QR Code haiwezi kuwa njia ya udhibiti wa jezi feki

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Sijajua kama huu utaratibu uliowekwa wa mzabuni wa jezi za Simba JayRutty kuweka QR Code katika jezi kama ni njia sahihi ya kudhibiti jezi feki.

Ninavyofahamu mimi ukishajua hiyo QR Code inatakiwa kukupeleka kwenye website na ukurasa gani, hata mimi ukinipa dakika 2 naweza kuitengeneza sasa hivi hapa nikiwa geto nimevaa boksa. Wahuni wanaprint katika vikaratasi vidogo wanashona fasta tu.

Uamuzi ambao nimeupenda ni wa kuzisambaza jezi katika ofisi za posta nchi nzima. Huu ni ubunifu mzuri sana ukizingatia changamoto za usambazaji tulizonazo nchini na ukosekanaji wa wasambazaji wenye maduka mengi nchi nzima. Ambacho sina uhakika ni kama huu utakuwa utaratibu endelevu ili mzigo ukiisha katika kituo fulani stock mpya inaletwa bila kuchelewa. Pia sina uhakika kama Posta wana maduka ndani ya ofisi zao au ndiyo ukifika pale unasubirishwa nusu saa wakatafute jezi zilipo maana tunazijua hizi taasisi za serikali na ufanyaji wao wa kazi. Na hapo haujakutana na mfanyakazi wa posta ambaye amerithi ushabiki wa Yanga, utaisoma namba.

Kuhusu tukio la leo, binafsi sijalienjoy. Tukio halikupangwa vizuri na maneno yalikuwa meengi kuliko burudani. Nilitaka nilete uzi niorodheshe mambo ambayo sijayapenda ila naona nikaushe tu, sina mzuka na mamipira yenu haya yaliyojaa siasa na ubabaishaji.
 
Sijajua hasa huu utaratibu uliowekwa wa mzabuni wa jezi za Simba JayRutty kuweka QR Code katika jezi kama njia ya kudhibiti jezi feki.

Ninavyofahamu mimi ukishajua hiyo QR Code inatakiwa kukupeleka kwenye website na ukurasa gani, hata mimi naweza kuitengeneza sasa hivi hapa nikiwa nimevaa boksa halafu nikaprint katika vikaratasi vidogo vikashonewa fasta tu.

Kuhusu tukio la leo, binafsi sijalienjoy. Tukio halikupangwa vizuri na maneno yalikuwa meengi kuliko burudani. Nilitaka nilete uzi niorodheshe mambo ambayo sijayapenda ila naona nikaushe tu.
Mtengemezaji n fake

Semaji fake..timu ..f...
 
Huu ni mfano wa QR Code niliyotengeneza hapa sasa hivi dkk 0 tu. Inakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa Diadora.

1000121374.jpg
 
Sijajua kama huu utaratibu uliowekwa wa mzabuni wa jezi za Simba JayRutty kuweka QR Code katika jezi kama ni njia sahihi ya kudhibiti jezi feki.

Ninavyofahamu mimi ukishajua hiyo QR Code inatakiwa kukupeleka kwenye website na ukurasa gani, hata mimi ukinipa dakika 2 naweza kuitengeneza sasa hivi hapa nikiwa geto nimevaa boksa. Wahuni wanaprint katika vikaratasi vidogo wanashona fasta tu.

Uamuzi ambao nimeupenda ni wa kuzisambaza jezi katika ofisi za posta nchi nzima. Huu ni ubunifu mzuri sana ukizingatia changamoto za usambazaji tulizonazo nchini na ukosekanaji wa wasambazaji wenye maduka mengi nchi nzima. Ambacho sina uhakika ni kama huu utakuwa utaratibu endelevu ili mzigo ukiisha katika kituo fulani stock mpya inaletwa bila kuchelewa. Pia sina uhakika kama Posta wana maduka ndani ya ofisi zao au ndiyo ukifika pale unasubirishwa nusu saa wakatafute jezi zilipo maana tunazijua hizi taasisi za serikali na ufanyaji wao wa kazi. Na hapo haujakutana na mfanyakazi wa posta ambaye amerithi ushabiki wa Yanga, utaisoma namba.

