Putin katelekeza wanajeshi wake toka vita ianze miezi 8 sasa hajawahi watembelea askari wake walio msitari wa mbele Ukraine

Putin katelekeza wanajeshi wake toka vita ianze miezi 8 sasa hajawahi watembelea askari wake walio msitari wa mbele Ukraine

Obama alienda libya? Na Bush kule iraq kule afganistan hata trump hakufika mpaka wanajesh wameondoka mwakajana
Hivi unaelewa hara ulichoandika? Libya na Iraq zilipigwa kwa azimio.la umpja wa mataifa lililotoa agizo la kuundwa kwa Jeshi la kimataifa coalition army kwenda kutandika Saddam Hussein na Ghadafi
Ni kama Sisi JWTZ Ikiwa kwenye Jeshi chini ya Umoja wa Nchi za Afrika huwezi sema Mbona Raisi haendi kutembelea!!

Urusi inaipiga Ukraine peke yake kama Sisi tulivyokuwa tukiipiga Uganda peke yetu.Nyerere alikuwa akienda msitari wa mbele kuonana na wanajeshi

Putin kajifungia ndani kama mwali Kremlin vita kaanzisha yeye peke yake ,amiri Jeshi akiwa yeye sio makamanda wa coalition army au Umoja wa mataifa!!
 
Wewe ndio .Vita ya Iraq na Libya alifanya na coalition army chini ya Umoja wa mataifa

Usilinganishe na uvamizi wa Urusi kwa ukraine
Marekani huwa wanaenda vita wenyewe?huna wanaenda na wenzao.coalition chini ya umoja wa mataifa ya upuuzi Tu.Mwanaume urusi anaenda vitani mwenyewe.
 
Marekani huwa wanaenda vita wenyewe?huna wanaenda na wenzao.coalition chini ya umoja wa mataifa ya upuuzi Tu.Mwanaume urusi anaenda vitani mwenyewe.
Putin kama mwanaume si alitishia yeyote atakayemsaidia Ukraine atamwonyesha cha mtema kuni Mbona kaufyata wababe wanatangaza mchana kweupe kuwa tunamsaidia Ukraine .Yeye kajificha kwenye mashimo hataki hata kwenda kutembelea Askari wake vitani.
 
Putin ana majukumu mengi, Zelensky Kwa Sasa jukumu lake ni Moja tu,Vita!
Kweli ana majukumu mengi sana mpaka anaogopa kushiriki misiba tena ya kitaifa, kwenye vikao ofisin kwake anakaa mbali mnoo na wenzake.
 
Sisi kama warusi wa morogoro kilosa hatuungi mkono jambo hili. Haiwezekani kipondo tupewe na bado mnamtaka mtume wetu putin aje vitani mumuue, hili haliwezekani. Takbiirrrrrr!
😜🤪😆🤣🤪🤪👻
 
Vita ikilipuka amiri Jeshi mkuu huwa ana kawaida kuwatembelea wapiganaji walio msitari wa mbele vitani kuongea nao na kuwatia moyo na kuwasikiliza

Raisi Zelensnkyy wa Ukraine amekuwa akiwatembelea mara kwa mara Askari wake walio mstari wa mbele na kupokelewa kwa shangwe na Askari wake

Putin katelekeza wanajeshi wake toka vita ianze miezi 8 sasa hajawahi watembelea askari wake walio msitari wa mbele hata kukanyaga tu maeneo ambayo Urusi inasema imeyateka yako mikononi mwao.Putin hajawahi kanyaga msitari wa mbele uwanja wa vita.Katelekeza watoto wa watu vitani yeye anakula kuku kwa mrija Kremlin akiangalia vita kwenye Television vijana wake wakitwangwa na makombora ya Himars

Putin ni Amiri .jeshi mkuu wa ajabu kuliko wote.Yeye anaogopa kwenda halafu anasokomeza watoto wa wenzie waende.Au hajiamini na hawaamini wanajeshi wake kuwa akienda aweza asirudi ?
Hivi amiri jeshi akiingia kuwatembelea askari wake vitani lazima ninyi raia wa periphery mjue? Najaribu kuwaza kwa sauti kwa kuwa najua wajua kuwa Media za Magharibi hazitangazi habari za Urusi vitani na RT imechomolewa hewani.

Vv
 
Kweli ana majukumu mengi sana mpaka anaogopa kushiriki misiba tena ya kitaifa, kwenye vikao ofisin kwake anakaa mbali mnoo na wenzake.
Mazishi ya Raisi Mstaafu wa Urusi Mikhail Gorbachev ,Raisi Putin hakwenda mazishi hapohapo Moscow hakwenda anaogopa kudunguliwa.Warusi kwa maelfu wamemzika Raisi wao mstaafu siku kadhaa ziliizopita tarehe Tatu mwezi huu.Yeye kajichimbia kwenye mahandaki kusikojulikana!!
 
Zelensky ni mchekeshaji na kuwa mstari wa mbele ni sehemu ya jukumu lake kama mwanasesere
 
Mazishi ya Raisi Mstaafu wa Urusi Mikhail Gorbachev ,Raisi Putin hakwenda mazishi hapohapo Moscow hakwenda anaogopa kudunguliwa.Warusi kwa maelfu wamemzika Raisi wao mstaafu siku kadhaa ziliizopita tarehe Tatu mwezi huu.Yeye kajichimbia kwenye mahandaki kusikojulikana!!
Gorbachev aliitwa msaliti wa taifa..
 
Putin kama mwanaume si alitishia yeyote atakayemsaidia Ukraine atamwonyesha cha mtema kuni Mbona kaufyata wababe wanatangaza mchana kweupe kuwa tunamsaidia Ukraine .Yeye kajificha kwenye mashimo hataki hata kwenda kutembelea Askari wake vitani.
Tatizo hujui chochote hiyo ni kawaida nchi hizi Kubwa kuipelekea nchi hasimu silaha mfano Syria urusi aliwapa silaha serikali na marekani aliwapa silaha waasi au Korea war.urusi na China waliwasaidia NK na marekani waliwasaidia SK Kwa hiyo haya ni mambo ya kawaida.shida yenu nyie Team NATO sijui hamjui Historia.
 
Putin ni muoga sana, kuna hadi chawa wake wanamlia rada.
 
Hivi amiri jeshi akiingia kuwatembelea askari wake vitani lazima ninyi raia wa periphery mjue? Najaribu kuwaza kwa sauti kwa kuwa najua wajua kuwa Media za Magharibi hazitangazi habari za Urusi vitani na RT imechomolewa hewani.

Vv
Putin anaweza akaenda Ukraine na RT isitangaze?
 
Back
Top Bottom