LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,122
- 9,209
- Thread starter
- #81
SEHEM YA 11
Tayari ni
saa kumi na mbili za jioni siku
iliyofuata na wageni walioalikwa katika
sherehe ya kifamilia ya kumpongeza
Monica kwa kutajwa kuwa msichana
mrembo kuliko wote Afrika,walikwisha
anza kuwasili katika jumba la kifahari la
bilionea
mzee
Benedict
Mwamsole.Kulikuwa na bendi ya muziki
ikipiga kuwatumbuiza wageni waliowahi
kuwasili bila kusahau vyakula na vinywaji
vya kila aina.
Saa mbili za usiku muongoza
shughuli akawataarifu wageni walikwa
kuwa muda wa kuanza shughuli ulikuwa
umewadia na hivyo kila mtu anatakiwa
achukue nafasi yake .Huku bendi
ikiendelea
kutumbuiza
Nathaniel
Mwamsole kaka wa Monica akashuka
ngazi
akitokea
ghorofani
akiwa
ameongozana na msichana mmoja
mrembo
sana.Wageni
wakasimama
wakimshangilia na akaelekezwa sehemu
ya kukaa.Baada ya dakika tano Mzee
Benard akiwa ameshikana mkono na
mkewe nao wakashuka ngazi taratibu
wakipita katika zuria jekundu ,watu wote
wakasimama
wakiwashangilia.Mzee
Benard akaelekezwa sehemu yake ya
kukaa iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya
familia
“ Waheshimiwa wageni waalikwa
tunayemsubiri hivi sasa ni malkia wa
Africa ambaye atashuka muda si
mrefu.Naomba mara tu atakapotokea
wote tusimame tumshangilie kwa nguvu
huku tukiongozwa na bendi. “ akasema
muongoza
shughuli.Watu
wote
walioalikwa katika sherehe ile waliopata
zaidi ya mia mbili walielekeza macho yao
mlangoni kumshuhudia mwanamke
mrembo
kuliko
wote
Afrika
atakapotoka.Baada ya kama dakika tano
hivi mlango mkubwa ukafunguliwa
akajitokeza mwanamke mwenye uzuri
usioelezeka na wageni wote wakashangilia
kwa nguvu.Taa zote zikawashwa na eneo
lote likawa jeupe kwa mwanga.Monica
akashuka ngazi taratibu na kutembea
katika zuria jekundu kwa madaha huku
akipunga mkono.Mzee Benard na mkewe
wakampokea Monica na kwenda
kumkalisha
katika
kiti
maalum
kilichoandaliwa kwa ajili yake.Sherehe
ikaanza rasmi.
Ilikuwa ni sherehe nzuri ya kukata
na shoka.Kila aliyekuwamo mle ndani
alisuuzika vilivyo.Kulikuwa na kila aina ya
knywaji na chakula.Ratiba ya mwisho
ilikuwa ni muziki na vinywaji.Baada tu ya
kufungua muziki na watu kujimwaga
kuusakata
muziki,Monica
akaanza
kuzunguka ukumbini akisalimiana na
watu mbali mbali waliohudhuria sherehe
ile na hatimaye akawasili katika meza
aliyokuwa amekaa Dr Marcelo na watu
wengine watatu.Akawasalimu na kuketi
maongezi na vinywaji vikaendelea.
“ Dr Marcelo would you mind if I
show you around? Akauliza Monica na kwa
haraka Dr Marcelo akainuka wakaondoka
pale bustanini wakaelekea katika sehemu
nyingine kulikokuwa na bwawa la
kuogelea.
