QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 97

Monica cha kumueleza kuhusiana na ombi
la David Zumo la kutaka kumuoa.Naomba
Monica akubali kwani inaweza ikaleta
amani kidogo kwa Ben na kuupoza upepo
huu mbaya unaoanza kuvuma.Endapo
akikataa basi mambo yanaweza kuwa
magumu sana kwa upande wangu.”
Akawaza Janet huku akivaa nguo zake na
yeye akaondoka
“ Dah ! bado siamini maneno
aliyonieleza Janet kuwa Monica ni
mwanangu.Lakini Janet hawezi kusema
uongo kwa jambo kubwa kama hili.Lazima
kweli Monica atakuwa ni
mwanangu.Nilikwisha kata tamaa kabisa
ya kumpata mrithi wangu lakini hatimaye
nimempata.Nina furaha iliyopitiliza.”
Akawaza Ernest akiwa katika gari lake
akirejea ikulu
“ Hata hivyo kuna mambo ambayo
natakiwa kuyafanya.Kwanza kabisa
nataka nipate uhakika kuwa kweli Monica
ni mwanangu kwa kufanya kwa siri
kipimo cha vinasaba.Jambo hili ni la
muhimu na linatakiwa kufanywa kwa siri
kubwa sana.Baada ya kupata uhakika
kama kweli Monica ni mwanangu kuna
suala la pili kubwa ambalo limekuwa
linaniumiza kichwa toka nilipolisikia ni
hili la kwamba David Zumo anataka
kumuoa Monica.Hili ni jambo ambalo
silikubali kabisa kwani japokuwa wote ni
marais lakini sina maelewano mazuri na
David Zumo kwa hiyo sitaki kabisa mtu
huyu amuoe mwanangu Monica.Nitafanya
kila linalowezekana hadi jambo hili
lishindikane.Kuhusu Ben huyu hawezi
kuniumiza kichwa nitatafuta namna ya
kumdhibiti ” Akaendelea kuwaza Ernest
Alifika ikulu akaoga na kubadili
nguo kisha akamuita Mukasha mmoja wa
wasaidizi wake anayemuamini sana .
“ Mukasha kuna jambo ninataka
unisaidie”
“ Ndiyo mzee” akajibu Mukasha kwa
adabu
“ Nahitaji kumpata kijana moja
mahiri sana katika mambo ya uchunguzi
ambaye ninaweza kumuamini na
kumtumia katika kazi zangu binafsi za
kiuchunguzi na ambaye ni mkweli na
hatatoa
siri
za
mambo
nitakayomtuma.Unaweza
kunitafutia
kijana huyo miongoni mwa vijana
tulionao? Akauliza mheshimiwa rais
Ernest Mkasa.Mzee Mukasha akainama
akakuna kichwa kidogo akafikiri halafu
akasema
“ Mheshimiwa rais sina hakika kama
unaweza ukakubaliana nami kwa hili
nitakalokwambia” akasema Mukasha
“ Mukasa nieleze chochote
nitakusikiliza .” Akasema Ernest
“ Mheshmiwa rais kuna jambo
ambalo sina hakika kama unalifahamu na
kama unalifahamu basi hauna taarifa za
kutosha kuhusiana nalo”
“ Ni jambo gani hilo Mukasha?
Nieleze usihofu tafadhali.Najua kuna
mambo mengi ambayo siyafahamu na
ninafichwa ila wewe kama mtu wangu wa
karibu kama kuna jambo unalifahamu
naomba usinifiche tafadhali.Nieleze
ukweli wote”
“ Sawa mheshimiwa rais” akasema
Mukasha na kukohoa kidogo halafu
akasema
“ Mwaka mmoja kabla haujaingia
madarakani raia saba wa Tanzania
madereva wa malori yaliyobeba chakula
kupeleka nchni Somalia walitekwa nyara
 
SEHEMU YA 98


na wanamgambo wa kikundi cha
Alshabaab.Wanamgambo hao waliitaka
serikali ya Tanzania itoe kiasi kikubwa
cha fedha ili wawaachie watu hao lakini
serikali ya Tanzania haikuwa
tayari.Walitoa muda ambao kama
Tanzania ingeshindwa kulipa kiasi hicho
cha fedha basi wangewaua madereva hao
.Rais aliyekuwa madarakani wakati huo
hakuwa tayari kukubaliana na matakwa
ya wanamgambo hao hivyo akaunda
kikosi kidogo cha watu ambao aliwatuma
kwenda Mogadishu kuwakomboa
madereva hao.” Akasema Mukasha
“ Ninalifahamu jambo hilo” akasema
rais
“ Nakubali mheshimiwa rais hili ni
jambo linalofahamika na watu wengi
lakini kuna jambo ambalo wengi
hawalifahamu kuhusiana na kikos hicho
cha wanajeshi ishirini na sita kutoka
katika kikosi cha kupambana na ugaidi
kilichotumwa kwenda kuwarudisha
nyumbani watanzania waliotekwa na
Alshabaab.”
“ Kulikuwa na jambo gani Mukasha?
Akauliza Ernest
“ Kulikuwa na mtu mmoja kutoka
idara ya ujasusi ambaye ndiye
aliyewaongoza wanajeshi hao kufika
mahala walipokuwa wamefichwa
madereva hao waliotekwa.Kijana huyo
anaitwa Austin January lakini jina lake
halijatajwa katika orodha ya watu
waliokuwemo katika kikosi hicho.”
“ Austin January? Akauliza Ernest
“ Ndiyo mzee.” Akajibu Mukasha na
baada ya muda akaendelea
“ Kikosi kile kilichotumwa
kilifanikiwa kupambana na wanamgambo
wa Alshabaab na kufanikiwa kuwakomboa
mateka na kuwarudisha nyumbani lakini
Austin January hakurejea tena nyumbani.”
“ Nini kilitokea? Alikufa? Akauliza
Ernest
“ Ilitolewa taarifa fupi tu kwamba
Austin alipotea katika mapambano na
hawakujua aliko . Walihitimisha kwamba
kuna uwezekano mkubwa atakuwa
aliuawa.Lakini ukweli wa jambo hili uko
hivi,Austin hakufa kama ilivyodaiwa bali
wakati wakiendelea na mapambano dhidi
ya wanamgambo alipigwa risasi na mmoja
wa wanajeshi wa Tanzania makusudi
kabisa kwa lengo la kumuua na
akatelekezwa hapo akiwa hana
fahamu.Alipopata fahamu alijikuta akiwa
katika kambi ya wanamgambo wa
Alshabaab ambao walimtibu na alipopona
walihitaji kulipwa fedha nyingi sana ili
wamuachie.Austin alifahamu kabisa
kwamba alipigwa risasi makusudi hivyo
hakutaka tena msaada wowote kutoka
serikali ya Tanzania .Aliyemsaidia
kumkomboa kutoka kwa mikono ya
Alshabaab kwa kulipa fedha nyingi sana ni
baba wa mchumba wake mfanya biashara
tajiri ambaye alilipa kiasi cha fedha
kilichokuwa kinahitajika na Austin akawa
huru.Hakurejea tena Tanzania na kwa
sasa anaishi nchini Afrika kusini ambako
ameachana kabisa na mambo mengine
yote na anafanya kazi ya kusimamia
miradi ya baba mkwe wake.Ana maisha
mazuri hivi sasa na anatarajia kufunga
ndoa hivi karibuni na mpenzi wake
Marie.”
“ Oh my God !! Umezipata wapi
taarifa hizi? Akauliza Ernest
“ Nina ukaribu na huyo tajiri ambaye
alimsaidia Austin kutoka mikononi mwa
 
