QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

dah mkuu kipyenga kinapulizwa afu unapiga pause[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
SEHEMU YA 81


wili mzito sana mama kama vile
nimebeba gunia zito.Siwezi hata
kunyanyua mguu.” Akasema Yolanda huku
machozi yakimtoka
“ Basi usijali mwanangu .Ndani ya
muda mfupi toka sasa utakuwa mzima
tena.” Akasema Agatha akaikunja mikono
yake kifuani na kufumba macho baada ya
muda akasema
“ Mio Dio beliee,si prega I mostrare il
proprio patere e quarine questo poverto
bambiko
” alikuwa anaoangea kwa
kiitalinao akimaanisha
“ Mungu wangu nakuamini,tafadhali
onyesha nguvu zako na umponye mtoto
huyu”
Agatha akamsogelea Yolanda na
kumuwekea mkono wa kulia katika paji la
uso akasema
“ Svegliarsie Camminare.Mai male di
nuovo
” akimaanisha “ Inuka na tembea na
usiumwe kamwe”
Taratibu Yolanda akaanza kuhisi
wepesi wa mwili akainuka na kusimama
akatembea hatua mbili akaongeza
nyingine mbili.Hakuyaamini macho yake
.Ule uzito wote aliokuwa akihisi kama vile
amebeba
gunia
la
mchanga
ulitoweka.Alijiona mwepesi kama karatasi
“ This is a miracle!! Akasema Ernest
kwa mshangao mkubwa.Agatha hakujibu
kitu zaidi ya kutabasamu .Ulikuwa ni
mshangao kwa kila mtu.Akamuamuru
Yolanda ajaribu kukimbia na akafanya
hivyo.Akamuwekea mkono kichwani na
kusema.
“ Gracie ll mio lord.I fara’ ris
parmiare Voie solo per il rest o della mia
vita”
akimaanisha

Ahsante
Mungu
wangu.Nitakutumikia wewe pekee kwa
maisha yangu yote yaliyobaki”
“ Mama umepata wapi nguvu hii ya
kuponya? Akauliza Yolanda
“ Agatha akamtaka Yolanda aendelee
kupumzika akamshika mkono mume
wake wakatoka mle chumbani.Bado
Ernest alikuwa katika mshangao mkubwa
kwa kile alichokifanya mke wake.Hata
baada ya kuingia chumbani kwao Ernest
Mkasa aliendelea kumtazama Agatha kwa
mshangao mkubwa
“ What ?..mbona unanitazama hivyo
Ernest? Akauliza Agatha
“ Nimeshangazwa na kustushwa sana
kwa jambo ulilolifanya kwa Yolanda”
What was that? mazingaombwe?
“ Si mazingaombwe Ernest.That was
a real thing”
“ real thing? Toka lini umekuwa na
nguvu za kuponya? Akauliza Ernest
“ Ernest mambo yamebadilika siku
hizi.Vitu vidogo vidogo kama hivi mtu
yeyote anaweza akafanya.Si vitu vigumu
tena kama tulivyokuwa tunafikiri.Kwa
mfano naweza kufanya kitu kidogo tu sasa
hivi ambacho unaweza kufikiri
hakiwezekani” akasema Agatha na
kumsogelea Ernest akamshika machoni na
kusema

Tio
ordino
di
essepe
cieco”
akimaanisha “ Ninakuamuru kuwa kipofu”
“ Do you see anything Ernest? Agatha
akamuuliza mumewe
“ No ! I cant see anything.It’s
dark...what the hell are you doing Agatha?
Please give me back my vision now !!
akasema Ernest kwa ukali.Agatha
akacheka kidogo na kusema
 
maana wadau mnaona kama nafanya kusudi harafu sie wengine mishe zetu sio zakutulia sehemu moja nawezanikawa online lkn nipo mbali kabisa na home au safarini hivyo bora tuweke ratiba ya kihivi iwe week end mpaka week end ikitokea bahati nabwaga kabla hata ya week end katikati ya wiki.ila mwisho wa week ndio naweka ya kutosha kusoma week nzima mwaonaje
Hakuna tatizo LEGE, tunakuelewa sana.
 
