QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Mkuu naomba husiwe umefanya lolote hadi hili vumbi la Dodoma litulie.
 
kwahiyo nisiweke mkuu itakuwa sio sawa kabisaa.nitawakosea wadau wengine ww fanya uweke kituo na alama ulipoishia maliza ya domu then utakuja huku kuendelezaaa
Achana nae mkuu, anakuchelewesha, shusha vitu...time imekatika.
 
Sasa nakuona online LEGE....fanya mambo mkuu, tumekusubiri sana.
tukubaliane jambo mojaa.mda kwangu ni tatizo sana naomba nifanye hivi niibwage ndefuu sanaa mpaka season hii inakwisha harafu nipige brake ndefuu au niwe naweka kidogo kidogo kila siku nipatapo mdaaa
 
Karibu mkuuu. Dah cjalala nakusubiri..... Legee hii riwaya imeniingia kwnye kila mshipa wangu ( in prezd Joshua voice)[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
tukubaliane jambo mojaa.mda kwangu ni tatizo sana naomba nifanye hivi niibwage ndefuu sanaa mpaka season hii inakwisha harafu nipige brake ndefuu au niwe naweka kidogo kidogo kila siku nipatapo mdaaa
Sawa tu mkuu. We weka tu[emoji5]
 
maana wadau mnaona kama nafanya kusudi harafu sie wengine mishe zetu sio zakutulia sehemu moja nawezanikawa online lkn nipo mbali kabisa na home au safarini hivyo bora tuweke ratiba ya kihivi iwe week end mpaka week end ikitokea bahati nabwaga kabla hata ya week end katikati ya wiki.ila mwisho wa week ndio naweka ya kutosha kusoma week nzima mwaonaje
 
tukubaliane jambo mojaa.mda kwangu ni tatizo sana naomba nifanye hivi niibwage ndefuu sanaa mpaka season hii inakwisha harafu nipige brake ndefuu au niwe naweka kidogo kidogo kila siku nipatapo mdaaa
Bwaga sepa mkuu, Siku na majukumu vinatofautiana. Liwezekanalo Leo lisengoje kesho. Badili mpaka ID kama raia wakiongeza usumbufu.
 
tukubaliane jambo mojaa.mda kwangu ni tatizo sana naomba nifanye hivi niibwage ndefuu sanaa mpaka season hii inakwisha harafu nipige brake ndefuu au niwe naweka kidogo kidogo kila siku nipatapo mdaaa
Mkuu bwaga ndefu then jipe likizo maana watu wanakupa stress Mara lege shusha vitu wakati upo busy.. Fanya hivo mkuu Naamin hakutakuwa na malalamiko
 
SEHEMU YA 76


Oh y gosh !! ..” akawaza Monica na
kutabasamu.David akagundua kuwa tayari
Monica ameona kilichotokea.
“ Monica nilikueleza hapo awali
kuwa naomba unichukulie na madhaifu
yangu na hili ni mojawapo ya udhaifu
wangu kwako.Kila nikuonapo napatwa na
msisimko wa ajabu sana na kushindwa
kujizuia hali hii kunitokea.Naamini
sintakuwa kero kwako.Lakini naomba
niweke wazi kwamba si kila wakati hali hii
hunitoea bali ni pale tu ninapokuwaza au
nikiwa karibu yako kama hivi.Monica ni
wazi umeiteka akili yangu na kwa sasa
ninakuwaza wewe tu.Sikuwahi kutokewa
na hali hii hapo kabla na hata mke wangu
Pauline hakuwahi kuipeleka mbio akili
yangu kama ilivyotokea kwako.” Akasema
David na kunyamaza akamtazama
Monica.Walitazamana kwa zaidi ya
sekunde kumi na kila mmoja alionekana
kama vile kuna kitu anataka kumueleza
mwenzake.David akaushika mkono wa
Monica na kusema
“ Monica nahitaji kujua wewe
unajisikia vipi ukiwa karibu nami kama
hivi? Unahisi chochote? Unahisi msisimko
wowote ? Nieleze tafadhali nahitaji sana
kujua”
Monica akamtazama David usoni
kwa makini na kusema