SEHEMU YA 99

Alshabaab.Sababu ya kutaka kuuawa
mpaka leo hakuna anayeifahamu imebaki
ni siri yake Austin lakini kuna hisia
kwamba kuna watu ndani ya serikali
ambao walitaka kumuua kwani
inaonekana kuna suala ambalo
aliligundua linalowahusisha watu
wakubwa serikalini na ndiyo maana
akatakiwa kuuawa .Ni kijana mtiifu sana
,anayejituma na asiyependa kupindisha
ukweli.Kama kweli unahitaji kijana
mwaminifu ambaye unaweza kumtuma
kufanya kazi zako binafsi basi
ninakushauri kumtafuta Austin.Tunao
vijana wengi wazuri hapa katika idara
yetu ya usalama wa taifa ambao wanaweza
wakafanya kazi vizuri lakini hakuna kama
Austin.” Akasema Mukasha .Ukimya
ukatanda mle chumbani baada ya muda
Ernest akasimama akaenda kuegemea
kabati la vitabu akazama mawazoni na
baada ya muda akasema
“ Kwa maelezo haya mafupi
uliyonipa nimepata picha ya haraka
haraka kwamba Austin ni mtu sahihi
ninayemtaka lakini ugumu unakuja
namna ya kumpata.”
“ Mheshimiwa rais ili uweze
kumpata Austin itakubidi kwanza
uzungumze na baba mkwe wake.Ni mtu
wangu wa karibu nitamtafuta ili uweze
kuzungumza naye”
“ Jitahidi ili niweze kuzungumza
naye jioni ya leo nijaribu kumshawishi
kama anaweza kukubali kumruhusu
Austin aje kunifanyia kazi hata kama ni
kwa muda mfupi na niko tayari kumlipa
kiasi chochote cha fedha atakachohitaji”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais naomba
nikuweke wazi tu kuwa suala hili haliwezi
kuwa rahisi kwani kwa sasa Austin
ameachana kabisa na mambo haya ya
ujasusi na anajishughulisha na
biashara.Sina hakika kama atakubali ombi
lako” akasema Mukasha
“ Nitaongea vizuri na baba mkwe
wake na nina hakika yeye akimwambia
jambo hawezi akapinga.Nitatumia kila
aina ya ushawishi hadi Austin akubali
kuna kufanya kazi yangu.” Akasema
Ernest.
 
SEHENU YA 100

Ilikuwa ni siku ndefu sana kwa
Monica.Alizunguka sehemu mbali mbali na
Daniel akiwa na lengo la kutuliza kichwa
chake kutokana na mambo mengi
yaliyokuwa yanamsumbua na kubwa
likiwa ni suala la Dr Marcelo.
Saa kumi na mbili za jioni baada ya
kutoka hospitali kumuona Dr Marcelo
alirejea nyumbani kwao ambako alikuwa
na maongezi na wazazi wake usiku
huo.Aliekea moja kwa moja chumbani
kwake akaoga na kujiweka tayari kwa ajili
ya kukutana na wazazi wake.

Siku
imekuwa
ndefu
sana,namshukuru Daniel kwa kujitolea
kuungana nami siku ya leo na siku yangu
imekwenda vizuri.Nashukuru vile vile Dr
Marcelo naye anaendelea vizuri japokuwa
mpaka sasa hajaweza kuzungumza lakini
hali yake inatia matumaini .Namuombea
Mungu aweze kupona na wale wote
waliofanya kitendo kile cha kinyama
wakamatwe na kufikishwa mbele ya
sheria lakini hata hivyo bado kuna
maswali mengi ambayo ningependa
kumuuliza Dr Marcelo pindi atakapoanza
kuongea.Kuna mambo ambayo nahitaji
kuyafahamu kutoka kwake” akawaza
Monica akainuka na kutoka chumbani
kwake akaelekea sebuleni kwa wazazi
wake.
“ Monica,karibu sana..” akasema
mzee Benedict aliyekuwa amekaa sebuleni
akisoma gazeti
“ Ahsante baba,umeshindaje leo?
Akauliza
“ Nimeshinda salama Monica.Vipi
rafiki yako anaendeleaje? Akauliza mzee
Benedict
“ Anaendelea vizuri.Hali yake ni
tofauti na jana japokuwa bado hajaanza
kuzungumza
lakini
madakatari
wametuhakikisia kwamba atapona na
atarejea katika hali yake ya kawaida”
akasema Monica
“ Mungu atamsaidia atapona”
akasema mzee Benedict
“ Where is mother?
“ Bado hajarudi si unajua mama yako
huwa ana shughuli nyingi “ akasema mzee
Ben na mara simu yake ikaita .Akatazama
mpigaji halafu akainuka akasogea
pembeni akaipokea
“ hallow Gordon” akasema mzee
Benedict
“ Mzee nimekupigia kukupa majibu
ya ile kazi uliyonituma” akasema mtu wa
upande wa pili ambaye mzee benedict
alimuita kwa jina la Gordon.
“ Good..Tel me the good news.....”
akasema mzee Benedict na kulazimika
kugeuka baada ya kusikia sauti ya mke
wake akisalimiana na Monica baada ya
kurejea.
“ Mzee nimemfuatilia mama kama
ulivyonielekeza .Kwanza alikwenda ofisini
kwake halafu akatoka akaelekea saluni
akatumia kama dakika arobaini na tano
kisha akaondoka na kuelekea katika duka
la vipodozi .Alipotoka hapo akaelekea
katika kiwanda cha nguo ,ambako
alitumia kama nusu saa hivi halafu
akatoka na kuelekea White Rhino
hotel.Pale aliingia katika ofisi ya meneja
wa hoteli akatumia kama dakika kumi
halafu akatoka na kuelekea katika
presidential suit namba tano akaingia mle
na baadae rais aliwasili na akaelekea pia
katika chumba kile kile alichokuwamo
mama Janet.Walikaa mle kwa muda wa
zaidi ya nusu saa na kisha rais
akatoka.Baada ya dakika kumi toka rais
atoke mama Janet naye akatoka akaelekea
ofisini kwake ambako amekaa hadi jioni
hii na akatoka hakupita tena sehemu
nyingine yoyote akarejea moja kwa moja
nyumbani .Nimemuona akiingia ndani
ndipo nilipoamua kukupigia na kukujlisha
kuhusu mizunguko yote ya mama Janet
 
