Putin asema nchi za Magharibi zikiondoa vikwazo Urusi itauza nje chakula na mbolea

Putin asema nchi za Magharibi zikiondoa vikwazo Urusi itauza nje chakula na mbolea

Mrusi ana taka aondolewe vikwazo vingine ambavyo labda kweli vina husiana na usambazaji na malipo ya chakula ila hakuna kikwazo cha moja kwa moja kwenye chakula.
Kama meli zake haziruhusiwi kutoa nanga katika bandari yyoyote unataka aruhusu meli za yukraine zikachukue mizigo kwenye bandari zao zilizotekwa🤔
 
kwani aliyelalamika njaa Putin au wewe? Tutarudisha stoo sis....
Rudisheni tu,ikiwezekana wapeni hata Paka wa Putin wale,hakuna aliyewaomba lakini vikwazo viko pale pale.
 
Putin kwa mikwara mbuzi hajambo- mara ataangamiza dunia kwa nuklia, oh nitawalaza njaa msipoondoa vikwazo.
Ana mikwara ya kitoto sana na wameshamjulia kuwa ni debe tupu.Sasa hivi amenywea kwa Finland na Sweden kujiunga NATO.
 
Kama meli zake haziruhusiwi kutoa nanga katika bandari yyoyote unataka aruhusu meli za yukraine zikachukue mizigo kwenye bandari zao zilizotekwa🤔
Naweza kusema "ndio" kwa sababu si bandari zake
 
Uwe unauliza kama hujaelewa.
Ni hivi hao waweka vikwazo ndio walimpiga Putin si, u wajiomba aachie misosi; nayeye akasema ataachia misosi watakapoondoa vikwazo.

Hakuna Baunsa mbele ya njaa.
Kuna haja gani ya kuuliza wakati ninasoma mwenyewe taarifa moja kwa moja? Au wewe ni right-handman wa Putin? Vikwazo viko pale pale.
 
Naweza kusema "ndio" kwa sababu si bandari zake
Hizo zimeshakuwa za mrusi ikiwa ni pamoja na chakula kilichopo maeneo aliyoyateka,vinginevyo wafanye kama wanavyobadilishana mateka,wanataka chakula waondoe vikwazo,wanataka mbolea waondoshe vikwazo,wanamwaga mboga yeye ana mwaga ugali na maji ya kuoshea mikono na pia anaichafua mikono Yao🚶
 
Hizo zimeshakuwa za mrusi ikiwa ni pamoja na chakula kilichopo maeneo aliyoyateka,vinginevyo wafanye kama wanavyobadilishana mateka,wanataka chakula waondoe vikwazo,wanataka mbolea waondoshe vikwazo,wanawapa mboga yeye ana mwaga ugali na maji ya kuoshea mikono na pia anaichafua mikono Yao🚶
Hizi sio zama za mongolia una kwenda mahali na kusema hapa mpaka kule ni kwangu
 
Hizi sio zama za mongolia una kwenda mahali na kusema hapa mpaka kule ni kwangu
Kwa mazingira tunayozungumzia ndio imeshakuwa hivyo Sasa,Japo vyombo vya mabeberu havitaki wewe na Mimi tukausikia huo ukweli.Ila ni swala la Muda Tena kidogo TU mbivu na mbichi hadharani 🤔
 
Warusi wa JF wanasema vikwazo havimtishi Putin, sasa kama ni hivyo kwa nini analia lia wamuondolee? Akae na chakula chake ikiwezekana alishe hadi kunguni wa nyumbani kwake,vikwazo viko pale pale.
hapo anatafuta namna ya kutoka kwenye vikwazo ,vikwazo vimempa wakati mgumu.

Watu wanashindwa kuelewa we tu umewekewa vikwanzo na wengi ila wao wanasaidiana na kutatua matatizo yao ili wakukomoe ila huna msaada unapewa.

Vyakula na mbolea vilikuwa vinauzwa nje sasa hivi hali imebadilika ,vikwazo juu na ugumu wa maisha halafu huuzi nje.
 
Putin maji ya shingo,sidhani kama alijua kuwa ingekuja kumgeukia kiasi hiki.Katika Dunia hii huwezi kusurvive ukiwa umetengwa hata uwe mbabe kiasi gani? Ndiyo maana China katika hili kamwachia apambane na hali yake,pale UN akamute kupiga kura.
 
Rais Putin jana alisema Urusi inapanga kuuza nje chakula na mbolea ili kutoa mchango katika kukabiliana na msukosuko wa chakula duniani, lakini sharti lake ni kuwa nchi za magharibi zitaondoa vikwazo vilivyowekwa kutokana na madhumuni ya kisiasa.
Kwani si tulikubaliana kwamba vikwazo haviiumizi Russia?
 
Putin maji ya shingo,sidhani kama alijua kuwa ingekuja kumgeukia kiasi hiki.Katika Dunia hii huwezi kusurvive ukiwa umetengwa hata uwe mbabe kiasi gani? Ndiyo maana China katika hili kamwachia apambane na hali yake,pale UN akamute kupiga kura.
hao China na North Korea aliowategemea hawana msaada ,kiduku alikuwa anarusha rusha makombora ,Marekani na South Korea walipofanya zoezi tu akawa kimya, na akichokoza silaha zinapelekwa South Korea huo mda wa kusaidiana na Putin sijui atautoa wapi.

Putin hajiulizi wale aliokuwa anawategemea hatusikii waliompa silaha au msaada wa kifedha.
 
Kila siku tunakula tunashiba, dikteta abaki na mavyakula yake, na vikwazo havitolewi ng'o yeye aendelee kujilizaliza tu.
 
Warusi wa JF wanasema vikwazo havimtishi Putin, sasa kama ni hivyo kwa nini analia lia wamuondolee? Akae na chakula chake ikiwezekana alishe hadi kunguni wa nyumbani kwake,vikwazo viko pale pale.
Mmarekani wa Tandale upo vizuri sana. Wanaolia njaa ni wazungu
 
Back
Top Bottom