SEHEM YA PILI
Sauti ya ndege mkubwa aliyekuwa
akilia karibu na dirisha ilimstua Monica
toka katika usingizi .Huku akionekana
kukerwa na sauti ile iliyomstua usingizini
akainuka na kukaa.
“ oh no ! Huyu ndege ameniharibia
ndoto yangu tamu..” akawaza
Monica,akainuka
kitandani
na
kujinyoosha halafu akatazama saa ndogo
yenye nakshi za dhahabu iliyoko mezani
“ Ni saa mbili na robo sasa,muda
umekwenda sana natakiwa niwahi ofisini
leo nina miadi ya kuonana na Daniel
ambaye alisema atamleta rafiki yake
anayehitaji kuchangia katika mbio
tunazoziandaa.Nashukuru wadau wengi
wanazidi kujitokeza na kuniunga mkono
katika mpango wangu wa kujenga shule ya
watoto wenye mahitaji maalum.Nina
hakika jambo hili litafanikiwa kwani
limepata mwitikio mzuri kwa watu wengi
matajiri kwa wasio na uwezo.” Akawaza
huku akivaa nguo zake za mazoezi na
kujiandaa kwa ajili ya kufanya zoezi la
asubuhi.Ni kawaida yake kila aamkapo
asubuhi kutembea kwa miguu kilometa
kadhaa kabla ya kwenda ofisini.Alipokuwa
tayari akatoka na kwenda kwanza
kuwasalimu watumishi wake wa ndani
waliokuwa katika harakati zao za kawaida
za asubuhi akaongea nao mawili matatu
na kutoa maelekezo kadhaa kisha akatoka
nje na kusalimiana na kijana mtunza
mazingira na mwisho akawajulia hali
walinzi wake wanaolinda nyumba yake
halafu akaanza zoezi lake la
kutembea.Haya ndiyo maisha ya kila siku
ya Monica,kila asubuhi kabla hajafanya
chochote lazima kwanza ahakikishe
amewasalimu watu wote anaoishi nao
nyumbani kwake na kujua hali zao na
ndipo huendelea na ratiba nyingine za
siku.
“ Sikufanya makosa kuamua
kuhamia huku.Ni kuzuri ,kuna hewa safi
na utulivu wa kutosha.Japokuwa ni mbali
na mji lakini hiyo hainipi taabu
ninachohitaji mimi ni kuishi sehemu
tulivu kama hii kusikokuwa na makelele
wala uchafuzi wa hewa.Huku ninapata
hewa safi toka baharini tofauti na mjini”
akawaza Monica wakati akipanda kilima
kidogo.
“ Hata hivyo eneo hili bado jipya na
lina changamoto nyingi,miundo mbinu
bado si mizuri,hakuna maji ya
uhakika,umeme barabara n.k.Natakiwa
kukutana na wakaazi wa eneo hili na kwa
pamoja tujadili namna ya kuzitafutia
ufumbuzi
changamoto
zinazowakabili.Wanahitaji huduma za
afya,shule n.k so I must help them.I want
to change this place.Kwa sasa
panaonekana ni kijijini lakini ndani ya
miaka michache ijayo patakimbiliwa na
kila mtu .Nina ndoto ya kulifanya eneo hili
kuwa mji mzuri sana na wa kupendeza”
akawaza Monica akiendelea na mazoezi
yake
Alirejea nyumbani na moja kwa moja
akaelekea chumbani kwake akaoga na
kujiandaa kwa ajili ya kuanza shughuli
zake za siku.Alipomaliza kujiremba
akajitazama katika kioo na kutabasamu
halafu akawasha simu zake.Jumbe nyingi
zikaingia mfululizo akakaa kitandani na
kuanza kuzipitia kwa haraka haraka na
mojawapo ya jumbe hizo ulitoka kwa baba
yake ambao ulikuwa na neno moja tu
“Congraturations
” Monica akatabasamu
“ Baba ananipongeza kwa jambo
gani? Kuna chochote nimekifanya
kinachostahili pongezi? Ngoja nimpigie
niongee naye anieleze sababu ya
kunipongeza” akawaza Monica na
kumpigia simu baba yake.
“ Hallow Monica” akasema mzee
Benedict Mwamsole baada ya kupokea
simu ya Monica
“ Goodmorning dady”
“
Good
morning
my
sweetie,umeamkaje?
“ Nimeamka salama dady,vipi nyie
huko wote wazima?
“ Sisi sote wazima wa afya,hofu
kwako “
“ Mimi pia mzima dady.Nimepata
ujumbe wako sasa hivi” akasema Monica
huku akitabasamu
“ Nimekutafuta sana jana usiku
lakini simu yako haikuwa ikipatikana
ndiyo maana nikakutumia ujumbe
ule.Bado hujaacha tabia yako ya kuzima