Kuhusu tukio la leo, binafsi sijalienjoy. Tukio halikupangwa vizuri na maneno yalikuwa meengi kuliko burudani. Nilitaka nilete uzi niorodheshe mambo ambayo sijayapenda ila naona nikaushe tu, sina mzuka na mamipira yenu haya yaliyojaa siasa na ubabaishaji.
Issue siyo kujua kutengeneza QR Code. Tatizo lako hujui technology. QR code ipo na taarifa nyingi na ina husika na verification. Tuambie QR Code yako uliyoiweka security yake ni ipi na verification zake ni zipi.

Soma kuhusu QR Code kwanini inatumika kwenye payment systems

Unajiaibisha. Futa uzi wako huu.
 
Unachanganya QR Code na Barcode. Sina uhakika kama kuna unachoweza kunifundisha ambacho sikifahamu. Nimejua kutengeneza hizo QR Code kitambo saaana.

Nimetoa angalizo kwa nia njema tu maana mara kwa mara nimekuwa nasema watanzania wa leo wako mbele ya muda kuliko wanasiasa wanavyowachukulia. Wanunuzi wameambiwa wakiscan ikawapeleka kwenye website ya Diadora basi mchezo umeisha, ndiyo verification pekee wanayotakiwa kuizingatia.

Wewe chukulia mtu kama Mangungu anasema hakuziona jezi hadi jana. Hilo linaingia akilini kweli? Kwanza kwa kauli ile ilimpasa ajiuzulu mara moja.
 
Huu ni mfano wa QR Code niliyotengeneza hapa sasa hivi dkk 0 tu. Inakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa Diadora.

View attachment 3460729
Kuna kitu ukijui swala siyo kukupeleka kwenye site yao swala ni hiyo security trick wanayo tumia ....kama QR code inascaniwa sana wanaweza kuifunga either kwa kuweka limit ya scan mfano mwisho ni kuiscan mara 4 tu hivyo ukicopy moja utazalishia nguo mbili au moja tu feki
 
Hakuna kitu kama hiko. Mwenye control ya QR Code ni yule aliyeitengeneza.

Anyway siyo mwanzo mbaya katika kujenga utamaduni wa kununua jezi rasmi. Nadhani wangesisitiza watu kununua jezi katika vyanzo vya kuaminika lingekuwa na uzito na faida zaidi.

Ushauri wangu (ili muelewe kuwa uzi wangu una nia ya kujenga): Wangeenda mbali zaidi katika hilo suala la QR Code. Mfano, wangeambatanisha QR Code na serial number. Ukiscan, unaambiwa uingize serial number katika mfumo wa kujisajili na kuweka jina lako na namba ya simu. Ukishajisajili unatumiwa risiti. Serial number ikishasajiliwa mara moja haikubali tena. Ili kuwafanya wengi wachukue hatua, wape pia motisha kuwa kila wiki itakuwa inafanyika raffle ya kutoa zawadi mbalimbali kama raba, cash, nk.
 
Sijajua kama huu utaratibu uliowekwa wa mzabuni wa jezi za Simba JayRutty kuweka QR Code katika jezi kama ni njia sahihi ya kudhibiti jezi feki.

Ninavyofahamu mimi ukishajua hiyo QR Code inatakiwa kukupeleka kwenye website na ukurasa gani, hata mimi ukinipa dakika 2 naweza kuitengeneza sasa hivi hapa nikiwa geto nimevaa boksa. Wahuni wanaprint katika vikaratasi vidogo wanashona fasta tu.

Uamuzi ambao nimeupenda ni wa kuzisambaza jezi katika ofisi za posta nchi nzima. Huu ni ubunifu mzuri sana ukizingatia changamoto za usambazaji tulizonazo nchini na ukosekanaji wa wasambazaji wenye maduka mengi nchi nzima. Ambacho sina uhakika ni kama huu utakuwa utaratibu endelevu ili mzigo ukiisha katika kituo fulani stock mpya inaletwa bila kuchelewa. Pia sina uhakika kama Posta wana maduka ndani ya ofisi zao au ndiyo ukifika pale unasubirishwa nusu saa wakatafute jezi zilipo maana tunazijua hizi taasisi za serikali na ufanyaji wao wa kazi. Na hapo haujakutana na mfanyakazi wa posta ambaye amerithi ushabiki wa Yanga, utaisoma namba.

