QR Code haiwezi kuwa njia ya udhibiti wa jezi feki

Kudhibiti jezi feki kwa kutumia QR code inawezekana tu kama kila jezi itakuwa na namba ya tofauti, na mtu aki-scan aweze kufanya usajili i.e Jezi namba 10 inasajiliwa na Shabiki namba 5. Mtu mwingine aki-copy hiyo QR code, na akajaribu kufanya usajili, itamwambia hiyo code tayari imetumika, usininunue.
 
Umeshafanya utafiti ukajua ni asilimia ngapi ya hiyo 200K inaenda kwa mzabuni na asilimia ngapi inaenda kwa klabu?

Mbona serikali inanunua maelfu ya magari ya bei ya juu kila mwaka kama sisi ni maskini? Unataka kuniambia SGR imejengwa kwa kiwango duni kutokana na umaskini wetu? Unataka kusema zile ndege mpya za ATCL zilizoletwa katika kipindi hiki cha miaka 10 iliyopita ni za kiwango cha chini kutokana na umaskini wetu?

Ukienda katika maduka ya huko Ujerumani au Uingereza ukanunua shati au fulana ya $20 je litakuwa la kiwango hafifu?
Serikali yako inanunua magari Europe au Asia? Sasa hapa unaizungumzia serikali au wananchi maana umezungumzia SGR,ATCL ina maana hiyo miradi ndio inanunua jezi? On average based on stastics kipato cha mtanzania wa kawaida ni kiasi gani, ukishajua then fanya projections kujua wananchi wangapi wana uwezo wa kununua jezi ya 200k? Mnapenda sana kujidanganya.

Sasa kwani huko ulaya hamna fake? Unaweza pata shati 20usd ila quality yake haifanani na 100Usd.Halafu ulaya hawapangiania eti club inachukua kiasi gani baada ya kuuza jezi moja, mfano Arsenal mkataba wake na Adidas, analipwa 60m pounds kwa mwaka, so hanaga time ya kukatana baada ya kuuza jezi ,labda huku kwetu.
 
Nashindwa kujadiliana na wewe maana kwa maelezo yako haya ni wazi kuwa unaangalia mambo juu juu sana na umegoma kuumiza kichwa chako kuangalia ishu unayoiongelea kwa undani. Vitu unavyobisha tayari nimeshaviongelea na kuvijibu hapo juu ila kwa kuwa unaleta ubishi umeshindwa hata kuviona. Tuishie hapo.
 
Unachanganya QR Code na Barcode. Sina uhakika kama kuna unachoweza kunifundisha ambacho sikifahamu. Nimejua kutengeneza hizo QR Code kitambo saaana.

Nimetoa angalizo kwa nia njema tu maana mara kwa mara nimekuwa nasema watanzania wa leo wako mbele ya muda kuliko wanasiasa wanavyowachukulia. Wanunuzi wameambiwa wakiscan ikawapeleka kwenye website ya Diadora basi mchezo umeisha, ndiyo verification pekee wanayotakiwa kuizingatia.

Wewe chukulia mtu kama Mangungu anasema hakuziona jezi hadi jana. Hilo linaingia akilini kweli? Kwanza kwa kauli ile ilimpasa ajiuzulu mara moja.
Naomba nikusahihishe QR code ni aina ya barcode barcode mpaka sasa tuna aina mbili ambazo ni QR (quick response) code barcode na linear barcode ndo nilivyofundishwa na mwalimu wangu wa security
 
Achana na theory za darasani, hapa tunaongelea vitu practical vilivyotumika katika uhalisia
 
Nashindwa kujadiliana na wewe maana kwa maelezo yako haya ni wazi kuwa unaangalia mambo juu juu sana na umegoma kuumiza kichwa chako kuangalia ishu unayoiongelea kwa undani. Vitu unavyobisha tayari nimeshaviongelea na kuvijibu hapo juu ila kwa kuwa unaleta ubishi umeshindwa hata kuviona. Tuishie hapo.
Yaani unazunguka miradi ya serikali badala ya kipato cha mtanzania mmoja mmoja.Fanya projection then itakupa reality, hata hao Nike ,Puma,Adidas wanafanya projection kwa kuangalia kipato cha mtu mmoja mmoja, then baada ya hapo wanaweza kukadilia kwa bei yao watauza Jersey ngapi.Siku hizi kuna midata sayansi (computerized), data zipo kibao wakiproject wanajua hapa tunaenda kupoteza mda hapa au tunaenda kutengeneza hela.
 
Kudhibiti jezi feki kwa kutumia QR code inawezekana tu kama kila jezi itakuwa na namba ya tofauti, na mtu aki-scan aweze kufanya usajili i.e Jezi namba 10 inasajiliwa na Shabiki namba 5. Mtu mwingine aki-copy hiyo QR code, na akajaribu kufanya usajili, itamwambia hiyo code tayari imetumika, usininunue.
QR Code siyo namba bali ni mfumo unaokuwezesha kufikia mfumo mwingine au kupata taarifa fulani. Kuna post hapo juu nimesema jezi zingekuwa na serial number halafu kutumia hiyo QR Code kuingia katika mfumo wa kusajili serial number yako.

