QR Code haiwezi kuwa njia ya udhibiti wa jezi feki

Siyo wazo baya ila unaona vurugu za wiki mbili za kwanza jezi zinapotoka? Hawa wanunuzi uwaambie wapange mstari walipe online, ufanye uhakiki ndiyo umpe jezi? Hata haya mambo ya serial number tunayoongelea bado siyo rafiki sana katika uhalisia wetu.
Kwa hiyo hakuna mbinu ya kuhudumia wateja wengi kwa kufanya uhakiki ? Yaani mbinu ni nyingi tu maweza kununua jezi kwenye simu kisha nikapata code hiyo code nikaitumia dukani kuchukua jezi yangu
 
Mimi nitafanyaje sasa kama wewe umeamua kuacha kuongelea vitu kwa uhalisia ukaenda kuongelea vitu "technically"?

Nilichofanya ni kukuunga mkono kuwa technically inawezekana kuweka QR Code tofauti kwa kila jezi. Nimefanya tu kukazia kwa mifano zaidi ambayo technically inawezekana.
Sio ngumu kama unavyojaribu kuiweka... hata chupa za soda kila moja imeandikwa tarehe tofauti ya production, na inaweza ikawa tracked, itakuwa tshirt za mashabiki wa simba! QR code generation ni science nyepesi, na kuwa na mashine ya print label ndogo za QR sio issue.
 
Si kweli kwamba kila chupa ya soda ina tarehe tofauti na pia unapotaka na kusisitiza QR Code tofauti kwa kila jezi unakuwa haujaelewa hiyo QR Code inafanya nini hasa.

Nimeeleza sana hapo juu QR Code hii ya kwenye jezi inachofanya ni kukusaidia tu kirahisi kukupeleka katika website husika. Wangeweza kuweka kikaratasi kimeandiwa "Tembelea tovuti yetu ya www.diadora.com" ikawa haina tofauti. QR Code inakurahisishia wewe kuingia huko bila kutype au kukariri jina la hiyo website.

Sasa ukitengenezea QR Code 200,000 tofauti na zote zinakupeleka katika website hiyo hiyo kuna faida gani na inasaidia nini hasa?

Kama umefikia unachanganya expiration date na QR Code, naona kama namuelewesha mtu asiyetaka kuelewa.
 
Si kweli kwamba kila chupa ya soda ina tarehe tofauti na pia unapotaka na kusisitiza QR Code tofauti kwa kila jezi unakuwa haujaelewa hiyo QR Code inafanya nini hasa.

Nimeeleza sana hapo juu QR Code hii ya kwenye jezi inachofanya ni kukusaidia tu kirahisi kukupeleka katika website husika. Wangeweza kuweka kikaratasi kimeandiwa "Tembelea tovuti yetu ya www.diadora.com" ikawa haina tofauti. QR Code inakurahisishia wewe kuingia huko bila kutype au kukariri jina la hiyo website.

Sasa ukitengenezea QR Code 200,000 tofauti na zote zinakupeleka katika website hiyo hiyo kuna faida gani na inasaidia nini hasa? Naona kama namuelewesha mtu asiyetaka kuelewa.
Kwa mfano wa chupa... mashine ya kuchapa inaweza kuchapa tarehe tofauti

QR code sio lazima ziwe na taarifa sawa. You can encode any information. Kama umewahi kutumia QR code za parking ticket za Mlimani City utajua kuwa kila ticket in QR code ambayo ipo encoded na namba ya gari, pamoja na kwamba zinatoka mashine moja.

Kama imewezekana kwa namba za magari, inashindikana vipi kwa tshirt kuwa na QR code ambayo ina serial number ya tshirt?
 
Unaposema kila chupa ina tarehe tofauti ina maana chupa zinazozalishwa siku moja zina tarehe tofauti au kila chupa imewekwa sekunde iliyozalishwa ili kuitofautisha na nyingine?

Hizo nyogeza za serial numbers na mimi nimeshauri huko juu kama njia ya kweli ya kuzuia jezi zisizo rasmi badala tu ya kuweka QR Code ya kukupeleka katika website husika. Kwa hiyo kama umefika katika mtazamo huo nadhani kimsingi unakubaliana na nilichosema.
 
That was my point, kutengeneza unique QR sio kitu kigumu. Wawekeze hapo, kama Parking systems wanaweza kutengeneza unique QR, wao wanashindwaje? Logistics zake sio ngumu, ni kukosa uelewa. China hakuna mashine unaweza kutaka ukakosa, kama haipo watakutengenezea
 
Unarudi kule kule niliposema pia kuwa hatuna mifumo ya usambazaji wa jezi iliyo rafiki kwa malengo hayo. Hizo mashine utasizambaza wapi na nani atafanya kazi hiyo? Utazigawa bure hadi katika maduka ya jezi ya vichochoroni au utawaambia wazilipie? Kila timu itatoa mashine yake ya kuscan jezi zake?

Nashangaa wanaosema eti Nike au Adidas hawaji kisa hatuna mashabiki wa kulipia hizo jezi halafu wanatolea mifano ya Mamelodi Sundowns ambao hawafikii mashabiki wa Yanga na Simba, si kwa idadi wala kwa levo ya ushabiki.

Shida yetu kubwa ni mifumo ya kisasa ya usambazaji kuanzia maduka yanayotambulika, websites na mifumo ya usafirishaji ya uhakika kiasi kwamba unapoleta hizo QR Code, Barcodes, mashine, nk. ni rahisi kutumika kwa malengo kusudiwa.
 
Serialization inafanyika kwa mtengenezaji... sio kwa wasambazaji. Ila unawapa elimu wanunuaji, namna ya kutambua jezi feki kwa kutumia simu na QR.
 
Back
Top Bottom