SEHEMU YA 101


kwa siku ya leo” akasema Gordon.Mzee
Benedict akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Gordon ahsante sana .Umefanya
kazi nzuri .Naomba uendelee kumfuatilia
kwa wiki mbili zaidi na kila siku nataka
unipe majibu “ akasema mzee Benedict na
kukata simu akageuka akamtazama mke
wake aliyekuwa ameketi sofani akiongea
na Monica
“ I knew it.Nilijua tu kwamba lazima
watakuwa wanakutana.Na leo nina hakika
walikutana kujadiliana kuhusiana na
suala hili la Monica.Sasa nimeanza kupata
picha kumbe siku hizi zote Janet amekuwa
akinizunguka.Amekuwa na mahusiano ya
siri na Ernest mkasa.I swear I’m going to
destroy them both lakini kabla ya kufanya
chochote natakiwa kwanza kukusanya
ushahidi wa kutosha .Ngoja niendelee
kumchunguza Jane kwa wiki mbili zaidi
ninaamini kuna mambo mengine mengi
ambayo ninaweza kuyafahamu .” akawaza
Benedict na kurejea sebuleni .Baada ya
kuoga Janet akaungana na mumewe na
Monica wakapata chakula kisha wakaenda
kuketi barazani kwa ajili ya maongezi.
“ Monica najua umechoka sana kwa
mizunguko ya siku kwa hiyo naomba
nisichukue muda wako mwingi nataka
niende moja kwa moja katika lile ambalo
tumekuitia jioni ya leo.” Akaanzisha
mazungumzo mzee Benedict

Kwanza
kabisa
napenda
kukushukuru kwa kutukutanisha na mtu
mkubwa sana afrika na duniani rais David
Zumo.Ni mtu mzuri na ana moyo wa
kusaidia.Jana nimeongea naye mambo
mengi sana na ameniahidi mambo mengi
makubwa na mojawapo ikiwa kuniinua
hadi kufikia kiwango cha kuweza kuingia
katika kikao cha mabilionea mia moja wa
dunia .Hili si jambo dogo lakini kwa David
Zumo linawezekana na ameahidi
kuhakikisha linafanikiwa.” Akasema
Benedict
“ That’s good news.David ni mtu
mwenye moyo wa ajabu sana.Anaonekana
kuvutiwa mno na familia yetu.Tuna bahati
sana ya kuwa na ukaribu wa ghafla wa mtu
kama huyu.Baba hii ni fursa ambayo
hutakiwi kuiacha.Itumie vyema” akasema
Monica
“ Usemalo ni la kweli Monica familia
yetu imekuwa na bahati sana kwa kuwa na
ukaribu na David Zumo. Ni fursa ambao
tunatakiwa kuitumia kwani kuwa na
ukaribu na mtu mkubwa kama huyu si
suala dogo” akasema mzee Benedict halafu
ukapita ukimya mfupi
“ Monica kama nilivyokueleza kuwa
jana nimeongea mambo mengi na David
Zumo lakini miongoni mwa mengi
tuliyoongea kuna jambo kubwa “ akasema
Ben na kunyamaza kidogo kisha
akaendelea
“ David Zumo amevutiwa sana
nawe.Amekiri kwamba hajawahi kuona
mwanamke aliyemgusa mtima wake kama
wewe hivyo ameamua kuweka wazi hisia
zake kuwa anakupenda sana na anataka
kukuoa”
“ Baba !! akasema Monica kwa
mshangao
na
kusimama.Ni
wazi
alistushwa sana na kauli ile toka kwa baba
yake
“ Monica najua umestushwa sana na
kauli hii lakini .....”
“ Hakuna lakini..how could you do
this to me father? Akauliza Monica
 
SEHEMU YA 102


Monica
tafadhali
naomba
unisikilize “ akasema bi Janet akainuka na
kumshika mkono Monica akamketisha
chini.
“ Monica najua kauli hii aliyoisema
baba yako imekustua sana kwani si
taratibu zetu sisi watanzania jambo kama
hili kutamkwa namna hii.Masuala kama
haya ya mtu kumpenda Fulani na kufikiria
hata kumuoa hayajazoeleka kupitia kwa
wazazi bali muhusika mwenyewe kama
amemuona binti akampenda humfuata
akaongea
naye
wakakubaliana
wakaanzisha urafiki na baadae taratibu za
uchumba huanza na mwisho huwa ni ndoa
na hizo ndizo taratibu zetu tulizozizoea”
“ Exactly..Hata mimi ninafahamu
hivyo.Hata kama David Zumo anadai
kwamba ananipenda alipaswa kuongea
nami moja kwa moja na si kwa kuwatumia
ninyi kwani mwenye maamuzi ya mwisho
kama nikubali au nikatae ni mimi.!!
Akasema Monica kwa sauti ya juu
kidogo.Ben na mkewe wakabaki kimya
wakimtazama.Baada ya sekunde kadhaa
za ukimya Monica akasema
“ I’m sorry,sikupaswa kupandisha
sauti namna ile ni kutokana na mstuko
nilioupata.” Akasema Monica
“ Monica utatusamehe sana kwa
jambo hili lakini anachokisema baba yako
ni kukufikishia tu maneno aliyoyatamka
David zumo ambayo sisi baada ya
kuyatafakari tumeona ni jambo zuri
tu.Kwa kifupi ni kwamba David Zumo
hajaamua kutumia zile njia zetu za
kawaida
labda
kwa
ugeni
na
kutokufahamu taratibu zetu lakini bado
hakijaharibika kitu kwa kuamua
kutueleza sisi kile kilichopo moyoni
mwake.Ametuweka
wazi
kwamba
anakupenda,na lengo lake kubwa ni
kutaka kukuoa.Kwa muda mrefu sasa
tumekuwa
tunasubiri
siku
utakayotuambia kwamba tayari umepata
mchumba kwani umri unazidi kwenda na
hatujapewa taarifa zozote lakini baada ya
David Zumo kujitokeza tumeona ni
mpango wa Mungu kwani mwanaume
mwenye
vigezo
ambayo
wote
tunavihitaji.Monica mwanangu David
Zumo ni mwanaume ambaye kila
mwanamke anaota kuwa naye.Japokuwa
hatumfahamu undani wake lakini ni mtu
ambaye ukikaa naye dakika chache
unamfahamu ni mtu wa namna gani.Ni
mpole,mnyenyekevu,si mtu mwenye
kujikweza licha ya utajiri alionao,ni
mpenda watu ana moyo wa kusaidia na
sifa nyingine kede kede. Sisi kwa upande
wetu tumeona huyu ni mtu ambaye
anakufaa sana Monica.Vil......” Monica
hakumpa nafasi mama yake aendelee
akaingilia kati
“ Mama tafadhali naomba usiendelee
zaidi
nimekwisha
kusikia
na
kukuelewa.Nimelisikia ombi la David
Zumo .Ninamfahamu David na japokuwa
nimefahamiana naye kwa siku mbili tu
naweza kusema he’s a good man .Pamoja
na hayo siwezi kutamka chochote kwa
usiku huu kwamba ombi lake nimelipokea
ama vipi .Mimi pia nina mipango ya
maisha yangu kwa hiyo nipeni nafasi ya
kutosha kuweza kulitafakari jambo hili
kwa kina kabla sijatamka chochote. “
akasema Monica
“ Lakini Monica hakuna ubaya kama
tukilijadili suala hili kwa pamoja kwa
sababu ni suala lenye manufaa kwetu
 
