutoka Urusi.

"Lazima Mjuie, Tulijua kuwa watakuja na silaha hii butu, kwa sababu najua hawawezi kutupangia njia za kujilinda dhidi ya hatari tunayoiona, Nimeamua kufanya Operation ya Kijeshi kwa Serikali ya Kyiv kwa sababu za Usalama wa Russia na vizazi vyake vya kesho" Hakuna wa kunizuia, hakuna wa kutupinga, na hata wakiweka Vikwazo mara elfu moja, bado tuna Haki ya Kusimama Kulinda usalama wetu"..Na sasa Maumivu waliyotaka kwetu yamerudi milango mwao.

"Ni Wapuuzi kabisa, na hivyo vikwazo vyao mmeona matokeo yake, Sasa Nauli za Ndege kwenda Hanoi ama Macau zimekuwa mara Mbili na zaidi, lakini kwa Vile Mataifa hayo yanaongoza Vipofu yamezuia kutolewa habari hizo, Viongozi wao wanaendelea kufanya Mzaha na kujaribu kuwafumba watu wao"

"Nilipokea siku hiyo hiyo waliposema Russia isisafirishe Mafuta kwa Nchi za America, Ajabu siku tatu Baadae wamelalamika Bei za Mafita zimekuwa karibu mara mbili, na Mfumuko wa Bei za Bidhaa zao Hazielezeki kabisa, Ni Kichaa tu anayeweza kusema Eti Tunaumia sisi kuliko Ambaye Bidhaa zake zimepanda kwa 170.6%.

"Kwa sasa katika Ulaya Nzima penye Unafuu wa Maisha ni Russia tu, Wengine hata Gesi Imegeuka dhahabu, hupati gesi, watawala wao wamejipiga shaka kwa kujaribu kupambana na Russia"...Rais putin alinukuliwa akisema.

"Walitaka tukubali kuhatarisha usalama wetu kisa manufaa Kiduchu ya kiuchumi, Haiwezekani, hatukubali na siku yoyote ikiwa hivyo tutajibu vikali zaidi kuliko Operation ya Ukraine ".
 
Mpaka Putin anaingia vitani, haya yote alishayabaini na kuyafanyia mahesabu. Si mjinga. Vikwazo vinawaumiza wote, wa nje tena zaidi. Kila mtu, popote pale, atajikuta analipia gharama za kushupaza huku shingo.

Unabana kumkomoa Putin huku mzigo unarudi kutesa raia wako wanaotegemea gesi na mafuta 'rahisi' kutoka hukohuko ulipobana.

Kiburi cha Putin ni kuamini Ulaya inamhitaji yeye zaidi kuliko anavyoihitaji.
 
The last kick of a dying donkey.

Russia imekua kama kisiwa, hakuna ndege wala meli inayoweza kwenda ama kutoka Russia.

Hii ni failed state after 2 months ahead
Mpaka Putin anaingia vitani, haya yote alishayabaini na kuyafanyia mahesabu. Si mjinga. Vikwazo vinawaumiza wote, wa nje tena zaidi. Kila mtu, popote pale, atajikuta analipia gharama za kushupaza huku shingo.
 
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema mwisho wa siku Urusi hatimaye itaibuka na nguvu na uhuru zaidi baada ya kukabiliana na matatizo yaliyosababishwa na kile alichokiita vikwazo haramu vya nchi za Magharibi.

Putin alisema hakujawa na mbadala wa kile Urusi inachokiita operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kwamba Urusi sio nchi ambayo inaweza kukubali kuathiri uhuru wake kwa aina fulani ya faida za kiuchumi za muda mfupi.

Chanzo: Reuters

LONDON, March 10 (Reuters) - Russian President Vladimir Putin said on Thursday that Russia would ultimately emerge stronger and more independent after overcoming the difficulties caused by what he called the West's illegitimate sanctions.

Putin said there had been no alternative to what Russia calls its special military operation in Ukraine and that Russia was not a country which could accept compromising its sovereignty for some sort of short-term economic gain.



"These sanctions would have been imposed in any case," Putin told a meeting of the Russian government. "There are some questions, problems and difficulties but in the past we have overcome them and we will overcome them."

Source: ReutersView attachment 2146411
Anaongea kwa mtazamo kwamba wao pamoja na wamagharibi watasota kiuchumi nani ataibuka kwanza. Wamagharibi pamoja na makelele mengi hawakutegemea huyu jamaa ataenda kijeshi chap ivo na hawakuwa tayari. Aidha wangeshajiandaa mambo ya mafuta nk
... na sisi vitawi vya pembeni ndo tutaenda kwa upepo tukishikilia mkuti
 
Back
Top Bottom