LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,122
- 9,209
- Thread starter
- #61
SEHEM YA 9
iku ilikuwa ndefu sana na ilipotimu
saa mbili za usiku Monica akawasili
nyumbani kwa wazazi wake ambako
alikaribishwa kwa furaha kubwa .Kwa
pamoja walipata chakula cha usiku na
Monica akafahamishwa kuhusiana na
sherehe itakayoandaliwa pale pale
nyumbani kwao siku inayofuata kwa ajili
ya kumpongeza kwa mafanikio yake na
kubwa zaidi ni kwa yeye kutajwa kuwa
ndiye mwanamke mrembo zaidi barani
afrika.Baada
ya
mazungumo
yaliyowapeleka hadi saa tano za usiku
Monica akaaga na kutaka kuondoka lakini
wakati akielekea katika gari lake mama
yake akaomba waongozane ana jambo
anataka waongee.
“ Jambo gani mama? Akauliza Monica
wakati wakieleka katika gari.
“ Monica kuna jambo moja ambalo
nimekuwa nataka kuzungumza nawe kwa
muda mrefu kidogo lakini kwa kuwa
nafasi inakuwa finyu sana nimeona
niongee nawe sasa hivi.Ni kuhusu Yule
kijana rafiki yako Daniel mtoto wa mzee
Swai”
“ Ndiyo mama nakusikiliza” akasema
Monica
“ Nafahamu kuwa tumekuwa na
ukaribu mkubwa na familia yao,wewe na
yeye mmekuwa marafiki toka mkiwa
wadogo lakini kwa siku za karibuni
nimegundua ukaribu wenu umeongezeka
sana.Hilo ni jambo jema lakini ilinilazimu
kumfanyia uchunguzi ili kumfahamu ni
kijana wa aina gani,kuzifahamu tabia zake
yote hii ni ili kujua kama anaweza
akakufaa kama ukiamua kuingia naye
katika mahusiano .Utanisamehe kwa
kufanya hivyo bila kukutaarifu lakini ni
kwa ajili ya ya faida yako.”
“ Usijali mama hilo ni jambo jema na
zuri kwani si rahisi kumfahamu vizuri kila
mtu anayenizunguka” akasema Monica
“
Ahsante
Monica.Nilifanya
uchunguzi wangu na nikagundua kwamba
kijana Yule ni mchafu sana wa tabia.Ana
wanawake karibu kila kona ya
jiji.Anautumia utajiri alionao kwa ajili ya
kuwarubuni wanawake na kuwatumia
kimapenzi kisha huwaacha .Ni tabia
mbaya sana aliyonayo na ndiyo maana
nikataka nikuonye mapema ili ujihadhari
naye.Kaa naye mbali hafai kabisa yule
kijana .Jihadhari asije akakurubuni
ukaingia katika mtego wake.Ninafahamu
kuna kitu anakitafuta kwako kwa hiyo kaa
naye mbali kabisa” akasema Bi Janet.
“ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo
lakini hata mimi ninamfahamu vizuri
Daniel na nimekwisha chukua tahadhari
kubwa kuhusu yeye.Ninazifahamu tabia
zake ni chafu na ninakuhakikishia
kwamba hapa kwangu amekutana na
mwamba na hataweza kuleta uchafu wake
kwangu.” Akasema Monica
“ Ninashukuru kusikia hivyo
Monica.Chukua tahadhari kubwa na hasa
kwa sasa ambapo jina lako linavuma kila
kona ya dunia,watakuja wanaume wengi
watakaovutwa na umaarufu wako.
Jihadhari nao sana.”
“ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo
lakini unanifahamu vizuri msimamo
wangu hakuna yeyote atakayekuja kwa
tamaa zake atakayefanikiwa.” Akasema
Monica na wote wakacheka
“ Lakini Monica kuna jambo lingine
nataka nikuulize”
“ Uliza mama”
“ Ni muda mrefu sasa tumekuwa
tunasubiri taarifa toka kwako lakini
mpaka leo hii kimya”
“ Taarifa gani mama? Akauliza
Monica huku akicheka
“ Kuhusiana na mchumba.Mbona
hutuelezi chochote? Bado hujampata?
Akauliza Bi Janet na wote wakacheka
“ Mama suala hili linahitaji umakini
mkubwa sana katika kufanya uchaguzi
kwani siku hizi watu wamekuwa walaghai
mno na mapenzi ya kweli ni nadra sana
kupata kwa hiyo ninajitahidi kupata muda
wa kutosha kufanya uchaguzi na
uchunguzi wa kutosha kujiridhisha na
yule nitakayekuwa nimemchagua.Sitaki
niumizwe mama na ndiyo maana
nimekuwa makini sana katika
hilo.Endeleeni kusubiri kidogo na pindi
nikiwa tayari wewe utakuwa wa kwanza
kufahamu.” Akasema Monica
“ Nashukuru sana kusikia hivyo
Monica.Basi mimi nakutakia kila la heri na
ufanikiwe kumpata mwanaume bora na si
bora mwanaume.”