SEHEMU YA 103

sote.Sisi kama wazazi siku zote ni jukumu
letu
kuona
mwanetu
unampata
mwanaume bora ambaye unaweza ukaishi
naye bila matatizo na si bora mwanaume
na ndiyo maana baada ya David Zumo
kutoa yake ya moyoni tumeona ni mtu
ambaye anakufaa na anaifaa familia yetu.”
Akasema mzee Ben
“ Kwa kuongezea hilo alilolisema
baba yako,endapo utachagua kuolewa na
David Zumo utaingia katika ulimwengu
mwingine
kabisa
ulimwengu
wa
mabilionea.Utajiri wote wa David Zumo
utaumiliki wewe pale utakapomzalia
mtoto ambaye atakuwa mrithi wa mali
zake .Monica hii ni fursa kubwa
imejitokeza katika maisha yako ambayo
hutakiwi kuiacha.Mungu amekufungulia
milango ya Baraka zake kwa hiyo
unatakiwa uzitumie vyema fursa zote
unazoletewa.” Akasema bi Janet
“ Monica usisahau vile vile” akasema
Ben
“ wewe ni mtu ambaye umejitolea
kuihudumia jamii na una mipango mingi
kama huu wa kujenga shule ya watoto
walemavu,nafahamu una mpango pia wa
kujenga vituo vya kulelea wazee
wasiojiweza katika kila mkoa na mambo
mengine mengi lakini yote haya yanahitaji
fedha nyingi ambazo upatikanaji wake
unaweza kuchukua miaka mingi na
pengine malengo yako yasifanikiwe.Lakini
utakapochagua kuolewa na David Zumo
kila kitu ambacho umekuwa unakiota
kukifanya kitafanikiwa kwa sababu kile ni
kisima cha fedha.Utajenga mashule,vituo
vya
wazee
na
kila
unachokihitaji.Utajulikana dunia nzima na
utasaidia si Tanzania tu bali hata jamii
nyingine zenye uhitaji duniani.Monica hii
ni fursa ambayo unatakiwa uitumie”
akasema mzee Ben .Monica akawatazama
na kusema
“ Wazee wangu nimewasikia na
kuwaelewa yale yote mliyoniamba lakini
naona wote mmeegemea katika suala
moja tu la utajiri wa David Zumo.Kila
mnapoongea hamuachi kutaja utajiri na
fedha za David.Kama nikiamua kuolewa
na David si kwa sababu ya fedha bali moyo
wangu umenituma hivyo kwa hiyo hakuna
haja ya kujaribu kunishawishi kwa
kutumia kigezo cha fedha.Ni watu wangapi
ambao wamekimbilia kuolewa na watu
matajiri kwa kufuata pesa na mali lakini
wameishia kulia kila uchao? Hata ulalie
godoro la fedha lakini kama hampendani
kwa dhati ya mioyo yenu itakuwa kazi
bure kwani katu hamtakuwa na furaha
katika maisha yenu.Kwa hiyo wazee
wangu mimi nimewasikia na kama
nilivyosema naombeni mnipe muda wa
kulitafakari hili suala na nitawapa jibu
kwamba nimekubali ama vipi” akasema
Monica
“ Usijali Monica jipe muda ulitafakari
jambo hili kwa undani na uchambue faida
zake na hasara kama zipo halafu utatupa
jibu lakini sisi kama wazazi hatuna tatizo
lolote na jambo hili tumelipa Baraka zetu
kwani lina faida kwetu na kwako pia kwa
hiyo kila kitu tunakuachia wewe.”
Akasema mzee Benedict kisha akainuka
akaelekea chumbani kwake na kuwaacha
Monica na mama yake
“ Mama what you are trying to do is
unfair..Kwa nini lakini mnataka kufanya
kitu kama hiki? Kwa nini mmekubaliana
na mtu bila kwanza kukaa na mmi
mkanisikia na mimi nina mawazo na
 
