QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 26


Saa saba na dakika kumi na tisa
Monica aliwasili Jasmina Restaurant
walikopanga wakutane na Dr Marcelo kwa
ajili ya chakula cha mchana.Kitendo
alichokifanya Daniel kumfuata Marcelo na
kumtolea vitisho kilimuudhi sana Monica
na hivyo akampigia simu Dr Marcelo
akamuomba wakutane mchana ili waweze
kuongea kilichotokea.
Monica alishuka katika gari
akaangaza angaza na mara akamuona Dr
Marcelo
akimpungia
mkono
akamfuata.Walikaa sehemu tulivu huku
wakifurahia
mandhari
nzuri
ya
bahari.Muhudumu akafika na kuwasikiliza
wakaagiza chakula na wakati wakisubiri
chakula wakaendelea na maongezi
mengine
“ Dr Marcelo japokuwa sote tuna
shughuli nyingi za kufanya lakini nimeona
ni vyema kama tukakutana mchana huu ili
tuongelee kilichotokea asubuhi.” Akasema
Monica
“ I’m so sorry Monic..” akasema Dr
Marcelo lakini kabla hajamaliza Monica
akamzuia
“ Dr Marcelo mimi ndiye
ninayepaswa kukuomba samahani kwa
kilichotokea.Mimi ndiye chanzo cha haya
yote.I’m
so
sorry
Dr
Marcelo
nimekusababishia matatizo na rafiki yako
mkubwa” akasema Monica
“ Usijali Monica.Mimi na Daniel ni
marafiki wa siku nyingi .Hii ni mara yetu
ya kwanza kukorofishana lakini nina
uhakika tutaelewana tu.” Akasema Daniel
“ Baada ya kutoka kwako Daniel
alinipigia simu na kuniomba msamaha
lakini nikamwambia kwamba aje kwanza
akuombe msamaha ndipo arudi kwangu
kuniomba msamaha,alikuja tena kwako ?
akauliza Monica
“ Hapana hakurudi.Ninamfahamu
Daniel ni kijana mwenye kiburi sana hasa
kutokana na utajiri alionao na katu
hangeweza
kurudi
kuniomba
samahani.Yeye anadai kwamba mimi
ndiye niliyemuingilia katika mahusiano
yake,anadai wewe ni mpenzi wake.Ni
kweli? Akauliza Dr Marcelo na kumfanya
Monica atoe kicheko.
“ Hata kama wanaume wangeisha
kabisa katika dunia hii na angebaki Daniel
peke yake katu hawezi kuwa mpenzi
wangu.Ninamfahamu
vizuri
na
ninazifahamu tabia zake chafu.Ukaribu
wetu ni wa kawaida tu na hakuna zaidi ya
hapo.Kama nilivyokueleza kuwa mimi nay
eye tumekua pamoja toka tukiwa wadogo
na hata familia zetu ni marafiki” Akasema
Monica
Chakula kikaletwa wakaendelea kula
kimya kimya
“ Dr Marcelo ..” akaita Monica.
“ Naomba tafadhali mpuuze Yule
mjinga na maneno aliyoyasema.Yule bado
ni kijana na hana malengo yoyote zaidi ya
kuutumia kwa fujo utajiri wa baba yake
kwa anasa.Ninafurahi sana kukutana na
kijana kama wewe ambaye una malengo
makubwa na pamoja kwamba familia yako
ina uwezo lakini hujatopea katika anasa
na starehe na badala yake umeelekeza kila
shilingi unayoipata katika kuwahudumia
watu wenye matatizo.Endelea na moyo
huo Dr Marcelo na Mungu atakubariki na
atakuzidishia wewe na familia yako.”
“ Ahsante sana Monica kwa maneno
hayo yenye busara” akasema Dr Marcelo
“ Kuna jambo lingine ambalo nataka
nikushauri” akasema Monica
“ Nakushauri uvunje kabisa urafiki
na Daniel.Nimegundua si kijana mzuri na
hafai kabisa kuwa rafiki yako.Wewe na
yeye tabia zenu ni tofauti kabisa. Kifupi ni
kwamba hamuendani.Nakushauri tafuta
rafiki wa karibu mwenye tabia njema na
mwenye malengo makubwa ya maisha
tofauti na Daniel ambaye kila kukicha
yeye anawaza starehe tu” akasema Monica
“ Monica mawazo yako ni kama
niliyonayo kichwani.Nimewaza sana
kuhusu jambo hilo na nimekwisha
dhamiria kwamba mimi na Daniel urafki
wetu uishie hapa .Kwa kitendo
alichonifanyia leo sintaweza kabisa
kuendelea na urafiki naye” akasema Dr
Marcelo
“ Good.Thats a wise decision.”
“ Vipi kuhusu wewe ,? Nina wasi wasi
anaweza akaja kukuletea matatizo pia.”
Akasema Dr Marcelo
“ Hata mimi tayari nimekwisha anza
kuchukua hatua za kumuweka Daniel
mbali kabisa nami.Sitaki kabisa ukaribu
naye.Hata mama yangu amenishauri
nifanye hivyo na ndiyo maana ukaona hata
katika sherehe ile niliyofanyiwa ya
kupongezwa na familia sikumualika,yote
hii ni kwa sababu sitaki tena ukaribu
naye.Usijali hana uwezo wa kunifanya
chochote.Mimi ndiye muamuzi ni mtu gani
ninayetaka awe karibu yangu.” Akasema
Monica
“ Monica ninakuahidi hapa kwamba
Daniel akithubutu kukufanyia jambo
lolote lisilo la kistaarabu I swear I’ll
destroy him.Mimi ni mtu mzuri sana lakini
sintaweza kuvumilia hata kidogo
kumuona Daniel au mwingine yeyote
akikufanyia vurugu. Malaika kama wewe
unapaswa kuheshimika na kila mtu”
akasema Dr Marcelo na kutazamana na
Monica wote wakatabasamu.
“ Wow ! what a gentleman.Macho
yake yanaonyesha wazi anamaanisha
anachokiongea.Ni mapema sana kusema
lakini ninaziona kila dalili za mwanaume
Yule wa ndoto zangu kwa Dr Marcelo.Ana
kila
sifa
ya
mwanaume
bora.Kinachonishangaza ni kwa nini
kijana kama huyu mwenye kila kitu,ana
sura nzuri,ana moyo wa huruma na
anajali,ukiacha yote ni kijana tajiri,mpaka
leo hana mpenzi? Ana tatizo lolote? Nahisi
kuna mambo ya ndani yanayomuhusu
Marcelo ambayo napaswa kuyafahamu.”
Akawaza Monica.
Walimaliza kula kisha wakaendelea
na maongezi kuhusiana na mbio za nusu
marathoni zinazotarajia kufanyika siku
inayofuata.Baada ya kutoka hapo
wakaondoka wote na kuongozana kwenda
kuangalia maandalizi ya mbio hizo
yaliyokofikia.
 