David
nitakudanganya
nikikwambia kwamba ninahisi chochote
juu yako kwa sasa.Ni mapema mno kwa
hilo.Tumekutana na kufahamiana kwa
muda mfupi kwa hiyo bado sina hisia
zozote ila naomba jibu hili lisikukatishe
tamaa kwani kadiri siku zinavyosonga na
tunavyozidi kuwa karibu zaidi kwa mbali
naanza kuhisi mabadiliko,nahisi kama vile
kuna sumaku inanivuta kwako zaidi.”
Akasema Monica
Uso wa David Zumo ukajenga
tabasamu kubwa
“ Monica maneno yako
yananisisimua mno na kuufanya mwili
wangu wote utetemeke.Monica narudia
tena kusema kwamba ninajiona ni
mwenye bahati kubwa kuliko wanaume
wote kwa kukupata mwanamke kama
wewe.Nataka suala la ndoa yetu liende
haraka .Natak kila niamkapo asubuhi niwe
pembeni yako.oh Monica siwezi kuvumilia
tena.Tafadhali ....” Akasema David na
taratibu akambusu Monica busu ambalo
lilionekana kuitibua akili ya
Monica,akapatwa na msisimko wa aina
yake ,akajikuta akianza kuhema haraka
haraka .David Zumo ambaye alionekana
mjuvi sana wa mambo yale akaitumia
vyema nafasi ile kwa kuanza utundu
wake.Monica ambaye bado alikuwa mgeni
katika ulimwengu huu wa mapenzi
alimuachia David nafasi ya kuutawala
uwanja .Alihisi raha ya ajabu ambayo
hakuwahi kuipata hapo kabla
David Zumo aliridhika na maandalizi
aliyoyafanya na bila kupoteza muda
filimbi ikapulizwa na mtanange ukaanza.
 
tukubaliane jambo mojaa.mda kwangu ni tatizo sana naomba nifanye hivi niibwage ndefuu sanaa mpaka season hii inakwisha harafu nipige brake ndefuu au niwe naweka kidogo kidogo kila siku nipatapo mdaaa
Sawa LEGE, fanya hivyo
 
SEHEMU YA 77





DAR ES SALAAM - TANZANIA
Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania akiwa katika staili
yake ya kubadili muonekano ili
asitambulike kirahisi aliwasili katika
nyumba
anayoishi
Austin.Kama
ilivyokuwa kwa siku iliyotangulia Austin
aliwataka wale wote waliokuwa
wameongozana na Ernest wabaki nje
,akaingia ndani na rais pekee
“ Austin do you have anything to
drink in here? Akauliza Ernest .Austin
akamtazama na kuuliza
“ Unahitaji kinywaji gani?
“ Anything strong” akasema Ernest
.Austin akaenda jikoni ambako aliweka
chupa kadhaa za pombe kali akachukua
chupa moja kubwa ya pombe kali na
kurejea sebuleni
“ Rickot !!! .akasema Ernest na
kutabasamu baada ya kuiona pombe ile
aliyopewa na Austin
“ Mtengenezaji wa pombe hii anaitwa
Pineck Rickot raia wa ufaransa mwenye
asili ya Urusi.Mvinyo huu umewahi
kushinda tuzo kadhaa kubwa kama pombe
bora kabisa duniani.Ahsante Austin kwa
mvinyo huu” akasema Ernest na kumimina
katika glasi akanywa wote na kufumba
macho
“ It’s one of the strongest whysky in
the world” akasema Ernest .Austin
hakujibu kitu
“ Do you smoke ? akauliza Ernest
“ No !! akajibu Austin
Toka katika mfuko wa koti Ernest
akatoa mkebe ambao ndani yake ulikuwa
na sigara akatoa moja akaiwasha na
kupuliza moshi mwingi
“ Hii inaita Gurkha Black dragon.Hii
ni sigara ya bei ya juu zaidi duniani.You
can try one” akasema Ernest
“ No thank you “ akajibu Austin.
Ernest akavuta mikupuo kadhaa
kisha akasema
“ How’re you Austin ?
“ I’m ok “ Austin akajibu
“ Umepata mahitaji yote?
“ Usijali mzee nimepata kila kitu”
“ Good.” Akajibu Ernest a kuvuta tena
mkupuo mmoja akageuza shingo na
kutazama sebule yote
“ Natumai utakuwa umetazama
katika luninga hotuba niliyoitoa usiku
huu” akasema Ernest
“ Ndiyo mzee nimetazama.Hongera
sana .Ni mwanzo mzuri.Umeingia katika
historia ya dunia kama rais shujaa.Kitendo
hiki ulichokifanya leo kimefuta yale
mabaya yoye uliyoyafanya kwa wananchi
na kila raia huko aliko anakupongeza kwa
ushujaa huu.Hakuna aliyetegemea hata
mimi sikutegea kama ungekuwa na ujasiri
mkubwa wa namna hii.Ahsante
mheshimiwa rais kwa kuyasikiliza
mawazo yangu” akasema Austin.Ernest
akamimina whysky katika glasi na
kugugumia yote akafumba macho kwa
sekunde kadhaa na kuusiklizia ukali wa
ile pombe halafu akavuta mkupuo mmoja
wa sigara na kusema
“ It wasn’t easy my son”
“ I know “ akajibu Austin
“ Austin tuna maongezi marefu usiku
wa leo lakini kabla hatujaongea chochote
nataka unipe ripoti kuhusu kazi
zangu.Kuna maendeleo yoyote? Halafu
nilipewa taarifa kwamba kulitokea
mlipuko katika hospitali ya Mt Lucia hebu
nieleze una husiana nao? Akauliza
Ernest.Bila kupepesa macho Austin
akajibu
“ Mheshimiwa rais ninahusika na
jambo hilo.Mimi ndiye niliyetega hicho
kinachodaiwa ni mlipuko.”
“How could you do that Austin?
Huoni kuwa unajenga mazingira ya
kujulikana? Ni vipi kama ukifanyia
uchunguzi na ukagundulika? Vipi kama
 
