SEHEMU YA 79
nitakwenda kuonana naye tutakapomaliza
maongezi yetu” akasema Ernest ukapita
ukimya mfupi Ernest akasema
“ Austin leo nina furaha kubwa
kwani nimefanya jambo ambalo
sikutegemea
kulifanya.Nimeuzuia
muswada wa haki za binadamu
usipelekwe bungeni na kama haitoshi
nimelivunja baraza la mawaziri.Nimefanya
mambo haya mawili kutokana na ushauri
wako ulionipa jana usiku.Ahsante sana
kwa kunipa nguvu na ujasiri wa kuweza
kufanya haya niliyoyafaya.Kwa muda
mrefu nilikwisha choshwa kuwa kibaraka
wa Alberto’s lakini sikuwa na ujasiri wa
kuweza kupambana nao.Nimekuwa rais
kivuli kwa muda mrefu na sitaki
kuendelea tena kuwa kivuli huku
nikiwaacha watu wengine wafanye
maamuzi yote ya nchi .Wananchi ambao
ndio walionipigia kura wanateseka na
mimi sina namna ya kuwasaidia kwani
kila ninachokifanya lazima nipangiwe na
Alberto’s.Waliponichagua
wananchi
walikuwa na uhakika mkubwa wa maisha
yao kuboreka lakini mpaka leo bado
sijaitimiza ahadi hiyo.Nimeamua kutoka
kuwa kibaraka wa mashetani hawa na
kuwa rais wa watanzania.” Ernest
akanyamaza na kuendelea
“ Kingine kilichonipelekea nikafanya
maamuzi
haya
magumu
ni
Monica.Ikitokea Monica akawa mwanangu
naamini siku moja atakuwa na watoto na
sitaki wajukuu zangu wafahamu kwamba
babu yao alichangia kubomoa nchi kwa
kubariki matendo machafu ya mapenzi ya
jinsia moja,utoaji mimba n.k.Austin niko
tayari kwa mapambano.Nitapambana na
watu hawa hadi mwisho wangu.Najua
mwisho wangu utakuwa ni kuuawa lakini
kabla hawajaniua lazima nihakikishe
nimeikata mizizi yote ya Alberto’s hapa
nchini.Nataka niisafishe nchi.Nataka
niondoke madarakani taifa likiwa safi
kama lilivyoachwa na waasisi wetu”
akanyamaza na kumimina whysky katika
glasi akanywa
“ Mheshimiwa rais hiki ulichokifanya
umedhihirisha wazi kuwa wewe si
Alberto’s.Nitakuwa nawe bega kwa bega
na nitakulinda” akasema Austin
“ Ahsante sana Austin.Ninaamini ni
kwa maongozi ya Mungu tumekutana ili
uweze kupambana na genge hili lenye
kutaka kuiharibu dunia.Karibu sehemu
kubwa ya watu wanaonizunguka ni
Alberto’s.Makamu wa rais,waziri mkuu ,
mawaziri ,mkuu wa majeshi,wakuu wa
vyombo mbali mbali vya usalama,wote
hawa ni Albertos’ na nilipewa maelekezo
ya kuwateua kwa hiyo utaona ni namna
gani tulivyo na vita ngumu kwani tayari
Alberto’s wamekwisha otesha mizizi
imara hapa nchini.Wanaiongoza nchi
watakavyo na hii inaniumiza mno kwani
wananchi hawajui kuhusu Alberto’s bali
wananifahamu mimi.Nchi ikiyumba
lawama zote zitaniangukia mimi.Halafu
kingine kibaya zaidi hata mke wangu
Agatha naye ni mfuasi wa Alberto”
“ Oh my God !! akasema Austin kwa
mshangao
“ Even your wife? Akauliza
“ Yes even my wife” akajibu Ernest
na kimya kifupi kikapita Austin akauliza
“ Imekuaje hadi mkeo akaingia
katika kundi hili?
“ Austin swali lako linajibiwa kwa
historia na historia yangu mimi ni ndefu
lakini kwa kuwa tuko pamoja katika
mapambano haya nitakueleza japo kwa
ufupi” akanyamaza kidogo halafu akaanza
kumuhadhithis Austin Austin historia
yake