SEHEMU YA 82



torno vostra vision indietro”
Mara tu
alipotamka maneno hayo Ernest akaanza
kuona tena.Mwili ulimtetemeka kwa woga
“ Ernest tafadhali usiniogope.Hivi ni
vitu vya kawaida sana ambavyo mtu
yeyote anaweza akafanya na hata wewe
unaweza kufanya ukipewa nguvu.kwa hiyo
usinishangae kuona ninafanya mambo
kama haya” akasema Agatha
“ Agatha umejiingiza katika imani
gani hizo? Mambo haya tumezoea kuyaona
yakifanywa na hawa wanaojiita manabii
.Are you one of them?
“ I’m not one of them.Ernest kuna
mambo mengi ambayo mimi na wewe
tunahitaji kuzungumza.Ni mambo yenye
manufaa makubwa kwetu” akasema
Agatha na kuingia bafuni kuoga
akimuacha Ernest bado katika mshangao
“ Ama kweli hizi ndizo zile zama za
mwisho zilizotabiriwa katika vitabu.Yaani
Agatha naye amekuwa na nguvu ya
kufanya mambo kama haya? Katoa wapi
nguvu hiyo ya kufanya viini macho? Huko
alikotoka ndiko alikotoa nguvu hii.Nasikia
wananunua nguvu ya kufanya miujiza ili
kuwavuta waumini katika makanisa yao
lakini inasemekana pia nguvu hii
waitumiayo katika kufanya matendo haya
ya ajabu ajabu ili kuwahadaa watu ni
nguvu za giza.Kama ni kweli hilo
linalosemwa basi Agatha naye atakuwa
mfuasi wa imani hiz😵h my God !!
Amekosa nini huyu mwanamke hadi
ameamua kujiingiza katika mambo hayo?
Nakubali kuna mambo mengi machafu
tunayafanya lakini sikutegema kama siku
moja Agatha angejiingiza katika imani hizi
za kishetani.” Akawaza Ernest na
kustuliwa mawazoni na mkewe aliyetoka
kuoga.
Familia ilikutana mezani kwa
chakula na kila mmoja alikuwa na
mshangao juu ya kile kilichotokea kwa
Yolanda.Baada ya chakula kila mmoja
akaenda chumbani kwake kulala.
“ Agatha ni wakati sasa wa kunieleza
ukweli wa yale uliyoyafanya.Umetoa wapi
nguvu ya kufanya mambo yale? Naomba
nikuweke wazi uwa umeniogopesha mno
na kama hunielezi ukweli I swear
nitafanya jambo ambalo hukuwa
umelifikiria kabisa” akasema Ernest
“ What will you do? Akauliza Agatha
huku akitabasamu
“ I’ll forget what me and you have
,what we’ve been through and I’ll leave
you!! Akasema Ernest na sura yake
ikionyesha kutokuwa na masihara.Ghafla
tabasamu likatoweka usoni pa Agatha
“ Ok Ernest lets get serious
now.Nitakueleza ukweli na tafadhali
naomba unisikilize kwa makini sana hadi
nitakapomaliza.” Akasema Agatha
“ Nilielekezwa na rafiki yangu mmoja
anaishi afrika ya kusini kuhusiana na
kanisa jipya liitwalo Holy faith
ministry.Maelezo niliyopewa na huyo
rafiki yangu kuhusu kanisa hili yalinivutia
ikanilazimu kumtafuta askofu Gidion
Guchal.Nilifanikiwa kuonana naye
akaniombea na akanieleza mambo mengi
ambayo sikuwahi kuelezwa na mtu yeyote
hapo kabla.Alinieleza kila kitu kuhusu
maisha
yangu
nikashangaa
mno.Akanieleza kuwa hata mimi
ningeweza kuwa na uwezo kama ule
endapo ningehitaji.Nilitamani sana kuwa
na uwezo wa kufanya mambo ambayo
wengine hawawezi ,mambo makubwa
 