SEHEMU YA 78




ulichukuliwa na kamera za ulinzi
?Akauliza Ernest
“ mheshimiwa rais kwanza naomba
nikueleweshe kuwa mlipuko ule haukuwa
bomu bali ni fataki .Ni kama vile
unavyoona milipuko katika filamu huwa si
mabomu halisi kama wengi wanavyodhani
kwa hiyo ni kitu ambacho kisingeweza
kuleta madhaa yoyote makubwa zaidi ya
mstuko kwa baadhi ya wagonjwa
.Nililazimika kutumia njia hii ili kuleta
taharuki pale hospitali kwani bila kufanya
vile nisingeweza kuikamilisha kazi ile kwa
ufanisi na kwa wakati.Ulinieleza kwamba
Marcelo alikuwa anataka kuuawa kwa
hiyo ninaamini watu waliokuwa wanataka
kumuua lazima walikuwepo hapo hapo
hospitali kwa hiyo kitendo nilichokifanya
cha kusababisha taharuki pale hospitali
kilinipa nafasi ya kumchukua Marcelo
kirahisi kwani hakuna aliyekuwa na muda
wa kumfuatilia mwenzake .Kila mmoja
alikuwa anahaha kuokoa maisha
yake.Kingine ,nataka nikutoe wasi
wasi,kabla ya kufanya kazi yagu tayari
nilikwisha chunguza mfumo mzima wa
ulinzi ulivyo.Hakuna kamera yoyote
iliyofungwa na kwa kifupi naweza kusema
kwamba hakuna ulinzi pale hospitali
.Mheshimiwa rais kuwa na amani.I’m good
at this”akasema Austin
“ I believe you” akasema Ernest
“ kwa hiyo mheshimiwa rais “ Austin
akaendelea
“ Nilifanikiwa kumpata Marcelo
akiwa mzima na kwa sasa amepumzika
chumbani.”
“ Thank you Austin,thank you so
much” akasema Ernest na kuinuka
“ I need to se him” akasema
“ mheshimiwa rais kabla haujaenda
kuonana na Marcelo kuna jambo nataka
kulifahamu” akasema Austin
“Uliza Austin”
“ Unawafahamu wanaotaka kumuua
Marcelo? Kwa nini wanataka kumuua?
Ernest mkasa aliyekuwa amesimama
akaketi sofani na kujibu
“ Austin kwa kuwa wewe ni kijana
wangu nitakueleza ukweli.Marcelo
simfahamu na wala hatujawahi kuonana
na siwafahamu wanaotaka kumuua ni
akina nani.Nilipigiwa simu na rais wa
Congo mheshimiwa David Zumo
akaniomba nimsaidie kumuokoa Marcelo
dhidhi
ya
watu
wanaotaka
kumuua.Nilimtaka David anipe taarifa za
kina kuhusiana na Marcelo na
anihakikishie kama hahusiki katika
mambo ya kihalifu ,akanihakikishia
kwamba Marcelo hahusiki na genge lolote
la uhalifu.Kwa kuwa ni rais mwenzangu
nilikubali kumsaidia kwani ni kawaida
yetu sisi marais kusaidiana.Kwa hiyo
Austin sifahamu chochote kuhusu Marcelo
labda tukimuhitaji tunaweza kupata jibu
ni akina nani wanaotaka kumuua na kwa
nini” akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais kutokana na
maelezo hayo sidhani kama litakuwa
jambo la busara kuanza kumuhoji.Kwa
vile tayari yuko katika mikono salama ni
vyema kama tutasubiri maelekezo ya
David Zumo aliyekuomba umsaidie na
tusijiingize katika masuala mengine
yasiyotuhusu hasa katika wakati huu
ambao kuna mambo mengi mazito yako
mbele yetu” akasema Austin
“ Wazo lako zuri Austin.Ngoja
tuachane naye na tujielekeze katika
mambo yanayotuhusu lakini baadae
 
