Putin atoa masharti yake ya kumaliza vita yake na Ukraine, na hivyo kuondoa majeshi yake kwenye nchi hiyo

Soma historia .ussr- walichukua Yogoslavia mwaka 1968 chini ya masaa 24 .Putin na jeshi lake wamaonyesha udhaifu mkubwA.
imeichukua miaka 50s toka hio vita mpaka hii ya leo
nadhani umenielewa
 
Ingekuwa hivyo unavyoongea isingefika leo ya 7 russia hajatangaza kuipindua Ukrain, jua kazi inaendelea tena kwa umakini sana kumbuka majigambo ya russia tulijua hardly angechukua siku 2 tu
kama walivyochukua NATO kule IRAQ?
 
Tofautisha umbali wa Iraq mpaka Marekani, ukizingatia Iraq ilikua taifa kubwa lenye zana za kila aina. Urusi hapo jirani katafa kadogo kanamtoza kamasi kwenye all-out war.....aibu sana hii.
Wakati Marekani anavamia Iraq tayari Iraq alikuwa amewekewa vikwazo kwa zaidi ya miaka 10. Walikuwa hoi.

Iraq ya 1991 na ya 2003 ni tofauti.

Ukraine ya Sasa ina nguvu kuliko Iraq ya 2003.
 
vita ya iraq marekani alitumia siku ngapi kufika mji mkuu na washirika wake?
 
Urusi imetia aibu kubwa sana, kwa jeshi hili ni vizuri vile Putin hataki NATO wamsogelee zaidi kwani siku wakimwamkia ndani ya wiki wanakamata nchi yote. Anapigana bega kwa bega na Belarus ila output kubwa mpaka sasa ni kuvunja majengo. Zaidi ya nuclear warheads alizonazo hana maajabu yoyote.
 
Tayari kashaweka ukomo wa kutoa pesa bank na ukomo wa kiasi cha kusaforisha pesa nje ya Urusi, ni wazi vikwazo vinakaba pumzi.
 
vita ya iraq marekani alitumia siku ngapi kufika mji mkuu na washirika wake?

Ukraine ni jirani wa Urusi, huyo Urusi amewekeza wanajeshi 120,000 na kutumia zana za kila aina lakini mji wa Kiev umekua mfupa uliomshinda fisi, kule nyumbani Putin ametaharuki na kutahamaki, hapa nawaza anavyofoka.
 
Aisee mkuu yawezekana wewe ukawa na intelijensia na ufahamu mkubwa zaidi juu ya jeshi la Russia kuliko hata Defense Secretary wa Marekani General Lloyd Austin anayesema kuwa Russia bado wana uwezo na nguvu kubwa mno ya kuishambulia Ukraine ambayo bado hawajaamua kuitumia.

 
Kuna alisema ugali hudumaza akili, aliyechangia kasema Urusi ilisema inafanya operation ya masaa 24 itakuwa imemaliza kazi yake. Sasa wewe unakuja na mifano ya Somalia sijui na Afghanistan, hoja ya kumpinga ilikuwa ni wewe kuonesha kwamba Russia haikuwahi kutoa tamko la vile au kutaka aweke chanzo cha habari yake.
 
Punguza munkari, uongozi wa NATO ni rotational na sasa uongozi upo kwa Ufaransa, ndio maana unaona Macron anafanya mawasiliano kwa niaba ya NATO.
 
Western media propaganda zinashindwa to capture global attention. Kila nikipitia websites zao naona bado habari ni zile zile za a 'dying horse'
Na huko urusi je, unafahamu masharti waliyopewa vyombo vya habari?!!jana mama mmoja anaishi urusi anahojiwa kwanini urusi inashambulia majengo na wananchi, alikataa kabisa akasema yeye anachokiona kwenye tv, magazeti ya urusi ni kuwa wamekwenda kulinda amani hawawezi kuwaua ndugu zao wa ukraine!!hicho unachosema ni propaganda za ulaya magharibi!!
Hatuwezi kumlaumu huyo mama kwani anachoonyeshwa na kukisikia kupitia vyombo vya habari vya Urusi ni hicho alichokisema!!
Putin anaamini kwwnye mabavu zaidi lakini wengine wanaamini kwenye kubana kwa akili, na hilo litamuumiza sana!!kwani hadi sasa wananchi wake wameanza kuonja machungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…