Putin asema nchi za Magharibi zikiondoa vikwazo Urusi itauza nje chakula na mbolea

Putin asema nchi za Magharibi zikiondoa vikwazo Urusi itauza nje chakula na mbolea

Kila siku tunakula tunashiba, dikteta abaki na mavyakula yake, na vikwazo havitolewi ng'o yeye aendelee kujilizaliza tu.
Ulaya wamekubali kulipa kwa Rubo ili waendelee kula gesi ya mrusi. Pia wameanza kumpigia magoti ili awauzie chakula na mbolea.
 
Ulaya wamekubali kulipa kwa Rubo ili waendelee kula gesi ya mrusi. Pia wameanza kumpigia magoti ili awauzie chakula na mbolea.
Mrussi wa kilongawima bwana [emoji3][emoji3]
 
Mmarekani wa Tandale upo vizuri sana. Wanaolia njaa ni wazungu
Mrussi wa kilongawima akiwafokea wazungu baada ya yeye kushiba ugali na mnafu uliopikwa kutumia kuni na maji yaliyofuatwa km 5 na mama watoto [emoji3]
 
Ukiona hivyo jua vikwazo vimemshika pabaya mrusi

Marekani wakulima wamekubali kulima mara nne zaidi kuzalisha ziada ya chakula kuuza Ulaya na viwanda vya mbele vya nchi za Magharibi vimeongeza uzalishaji mbele

Tanzania tutumie hiyo fursa soko la chakula Ulaya kubwa mno hasa ngano kwa sasa
Wakiongeza uzalishaji kesho chakula kitapatikana
Katika hio miezi ambayo kutakua hakuna chakula itakuaje
Hayo masuala yote sio marahisi nandio maana miaka yote wanakaa wanalishwa lishwa
RUSSIA sio ZIMBABWE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona hivyo jua vikwazo vimemshika pabaya mrusi

Marekani wakulima wamekubali kulima mara nne zaidi kuzalisha ziada ya chakula kuuza Ulaya na viwanda vya mbele vya nchi za Magharibi vimeongeza uzalishaji mbele

Tanzania tutumie hiyo fursa soko la chakula Ulaya kubwa mno hasa ngano kwa sasa
Wew ndio mgum kabisa kuelewa.
Marekan angekua na uwezo wa kulisha ulaya yote, hiyo njaa ingetoka wapi?
Kiufupi mmejitekenya wenyewe, kubalini matokeo.
 
Ukiona hivyo jua vikwazo vimemshika pabaya mrusi

Marekani wakulima wamekubali kulima mara nne zaidi kuzalisha ziada ya chakula kuuza Ulaya na viwanda vya mbele vya nchi za Magharibi vimeongeza uzalishaji mbele

Tanzania tutumie hiyo fursa soko la chakula Ulaya kubwa mno hasa ngano kwa sasa
Ngano sisi wenyewe hatuna,tutapata wapi ya kulisha Ulaya.Wambembeleze Putin tu awapelekee.Kule Ukraine ngano zinaota kama uyoga bila mbolea.
 
Watanzania wa kuongeza uzalishaji ni wenye mtazamo kama wako au una zungumzia warusi na wale wanaofanana nao🤔
 
Ngano sisi wenyewe hatuna,tutapata wapi ya kulisha Ulaya.Wambembeleze Putin tu awapelekee.Kule Ukraine ngano zinaota kama uyoga bila mbolea.
Na inapoota hiyo ngano kashapateka mrusi,na yule jamaa yao anaota atairudisha kwake,ila hakumbuki hata Cremia miaka mingapi imepita na hajaweza irudisha kwake🚶
 
Mrusi u super power wake kamishina pumzi ya silaha kukimbilia kwenye chakula!! Misilaha take yote anajidai nayo haijaleta matokeo tarajiwa !! Kalimbilia kwenye chakula!! Ushahidi kuwa vita yake ya kutumia silaha haijaleta matokeo chanja!!

Ila vikwazo alivyowekewa vimemshikisha adabu
 
Mrusi u super power wake kaishiwa pumzi ya silaha kakimbilia kwenye chakula!! Misilaha take yote anajidai nayo haijaleta matokeo tarajiwa !! Kalimbilia kwenye chakula!! Ushahidi kuwa vita yake ya kutumia silaha haijaleta matokeo chanja kwake ila vikwazo vya Magharibi vimemshikisha adabu ndio maana analia viondolewe
 
Mrusi u super power wake kamishina pumzi ya silaha kukimbilia kwenye chakula!! Misilaha take yote anajidai nayo haijaleta matokeo tarajiwa !! Kalimbilia kwenye chakula!! Ushahidi kuwa vita yake ya kutumia silaha haijaleta matokeo chanja!!

Ila vikwazo alivyowekewa vimemshikisha adabu
Kama Haina matokeo tarajiwa,wanaojidai Wana ubongo wa kenge wanalialia nini wao pamoja na mabeberu wanao wachochea wenye ubongo wa kenge kuendelea kuona mambo Yako sawa na hakuna kilichotokea au kubadilika🤔
 
Jion ya leo kuna majimbo mawili ya ukraine yamechukuliwa na Urusi. Habari zisizo rasimi ni kuwa ayo maeneo yamekutwa yapo wazi wanajesh wameshakimbia.
 