SEHEMU YA 79



nitakwenda kuonana naye tutakapomaliza
maongezi yetu” akasema Ernest ukapita
ukimya mfupi Ernest akasema
“ Austin leo nina furaha kubwa
kwani nimefanya jambo ambalo
sikutegemea
kulifanya.Nimeuzuia
muswada wa haki za binadamu
usipelekwe bungeni na kama haitoshi
nimelivunja baraza la mawaziri.Nimefanya
mambo haya mawili kutokana na ushauri
wako ulionipa jana usiku.Ahsante sana
kwa kunipa nguvu na ujasiri wa kuweza
kufanya haya niliyoyafaya.Kwa muda
mrefu nilikwisha choshwa kuwa kibaraka
wa Alberto’s lakini sikuwa na ujasiri wa
kuweza kupambana nao.Nimekuwa rais
kivuli kwa muda mrefu na sitaki
kuendelea tena kuwa kivuli huku
nikiwaacha watu wengine wafanye
maamuzi yote ya nchi .Wananchi ambao
ndio walionipigia kura wanateseka na
mimi sina namna ya kuwasaidia kwani
kila ninachokifanya lazima nipangiwe na
Alberto’s.Waliponichagua
wananchi
walikuwa na uhakika mkubwa wa maisha
yao kuboreka lakini mpaka leo bado
sijaitimiza ahadi hiyo.Nimeamua kutoka
kuwa kibaraka wa mashetani hawa na
kuwa rais wa watanzania.” Ernest
akanyamaza na kuendelea
“ Kingine kilichonipelekea nikafanya
maamuzi
haya
magumu
ni
Monica.Ikitokea Monica akawa mwanangu
naamini siku moja atakuwa na watoto na
sitaki wajukuu zangu wafahamu kwamba
babu yao alichangia kubomoa nchi kwa
kubariki matendo machafu ya mapenzi ya
jinsia moja,utoaji mimba n.k.Austin niko
tayari kwa mapambano.Nitapambana na
watu hawa hadi mwisho wangu.Najua
mwisho wangu utakuwa ni kuuawa lakini
kabla hawajaniua lazima nihakikishe
nimeikata mizizi yote ya Alberto’s hapa
nchini.Nataka niisafishe nchi.Nataka
niondoke madarakani taifa likiwa safi
kama lilivyoachwa na waasisi wetu”
akanyamaza na kumimina whysky katika
glasi akanywa
“ Mheshimiwa rais hiki ulichokifanya
umedhihirisha wazi kuwa wewe si
Alberto’s.Nitakuwa nawe bega kwa bega
na nitakulinda” akasema Austin
“ Ahsante sana Austin.Ninaamini ni
kwa maongozi ya Mungu tumekutana ili
uweze kupambana na genge hili lenye
kutaka kuiharibu dunia.Karibu sehemu
kubwa ya watu wanaonizunguka ni
Alberto’s.Makamu wa rais,waziri mkuu ,
mawaziri ,mkuu wa majeshi,wakuu wa
vyombo mbali mbali vya usalama,wote
hawa ni Albertos’ na nilipewa maelekezo
ya kuwateua kwa hiyo utaona ni namna
gani tulivyo na vita ngumu kwani tayari
Alberto’s wamekwisha otesha mizizi
imara hapa nchini.Wanaiongoza nchi
watakavyo na hii inaniumiza mno kwani
wananchi hawajui kuhusu Alberto’s bali
wananifahamu mimi.Nchi ikiyumba
lawama zote zitaniangukia mimi.Halafu
kingine kibaya zaidi hata mke wangu
Agatha naye ni mfuasi wa Alberto”
“ Oh my God !! akasema Austin kwa
mshangao
“ Even your wife? Akauliza
“ Yes even my wife” akajibu Ernest
na kimya kifupi kikapita Austin akauliza
“ Imekuaje hadi mkeo akaingia
katika kundi hili?
“ Austin swali lako linajibiwa kwa
historia na historia yangu mimi ni ndefu
lakini kwa kuwa tuko pamoja katika
mapambano haya nitakueleza japo kwa
ufupi” akanyamaza kidogo halafu akaanza
kumuhadhithis Austin Austin historia
yake
 