SEHEMU YA 83




kushinda uwezo wa mwanadamu kwa hiyo
nikajiunga rasmi na kanisa hilo.Baba
askofu Gidion alituchagua watu watano
kwa ajli ya kwenda hija katika makao
makuu ya kanisa letu huko
Italia.Tulipofika tukapokewa na mtu
mmoja anaitwa Giovanni.Siku Iliyofuata
ndipo tulipoelezwa rasmi dhumuni la
ziara yetu ile .Tulielezwa kwamba
tumepelekwa pale ili kuingizwa rasmi
katika jumuiya ya Alberto’s.Hakuna
miongoni mwetu aliyeelewa chochote
kuhusiana na Alberto’s hivyo tukataka
kufahamu na tukafahamishwa kwa kina.”
Akanyamaza na baada ya muda
akaendelea.
“ Mwaka 1894 Kardinali Albert
Mcrecks wa California alianzisha vugu
vugu la uasi ndani ya kanisa kwa
kuwashawishi wenzake waunge mkono
mpango wake wa mageuzi ndani ya kanisa
mpango ambao alitarajia kuwasilisha kwa
kiongozi wa kanisa hilo duniani.Mpango
huo ulilenga kulishawishi kanisa katoliki
likubali mabadiliko na kuruhusu makasisi
wake kuoa,kutambua makundi mbali
mbali hasa ya watu wanaoshiriki mapenzi
ya jinsia moja,kuruhu utoaji mimba
n.k.Alberto Alifanikiwa kupata uungwaji
mkono mkubwa na vugu vugu la
mabadiliko ndani ya kanisa likapamba
moto.Aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo
kwa wakati huo alikasirishwa sana na
jambo hilo na hivyo akamvua daraja
Alberto pamoja na wenzake wote
waliomuunga mkono.Baada ya kufukuzwa
na kuvuliwa daraja.Alberto bado
aliendelea na msimamo wake wa mageuzi
na sasa alitaka kufanya mageuzi makubwa
duniani .Alipotea kwa meizi sita na
aliporejea alidai kuwa alikuwa katika
maombi makubwa mahala pa siri na
Mungu akamtuma aje afanye mabadiliko
makubwa duniani na hapo ndipo jumuiya
ya Albertos ikaanzishwa.Alianza kwa
kutengeneza mtandao wake uliopata
nguvu kutokana na kuungwa mkono na
viongozi
hasa
wa
mataifa
makubwa.Alberto alikuwa na nguvu
kubwa ya ushawishi kwa hiyo alifanikiwa
kuwashawishi viongozi wengi wa mataifa
makubwa wakamkubali na kujiunga
naye.Katika kujenga mtandao wake
alianzia na mataifa ya Amerika na ulaya
na baadae akafika hadi bara Asia na
kuotesha mizizi .Alberto kwa kwanza
alipofariki ,alifuata Alberto wa pili na sasa
yuko Alberto wa tatu ambaye ni kijana
zaidi na mwenye nguvu kubwa.Baada ya
kazi kubwa kufanyika katika mataifa ya
Amerika na ulaya Alberto wa tatu
ameamua kuelekeza nguvu barani
Afrika.Wanataka kuibadili Afrika na tayari
wamekwisha ingia na kuotesha
mizizi.Haikuwa kazi ngumu kwa nchi za
afrika kukubaliana nao kwani walitumia
kigezo cha umasikini wa nchi hizi
kuzishinikiza zifuate masharti yao.Kwa
kutumia mataifa makubwa ambayo
yamekuwa yakitoa misaada mikubwa
,nchi zote za Afrika zimetakiwa kutunga
sheria zao na kutambua haki za watu
wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.Tayari
nchi nyingi za Afrika zimekubaliana na
sharti hilo na zimetunga sheria
kukubaliana na mambo hayo.Nchi pekee
ambayo imewapa ugumu mkubwa kuingia
ni Tanzania kutokana na misingi imara
iliyowekwa na waasisi wa taifa hili .Kwa
sababu hiyo wameunda timu ya watu kumi
ambayo itahakikisha Alberto’s wanaingia
 
SEHEMU YA 84



Tanzania.Mimi ni miongoni mwa watu hao
kumi”
“ Oh my God !! akasema Ernest kwa
mshangao
“ Ernest naomba usiongee chochote
kwanza hadi nitakapomaliza.Naomba
uendelee kunisikiliza.” Akasema Agatha
“ Mimi na wenzangu tuliochaguliwa
,tumekula kiapo mbele ya mkuu Alberto
wa tatu kuhakikisha kuwa tunafanya kila
tuwezalo kuondoa vizingiti vyote
vinavyofanya Alberto’s washindwe
kupenya na kufanya kazi zao nchini
Tanzania.Tumepewa nguvu ya kufanya
mambo ambayo binadamu wengine
hawawezi kuyafanya.Nimekuwa mtu mpya
.Nimeweka agano mbele ya Alberto mkuu
la kuwa mtiifu na kufuata maelekezo yote
anayoyatoa.Kwa hiyo basi tumepewa kazi
kubwa ya kufanya na kazi ya kwanza
ambayo tunatakiwa kuifanya ni
kutengeneza serikali.Tunataka rais
,makamu wa rais ,waziri mkuu na
mawaziri wote wawe ni Alberto’s
.Tukilifanikisha hilo basi tutakuwa
tumeotesha mzizi na Tanzania
itabadilika.Tunataka Tanzania mpya.”
Agatha akanyamaza akamtazama
mumewe ambaye uso wake ulijikunja
kqwa hasira .Agatha hakujali akaendelea
“ Ernest nafahamu jambo hili
limekustua sana lakini ni suala ambalo
lina manufaa makubwa si kwetu pekee
bali kwa nchi na dunia kwa hiyo nakusihi
usikasirike mpendwa wangu kwani kuna
jambo kubwa umeandaliwa na ambalo
hukuwa umelitarajia kabisa” akanyamza
kidogo akaendelea
“ Baada ya kupewa jukumu la
kuhakikisha tunaandaa serikali ambayo
itakuwa
chini
ya
Alberto’s,nimekupendekeza wewe uwe
rais mpya wa Tanzania.”
“ Nini ?? Akauliza Ernest kwa
mshangao
“ Nimekupendekeza uwe rais wa
Tanzania.Utaongoza serikali itakayokuwa
chini yetu.Wew................”
“ Stop Agatha!!!..stop!!...!! akasema
Ernest kwa hasira
“ Wewe na hao mashetani wenzako
ni mataahira.Agatha kitu gani umekosa
hadi ukaingia katika mambo haya ya
kishetani? Please Agatha toka huko
ulikoingia haraka sana.I need back my old
Agatha,the one I married and not you!!
Akasema Ernest kwa ukali
“ Ernest I’m still the same Agatha,
your one and only wife.From now you are
going to listen to me and do whatever I tell
you to do.You here me? Akasema Agatha
kwa ukali
“ Mimi ndiye mwenye amri ya
mwisho ndani ya nyumba hii na
utanisikiliza mimi pekee.Nataka uchukue
simu na uwapigie hao mashetani wenzako
uwaambie kwamba hutashiriki tena
katika mambo yao ya kishetani na baada
ya hapo hautaruhisiwa tena kutoka nje ya
nyumba hii.Umenisikia Agatha? Akasema
Ernest huku mwili ukimtetemeka kwa
hasira
“ Una dakika mbili za kuchukua simu
na kuwapigia hao wenzako ama sivyo
uchukue kila kilicho chako na uondoke
katika nyumba hii.Nadhani umenielewa
vizuri na wala sitishwi na huo uchawi
wako .Nitahakikisha kila mtu anafahamu
ni mambo gani wewe na hao mashatani
wenzako mnayafanya.” Akasema Ernest
 
