Putin anatakiwa kukutana na nchi kama Finland ambayo sasa naona ameanza kuichokonoa, atashangaa NATO ipo Moscow

Putin anatakiwa kukutana na nchi kama Finland ambayo sasa naona ameanza kuichokonoa, atashangaa NATO ipo Moscow

Finland ni wapole sana sidhani kama wanajua vita.
Wapole wakati ndiyo nchi insyoongoza kwa raia wake kuwa na furaha? Ogopa sana nchi ambayo raia wote wako extremely happy with their country, yaani ukianzisha vita nao kila mmoja atashika silaha kutetea nchi yao tena buree
 
Finland ni taifa pole sana na ndio maana Stalin wa Urusi akaivamia na Cha moto alikipata.....Finland anapoilinda nchi yake yupo tayari kushirikiana na mtu yoyote

Ikumbukwe tu alishirikiana na NAZI jerumani dhidi ya Soviet hivyo hawezi shindwa shirikiana na NATO

Putin kashindwa zicheza karata vizuri kidiplomasia na wazungu wenzie Sasa hajiimalishe tu na bara la Asia
Hajiimalishe [emoji3582]
Ajiimarishe [emoji3581]
 
Wapole wakati ndiyo nchi insyoongoza kwa raia wake kuwa na furaha? Ogopa sana nchi ambayo raia wote wako extremely happy with their country, yaani ukianzisha vita nao kila mmoja atashika silaha kutetea nchi yao tena buree

Kuwa serious, Finland na urusi wapi na wapi? Marekani na Nato wangelikua na ubavu wangemsaidia ukrein. Huo ubavu hawana, sembuse kafinland!! Acheni story za vijiweni bwana.
 
Russia anatakiwa kukutana na wendawazimu kama Finland, hao ndiyo hata yeye Russia anawagwaya.
Mwaka 1939 aliivamia Finland ili kuitanua himaya yake ya Soviet, pamoja na uhodari wa Jeshi lake na vifaa vyake vya kivita Russia aliishia kupata hasara kubwa sana kwenye ile winter war, zaidi akaishia kufukuzwa uanachama kutoka The League of Nations kabla haijabadilika na kuwa UN.
Baada ya vita kuu ya pili ya dunia akaendelea kuzitisha na kuzimavamia nchi za Ulaya ili kuziunganisha ma Soviet na kwa kuwa alikua ni giant, hivyo hakukua na wa kumzuia. Ndipo mwaka 1949 Ulipoanzishwa Umoja wa kujihami wa nchi za Ulaya (NATO), NATO ilianzishwa ili kujihami na Russia and nobody else. Finland hakutaka kujiunga, maana alishaamua hamuogopi na akimleta zake watamalizana.

Hivi majuzi Russia alipowaonya majirani zake kuwa yeyote atakayetaka kujiunga na NATO lazima amshikishe adabu na kweli Ukraine akaanza kusumbuliwa waswahili wanasema akakiona cha moto, ndipo Finland akatangaza kujiunga na NATO, yaani ni kama vile kumwambia “wapangie hao hao mambwiga, mimi huna la kunifanya" na akaenda mbali zaida kwa kuagiza Israeli SPYDER air defense system, mfumo ambao Ukraine aliuomba vita ilipoanza ili kulinda anga lake, lakini Russia alipoona hivyo akaanza kulalamika na kuitisha Israel kuwa Russia haitahusika na Ulinzi wa assets za Israel mchini Syria, kitu ambacho haki make sense, kwani Israel hama anachomtegemea Russia huko Syria maana hata ule mfumo wa Russia wa S-300 hundred si lolote kwa Israel kutimiza mission zake.

Pamoja na hayo Israel aliamua ku back off na kutompatia Ukraine mfumo ule sababu aliona si busara kuupeleka mfumo ule wakati huu vita na yeye ana maslahi na ukaribu na nchi zote mbili, na ndiyo iliyopelekea hata Moscow ikubali Israel kuwa mediator kwenye vita hii.

Lakini Finland ameshaagiza mzigo wake na anaenda kufungiwa,

Leo waziri wake wa Ulinzi amemkumbusha Urusi kwamba ntakulisha biscuit kwenye Vita ya kwenye baridi kama hapo awali cheza uone” hii imakuja baada ya Urusi kusema kwamba Endapo Finland itajiunga atapata Tabu sana”

Wataalamu wa Masuala ya Saikolojia wamemzunguka Putin kumshauri kila mara baada ya kuona kila mission yake haitimii

Mfano Kumrejesha Kibaraka wake UKRAINE na kuiangusha Dola ya Zelensky kaishia kupata hasara yeye


Britanicca
putin ni beberu hatari sana!
Hana tofauti na hitler
 
Usichokijua kutokana na kushindwa huko kwa Russia miaka ile, ili warusi kuondoka ulitengenezwa mkataba ambao Finland iliachia 10 percent. Ardhi hii Ni sehemu ya Russian Federation. Hiyo huitwa Keralia.
Rudi class shee
Hiyo ilitokea baada ya kipigo bila kipigo USSR wasingekubali. Alichakazwa vibaya sana.
 
... Na mwaka 1903 pia Urusi ilipigwa vibaya sana na Japan hadi akanyang'anywa vile visiwa vya Kurill Islands. Hawa warusi wana historia ya kupigwa na vinchi vidogo vidogo sana na tuweke macho hata hapa kwa Ukraine atakula kipigo cha kufa mtu,
 
Hao NATO pamoja na baba yao US na mama yao England wamenyooshwa na Putin.
Hawajathubutu kuingia kwenye mipaka ya Ukraine licha ya Ukraine kulawitiwa mchana kweupe na Mrusi.
Libya kuna NATO?
Vipi NATO haikutia mguu ndani ya Libya?
If yes, mbona hawajatia mguu Ukraine?
Russia alitakiwa avamie mataifa ya Nato yanayoifadhili Ukraine kwa fedha na silaha, lakini hawezi kuthubutu kwani wanafahamu itasababisha historia ya Russia iandikwe upya.
 
Russia alitakiwa avamie mataifa ya Nato yanayoifadhili Ukraine kwa fedha na silaha, lakini hawezi kuthubutu kwani wanafahamu itasababisha historia ya Russia iandikwe upya.
Na hao NATO walitakiwa wakampige Mrusi nyumbani kwake yaani wakafanye special operation huko ndipo watakapotekenywa na mzee baba Putin
 
Jerumani au Germany niliandika hivyo ili nikusaidie wale wenye matatizo ya uchungu ambao unapelekea kujiua au depression. Ebu katibiwe kwanza mtindio wa ubongo

Halafu ukipona kajifunze historia sababu ilo SoMo sio lazima ukae darasani kwahiyo usiogope na elimu yako ya kuunga unga ya darasa la 7B
Hahaha...yaani pamoja na kujikunja kote huko bado umekosea kuandika!! Ilo ndo mdudu gani??? Unaonekana hata kiswahili hujafunza wewe! Unapaswa kuandika Hilo badala ya ilo!! Nchi hii ni ngumu sana kupiga hatua kimaendeleo mana watu wake hawajui hata basics za lugha yao!
 
Kuwa serious, Finland na urusi wapi na wapi? Marekani na Nato wangelikua na ubavu wangemsaidia ukrein. Huo ubavu hawana, sembuse kafinland!! Acheni story za vijiweni bwana.
sijui huwa wana waza nini apo mwenyewe Ukraine wametoa misaada yote ya silaha bado wana twangwa kweli kweli na sasa hivi ndio kichapo haswa kina tembezwa
 
Back
Top Bottom