SEHEMU YA 27

Saa kumi na mbili kasoro za jioni Bakari
mmoja wa wafanyakazi wa Bi Janet
ambaye humtumia katika shughuli zake
mbali mbali,alirejea katika makazi ya
Benedict Mwamsole na kumkuta Bi Jane
tayari amekwisha rejea nyumbani . Moja
kwa moja akamfuata na kumpa majibu ya
kazi aliyokuwa amemtuma jana yake.
“ Madam kazi uliyonituma
nimeimaliza na haya hapa ni majibu yake.”
Akasema Bakari akiwa amesimama mbele
ya Bi Janet kwa adabu
“ Ahsante sana Bakari kwa
kuikamilisha kazi hii kwa haraka.”
Akasema Bi Janet na Bakari akamkabidhi
bahasha .
“ Humu kuna kila kitu kuhusiana na
Dr Marcelo” akasema Bakari
“ Una hakika taarifa zote zilizomo
humu ni sahihi? Akauliza Bi Janet
“ Ndiyo Madam .Taarifa zote zilizomo
humo ni za uhakika “ akasema Bakari.
“ Good.” Akasema Bi Janet,akachana
hundi na kumpatia Bakari,akatoa karatasi
zilizokuwamo katika bahasha ile akaanza
kuzipitia
moja
baada
ya
nyingine.Kulikuwa na nyaraka kadhaa
zikionyesha mambo mbali mbali
kuhusiana na Dr Marcelo kuanzia taarifa
zake za kifedha,mali anazomiliki
n.k.Ilimchukua zaidi ya saa moja na nusu
kuipitia ripoti ile kuhusiana na Dr Marcelo
akavuta pumzi ndefu na kumuita
mtumishi wake amletee maji ya kunywa
kisha akazama katika dimbwi la mawazo
“ Dr Marcelo is a good guy .A very
good guy na anaweza kusema kwamba
huyu kijana anaweza kumfaa sana
Monica.Hana sifa yoyote mbaya kama Yule
mshenzi Daniel .Anatoka katika familia
tajiri ,ni msomi mzuri,hajawahi kuoa na
ana kila sifa nzuri lakini ana tatizo moja
kubwa ambalo siwezi kukubali akawa na
Monica japokuwa kuna kila dalili kwamba
Monica ameanza kuvutiwa naye.” Akavuta
pumzi ndefu na kutazama tena karatasi
zile kwa makini
“ Dr Marcelo ana saratani ya damu
!!.Oh my God why it have to be him?? Hii
ina maana hana maisha marefu kwa
sababu ya ugonjwa wake huu kwa hiyo
siwezi kukubali akawa na Monica.Siko
tayari kumuona mwanangu akiwa mjane
katika umri mdogo.Inaniuma kumkosa
kijana kama huyu lakini sina namna
nyingine ya kufanya zaidi ya
kuwatenganisha haraka sana kabla ya
mahusiano yao hayajafika mbali na kuota
mizizi.Mungu atamjalia Monica na siku
moja atampata mwanaume wa ndoto zake
ambaye hatakuwa na tatizo lolote”
akawaza Bi Janet na kuinuka akaelekea
chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 28