Hakuna kampuni duniani itakayokaa itengeneze QR Code tofauti kwa kila jezi. Hiko kitu hakiwezekani maana kama lengo ni kudhibiti uharamia njia hiyo haiwezi kuwa na faida yoyote zaidi ya kujichosha tu.
 
Yaani unazunguka miradi ya serikali badala ya kipato cha mtanzania mmoja mmoja.Fanya projection then itakupa reality, hata hao Nike ,Puma,Adidas wanafanya projection kwa kuangalia kipato cha mtu mmoja mmoja, then baada ya hapo wanaweza kukadilia kwa bei yao watauza Jersey ngapi.Siku hizi kuna midata sayansi (computerized), data zipo kibao wakiproject wanajua hapa tunaenda kupoteza mda hapa au tunaenda kutengeneza hela.
Kweli mkuu ndiyo Maana kampuni zote kubwa zipo Nchi za Kiarabu mfano Morocco, Egypt, Tunisia, Ndiyo maana timu zao zinakua na jezi nzuri na ata ukiangalia Mashabiki wao wakiwa Uwanjani unaona kabisa ni Wananchi wenye Maisha mazuri, mkuu ukitaka kujua nchi yenye wananchi wenye kipato kizuri wewe angalia mashabiki wanaoingia uwanjani utapata kipimo kizuri, yani angalia mashabiki wa Tanzania wanaoingia kutazama mechi ya Taifa stars au Mechi za Simba na Yanga utaona nitofauti kimuonekano na mashabiki wa nchi za Algeria, Tunisia na Egypt wananchi wa nchi hizi wamependaza na wanaonekana siyo walala Hoi. Ata baadhi ya nchi mfano Angola, Namibia South Africa kidogo na wao wananchi wao siyo choka mbaya kama sisi.
 
Basi ni usanihi tu
Hakuna kampuni duniani itakayokaa itengeneze QR Code tofauti kwa kila jezi. Hiko kitu hakiwezekani maana kama lengo ni kudhibiti uharamia njia hiyo haiwezi kuwa na faida yoyote zaidi ya kujichosha tu.

Dawa ni ama kuuza na kununua jezi katika maduka maalum yanayotambulika na si pengine pamoja na/au kuwa na serial number kwa kila jezi ambapo mtu anaweza kuscan QR Code na kuisajili jezi yake wakati anainunua.
 
Dawa ni timu kuwa na control number ya mawakala wa kuhuza jezi mteja analipa online kwa kutumia control number ya wakala kisha wakala nanalipwa na timu
 
Siyo wazo baya ila unaona vurugu za wiki mbili za kwanza jezi zinapotoka? Hawa wanunuzi uwaambie wapange mstari walipe online, ufanye uhakiki ndiyo umpe jezi? Hata haya mambo ya serial number tunayoongelea bado siyo rafiki sana katika uhalisia wetu.
 
Sijajua kama huu utaratibu uliowekwa wa mzabuni wa jezi za Simba JayRutty kuweka QR Code katika jezi kama ni njia sahihi ya kudhibiti jezi feki.
1756898939755.png

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Dkt.Suleiman Jafo(Mb) ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) @tbs_viwango na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) @brela_tanzania kuhakikisha bidhaa zote nchini zinasajiliwa kwa kutumia barcode ili kuziwezesha kupata soko la ndani na nje ya nchi.

Amebainisha hayo wakati wa utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya taasisi za Serikali zilizochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara TBS, BRELA pamoja na GS1 Tanzania Mei 20, 2025 jijini Dar es Salaam.

Aidha Dkt. Jafo amesema kuna umuhimu wa usajili wa barcode kwa bidhaa zote zinazozalishwa hapa nchini kwani kutaiwezesha serikali na wizara kufuatilia mapato ya uzalishaji wa taifa na kukusanya takwimu za uhakika za bidhaa zote zinazozalishwa Tanzania na kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi za kupanga na kukuza uchumi.

Dkt. Jafo pia ameeleza kuwa ushirikiano huo utaleta ushirikiano bora kati ya taasisi, hatimaye kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania na kuongeza ushindani wa kimataifa wa bidhaa zinazotengenezwa na Tanzania.