SEHEMU YA 104

mipango ipi? Kwa mara ya kwanza
napenda
kuwaambia
kwamba
hamjanitendea haki.Haya ni maisha yangu
na mimi ndiye ninayechagua nani niwe
naye nani atanifaa na siangalii kama ni
tajiri au masikini bali ninachoangalia
mimi ni mapenzi ya kweli.Ninyi
mmeangalia upande mmoja tu wa utajiri
na ndiyo maana mmekubali kirahisi ombi
la David na japokuwa hamjanieleza nina
hakika
lazima
mtakuwa
mmemuhakikishia David kwamba jambo
hili
linawezekana
na
mumempa
matumaini makubwa kwamba ombi lake
lazima litakubaliwa.Kwa nini mmenifunga
mikono namna hii? Kweli mama
hamjanitendea haki” akasema Monica na
kuinama chini
“ Monica naomba usikwazike
mwanangu kwa jambo hili.Sisi hatujaamua
kitu chochote bali tumekufikishia ujumbe
tu na mwamuzi wa yote ni wewe.Sisi
hatuna maamuzi yoyote juu ya maisha
yako lakini pale tunapoona tunahitaji
kutoa ushauri wetu basi kama wazazi
lazima tufanye hivyo.Kwa hiyo Monica
usihuzunike na kudhani labda sisi
tunakupangia maisha yako lakini wewe
ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu
hatima ya maisha yako” akasema Janet
“ Lakini mama kwa namna jambo
hili mlivyoliweka ni wazi kwamba tayari
mmekwisha amua kwamba niolewe na
David Zumo.Mmeweka msisitizo mkubwa
sana kwa jambo hili kwa sababu
amewaahidi kuwasaidia kiuchumi na
kuwa matajiri wakubwa duniani.Thats not
fair at all” akasema Monica
“ Monica sisi kama wazazi siku zote
huwa tunahitaji wanetu waishi maisha
mazuri na ndiyo maana hatulali ili
kuhakikisha tunawajengea watoto maisha
yaliyo bora na yenye furaha.Sisi
hatujakulazimisha kuolewa na David
Zumo lakini kwa mtazamo wetu tumeona
David Zumo ni mtu ambaye anaweza
akakufaa sana kutokana na sifa
alizonazo.Miaka inazidi kwenda Monica na
hadi sasa bado hujatuletea mchumba
unataka kuolewa lini mwanangu? Unataka
ufunge ndoa wakati sisi tumekwisha
fariki? Huu ni wakati wako mzuri sana wa
kuingia katika maisha ya ndoa na kwa
kuwa amejitokeza mwanaume ambaye sisi
tunaona anakufaa basi usiiache nafasi
hii.Kila mwanamke katika hii dunia
anaota kuolewa na mwanaume bora
mwenye uwezo anayeweza kumtunza na
kwako ametokea mwanaume wa aina hiyo
ambaye ni tajiri mkubwa wa afrika kwa
nini basi umuache? Mimi kama mama
yako nakushauri Monica kama bado huna
mchumba hadi sasa basi David anakufaa
sana.Hata kama unahisi humpendi kwa
sasa lakini ukiwa naye utajifunza
kumpenda
na
utafurahia
kuwa
naye.Achana na hayo mambo ya moyo
ambayo yamekuwa yakitamkwa kila siku
kwamba sijui moyo umependa ni uongo
mtupu zama zimebadilika na siku hizi
wengi wanaangalia sana kutimiza ndoto
zao na mengine yote yatakuja huko huko
mbele ya safari.” Akasema Janet.Monica
akainama akaonekana kujawa na mawazo
mengi .Akainua kichwa na kusema
“ Mama sijawahi hata mara moja
katika maisha yangu kuhisi kwamba
hamnitendei haki lakini kwa hili
mlilonifanyia ni wazi hamjanitendea haki
kabisa.Mnataka niolewe na mtu ambaye
licha ya kwamba ana pesa lakini tayari ana
 
SEHEMU YA 105


ndoa yake !! “ akasema Monica na
kuinamisha kichwa
“ Monica hili lisikuogopeshe ,David
ana mke ndiyo lakini mpaka leo hii mke
wake hajaweza kumzalia mtoto.Hawezi
kushika mimba.Hii ni nafasi yako sasa ya
kuumiliki utajiri wa David kwa kumzalia
mtoto ambaye atakuwa mrithi wa mali
zake.Monica mimi ni mwanamke na kama
nafasi hii ningeipata enzi za usichana
wangu
katu
nisingekubali
iniponyoke.Ninakwambia hivyo kama
mama yako kwa sababu ninapenda maisha
yako yawe mazuri.Lakini hata hivyo wewe
ndiye muamuzi wa maisha yako.Utaamua
mwenyewe unataka kuishi maisha ya
namna gani.Ila nakushauri Monica fikiria
na fanya maamuzi yenye kufaa” akasema
bi Janet akaagana na Monica na kila
mmoja akaelekea chumbani kwake.
“ Umejaribu kumshawishi? Akauliza
Benedict

Uphhh..nimejitahidi
sana
kumshawishi na kumueleza kuhusu faida
zitakazopatikana
endapo
atakubali
kuolewa na David Zumo.Anaonekana ana
msimamo lakini kwa sasa bado
amestushwa na suala hili hakuwa
amelitegemea ninaamini atakapokaa
akatulia akatafakari anaweza akafanya
maamuzi mazuri.Nimejitahidi sana kumpa
somo na kama akipuuzia shauri
zake.Nafasi kama hizi huwa hazitoke mara
mbili.Wanawake wengi wanaota kupata
bahati kama hii na hawaipati yeye kaipata
na anaweka misimamo yake kama
mwanasiasa.” Akasema Janet
“ Amechukua tabia yako ya kuwa na
msimamo usioyumba .Nakumbuka misuko
suko iliyokupata wakati ule ulipopata
mimba ukiwa bado shuleni na kila mtu
akakutaka
ukaitoe.Familia
yako
wakakutaka uchague shule au mapenzi na
ukachagua mapenzi.Hukuyumba na wala
hukupepesa macho kuchagua kuwa na
mimi na tabia hii ndiyo anayo Monica.”
Akasema Benedict
“ Oh Ben bado unazikumbuka
nyakati zile.Katu siwezi kusahau namna
familia yangu ilivyosimama na kunitaka
nikaitoe mimba ya Nathan.Kwa wakati ule
sikuwa na kitu chochote nilichokuwa
ninakifikiria katika akili yangu zaidi
yako.Ulikuwa umenikaa katika kila
mshipa wa mwili wangu.I was madly in
love with you,my first love” akasema Janet
na wote wakacheka.
“ Kwa kweli ule ulikuwa ni mfano wa
penzi la kweli.Hukusita kunichagua kijana
masikini kama mimi ambaye kwa ule
sikuwa na mbele wala nyuma .Nililazimika
kukatisha masomo ili niweze kutafuta
kibarua cha kuweza kukutunza wewe na
mtoto.Lazima nikiri kwamba sijawahi
kuwa na wakati mgumu kama ule lakini
kila niliporejea nyumbani ulikuwa na
tabasamu usoni na ulikuwa ndiye mfariji
wangu
mkubwa.Pamoja
kwamba
hatukuwa na fedha ,tulikuwa na maisha ya
taabu but we were happy.Tuliishi maisha
ya furaha hadi pale tulipokutana na
Ernest.” Akanyamaza na kutazama
chini.Wote wakabaki kimya
“ He changed our happy life.He
changed us.He took our love away.He
turned us to monsters” akasema Benedict
kwa sauti ya unyonge
“ Please Ben don’t say that.You are
hurting me “ akasema Janet
“ It’s not me hurting you it’s the
truth” akasema Ben