SEHEMU YA 80



DAR ES SALAAM – 2001
Saa nne na dakika nane za usiku
ndege aliyopanda bi Agatha ikatua katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es
salaam.Bi Agatha akiwa ameongozana na
waumini wenzake wanne pamoja na
askofu wa kanisa lao wakitokea Italia
katika safari ya kidini wakashuka
ndegeni.Uwanjani hapo bilionea Ernest
Mkasa tayari alikisha fika kumpokea
mkewe.Baada ya kukamilisha taratibu za
uwanjani hapo bi Agatha akatoka na
kulakiwa na mumewe Ernest
“ Pole sana kwa safari” akasema
Enest ,mizigo ya Agatha ikapakiwa garini
wakaondoka kuelekea nyumbani
“ Ernest nipe taarifa za maendeleo ya
Yolanda” akasema Agatha wakiwa garini
wakielekea nyumbani
“ Kwa sasa ana nafuu ya kutosha
lakini bado hajaweza kutembea
vizuri.Daktari anafika kila siku kumpa
mazoezi” akajibu Ernest
“ Ernest what real happened?
Uliponigia simu kunitaarifu kuwa Yolanda
ameanguka ghafla na kupoteza fahamu
ulikuwa kwenye taharuki kubwa” Agatha
akauliza
“ I don’t know exactly what
happened .Nilipigiwa simu na mwalimu
akanifahamisha kuwa Yolanda ameanguka
ghafla na kupoteza fahamu.Alikimbizwa
hospitali akapatiwa huduma na
alipozinduka madaktari wakamfanyia
uchunguzi wa kina kufahamu
kilichosababisha apoteze fahamu lakini
hawakugundua chochote.Hata hivyo
wamemshauri apunguze uzito kwani
alionao ni mkubwa kulingana na umri
wake” akasema Ernest
“ She’ll be fine” akajibu Agatha
.Ernest akauliza
“ Vipi safari yenu ilikuaje?
“ Safari yetu ilikuwa nzuri na yenye
mafanikio makubwa.Tutaongea zaidi
baadae lakini kwa sasa naomba uniache
kidogo niingie katika maombi mazito kwa
ajili ya Yolanda” akasema Agatha na
kufumba macho akajiegemeza kitini
“ Bado ninajiuliza sana kuhusiana na
kilichomfanya Agatha ahame dhehebu
lake la awali na kujiunga na dhehebu hili
jipya.Kinachonishangaza zaidi ni kwamba
toka amejiunga katika dhehebu hili jipya
amekuwa mtu wa ibada lakini matendo
yake bado hayajabdilika hata kidogo.Kuna
biashara zetu nyingi ambazo si halali na
zinatuingizia fedha nyingi lakini sijawahi
kusikia hata siku moja akiongelea kuhusu
biashara hizo na badala yake amekuwa
akichukua pesa zinazotokana na biashara
hizo na kuzipeleka kanisani.Ngoja
nimuache na imani yake” akawaza Ernest
Walifika nyumbani na moja kwa
moja baada ya kushuka garini wakaelekea
katika chumba cha Yolanda mtoto wao
ambaye anaumwa ugonjwa usiojulikana.
“ my baby !! akasema Agatha na
kumkumbatia mwanae
“ Unajisikiaje sasa ?
“ Najisikia kidogo afadhali”
“ Can you walk? Akauliza Agatha
 
Back
Top Bottom