Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Xhing Chong katoka china kaja kulima Tz we bishoo mmoja hujawahi kufika hata Nairobi eti hutaki kulima kisa una makaratasi ya Uni

Alaf wanamkamata kosa lake nn? Au wanatafuta mtu wa kumuangushia jumba bovu ili wajisafishe wao waonekane wawajibikaji ila muwekezaji ndo anahujumu?
 
#HABARI BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imemkamata mkulima mkubwa raia wa China anayefanya kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Kidogozelo Kitongoji cha Migudeni wilayani Chalinze akivuta Maji katika Mto Ruvu kwa kutumia mashine yenye uwezo wa kuvuta maji Lita milioni moja kwa saa. https://t.co/sdJ6JzZ2Ck
View attachment 2016510

Bwana Msabaha aliwahi ita hii kuwa "Mbagusiro."

Kwani:

1. Kiasi gani cha cubic metres za maji Ruvu inaendelea kumwaga baharini?
2. Shida ya maji iko Dar peke yake?

Wameshasingiziwa ng'ombe, sasa mchina na bado!
 
Mtu mpaka anajivutia maji kiasi hicho.....wahusika wako tu....wako tu.....shameful!!!
 
Unyanyasaji
Mnaimiza watu wawekeze kwenye kilimo cha kisasa mnasema kina tija kuliko kilimo cha kutegemea Mvua.
Mtu anayemwagilia maji anaonekana ni hatarishi kwa Nchi
Watu wakifanya kwa vitendo wanazuiliwa. Hao watu waende wapi hayo mazao anayomwagilia Maji yatakauka .
Akienda kuuza vitu kupanga chini anakuwa Mmchinga mnampelekea Polisi anakamatwa.

Toka uhuru mpaka leo umeme na maji shida CCM.
Uchumi umefunguka wawekezaji wanakuja Mchina anakuja kulima baada ya kuvutiwa na Fursa ya Rais anakamatwa.
Wachina wawekezaji kwenye kilimo ni vizuri wakaandamana
 
Hizo sheria wanatoa kwa wakazi wote wa Ruvu, au mpaka majanga yatokee ndio wanafumua makarabrasha ya sheria, sidhani kuna mtu mjinga atakae ambiwa hapo kuna moto na bado akaenda,
Ipo Sheria ya Bonde la Ruvu na matumizi ya maji kama ana vibari amepona kama ana Vibari amepotea kama mwana Nzilaha
 
Huyo mwekezaji wa mbogamboga angekuwa awamu ya Mobutu kule Zaire angepewa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha😂😂

8B695F8F-C234-418E-B5AB-A888FDFA0CED.jpeg
 
Ukiangalia kwenye hiyo Picha nyuma ya huyo Mwekezaji wa Kichina utaona Mto Ruvu ulivyokauka.

Halafu tunamshambulia Januwari Makamba.
 
Back
Top Bottom