Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Unapoanzisha kampuni ya microfinance unapaswa kuzingatia changamoto zote za wateja unaoenda kuwahudumia. Hapa ndipo umuhimu wa dhamana dhidi ya mkopo unahitajika na tathmini ya biashara ya mkopaji ili kubaini uwezo wake wa kulipa. Kama hayo hayawezekani basi biashara ya microfinance huwezi, wekeza hela zako kwenye shughuli zingine. Imagine kama leo hii mabenki yangeanza kitumia njia hii ya Oya ya kudai madeni, je, ingekuaje?
 
Swala la kuweza kulipa linabaki kuwa wajibu wa mkopaji.
Ni wajibu wa Taasisi ya Fedha kufanya Utafiti kitaalamu na kujiridhisha kuwa mwombaji wa mkopo ana capacity kulipa mkopo au la Ili kuepuka kutengeneza bad debts, labda kama huna Elimu na masuala ya Fedha.

Ukiona Taasisi inaibuka kukimbizana kukabana na wakopaji, jua huo ni utakatishaji Fedha.
 
Mabenk hayana msaada kwa mtu wa hali ya chini. Yenyewe yanakopesha watu ambao tayari wanapesa. So usilinganishe kabjsa.
 
Nadhani kwa level ya umaskini wa wengi kifedha..hii mikopo ya vimicrofinance vingi vilivyopo mitaani na vya kwenye APPs BOT wafute tu na waweke sheria hakuna kuanzisha zibaki bank na taasisi nyinyine kubwa kubwa zio hizi za kuuana , kukaushana damu , kuleteana mattress, mana hali ya uhitaji wa vimkopo hivi mitaani ni kubwa sana..bora solution ya shida za watu isipatikane kirahisi rahisi kama ivi mwishowe Majuto pande zote. Yani ningekuwa mimi futa vyote....la wakopeshaji hao wafate taratibu japo najua nao wagumu sababu riba zao pia hazifati uhalisi, ...unajua ukianzisha mikopo wateja utawapata tu kwakuwa shida zimewabana watu , mtu anapokopa anajipa matumaini atalipa..ila mda wiki moja sio rahisi kama huna biashara...na wakati mwingine mtu anakopa sio kwamba alikuwa na shida kubwa sana ila kwasbab mikopo ipo anakopa....something must be done on this hata kama sio huo ushauri..wenye mitaji yao wataokolewa lakin amani mitaani itakuwepo
 
Wafute vyote tuwe unaasaidiana sisi kwa sisi kama zamani.
 
I agree 100%
 
Na ninaamini kuwa kuna sheria nzuri za BOT(kwenye makaratasi) katika kuthibiti hizi microfinances BUT kama kawaida yetu hakuna usimamiaji na uthibiti wake matokeo tasisi hizi zinajichukulia sheria mikononi na kuona kuwa kupiga,kuteka, kutesa hata kuua ni sehemu ya ku enforce debt collection!!
 
Kabisa. Na lengo la kuenforce debit repayment ni sawa lakini sio enforcing iwe ni kucreate other mistakes, kama hivo hao maafisa watakabiliwa na kesi ya mauaji..mwenye kampuni hahusiki atawaruka tu..sababu ile ni kampuni yenyewe utaathirika kwakuwa wateja au wanajamii wengine hawataitaka tena hio kampuni na sio hivyo tu pengine kuna waliokopa wengine mda wa kurejesha bado basi watatumia mwanya huu huu wa mgogolo huu kutorejesha sababu kama kampuni wataingiwa na kupooza fulani
 
Wwe sisi tunaongelea mikopo ya pesa ya kula tu wwe unakuja na mikopo yako ya kujenga maghorofa!!
 
Na ndio lengo la serikali ya CHURA kwa watanganyika. BOT haina meno zidi ya hz kampuni zenye asili ya znz. Na bado mpk muishe watanganyika.Ukijua jina la mmiliki wa kampuni hii na watu wake wa karibu lazima udate tu.
All the best
Duh,
Kwamba kampuni uchwara ya kukopesha ya OYA OYA ni ya kutoka Zanzibar?!
 
Mimi nawataka san hawa OYA ili tuoneshane nani zaid shenz taip yao ! Na mkurugenzi wao pia atiwe ndani manake ndo aliwatuma wapuuzi hawa.Asiachiwe ili iwe fundisho kwa takataka zingine kama hao OYA
 
Hawa OYA inafaa kuwapulizia Opium kwenye vigari vyao.
Nilishuhudia wanamtukana jirani yangu matusi ya nguoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…