aada ya kuwasili jijini Dar es
salaam, David Bikumbi Mukaya Zumo rais
wa jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo
alipokelewa na waziri wa mambo ya nchi
za nje wa Tanzania katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius nyerere
halafu akapelekwa moja kwa moja katika
hoteli atakayofikia ambako alipata
mapumziko mafupi kabla ya kuelelekea
ikulu kuonana na rais wa Tanzania Ernest
Mkasa ambaye alikuwa na mazungumo
naye ya faragha kabla ya kuanza kikao cha
maraisi wa nchi za maziwa makuu.
Alipokewa ikulu na mwenyeji wake
wakawa na mazungumzo ya faragha na
baada ya hapo akaelekea katika hoteli ya
White Panda ambako kuliandaliwa
mkutano kati yake na raia wa kongo
wanaoishi nchini Tanzania.Aliongea nao
mambo mengi na kisha akarejea hotelini
kwake kujipumzisha na kujiandaa kwa
ajili ya mkutano wao unaotarajiwa kuanza
kesho.
Saa moja za jioni Jean Pierre Muyeye
msaidizi wa David Zumo akarejea.Toka
walipowasili Dar es salaam Muyeye
alikuwa anafanya kazi moja tu aliyotumwa
na mkuu wake ya kufuatilia na kukusanya
taarifa kuhusiana na binti afrika Monika
Mwamsole.
“ Nipe taarifa nzuri Muyeye”
akasema David Zumo akiwa sebuleni
amepumzika akipata mvinyo
“ Mkuu nimeifanya kazi uliyonituma
na nimeikamilisha.” Akasema Muyeye
“ Kazi nzuri sana Muyeye.Nipe taarifa
hizo” akasema David Zumo.
Jean Pierre Muyeye akamueleza
David kila kitu alichokipata kuhusiana na
Monica.Uso wa rais huyu tajiri barani
Afrika ukajenga tabasamu kubwa sana
baada ya Muyeye kumaliza kumpa taarifa
ile. Akainuka na kumimina mvinyo katika
glasi akampatia Muyeye
“ Muyeye unastahili kunywa pamoja
nami mvinyo huu ghali zaidi ambao
hunywewa na watu maarufu.Mambo
uliyoyafanya ni makubwa na unastahili
kunywa pamoja nami” akasema David na
kugonganisha glasi
“ Umenifurahisha sana Muyeye kwa
kazi hii uliyoifanya hadi ukapata taarifa
hizi.Naomba nikiri kwamba kwa upande
wako unaweza ukaona ni kazi ndogo
umeifanya lakini kwangu mimi ni kitu
kikubwa sana umekifanya.” Akasema
David na kunywa funda moja
“ Kazi hii ya leo ni hatua ya
kwanza.Kesho nataka tuingie katika hatua
ya pili.Nataka kesho ushiriki katika mbio
hizo fupi kama mwakilishi wangu na
baada ya mbio hizo nataka uonane na
Monica
umfikishie
ujumbe
wangu.Mweleze kwamba ninahitaji
kuonana naye kesho jioni kwa chakula cha
usiku hapa hotelini kwa lengo la kujadili
kuhusiana na mradi wake wa ujenzi wa
shule
ya
watoto
wenye
ulemavu.Nimeguswa sana na ninahitaji na
mimi kuchangia katika mradi
huo.Ninataka kujadili pamoja naye
anieleze kwa kina ni sehemu ipi hasa
ninayoweza kuchangia ” akasema David
Zumo
“ Mkuu nitafanya kama ulivyoagiza
na kesho utakutana na Monica.” Akasema
Muyeye na kuzidi kumfurahisha David
Zumo
“ Monica mwamsole ..!! akasema
David kwa kunong’ona baada ya Jean
Pierre Muyeye kutoka.Akaifungua
kompyuta yake na kuzitazama tena picha
za Monica zilizopo mtandaoni akanywa
funda kubwa la mvinyo akatabasamu
“ Huyu ndiye hasa mwanamke
anayepaswa kuwa na mtu kama mimi.Ana
kila sifa ya mwanamke ninayemtaka.
Naapa katu sintamuacha lazima nimpate
,Monica lazima awe wangu .Nitatumia kila
nguvu niliyonayo mpaka nihakikishe
ninampata kimwana huyu anayeikimbiza
Afrika.Uzuri wake umenisisimua mno na
siwezi kukubali mwanamke mrembo
kama huyu asiwe wangu”
 
kama umemaliza na unakesha mm nakuwekea muziki .kama unaweza kukesha mpaka mida ya wanga
Kwenye hizi stori udingizi naweka kando mkuu, na kesho naomba ruhusa job jicho likiwa nyanya[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
LEGE LEGE LEGE Now you are talking ......please usisahau kunitag hii shughuli ikianza.
 
Waoooi nisipite kimya kimya bila kumpongeza mwandishi wa story hii..uko vizuri mkuu big up susha mambo tuburudishe nafsi zetu[emoji3][emoji3][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom