Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Pwani: Mtambo wa kuvuna maji lita milioni moja kwa Saa, wakamatwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu

Mtanzania bwana?
Kazi anayofanya ni nzuri sana tena kwa faida yetu sote. Sema tatizo ni upungufu wa maji tu! Otherwise Mimi nampongeza sana.
Nina uhakika mkubwa sana kwamba wengi tunafaifika na mradi huo.
Tusimtukane jamani, angekuwa analima bangi sawa!
 
Ukiangalia kwenye hiyo Picha nyuma ya huyo Mwekezaji wa Kichina utaona Mto Ruvu ulivyokauka.

Halafu tunamshambulia Januwari Makamba.
Ushawahi kufika ruvu nyakati zote za mafuriko na kiangazi
Kwa miezi hii ruvu kukauka ni kawaida sana hata mwaka jana na juzi hali ilikua ivyo unavuka kwa miguu kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
 
#HABARI BODI ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imemkamata mkulima mkubwa raia wa China anayefanya kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Kidogozelo Kitongoji cha Migudeni wilayani Chalinze akivuta Maji katika Mto Ruvu kwa kutumia mashine yenye uwezo wa kuvuta maji Lita milioni moja kwa saa. https://t.co/sdJ6JzZ2Ck
View attachment 2016510
Kama ni mkulima wa mboga! Je? Anaziuza hapa hapa wananchi wanafaidi au anasafirisha nje?
Kwani ameanza jana au alikuwepo muda. Hakuna haja ya kupaniki hawa ndio CCM. Shamba alilipataje au alivamia?!.
 
Hizo sheria wanatoa kwa wakazi wote wa Ruvu, au mpaka majanga yatokee ndio wanafumua makarabrasha ya sheria, sidhani kuna mtu mjinga atakae ambiwa hapo kuna moto na bado akaenda,
Mwendazake alikuwa hajali mambo ya Mazingira kwa maelezo kwamba ni wapiga kura
 
Kule kanda ya ziwa mnauziwa maji kwenye madumu wakati ziwa la maji fresh limewazunguka.Kama haina madhara aachiwe tu mlitaka anunue ya dumu wakati mto upo karibu
 
Kitu kingine mnatakiwa kujiongeza.
Kwa jiografia ya ruvu kuanzia mwezi wa nane mpaka wa 12 ndio kipindi cha watu kulima mboga mboga. Na kuanzia huo mwezi wa kwanza mpaka wa sita hapo ni kilimo cha mounga kwa sababu ukifika wa 3 mto huwa unafurika sana.
Sasa huyo mchina yupo kwenye mzunguko huo wa kulima mboga na pia kulimo cha mboga utaratibu wake sio wa kupanda mbegu leo kesho uvune ni wastani wa miezi mitatu. Mtu kashapambana kitalubi huko toka mwezi wa nane kaleta mazao shambani na anaendelea kumwagilia leo uje umwambie aache inawezekana kweli?
Wangemuacha amalize tu kilimo chake kisha atulie ndio ustaarabu hup.
 
Back
Top Bottom