SEHEMU YA 85




No Ernest you dont have to do that
and you cant do that.Kwa sasa maisha
yako nimeyashika mimi na ndiyo maana
nikakwambia kwamba utafuata kila
nitakachokuamuru”
Ernest Mkasa akacheka kidogo na
kusema
“ Sikujua kama unaweza kuwa
mjinga kiasi hiki .Ninakuambia huwezi
kuniamuru chochote na ninarudia tena
kukuonya kuwa sikuogopi hata kama una
nguvu zako za kishetani” akasema Ernest
“ Sikiliza Ernest ,tayari nimekwisha
weka agano na mkuu Alberto kwamba
wewe ndiye utakayekuwa rais wa
Tanzania .Niliulizwa mara tatu kama
ninaliweza jukumu hilo la kukushawishi
ukubali kuwa rais nikasema ndiyo na hapo
likafanyika agano kati yangu na Alberto
mkuu kwamba nitakaposhindwa kutimiza
kile tulichokubaliana basi watoto wetu
wote watapotea.Kwa ufupi tu ni kwamba
watoto wetu nimewaweka dhamana na
endapo nitashindwa kufanya kile
nilichokiahidi yaani kukushawishi ukubali
kuwa rais wa Tanzania basi wote
watakufa”
“ Oh my God !!! akasema Ernest
akiwa amejishika kiuno akimtazama
mkewe kwa hasira
“ Suala hili halitaishia kwa watoto tu
bali kama utaendelea na ukaidi wako basi
itafuata zamu yako na mimi nitakuwa wa
mwisho.You will die Ernest.The whole
family will die.Kwa nini tufike huko
Ernest? Kwa nini tuwapoteze watoto wetu
wakati unao uwezo wa kuwaokoa.Just say
yes and our family will be saved.Ernest
kubali kuwa rais wa Tanzania ambayo ni
nafasi ya juu kabisa,ikubali heshima hii
kubwa na utakuwa mtu mkubwa mwenye
nguvu,utajulikana duniani kote,utajiri
wako utaongezeka maradufu.Kukubali
kwako kuwa rais haimaanishi kwamba
utakuwa mfuasi wa Alberto’s.Tutakuweka
katika nafasi ya juu kwa ajili ya kutusaidia
katika baadhi ya masuala yetu Fulani
Fulani.Tunataka Tanzania ipokee
mabadiliko na tunatakuhitaji sana
utusaidie mabadiliko haya yafanikiwe kwa
hiyo basi unapaswa kuanza kulitafakari
suala hili kwa mapana kwa manufaa yetu
na watoto wetu utakapokuwa tayari
utanitaarifu.
Ernest Mkasa akawasha sigara
nyingine akavuta mikupuo kadhaa
akamtazama Austin
"Hivyo ndivyo ilivyokuwa Austin
.Thats how my wife became a devil”
akasema Ernest
“ This is going to be hard than I
thought” akanong’ona Austin .Ernest
akamimina mvinyo katika glasi akanywa
na kusema
“ Nilimchukia sana Agatha na toka
siku ile sikuweza hata kulala naye kitanda
kimoja.Baada ya mwaka mmoja
akanikumbusha kama tayari nimefanya
maamuzi
kuhusu
lile
suala
aliloniambia.Hapo ugomvi ukaibuka
upya.Sikuwa tayari kwa jambo lile.Miezi
mitatu baadae watoto wetu wote watatu
wakiwa katika gari wakitokea Dodoma
katika sherehe ya mmoja wa marafiki zao
walipata ajali mbaya ya gari na wawili
wakapoteza maisha papo hapo ,mmoja
akawa
mahututi
akakimbizwa
hospitali.Tukiwa hospitali kufuatilia hali
ya mwanetu aliyekuwa mahututi ,Agatha
akiwa na uso mkavu kabisa akaniambia
kwamba vifo vya watoto wetu
 