“ Ahsante mama nakuahidi
nitakuletea mwanaume ambaye wewe
mwenyewe utamkubali na utampenda pia”
akasema Monica akaagana na mama yake
iku ilikuwa ndefu sana na ilipotimu
saa mbili za usiku Monica akawasili
nyumbani kwa wazazi wake ambako
alikaribishwa kwa furaha kubwa .Kwa
pamoja walipata chakula cha usiku na
Monica akafahamishwa kuhusiana na
sherehe itakayoandaliwa pale pale
nyumbani kwao siku inayofuata kwa ajili
ya kumpongeza kwa mafanikio yake na
kubwa zaidi ni kwa yeye kutajwa kuwa
ndiye mwanamke mrembo zaidi barani
afrika.Baada
ya
mazungumo
yaliyowapeleka hadi saa tano za usiku
Monica akaaga na kutaka kuondoka lakini
wakati akielekea katika gari lake mama
yake akaomba waongozane ana jambo
anataka waongee.
“ Jambo gani mama? Akauliza Monica
wakati wakieleka katika gari.
“ Monica kuna jambo moja ambalo
nimekuwa nataka kuzungumza nawe kwa
muda mrefu kidogo lakini kwa kuwa
nafasi inakuwa finyu sana nimeona
niongee nawe sasa hivi.Ni kuhusu Yule
kijana rafiki yako Daniel mtoto wa mzee
Swai”
“ Ndiyo mama nakusikiliza” akasema
Monica
“ Nafahamu kuwa tumekuwa na
ukaribu mkubwa na familia yao,wewe na
yeye mmekuwa marafiki toka mkiwa
wadogo lakini kwa siku za karibuni
nimegundua ukaribu wenu umeongezeka
sana.Hilo ni jambo jema lakini ilinilazimu
kumfanyia uchunguzi ili kumfahamu ni
kijana wa aina gani,kuzifahamu tabia zake
yote hii ni ili kujua kama anaweza
akakufaa kama ukiamua kuingia naye
katika mahusiano .Utanisamehe kwa
kufanya hivyo bila kukutaarifu lakini ni
kwa ajili ya ya faida yako.”
“ Usijali mama hilo ni jambo jema na
zuri kwani si rahisi kumfahamu vizuri kila
mtu anayenizunguka” akasema Monica
“
Ahsante
Monica.Nilifanya
uchunguzi wangu na nikagundua kwamba
kijana Yule ni mchafu sana wa tabia.Ana
wanawake karibu kila kona ya
jiji.Anautumia utajiri alionao kwa ajili ya
kuwarubuni wanawake na kuwatumia
kimapenzi kisha huwaacha .Ni tabia
mbaya sana aliyonayo na ndiyo maana
nikataka nikuonye mapema ili ujihadhari
naye.Kaa naye mbali hafai kabisa yule
kijana .Jihadhari asije akakurubuni
ukaingia katika mtego wake.Ninafahamu
kuna kitu anakitafuta kwako kwa hiyo kaa
naye mbali kabisa” akasema Bi Janet.
“ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo
lakini hata mimi ninamfahamu vizuri
Daniel na nimekwisha chukua tahadhari
kubwa kuhusu yeye.Ninazifahamu tabia
zake ni chafu na ninakuhakikishia
kwamba hapa kwangu amekutana na
mwamba na hataweza kuleta uchafu wake
kwangu.” Akasema Monica
“ Ninashukuru kusikia hivyo
Monica.Chukua tahadhari kubwa na hasa
kwa sasa ambapo jina lako linavuma kila
kona ya dunia,watakuja wanaume wengi
watakaovutwa na umaarufu wako.
Jihadhari nao sana.”
“ Ahsante mama kwa tahadhari hiyo
lakini unanifahamu vizuri msimamo
wangu hakuna yeyote atakayekuja kwa
tamaa zake atakayefanikiwa.” Akasema
Monica na wote wakacheka
“ Lakini Monica kuna jambo lingine
nataka nikuulize”
“ Uliza mama”
“ Ni muda mrefu sasa tumekuwa
tunasubiri taarifa toka kwako lakini
mpaka leo hii kimya”
“ Taarifa gani mama? Akauliza
Monica huku akicheka
“ Kuhusiana na mchumba.Mbona
hutuelezi chochote? Bado hujampata?
Akauliza Bi Janet na wote wakacheka
“ Mama suala hili linahitaji umakini
mkubwa sana katika kufanya uchaguzi
kwani siku hizi watu wamekuwa walaghai
mno na mapenzi ya kweli ni nadra sana
kupata kwa hiyo ninajitahidi kupata muda
wa kutosha kufanya uchaguzi na
uchunguzi wa kutosha kujiridhisha na
yule nitakayekuwa nimemchagua.Sitaki
niumizwe mama na ndiyo maana
nimekuwa makini sana katika
hilo.Endeleeni kusubiri kidogo na pindi
nikiwa tayari wewe utakuwa wa kwanza
kufahamu.” Akasema Monica
“ Nashukuru sana kusikia hivyo
Monica.Basi mimi nakutakia kila la heri na
ufanikiwe kumpata mwanaume bora na si
bora mwanaume.”
“ Ahsante mama nakuahidi
nitakuletea mwanaume ambaye wewe
mwenyewe utamkubali na utampenda pia”
akasema Monica akaagana na mama yake