Shida ya Putin ndo hiyo , akipiga nyuklia na yeye ameisha. Warusi wako tayari wateketee kisa wanataka mikoa 4 ya Ukraine? Hiyo ni sababu ndogo ya kusababisha vita ya 3 ya dunia. Pia siku nyingine atavamia nchi yoyote jirani halafu atishie nyuklia. USA, UK, France, wana nyukilia. Huwezi tishia nyuklia na wakati na wao wanazo nyuklia, anaona wazungu wa NATO ni waoga wa vita ndo maana anajaribu kutishia, mwenzake China hawezi kujiingiza kwenye vita vya nyuklia. Uzuri vita vya nyuklia havina mshindi atalipwa na wao watalipua, makombora yatakuwa yanapishana angani na baharini. Mwenye air defence system nzuri ndo atapona.Ila kuna uwezekano mkubwa wa Rusia kuwahi kuteketea kabla ya nchi zote za NATO, Africa tujiandae kupokea wakimbizi toka Rusia na Nchi za NATO