Qatar ilipata utajiri kutokana na gesi. Kwanini Tanzania ilizuia miradi ya gesi?

Hujui kuwa Tz na Kenya wameingia mkataba wa kuuziana gesi?
 
Mihemko tu ...unafikria investment ya gas ni rahisi kwamba wanafanya package kweny viroba🤔🤔..
Lazima waibadili iwe liquefied gas then ndo isafirishwe na kumpeleka ulaya sio kitoto iko logistics yake gharama ni kubwa labda kuuza majirani zetu.

Huo mradi nafikiria ungekula pesa ndefu kuliko ule wa umeme ..
 
Angalau basi tungeuza nchi jirani kama Kenya
Kama soko lipo pesa ni za wawekezaji sio zetu
 
Unaogopa Nini nawakati unaushaidiiii, wa hicho ulichokibwabwaja.

Njoooo hadharani upongezweee na wananchiiiiiiiii
Sina muda wa kwenda kuitisha mikutano ila misukule nyie hamuwezi lolote, ndio maana hata mwendawazimu yule alitumia jeshi kuzuia mikutano akiogopa spana..!

Lissu alikuja akamtukana sana, misukule mlimfanya nini?
 
Tukiachana na siasa na maneno ya majukwaani, Maamuzi ya mwenyekiti na raisi wa awamu iliyopita ya kuachana na gesi yalipata baraka za chama na watanzania walikubali mbadala uliopendekezwa.

Mafanikio ya hii nchi yanatokana na chama cha mapinduzi, makosa yalikipa chama changamoto mpya na malalamiko yalifanyiwa kazi na chama.

Pamoja na yote, CCM ni chama pekee chenye uwezo wa kupewa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi hii.
 
Ilikuwaje CCM kipindi cha Kikwete ikaona mradi unafaa, kipindi cha Magufuli ikaona mradi haufai, na sasa kipindi cha Samia inaona mradi unafaa?
 
Tupo hapa tulipo sababu ya tulichokuwa tukikifanya tangu uhuru na sio alichokuwa akifanya JPM kwa miaka 5 pekeyake.
Kwa hiyo Magufuli hana kosa? Kuachana na mradi mkubwa kama ule haikuwa kosa?
 
Kwa hiyo Magufuli hana kosa? Kuachana na mradi mkubwa kama ule haikuwa kosa?
Magufuli sio raisi wa kwanza kuachana na mradi. Nchi inaongozwa na sera za chama. Nchi ipo hapa ilipo sababu ya tulichokuwa tukikifanya tangu uhuru. JPM kaendeleza walipoishia wengine. Kama nchi inaruhusu mwenyekiti wa chama tawala kufanya maamuzi kwa niaba ya wote utamlaumuje mwenyekiti kwa kufanya maamuzi? JPM alifanya sehemu yake kwa ufasaha kabisa.
 
Hoja ya kujibu hii mada ndio hii sasa
 
Ilikuwaje CCM kipindi cha Kikwete ikaona mradi unafaa, kipindi cha Magufuli ikaona mradi haufai, na sasa kipindi cha Samia inaona mradi unafaa?
Maamuzi ya uwekezaji upi ufanyike na upi usubiri hutokana na mambo mengi ikiwemo vyanzo vya fedha.

Ukifuatilia bajeti za JMT tangu utambulisho wa gesi mpaka maamuzi ya awamu ya 5 ya kusitisha kwa muda hutaona sababu ya kuuliza swali hili ulilouliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…