SEHEMU YA 86



nimevisababisha mimi kwa kiburi
changu.Alinikumbusha agano alilolifanya
na hao wenzake na kwamba alishindwa
kulitimiza na hiyo ndiyo adhabu
yake.Aliniambia kwamba nina dakika
ishirini tu kufanya maamuzi ili nimuokoe
mtoto wetu aliyebaki.Nilikuwa na hasira
kali na wakati huo nilitamani nimkate
shingo nimmalize kabisa” Ernest
akanyamaza akainamisha kichwa na
baada ya muda akainua kichwa na kufuta
machozi na kusema
“ I’m sorry for this
Austin.Nimekumbuka mbali sana.Napatwa
na uchungu mkubwa nikiwambuka
wanangu.Anyway tuendelee na maongezi
yeu” akavuta mikupuo miwili ya sigara na
kuendelea
“ Pamoja na kuwapoteza watoto
wangu wawili lakini bado nilikuwa na
moyo mgumu sana kukubaliana na
Agatha.Baada ya dakika ishirini kama
alivyosema, mwanangu wa tatu akapoteza
maisha.Agatha akanieleza kwamba
nisipofanya maamuzi ndani ya dakika
thelathini
itakuwa
ni
zamu
yangu.Niliogopa sana na ikanilazimu
kukubali wanachokitaka .Hivyo ndivyo
ilivyokuwa hadi nikawa rais.Kuna mambo
mengine mengi yalitokea ikiwemo kifo cha
rais Ferdinand aliyefariki kwa ajali na
yote hii ikiwa ni mipango ya Alberto’s na
baada ya kifo chake ukafanyika uchaguzi
na mimi nikawa rais mpya.Austin hapa
nilipo nina kisasi kikubwa sana kwa
Alberto’s na muda mrefu nilipanga siku
moja lazima nilipize kisasi ila nilikosa mtu
wa kuungana naye katika mapambano
haya kwani wengi wa watu
wanaonizunguka ni wafuasi wa
Alberto’s.Kwa hiyo Austin naamini tayari
umekwisha pata picha halisi ya vita
tunayokwenda kuipigana.It’s not an easy
war.These
people
are
very
powerfull.Wameiteka sehemu kubwa ya
dunia na wamesimika utawala
wao.Wanataka kuitawala dunia .Kwa sasa
wamehamishia
nguvu
zao
Afrika.Wanataka bara lote la Afrika
lipepee bendera yao na tayari
wamekwisha anza kupata mafanikio
kwani kati ya nchi 54 za bara la Afrika
nchi 36 tayari tayari wamekwisha
fanikiwa kuingia na zilizobaki aidha ziko
katika mchakato au ushawishi
unaendelea.Austin hii ni jamii yenye
kumuabudu shetani na ndiyo maana
mambo yao yote ambayo wanataka
kuyahalalisha duniani ni yale
yanayokwenda kinyume na matakwa ya
Mungu.Kwa hiyo Austin vita tunayoipigana
ni kubwa . As far as God is on our side we’ll
win” akasema Ernest.Austin akamtazama
kwa muda kisha akasema
“ Mheshimiwa rais,ninawafahamu
Albertos.Ninafahamu nini wanakifanya
hivi sasa duniani kwa hiyo ninafahamu
ugumu wa vita tunayokwenda kupigana”
akasema Austin na kufumba macho kwa
sekunde kadhaa na kusema
“ Sijawahi kumueleza mtu yeyote
jambo hili na kwa mara ya kwanza leo
ninaufungua mdomo wangu na
kulitamka.”
“ Jambo gani hilo? Akaulzia Ernest
“ Niliugundua mpango wa siri wa
kutaka kumuua rais Ferdinand uliokuwa
umesukwa na watu walioko ndani ya
serikali ambao kama ulivyosema kuwa
ulikuwa ni mpango wa Alberto’s.Baada ya
kuugundua mpango huo nilianza harakati
 