“ Baada ya kuanza kupata fedha
maisha yetu yalibadilika.Kila kitu
kikabadilika.” Akasema Ernest
“ Si kweli Ben,mambo yalibadilika
kiuchumi
lakini
mapenzi
yetu
hayakubadilika.Ni kweli tulipitia vikwazo
kadhaa katika kuelekea maisha mazuri na
kuna nyakati tulitetereka lakini bado
tumesimama pamoja hadi leo.I loved you
Ben and I will always love you” akasema
Janet
“ Are you sure that you still love me?
Akauliza benedict
“ yes I do” akajibu Janet
“ Ben tusihukumiane kwa mambo
yaliyopita ndiyo maana nikasema kwamba
kuna nyakati tulitetereka .Sote tulifanya
makosa,tusameheane
na
tuangalie
yaliyoko mbele yetu.NInakupenda sana”
akasema Janet na kumbusu Ben
“ What a liar.Unadhani sifahamu
mambo unayoyafanya ? Laiti ningegundua
mapema namna ulivyo katu nisingekubali
kujiingiza katika mapenzi na wewe nyoka
mkubwa we” akawaza Ben
 
SEHEMU YA 106



onica aliingia chumbani kwake na
kuketi sofani .Alihisi kichwa kizito
kutokana na kujawa na mawazo
mengi.Jambo aliloelezwa na wazazi wake
usiku ule lilimchanganya mno akili yake
“ Sikutegemea kabisa kusikia hiki
nilichokisikia usiku wa leo toka kwa
wazazi eti Davi Zumo anataka kunioa”
akawaza halafu akavua viatu na kujilaza
sofani
“ David Zumo ni mtu mkubwa,ni rais
mwenye nguvu na tajiri namba moja
Afrika.Kusema kwamba amenipenda na
anataka kunioa si kitu kidogo.Hili ni
jambo kubwa kwake,kwangu na kwa nchi
zetu pia.Ninatakiwa kutafakari kwa
makini sana kuhusu suala hili na
kuchukua maamuzi yenye kufaa.Oh m y
gosh ! kichwa changu nahisi kimejaa na
kinashindwa kufikiri sawa sawa”
akainuka akabadili mavazi akatoka na
kuelekea katika bwawa la kuogelea
akajitumbukiza
majini
akaanza
kuogelea.Mara nyingi awapo na jambo
kubwa linalomsumbua kichwa chake
hupenda sana kuogelea.Wakati akiogelea
bado kichwa chake kiliendelea kujaa
mawazo kuhusiana na David Zumo.
“ Nilijiuliza sana sababu ya David
Zumo kutoa msaada ule mkubwa kumbe
alikuwa na lengo lake na msaada ule
alionipa ni moja kati ya njia za kutaka
kufanikisha lengo lake la kuanzisha
mahusiano na mimi.Amenifahamu kwa
muda gani hadi afikie hatua ya kufanya
maamuzi ya kutaka kunioa? Nia yake ya
kutaka kunioa inatoka moyoni au
amevutiwa tu na uzuri wangu? Ninahisi
yawezekana akawa amevutiwa na uzuri
wangu na hasa baada ya kutangazwa
mrembo zaidi Afrika na anataka kutumia
jina na utajiri wake kunipata.Endapo
angekuwa na nia ya dhati kwangu
angeweza kuieleza mimi mwenyewe wazi
wazi lakini hakufanya hivyo na badala
yake akawaeleza wazazi ili wao
wanishawishi mimi nikubali kuolewa
naye.Thats an old style.Wazazi nao kwa
tamaa ya utajiri walioahidiwa
wanajitahidi kufanya kila wawezalo
kunishawishi nikubali kuolewa na
David.Sijawahi kubishana nao hata mara
moja na wanaitumia fursa hiyo
kunishawishi.I’m confused and I don’t
know what to do” akawaza na kuzama
chini halafu akaibuka
“ Kwa mara ya kwanza katika maisha
yangu
nitatofautiana
na
wazazi.Sintakubaliana nao kwa hiki
wanachotaka nikifanye” akawaza na
kuzama tena chini ,akaibuka
“ Simfahamu David Zumo
kiundani,sizifahamu tabia zake,sifahamu
ananipenda kiasi gani.Ninafahamu kitu
kimoja tu kuhusu David kwamba ni tajiri
namba moja Afrika.Zaidi ya hilo sifahamu
chochote kuhusu yeye na siwezi kukubali
au kufurahia kuolewa na bilionea huyu
ambaye bado simfahamu vyema.”
Akaendelea kupiga mbizi kuzunguka
bwawa.
“ Suala la ndoa si suala rahisi kama
wao wanavyolichukulia.Ni jambo
linalohusu moyo zaidi kuliko mali .Kama
isingekuwa matatizo yaliyomtokea Dr
Marcelo ,ni mwanaume ambaye tayari
nilikwisha aanza kuvutiwa naye .Ana sifa
nyingi kati ya zile ninazozihitaji kwa
mwanaume wa maisha yangu,lakini naye
kama ilivyo kwa David Zumo bado
simfahamu vyema na kuna mambo mengi
ambayo nahitaji kuyafahamu kuhusu yeye
lakini kwa sasa its already late.kwa
mambo yaliyotokea mimi na yeye
tutaendelea kuwa marafiki wa kawaida
tu.Namuomhea aweze kupona na aendelee
 
