Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Waliponyanyua fimbo zao makusudi lilikuwa nini wakati yeye sio mdaiwa? Walidhamiria kudhuru mwili, kusababisha maumivu, bila kujua mtu amatembea na madude gani. Ona sasa.. na kama ndio tabia yao kuumiza wadaiwa wao, waozee tu jela iwe funzo
Lipeni madeni ya watu dawa ya deni ni kulipa
 
450k per week lazm uwe mwehu ni biashara gan inakupa faida hiyo..
Kila nikichanganua nifanye nini niingize 450k per week akili imegonga mwamba,

na u PRO wangu wote na biashara za hapa na pale sijioni ku make hiyo pesa zaidi

ya wao kunifanya MSUKULE wao, RIBA yao hiyo naiweza vizuri tu kwa Mtaji huo wa 4m

kinachonishinda ni hiyo TIMELINE yao ya rejesho la WIKI, nishawambia sana wakitaka

kunikopesha wakubali niwape rejesho kwa MWEZI sio wiki,Hawataki ila kazi ni kunisumbua

kila siku wanipe hela,yani hawa wajinga wanakopesha halafu hawajiamini na hela zao kama zitarudi

ndio mana wameweka rejesho la wiki wiki, Shida mimi sio REJESHO shida ni Hela kuirudsha ndani ya wiki.
 
Binadamu wamekua waovu mno.

Wangekua wanapokea hata kidogo kidogo mpaka deni liishe.

Pesa kitu gani aisee, mbona inazungumzika tu.

Tuwe waungwana jamani tujali na wengine.

Mtu mpaka kakopa ujue ana uhitaji ni kwenda nae taratibu tu.
Acha tu ndugu yangu imenisikitisha sana, hivi uhai wa mtu kwa 300K? Walishindwaje kwenda naye mdogo mdogo, anyway kifo ni kifo tu. (Madam president)
 
Nasema hivi:
Kama umekopa mkopo lipa kwa wakati kama mlivyokubaliana na sio ubabaishaji.
Watu hawataki kulipa madeni ya watu.
Na wanakuwa na ujeuri kabisa, Kwanini?
Lipeni bana Hela za watu kama mlivyokubakubaliana
 
Kukopa bila kulipa ni wizi kwa njia ya ulaghai .
Ni wizi wa kuaminiwa.
Kuna familia nimewaambia sitaenda kuwashitaki kwa kesi ya madai ili wanilipe watakavyo la hasha,
Nitafungua kesi ambayo hawataamini.

Lipeni madeni ya watu.

Fikiria mtu anadaiwa mamilioni na Watu lakini anajenga ghorofa, hiyo si ni dharau aisee!

Hapana haikubaliki.
 
Kuna jamaa yeye Kasema muda wa kwenda kumshitaki mdeni wake ambae ni miaka mingi imepita muda hana wa kwenda kupoteza mahakamani,
Kasema atajua cha kumfanya,
Nikamwambia nipe mbinu,
Kasema Mbinu ziko nyingi za kumkomesha bandidu.
 
Kasema hata kumchomea nyumba anayoishi ili apate hasara itakuwa Sawa ili awe amelipa deni lake kiaina na awe amelipa na riba ya 200% ili wakose wote.

Nikamwambia umefika mbali sana,
Lakini jamaa huenda anamaanisha,
Lipeni madeni ya watu.
 
Ila kuna watu wana mioyo migumu jamani!
Unakopa hulipi na unapata amani ya moyo kabisa?
Ukilala unapata na usingizi kabisa?

Mtu wa hivyo dhamira ilishakufa ndani yake.

Huyo ni Sawa na muuaji/jambazi/mchawi

Mtapata laana na vizazi vyenu

Kulipa deni kwa wakati ni kipimo cha imani.
 
Back
Top Bottom