SEHEMU YA 87



za kutaka kuzuia jambo hilo lisifanikiwe
na ndipo ulipofanyika mkakati wa
kuniua.Nilitaka sana kumuokoa rais
Ferdinand lakini sikuweza kwani
nilinusurika kufa Somalia na sikurejea
tena Tanzania na baadae rais Ferdinand
akafariki katika ajali.” Akanyamaza na
kumtazama Ernest
“ Mheshimiwa rais nitakulinda kwa
hiyo usihofu. walijaribu kuniua mara ya
kwanza wakashindwa na sasa ni zamu yao
kuishi kwa uoga.Tukishirikiana pamoja
tunaweza kabisa kuwashinda hawa
mashetani .Anyway tuweke kwanza
pembeni suala hilo tuongelee kuhusiana
na kazi ulizonikabidhi.Moja kati ya kazi
ulizonituma nimeikamilisha ambayo ni
kumtoa hospitali Dr Marcelo .Kazi ya pili
ni kuhusiana na Monica.Nimepanga
kuanza kuifanya kazi hiyo kesho .Ili
kujenga ukaribu na mazoea na Monica
itanilazimu nijihusishe katika mambo
anayoyapenda .Monica ni mtu anayejitoa
sana kwa jamii hasa kwa watoto na wazee
wasiojiweza .Nimeamua nipitie upande
huu ili kujenga ukaribu na Monica.Kwa
hiyo mheshimiwa rais I’m going to need
money,lots of money.Nahitaji kujenga
muonekano mzuri wenye hadhi ili Monica
anikubali kwa haraka”
“ Usijali kuhusu fedha
Austin,utapata kiasi chochote cha fedha
unachokihitaji ili mradi kazi yangu
ifanyike.Lakini kuna jambo moja nahitaji
kulifahamu toka kwako.Nikikutazama you
are very handsome.Muonekano wako
ukijumlisha na kiasi kikubwa cha fedha
nitakachokupatia
vinaweza
kumchanganya mwanamke yeyote .Nataka
kufahamu aina ya ukaribu unaotaka
kutengeneza na Monica.Are you going to
make her fall for you?
Austin akatabasamu na kusema
“ Usihofu mheshmiwa rais ,siwezi
kufanya jambo kama hilo.Niwapo kazini
huwa ninaielekeza akili yangu katika kazi
tu na si mambo mengine.I’m always
proffesional.Isitoshe tayari nina mchumba
na tunapendana sana”
“ Good.I’m glad to hear that.Austin
kama kuna chochote ambacho unakihitaji
tafadhali usisite kunieleza” akasema
Ernest
“ Ahsante mheshimiwa rais
,nashukuru sana nitakupa orodha ya
mahitaji yangu ila kuna jambo ambalo
nataka niliweke sawa kwako.Ni kuhusu
usalama wako.Unawamini walinzi wako?

Tena
umenikumbusha
Austin.Nilipanga kujadili nawe juu ya
suala hilo hilo la ulinzi wangu.Ninaweza
kusema kwamba sina ulinzi wa
uhakika.Ninasema hivyo kwa sababu kuna
kitu kimetokea leo muda mfupi kabla ya
kutoa hotuba yangu watu wawili
nisiowafahamu waliingia chumbani
kwangu tena wakiwa na bastora
zilizofungwa viwambo vya kuzuia sauti na
wakanionya kwamba nisithubutu
kuhutubia.Najua watu wale walitumwa na
Alberto’s ili kuniogopesha na
kunithibitishia kwamba wana nguvu
kubwa ya kuweza kufanya lolote muda
wowote
wautakao.Tukio
lile
limeniogopesha sana na kunifanya
nisiwaamini kabisa walinzi wangu ila
kuna walinzi wawili au watatu hivi ambao
ninaweza kuwaamini wale ambao
ninakuja nao hapa.Ukiacha hao mtu
 