Inabidi tujifunze ....kuwa omba omba siyo vizuri tulime vyetu mbona tuna maeneo mengi yenye rutuba
 
Ulaya wamekubali kulipa kwa Rubo ili waendelee kula gesi ya mrusi. Pia wameanza kumpigia magoti ili awauzie chakula na mbolea.
Uongo, kwa akili yako chakula Cha urusi ni kitamu sana au urusi pekee ndo inazalisha chakula hapa duniani?! China hailazimishi kulipa kwa yuan lakini uchumi wake unapaa, na Japan kadhalika. Walipe kwa hela yoyote Ile shida ni iko palepale, vikwazo.
 
Ukiona hivyo jua vikwazo vimemshika pabaya mrusi

Marekani wakulima wamekubali kulima mara nne zaidi kuzalisha ziada ya chakula kuuza Ulaya na viwanda vya mbele vya nchi za Magharibi vimeongeza uzalishaji mbele

Tanzania tutumie hiyo fursa soko la chakula Ulaya kubwa mno hasa ngano kwa sasa
kuna watu wengine inabidi mpimwe akili kabisa.

NIMEKOPY NA KUPEST DW SWAHILI

Putin awaonya Scholz na Macron dhidi ya kuipa silaha Ukraine​

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewatahadharisha viongozi wa Ujerumani na Ufaransa dhidi ya kupeleka msaada wa silaha nchini Ukraine, akisema hatua hiyo inaweza kuzidisha hali ya ukosefu wa utulivu katika nchi hiyo.

Kombobild Russland Frankreich Putin und Macron

Ikulu ya Kremlin imesema Putin amewaambia Rais Emmanuel Macron na Kansela Olaf Sholz kuwa kuendelea kuipatia Ukraine silaha ni "hatari", akionya juu ya hatari ya kuzidisha mzozo wa kibinadamu.
Katika mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi hao wawili leo Jumamosi, Putin amesema pia Urusi iko tayari kujadili juu ya njia za kuiwezesha tena Ukraine kusafirisha nafaka kutoka bandari ya bahari nyeusi.
"Kwa upande wake, Urusi iko tayari kusaidia kulitafutia ufumbuzi suala la usafirishaji wa ngano, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa nafaka za Ukraine katika masoko ya nje kutoka bandari ya bahari nyeusi,” Ikulu ya Kremlin imesema.
Soma pia:Wafaransa wapiga kura katika duru ya pili ya urais
Urusi na Ukraine ni miongoni mwa wauzaji wakubwa wa ngano duniani, wakati Urusi pia ikiwa muuzaji muhimu wa mbolea katika soko la kimataifa. Ukraine inasifika kwa uuzaji wa mahindi na mafuta ya alzeti.
Kremlin imeongeza kuwa, Putin alimjulisha Macron na Scholz kuwa Urusi iko tayari kuongeza mauzo ya nje ya mbolea na bidhaa nyengine za kilimo iwapo tu vikwazo dhidi yake vitaondolewa- ombi ambalo amelitoa katika mazungumzo yake na viongozi wa Italia na Austria katika siku za hivi karibuni.
Scholz na Macron wamtaka Putin kufanya mazungumzo na Zelenksy
EU Gipfel Scholz und Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Ukraine na mataifa ya Magharibi yameishtumu Urusi kwa kutumia mzozo wa chakula uliosababishwa na uvamizi wake nchini Ukraine kama silaha ya kivita. Mzozo huo umesababisha bei ya bidhaa za vyakula, nafaka, mafuta ya kupikia, na mbolea kupanda maradufu duniani kote.
Hata hivyo, Urusi imezinyooshea kidole cha lawama nchi za Magharibi kwa hali hiyo kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Moscow.
Soma pia: Macron, Scholz waepuka kutaja mauaji ya Ukraine kuwa "halaiki"
Kremlin imesema pia kuwa Putin yuko tayari kuanza tena mazungumzo na Ukraine."Hali ya mazungumzo ya amani iligusiwa katika mazungumzo ya leo kati ya Putin na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani. Rais Vladimir Putin amethibitisha utayari wa Urusi kuanza tena mazungumzo hayo,” Kremlin imesema.

0 seconds of 0 secondsVolume 90%

Tazama vidio02:26

Kansela Scholz azungumzia ziara yake Afrika​

Aidha viongozi hao wa Ujerumani na Ufaransa wamemtaka Rais Putin kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenksy.
Ofisi ya Kansela huyo wa Ujerumani imesema, wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu yaliyodumu saa moja na dakika 20 kati yao na Putin, viongozi hao wawili wa Umoja wa Ulaya EU walisisitiza juu ya kusitishwa mara moja mapigano na kuondolewa kwa vikosi vya Urusi nchini Ukraine.
Macron na Putin wamemtolea mwito Putin kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Zelenksy na kutafuta suluhusisho la kidiplomasia kwa mzozo huo.
 
Back
Top Bottom