“ Nyumba yenu ni kubwa sana na
nzuri” akasema Dr Marcelo
“ Hapa ni kwa wazazi wangu mimi
siishi hapa kwa sasa.Ni nyumba kubwa na
hata kama sote tungeamua kuishi hapa
bado tungetosha kabisa kwani kuna
vyumba vya kutosha” akajibu Monica
wakati wakiketi katika meza iliyokuwa
imeandaliwa vinywaji .Dr Marcelo
akamtazama Monica na kutabasamu
“ Hongera sana Monica .Usiku wa leo
umependeza kupita maelezo.Umebarikiwa
uzuri wa ajabu sana na sintachoka kurudia
tena na tena kuwa waliokutaja kuwa
mwanamke mrembo afrika hawakukosea
kabisa.Unastahili heshima hiyo kutokana
na uzuri ulio nao” akasema Dr Marcelo
“ Ahsante sana Dr Marcelo.Hata
wewe umependeza sana nadhani kupita
vijana wote waliohudhuria sherehe hii”
akasema Monica na wote wakacheka
“ Sijamuona Daniel,kwa nini
hajahudhuria?
Dr
Marcelo
akauliza.Monica akanywa funda moja la
mvinyo mwepesi na kusema
“ Daniel hujamuona hapa kwa
sababu sikumualika.” Akasema Monica
“ Hukumualika?!! Dr Marcelo
akashangaa
“ Ndiyo sikumualika.Hii ni sherehe
yangu na ninachagua watu wa
kuhudhuria.Sikutaka Daniel ahudhurie”
akasema Monica
“ Unajua nimeshangaa kidogo kwa
sababu ninavyofahamu wewe na Daniel ni
marafiki wakubwa.Kuna tatizo lolote
limetokea kati yenu? Akauliza Dr Marcelo
“ Hapana hakuna tatizo lolote ila
niliamua tu kutokumualika Daniel”
akasema Monica
“ Dr Marcelo let’s forget about
Daniel, ni masuala yangu mimi na yeye
kwa hiyo yasichukue muda wetu.Kwanza
napenda kukushukuru sana kwa kufika
ingawa nilitegemea ungekuwa na ubavu
wa pili pembeni yako lakini hakuna
kilichoharibika” akasema Monica na wote
wakaangua kicheko
“ Kama nilivyokueleza jana Monica
kuwa bado sijafikia daraja hilo” akajibu Dr
Marcelo
Tayari ni
saa kumi na mbili za jioni siku
iliyofuata na wageni walioalikwa katika
sherehe ya kifamilia ya kumpongeza
Monica kwa kutajwa kuwa msichana
mrembo kuliko wote Afrika,walikwisha
anza kuwasili katika jumba la kifahari la
bilionea
mzee
Benedict
Mwamsole.Kulikuwa na bendi ya muziki
ikipiga kuwatumbuiza wageni waliowahi
kuwasili bila kusahau vyakula na vinywaji
vya kila aina.
Saa mbili za usiku muongoza
shughuli akawataarifu wageni walikwa
kuwa muda wa kuanza shughuli ulikuwa
umewadia na hivyo kila mtu anatakiwa
achukue nafasi yake .Huku bendi
ikiendelea
kutumbuiza
Nathaniel
Mwamsole kaka wa Monica akashuka
ngazi
akitokea
ghorofani
akiwa
ameongozana na msichana mmoja
mrembo
sana.Wageni
wakasimama
wakimshangilia na akaelekezwa sehemu
ya kukaa.Baada ya dakika tano Mzee
Benard akiwa ameshikana mkono na
mkewe nao wakashuka ngazi taratibu
wakipita katika zuria jekundu ,watu wote
wakasimama
wakiwashangilia.Mzee
Benard akaelekezwa sehemu yake ya
kukaa iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya
familia
“ Waheshimiwa wageni waalikwa
tunayemsubiri hivi sasa ni malkia wa
Africa ambaye atashuka muda si
mrefu.Naomba mara tu atakapotokea
wote tusimame tumshangilie kwa nguvu
huku tukiongozwa na bendi. “ akasema
muongoza
shughuli.Watu
wote
walioalikwa katika sherehe ile waliopata
zaidi ya mia mbili walielekeza macho yao
mlangoni kumshuhudia mwanamke
mrembo
kuliko
wote
Afrika
atakapotoka.Baada ya kama dakika tano
hivi mlango mkubwa ukafunguliwa
akajitokeza mwanamke mwenye uzuri
usioelezeka na wageni wote wakashangilia
kwa nguvu.Taa zote zikawashwa na eneo
lote likawa jeupe kwa mwanga.Monica
akashuka ngazi taratibu na kutembea
katika zuria jekundu kwa madaha huku
akipunga mkono.Mzee Benard na mkewe
wakampokea Monica na kwenda
kumkalisha
katika
kiti
maalum
kilichoandaliwa kwa ajili yake.Sherehe
ikaanza rasmi.