SEHEMU YA 107

na maisha yake” Monica akatoka ndani ya
maji akaelekea chumbani kwake
“ Ni lini basi nitampata mwanaume
wa ndoto zangu ambaye hatakuwa na
kasoro? Kila mwanaume ninayempata na
kudhani labda anaweza kunifaa nagundua
ana kasoro Fulani.Lakini sichoki kusubiri
,ninaamini siku moja nitampata tu
mwanaume aliyeumbwa kwa ajili yangu
.Nitaendelea kumuomba Mungu ili iwe
mapema zaidi kwani jambo hili
linaniumiza sana moyo wangu.Nadhani ni
muda muafaka sasa wa kuwa na mume
,kuwa na familia .Sitaki kupata watoto
wakati nikiwa na umri mkubwa.” Akawaza
akiwa amejilaza kitandani na mara sura ya
David ikamjia akatabasamu
“ David Zumo “ akasema kwa sauti
ndogo halafu akainuka na kwenda kuketi
sofani
“ Kwa muda mfupi niliokutana naye
kuna vitu kadhaa nimevigundua
kwake.Ana sura nzuri,anaonekana anajali
na mwenye moyo wa kusaidia japokuwa
naamini msaada ule mkubwa alionisaidia
ulikuwa kwa ajili ya kujenga ukaribu kati
yangu na yeye lakini anaonekana ana roho
nzuri.” Akainuka na kurejea kitandani
“ Kama ningekuwa tayari
ninamfahamu vizuri,naona David
angeweza kunifaa sana lakini tatizo bado
simfahamu vyema halafu moyo wangu
unakuwa mzito kumkubali japokuwa
naamini kuna faida nyingi ambazo naweza
kuzipata kama nikikubal kuolewa
naye.Faida
kubwa
hasa
ni
kiuchumi.Nikiwa na David nitaweza
kutekeleza miradi yangu mingi
ninayokusudia kuianzisha hapa nchini
hususan ule mradi wa kujenga kambi za
wazee kila mkoa kila wilaya.David ni mtu
mwenye pesa na anaweza akanisaidia hilo
likawezekana na taasisi yangu inaweza
kujulikana duniani kote na kupata
wafadhili wengi.Jina langu litakuwa
kubwa na kujulikana duniani kote” Ghafla
Monica akastuka kama aliyekuwa
usingizini.”
“ Oh my gosh !! sijui kwa nini
ninawaza mambo kama haya ambayo ni
wazi hayawezekani.Siwezi kuolewa na
David Zumo hata kama ni rais na tajiri
namba moja Afrika.Nitaolewa na mtu
ambaye moyo wangu utamridhia na si mtu
kwa sababu ya utajiri wake.Bado ninayo
imani kwa mungu kwamba ataniletea
mwanaume Yule ambaye amemuandaa
kwa ajili yangu.” Akawaza Monica na mara
akajiwa na wazo
“ Lakini mbona inaonekana kama
suala hili nimelifanyia maamuzi ya haraka
sana? Akajiuliza
“ Ni kweli jambo hili nimelitolea
maamuzi ya haraka sana .Kuna ubaya gani
endapo nitalipa walau muda kidogo? Mimi
nadhani hili ni wazo zuri,nilipe nafasi
jambo hili nilitafakari kwanza kabla ya
kutoa maamuzi ya haraka haraka.Hakuna
ubaya wowote endapo nitaamua kujipa
muda katika suala hili na papo hapo
nitakuwa nikimsoma David Zumo ni mtu
wa namna gani na pengine ninaweza
nikajikuta nikibadili mawazo” akawaza
“ Kama nikiamua kulipa nafasi suala
hili basi itanilazimu kujenga ukaribu na
David .Oh my gosh ! I’m so
scared”...akatazama juu kwa sekunde
kadhaa na kuendelea kutafakari
“ Kuna sauti inaniambia kwamba
nisiogope,niwe jasiri.Ngoja niisikie sauti
 
SEHEMU YA 108

hiyo na nilikabili suala hili .Yawezekana
ikawa ni bahati yangu na ninaipiga teke.”
Akawaza Monica na kuanza kuutafuta
usingizi
*******************
Imekwisha timu saa tano za usiku
,bado rais wa Tanzania Ernest Mkasa
alikuwa ofisini kwake akiwa na
mkurugenzi wa habari wa ikulu
wakijadiliana masuala kadhaa,mara
mlango ukafunguliwa akaingia mzee
Mukasha.Rais alipomuona Mukasha
akamuomba mkurugenzi wa habari
waonane asubuhi wamalizie maongezi yao
akamkaribisha Mukasha.
“ karibu Mukasha “ akasema Rais
.Mukasha akaeti sofani
“ Mheshimiwa rais nimefanikiwa
kumpata Mr Boaz” akasema Mukasha
“ That’s good news.Umezungumza
naye chochote?
“ Hapana mheshimiwa rais,sijaongea
naye chochote ila nimemueleza kwamba
wewe ndiye unayetaka kuzungumza
naye.Kwa sasa yuko katika biashara zake
Comoro na ameniomba nimpigie baada ya
dakika kumi na toka tulipoongea simuni
hadi sasa tayari muda huo umekwisha
pita.Ngoja nimpigie” akasema Mzee
Mukasha na kuzitafuta namba za bilionea
Boaz akampigia.Simu ikaita na baada ya
muda ikapokelewa
“ hallow Mr Boaz,Mukasha
ninaongea ,niko na rais hapa.Tayari una
muda mzuri wa kuzungumza naye?
“ Ndiyo Mr Mukasha.Nipe
nizungumze naye” akasema Boaz na
Mukasha
“ Habari yako Mr Boaz” akasema
Ernest
“ Habari yako mheshimiwa rais?Pole
sana na majukumu mazito ya kuongoza
nchi” akasema Boaz
“ Ahsante sana Mr Boaz.Natumai hii
ni mara yetu ya kwanza kuzungumza.”
“ Ndiyo mheshimiwa rais.”
“ Nafurahi kukufahamu Mr
Boaz,naamini huu utakuwa ni mwanzo
mzuri wa kujenga mahusiano mazuri
baina yetu.Wafanya biashara wakubwa
kama ninyi mnapaswa kuwa karibu na
watu kama sisi ili tuweze kuwasaidia.Mimi
mwenyewe nimekuwa mfanya biashara
ninazifahamu
changamoto
wanazokumbana nazo wafanya biashara
kwa hiyo ukiwa karibu na mtu kama rais
ni jambo lenye manufaa makubwa.Kuna
nyakati unaweza kukwama lakini neno
langu moja tu likakukwamua” akasema
Ernest huku akicheka kidogo
“ Usemayo ni ya kweli mheshimiwa
rais.Umuhimu upo mkubwa lakini tatizo ni
namna ya kuwafikia ninyi wakubwa.”
Akasema Boaz.
“ Usijali Mr Boaz, nitakupatia namba
yangu ya simu na muda wowote ukihitaji
msaada wa aina yoyote ile utanitaarifu
nitakusaidia”
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais”
“ Mr Boaz nimeambiwa na Mr
Mukasha kwamba kwa sasa uko safarini
Canada kwa hiyo sitaki kuchukua muda
wako mwingi naomba nielekee moja kwa
moja katika suala la msingi lililonifanya
nikutafute” akasema Ernest na kunyamaza
kidogo kisha akasema
“ Mr Boaz ninataka kuzunguza nawe
kuhusiana na mtu mmoja anaitwa Austin
January”
 