Vilevile ameongeza kuwa Serikali ina matumaini kwamba mpango huo mpya wa barcode utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kupata soko la bidhaa zao kimataifa zaidi.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatuma Kange amesema ushirikiano huo utaimarisha mchakato wa usajili wa biashara ndogo na za kati (SMEs) kabla ya kubadilika na kuwa viwanda vikubwa na utaziwezesha taasisi kama BRELA na TBS kukusanya takwimu muhimu za wateja, zikiwemo kutoka kwa wafanyabiashara ambao bado hawajatekeleza misimbo hiyo na kuongeza mwonekano wa biashara kupitia chapa, na kwa wale waliosajiliwa na BRELA, watapata fursa ya kupata chapa ya bidhaa, alama za biashara na vyeti ambavyo ni muhimu kwa kutambulika sokoni,

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amesisitiza kuwa Makubaliano hayo yataleta manufaa makubwa katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuongeza elimu ya biashara kwa wajasiriamali, kuendeleza tafiti za haki miliki na kupanua wigo wa soko la bidhaa zinazozalishwa nchini.
 
View attachment 3463823

Nadhani ndiyo nilichosema. Jezi ziwe pia na barcode au serial number badala ya QR Code ya kukupeleka tu kwenye website ya mzabuni bila kuambiwa ufanye jambo lingine lolote la kuthibitisha uhalali wa bidhaa hiyo.

Kusajili barcode ni jambo moja ila iwe na mantiki iliyokusudiwa inabidi kila copy ya hiyo bidhaa inapoingia sokoni iwe na hiyo barcode iliyosajiliwa.

Swali linakuja, wauzaji wangapi wa hizi jezi nchini wana mifumo ya kuscan barcode? Ndiyo maana nimesifia wazo la kutumia duka la Posta maana hawa wana uwezo wa kuweka mfumo rasmi wa kuscan barcode na kumuwezesha mzabuni kusoma mauzo ya jezi na kudhibiti jezi zisizo rasmi.
 
QR Code siyo namba bali ni mfumo unaokuwezesha kufikia mfumo mwingine au kupata taarifa fulani. Kuna post hapo juu nimesema jezi zingekuwa na serial number halafu kutumia hiyo QR Code kuingia katika mfumo wa kusajili serial number yako.

Hakuna kampuni duniani itakayokaa itengeneze QR Code tofauti kwa kila jezi. Hiko kitu hakiwezekani maana kama lengo ni kudhibiti uharamia njia hiyo haiwezi kuwa na faida yoyote zaidi ya kujichosha tu.
Serial number registration ndio point yangu, ili mtu aweze kuhakiki serial number. As for uwezekano wa kutengeneza unique code for each product sio issue kabisa.
 
Sawasawa, tuishi humo kwenye serial number. Hauwezi kutengeneza QR Code tofauti kwa jezi 200,000. Ni sawa uwaambie watengeneze kila jezi iwe tofauti. Muda na rasilimali za kufanya hivyo haupo na hakuna faida yoyote kama lengo ni kuthibiti uharamia. Kumbuka ili mtengeneza bidhaa apate faida lazima bidhaa iwe mass produced.
 
Hakuna kitu kama hiko. Mwenye control ya QR Code ni yule aliyeitengeneza.

Anyway siyo mwanzo mbaya katika kujenga utamaduni wa kununua jezi rasmi. Nadhani wangesisitiza watu kununua jezi katika vyanzo vya kuaminika lingekuwa na uzito na faida zaidi.

Ushauri wangu (ili muelewe kuwa uzi wangu una nia ya kujenga): Wangeenda mbali zaidi katika hilo suala la QR Code. Mfano, wangeambatanisha QR Code na serial number. Ukiscan, unaambiwa uingize serial number katika mfumo wa kujisajili na kuweka jina lako na namba ya simu. Ukishajisajili unatumiwa risiti. Serial number ikishasajiliwa mara moja haikubali tena. Ili kuwafanya wengi wachukue hatua, wape pia motisha kuwa kila wiki itakuwa inafanyika raffle ya kutoa zawadi mbalimbali kama raba, cash, nk.
Mkuu Simba wameshawekewa hela ya jezi hawana hasara tena,kazi ni kwa Jayrutty.
 
Sawasawa, tuishi humo kwenye serial number. Hauwezi kutengeneza QR Code tofauti kwa jezi 200,000. Ni sawa uwaambie watengeneze kila jezi iwe tofauti. Muda na rasilimali za kufanya hivyo haupo na hakuna faida yoyote kama lengo ni kuthibiti uharamia. Kumbuka ili mtengeneza bidhaa apate faida lazima bidhaa iwe mass produced.
Technically inawezakana, swali ni uwekezaji utalipa?
 
Technically inawezekana pia kutengeneza kila jezi iwe tofauti unavyotaka wewe mshabiki tena wakuprintie kabisa jina lako huko huko Italia.
Naona umeamua kubishana for the sake of kubishana.
 
Mimi nitafanyaje sasa kama wewe umeamua kuacha kuongelea vitu kwa uhalisia ukaenda kuongelea vitu "technically"?

Nilichofanya ni kukuunga mkono kuwa technically inawezekana kuweka QR Code tofauti kwa kila jezi. Nimefanya tu kukazia kwa mifano zaidi ambayo technically inawezekana.
 
Back
Top Bottom