Kuhusu tukio la leo, binafsi sijalienjoy. Tukio halikupangwa vizuri na maneno yalikuwa meengi kuliko burudani. Nilitaka nilete uzi niorodheshe mambo ambayo sijayapenda ila naona nikaushe tu, sina mzuka na mamipira yenu haya yaliyojaa siasa na ubabaishaji.
Nimenunua jezi feki tena kwa anae tembeza barabarani sina smart phone ya ku scan halafu unikamate kwa jezi feki
 
Hakuna kitu kama hiko. Mwenye control ya QR Code ni yule aliyeitengeneza
Labda utengeneze na tovuti bandia inayo fanana na ya kampuni halisi vinginevyo ni ngumu kufanya unacho sema ...kuwa QR ielekee kwenye kampuni halisi na wao wasiweze kutambua kuwa hiyo QR CODE ina scaniwa mara kwa mara
 
Nimenunua jezi feki tena kwa anae tembeza barabarani sina smart phone ya ku scan halafu unikamate kwa jezi feki
Kama mshabiki ni wajibu wako kuhakikisha unanunua jezi halali. Kwa nini ununue jezi barabarani wakati umepewa vyanzo vya kuaminika vya kuipata jezi?
 
Where there are many people you can not stop stealing but you can control

Kwenye watu wengi huwezi kukomesha wizi bali unaweza kudhibiti

Wezi kumbe pia huwa wanaiba vitu ambavyo havihitajiki
 
Labda utengeneze na tovuti bandia inayo fanana na ya kampuni halisi vinginevyo ni ngumu kufanya unacho sema ...kuwa QR ielekee kwenye kampuni halisi na wao wasiweze kutambua kuwa hiyo QR CODE ina scaniwa mara kwa mara
Mambo hayaendi hivyo. Unajua jinsi websites zinavyofanya kazi? Maana ulichokisema kinatutoa kwenye QR Code kinatupeleka kwenye jinsi websites zinavyofanya kazi.
 
Ili kufanya hicho unacho sema ni lazima uunde kurasa feki yenye kufanana na kurasa halisi ya kampuni husika ya bidhaa unayo taka kuitengenezea QR CODE feki
 
Unachanganya QR Code na Barcode. Sina uhakika kama kuna unachoweza kunifundisha ambacho sikifahamu. Nimejua kutengeneza hizo QR Code kitambo saaana.

Nimetoa angalizo kwa nia njema tu maana mara kwa mara nimekuwa nasema watanzania wa leo wako mbele ya muda kuliko wanasiasa wanavyowachukulia. Wanunuzi wameambiwa wakiscan ikawapeleka kwenye website ya Diadora basi mchezo umeisha, ndiyo verification pekee wanayotakiwa kuizingatia.

Wewe chukulia mtu kama Mangungu anasema hakuziona jezi hadi jana. Hilo linaingia akilini kweli? Kwanza kwa kauli ile ilimpasa ajiuzulu mara moja.
Qr code ni bora zaidi ya bar codes. Qr code zinabeba taarifa nyingi zaidi in 3D kitu ambacho barcode haiwezi kufanya.
Kutengeza ni rahisi kwa sababu zipo app kibao tu za kuzigenerate.
Kuhusu kuzuia jezi fake naunga mkono kuwa haziwezi unless kila jezi iwe na msimbo maalum uliounganishwa na na database mtu akiscan iweze kucompare na kurudisha taarifa kwama ni OG au fake kitu ambacho najua ni gharama na sioni wakifanya.
Vitu vingine huwa ni mbwembwe tu za kunogesha mambo kama ilivyokuwa kwa nape na roboti lake
 
Back
Top Bottom