SEHEMU YA 88


mwingine ninayemuamini ni mzee
Mukasha msaidizi wangu”
Maelezo yale ya Ernest yakamfanya
Austin atakafakari kwa muda halafu
akasema
“ Mheshimiwa rais You are not
safe.Wewe ndiye mwanga wa mapambano
haya kwa hiyo unahitaji ulinzi wa uhakika
.Kwa ulinzi huo ulio nao sasa hivi anything
can happen.You need to be guarded by the
people you trust ,the people I trust “
akasema Austin
“ Unashauri tufanye nini Austin?
Akauliza Ernest
“ Nitaunda kikosi cha kukulinda
badala ya walinzi wako wa sasa”
“ Hilo linaweza kuwa gumu sana
Austin kwa sababu ulinzi wa rais ni jambo
ambalo lina taratibu zake ambazo siwezi
kuzikiuka”
“ Wewe ni rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania kwa hiyo
utalifanya hilo liwezekane.Bila kufanya
hivyo watakuua mheshimiwa rais.Watu
nitakaowateua ni watu ninaowaamini na
wenye mafunzo na uwezo wa hali ya juu
mno na endapo utawapa nafasi hiyo basi
kwa pamoja tutashirikiana vizuri katika
vita hii .Mheshimiwa rais hatutakuwa
tunaonana mara kwa mara kwa hiyo
lazima tutafute namna ya kufanya
mawasiliano baina yetu kuwa rahisi.Watu
hao ambao nataka wakulinde ndio
watakaokuwa kiungo muhimu kati
yetu.Bila kufanya hivyo mheshmiwa rais
you are a dead man.Watakuua kama
walivyomuua rais Ferdinand.Kitu kingine
unachopaswa kukifanya kwa haraka ni
kuhakisha unaungwa mkono na jeshi kwa
hiyo unapaswa haraka sana kutengua
uteuzi wa mkuu wa majeshi na kuteua
mkuu mpya wa majeshi.Napendekeza
nafasi hiyo apewe Luteni jenerali Lameck
Msuba.Ninamfahamu vyema Lameck ni
mtu mtiifu na mzalendo wa kweli.Jeshi
likiwa chini yake basi hauna tena hofu ya
kufanyika
uasi.Mheshimiwa
rais
nafahamu ugumu wa hiki ninachokueleza
lakini ili tufanikiwe lazima hayo
niliyokwambia yafanyike” akasema
Austin.
“ Austin ninakubali ombi lako ila
niachie
nikatafakari
namna
nitakavyofanya ili kulitekeleza jambo
hilo.”
“ sawa mheshimiwa rais,kalitafakari
na utakapokuwa tayari utanijulisha”
akasema Ernest.Austin akamchukua
mheshimiwa rais wakaongozana kuelekea
katika
chumba
alimo
Dr
Marcelo.Akaufungua mlango wa chumba
taratibu na Dr Marcelo ambaye tayari
alikuwa usingizini akastuka na kufikicha
macho
“ Halow Marcelo.” Akasema Austin
“ Austin” akasema Marcelo akainuka
kitandani na kuketi
“ Marcelo samahani kwa kukuamsha
lakini nimekuletea mgeni”
“ hallow Macelo “ akasema Ernest na
kuvua kofia na miwani yake na kumfanya
Dr Marcelo apigwe na butwaa
“ Mr President !!! akasema Marcelo
kwa mshangao
“ Relax Marcelo.Unajisikiaje? akauliza
Ernest
“ Ninajisikia vizuri mheshimiwa
rais.Nimestuka sana kukuona hapa mzee”
akasema Marcelo
 
SEHEMU YA 89



Marcelo nimekuja kujua maendeleo
yako na kama uko salama.Mimi ndiye
niliyemtuma Austin akutoe kule hospitali
baada ya kuombwa kufanya hivyo na rais
wa Congo David Zumo”
“ David Zumo?!!... Akauliza Marcelo
kwa mshangao mkubwa.
“ Ndiyo.David Zumo aliniomba
nifanye kila niwezao nikuondoe pale
hospitali “ akajibu Ernest
“ Nimestuka sana kwani sifahamiani
na David Zumo na sijui amepataje taarifa
zangu.” Akasema Marcelo .Austin na
Ernest wakatazamana.
“ Imekuaje David akazifahamu
taarifa zangu kwamba kuna watu
wanataka kuniua? This is weird” akasema
Marcelo
“ Swali hilo ni swali ambalo
tunapaswa tukuulize wewe” akasema
Ernest
“ Mimi kama nilivyosema awali
kwamba sifahamiani kabisa na David
Zumo .Wakati anakupa maelekezo ya
kunitoa hospitali hakukueleza jambo
lingine lolote?
“ Hapana hakunieleza chochote.Yeye
alichoniomba nikutoe hospitali kuna watu
wanataka kukuua na hakutoa maelekezo
mengine.kwa hivi sasa tunasubiri
maelekezo toka kwake” akasema Ernest.
“ Ahsante sana mheshimiwa rais kwa
kufanikisha kunitoa pale hospitali ambako
ni kweli kama alivyokueleza David
,maisha yangu yalikuwa hatarini” akasema
Marcelo.
“ Ni nani wanaotaka kukuua
Marcelo? Akauliza Austin
“ Hii ni hadithi ndefu kidogo lakini
kwa ufupi wanaotaa kuniua ni rafiki zake
baba”
“ Rafiki za baba yako? Kwa nini?
Akauliza Austin.
Marcelo akatafakari kidogo na
kusema
“ Baba yangu Dr Richard alikuwa
daktari wa saratani ya damu.Yeye ndiye
aliyenishawishi na mimi nisomee kuhusu
saratani.Kabla ya kifo chake alinipa kitabu
fulani nikihifadhi.Pamoja na kitabu hicho
alinipa namba za simu za mtu ambaye
nilitakiwa nimpigie ili nipate maelekezo
kuhusiana na kitabu hicho .Alinionya
kuhusu rafiki zake Fulani watatu kwamba
nisiwe karibu nao na kwamba ni watu
hatari sana.Kitabu alichonipa baba
nilikihifadhi katika kasiki na sikuwahi
kukifungua na wala sijui kuna nini
kiliandikwamo.Hivi majuzi nikiwa kazini
watu waliingia chumbani kwangu
wakafungua kasiki na kuchukua kitabu
hicho.Nikiwa bado natafakari aliyefanya
kitendo kile nikazikumbuka namba za
simu nilizopewa na baba kuwa nipige kwa
ajili ya maelekezo kuhusu kile
kitabu.Nilipiga lakini simu ikapokelewa
na kukatwa na jioni ya siku hiyo
nikapigwa risasi na watu nisiowafahamu
waliokuwa
katika
pikipiki
mbili.Nilikimbizwa
hospitali
wakafanikiwa kuokoa uhai wangu.Nikiwa
pale hospitali nilimuona mmoja wa wale
rafiki zake baba ambao alinionya nikae
nao mbali nikajua tayari maisha yangu
yako hatarini”akasema Marcelo
“ Unasema kuna mtu aliingia
chumbani kwako akafungua kasiki na
kuchukua kitabu ulichopewa na baba yako
,unadhani kitabu hicho ni sababa ya wewe
kupigwa risasi? Akauliza Austin
 