Ilikuwa ni sherehe nzuri ya kukata
na shoka.Kila aliyekuwamo mle ndani
alisuuzika vilivyo.Kulikuwa na kila aina ya
knywaji na chakula.Ratiba ya mwisho
ilikuwa ni muziki na vinywaji.Baada tu ya
kufungua muziki na watu kujimwaga
kuusakata
muziki,Monica
akaanza
kuzunguka ukumbini akisalimiana na
watu mbali mbali waliohudhuria sherehe
ile na hatimaye akawasili katika meza
aliyokuwa amekaa Dr Marcelo na watu
wengine watatu.Akawasalimu na kuketi
maongezi na vinywaji vikaendelea.
“ Dr Marcelo would you mind if I
show you around? Akauliza Monica na kwa
haraka Dr Marcelo akainuka wakaondoka
pale bustanini wakaelekea katika sehemu
nyingine kulikokuwa na bwawa la
kuogelea.
“ Nyumba yenu ni kubwa sana na
nzuri” akasema Dr Marcelo
“ Hapa ni kwa wazazi wangu mimi
siishi hapa kwa sasa.Ni nyumba kubwa na
hata kama sote tungeamua kuishi hapa
bado tungetosha kabisa kwani kuna
vyumba vya kutosha” akajibu Monica
wakati wakiketi katika meza iliyokuwa
imeandaliwa vinywaji .Dr Marcelo
akamtazama Monica na kutabasamu
“ Hongera sana Monica .Usiku wa leo
umependeza kupita maelezo.Umebarikiwa
uzuri wa ajabu sana na sintachoka kurudia
tena na tena kuwa waliokutaja kuwa
mwanamke mrembo afrika hawakukosea
kabisa.Unastahili heshima hiyo kutokana
na uzuri ulio nao” akasema Dr Marcelo
“ Ahsante sana Dr Marcelo.Hata
wewe umependeza sana nadhani kupita
vijana wote waliohudhuria sherehe hii”
akasema Monica na wote wakacheka
“ Sijamuona Daniel,kwa nini
hajahudhuria?
Dr
Marcelo
akauliza.Monica akanywa funda moja la
mvinyo mwepesi na kusema
“ Daniel hujamuona hapa kwa
sababu sikumualika.” Akasema Monica
“ Hukumualika?!! Dr Marcelo
akashangaa
“ Ndiyo sikumualika.Hii ni sherehe
yangu na ninachagua watu wa
kuhudhuria.Sikutaka Daniel ahudhurie”
akasema Monica
“ Unajua nimeshangaa kidogo kwa
sababu ninavyofahamu wewe na Daniel ni
marafiki wakubwa.Kuna tatizo lolote
limetokea kati yenu? Akauliza Dr Marcelo
“ Hapana hakuna tatizo lolote ila
niliamua tu kutokumualika Daniel”
akasema Monica
“ Dr Marcelo let’s forget about
Daniel, ni masuala yangu mimi na yeye
kwa hiyo yasichukue muda wetu.Kwanza
napenda kukushukuru sana kwa kufika
ingawa nilitegemea ungekuwa na ubavu
wa pili pembeni yako lakini hakuna
kilichoharibika” akasema Monica na wote
wakaangua kicheko
“ Kama nilivyokueleza jana Monica
kuwa bado sijafikia daraja hilo” akajibu Dr
Marcelo