SEHEMU YA 90



Ninahisi hivyo kwani tukio hilo
limetokea baada tu ya kitabu hicho
kutoweka” akajibu Marcelo
“ Unamfahamu mtu mwenye hizo
namba alizokupa baba yako ? akauliza
tena Austin
“ Hapana simfahamu”
Austin na Ernest wakatazamana
kisha Austin akasema
“ Suala hili linaonekana si suala
dogo.Ninasita kujiingiza huko kwa sababu
tayari kuna masuala mazito
yanayotukabili.Kwa kuwa tayari suala hili
liko katika mikono ya polisi basi hatuna
budi kuwaacha waendelee na uchunguzi”
akasema Austin
“ Uko sahihi Austin.Nitaweka mkazo
pia kwa jeshi la polisi wahakikishe
wanawasaka na kuwapata watu hao
waliotaka kukuua.Kwa sasa hadi hapo
tutakapopata maelekezo mengine toka
kwa David Zumo utaendelea kukaa hapa
pamoja na Austin.Hii ni sehemu salama
sana kwako kwa sasa.Utafuata yale yote
utakayoelekezwa na Austin”
“ Ahsante mheshimiwa rais.Mungu
awabariki sana” akasema Marcelo.Ernest
na Austin wakatoka mle chumbani
“ Suala la Dr Marcelo linaonekana ni
suala tata sana.David zumo ameingiaje
katika suala hili? Hicho kitabu alichopewa
na baba yake kina nini ndani yake?
Maswali haya yanalifanya jambo hili kuwa
gumu” akasema Ernest
“ Ni kweli mheshimiwa rais.Suala hili
linaoneana si suala jepesi.Ni suala pana
.Lazima kuna kitu kimejificha hapa na
ndiyo maana Marcelo anataka
kuuawa.Nahisi labda yawezekana ukawa
ni mtandao wa mambo haramu kama vile
madawa ya kulevya n.k Lakini hata mimi
uhusika wa David Zumo katika jambo hili
unanila akili sana.Anamfahamu Marcelo
lakini
Marcelo
hamfahamu
David.Inakanganya kidogo.Mheshimiwa
rais naomba tusiumize vichwa vyetu kwa
suala hili.Tuwaachie jeshi la polisi
watafanya uchunguzi wao na kupata
ukweli” akasema Austin wakaagana Ernest
akaondoka.
********************
Wakati rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ernest Mkasa
akiondoka katika nyumba anayoishi
Austin,ukumbi mmoja mdogo wenye
kuweza kuchukua watu zaidi ya hamsini
uliopo ndani ya jumba moja kubwa la
kifahari lililoko kandoni mwa bahari
,kikao kizito kilikuwa kinafanyika
kilichowakutanisha watu zaidi ya
arobaini.Katika ukumbi huo kulikuwa na
luninga nne kubwa ambazo kulikuwa na
watu wakionekana waliokuwa nje ya nchi
wakiunganana wenzao wa hapa Tanzania
katika kikao kile.Kikao kile kilihudhuriwa
na makamu wa rais wa Tanzania,waziri
mkuu aliyevuliwa madaraka pamoja na
baadhi ya viongozi na wafanya biashara
wakubwa ambao ni wajumbe wa kamati
kuu ya Alberto’s Tanzania.
“ Kabla ya kiongozi wa kikao
kuwasili kulikuwa na minong’ono ya hapa
na pale na wajumbe wakijadiliana hili na
lile.Kiongozi wa kikao kile aliyevaa suti
nyeusi mfanya biashara tajiri mtanzania
mwenye asili ya Ghana,Obi Ochukwu
akatokea akiwa ameongozana na wajumbe
 
maana wadau mnaona kama nafanya kusudi harafu sie wengine mishe zetu sio zakutulia sehemu moja nawezanikawa online lkn nipo mbali kabisa na home au safarini hivyo bora tuweke ratiba ya kihivi iwe week end mpaka week end ikitokea bahati nabwaga kabla hata ya week end katikati ya wiki.ila mwisho wa week ndio naweka ya kutosha kusoma week nzima mwaonaje
vyote sawa lege
 
Back
Top Bottom