SEHEMU YA 109


“ Austin?!! Boaz akastuka
“ Ndiyo Mr Boaz.Nimeelekezwa hivi
sasa ulo naye na anafaya kazi katika moja
ya kampuni zako”
“ Ndiyo mheshimiwa rais,Austin
anafanya kazi katika mojawapo ya
kampuni zangu nchini Afrika ya kusini”
“ Mr Boaz ninahitaji kuonana na
Austin” akasema Rais na kumfanya Boaz
atoe kicheko k idogo
“ Mheshimiwa rais hilo ni jambo
ambalo halitawezekana kwasasa.Austin
hawezi kurejea tena Tanzania kutokana
na mambo yaliyowahi kumtokea .Nadhani
utakuwa unafahamu mambo yaliyomkuta

“ Ndiyo Boaz ninafahamu japokuwa
tukio hilo lilitokea wakati bado sijaingia
madarakani na nilipoinga madarakani
nilipewa taarifa ya tukio hilo japokuwa
sikuelezwa ukweli wote.Nimeufahamu
ukweli hivi karibuni na ndiyo maana
nimekupigia kukuomba unisaidie
kuonana
na
Austin.Ningeweza
kuzungumza naye moja kwa moja lakini
nimeona ni vyema kama nikiongea nawe
kwanza kwani yuko chini ya himaya
yako.Please help me”
“ Hujakosea mheshimiwa rais na
ninakushukuru kwa busara hiyo lakini
sina hakika kama Austin anaweza
akakubali kuonana nawe.Hivi sasa
amekwisha sahau yote yaliyotokea na
anaishi maisha mazuri na si mimi wala
mtu yeyote anayeweza kumshawishi
Austin akakubali ombi lako.He hate
Tanzania” akasema Boaz
“ Mr Boaz tafadhasli naomba ujaribu
kwa kila namna unavyoweza kumshawishi
akubali kuonana nami,ni muhimu sana.”
Akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais natamani sana
kukusaidia,au labda unieleze unamuhitaji
Austin kwa jambo gani hasa?
“ Kuna kazi binafsi nahitaji
anifanyie”
“ Kazi ?! akasema Boaz na kutoa
kicheko kidogo
“ Austin amekwisha achana na hizo
kazi mheshimiwa rais.Nakushauri
mheshimiwa rais jaribu kutafuta kijana
mwingine miongoni mwa vijana wako
akufanyie kazi yako na usipoteze muda
kuhusu Austin”
“ Mr Boaz nakubaliana nawe
kwamba kutokana na mambo
yaliyomkuta Austin inaweza kuwa vigumu
kwake kukubali kuonana nami lakini kwa
kupitia kwako inaweza kuwa rahisi na
akalegeza msimamo wake.Mimi na wewe
tunaweza kuingia makubaliano kwani
jambo kama hili haliwezi kwenda hivi
hivi.Niko tayari kwa makubaliano yoyote
ili mradi nifanikiwe kuonana na
Austin.Niambie unahitaji nini nikupatie
nawe unisaidie nionane na Austin”
akasema Rais na Boaz akasikika akivuta
pumzi ndefu kisha akasema
“ Mheshimiwa rais wewe ni rais
wangu ,ninakuheshimu sana ,ninaiona nia
yako ya kutaka kuonana na Austin na
siwezi kufanya makubaliano yoyote nawe
katika suala hili kwani itakuwa ni
kukukosea
heshima
kiongozi
wangu.Nitakusaidia uweze kuonana na
Austin.Nitajitahidi kumshawishi japo
haitakuwa rahisi lakini naamini
atakubali.Ila ninachokuomba mheshimwa
rais pale nitakapokuja kwako kuomba
 
SEHEMU YA 110

msaada wako naomba usinitupe mkuu
wangu”
“ Mr Boaz nakushukuru sana na
ninakuahidi kuwa dakika yoyote ukihitaji
msaada wangu wa aina yoyote ile usisite
kunitaarifu nitakusaidia” akasema rais
“ Ahsante mheshimiwa rais kwa
ahadi hiyo.Sasa naomba nikuache
upumzike nitawasiliaa nawe tena baada ya
kuzungumza na Austin” akasema Boaz
akaagana na rais na kukata simu
“ Oh thank you Lord.Sasa nina
uhakika wa kumpata Austin.Boaz
ameonyesha uungwana mkubwa.By the
way huyu Boaz ni nani hasa?
Anashughulika na biashara gani? Akauliza
Ernest
“ Boaz ni bilionea mtanzania
anayemiliki biashara kubwa kubwa nchini
Afrika kusini.Amewekeza sana huko lakini
hata hapa nyumbani amewekeza pia ana
miradi kadhaa mikubwa.Nitajitahidi
kukusanya taarifa zake na kukuletea”
akasema Mukasha

Nitashukuru
sana
Mukasha.Ahsante kwa msaada huu
mkubwa wa kunikutanisha na Boaz na
hatimaye nitampata Austin .Naomba sasa
twende tukapumzike imekuwa ni siku
ndefu lakini yenye mafanikio makubwa”
akasema Ernest
******************
Monica alidamka saa kumi na mbili
za asubuhi na bila kuaga mtu yeyote
akaondoka kuelekea hospitali kumtazama
Dr Marcelo.Bado kichwa chake kiliendelea
kusongwa na mawazo mengi kuhusiana na
suala aliloelezwa na wazazi juu ya ombi la
rais David Zumo.Alifika hospitali lakini
hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani ya
chumba hicho kutokana na hali ya Dr
Marcelo kubadilika ghafla kwa hiyo
madaktari walikuwa katika heka heka za
kujaribu kuidhibiti hali hiyo.Ndugu na
jamaa wote waliofika kumjulia hali Dr
Marcelo walikuwa nje wakiwa na wasiwasi
mkubwa.Monica akiwa miongoni mwa
watu waliokuwa nje wakisubiri taarifa ya
daktari juu ya hali ya Dr Marcelo akastuka
baada ya kuguswa bega.Akageuka
kumtazama aliyemgusa akakutana na
Julieth dada yake Marcelo
“ Habari za asubuhi Monica.Naitwa
Julieth ni dada wa Marcelo”
“ Ninakufahamu Julieth.Tayari
Daniel alikwisha nitambulisha kwako”
“Good.Can I have a word with you
Monica? Akasema Julieth wakasogea
pembeni kidogo
“ Unasemaje Julieth? Akauliza
Monica
“ Monica kuna jambo nataka
kukuuliza ila utanisamehe kwa kuwa ni la
kibinafsi zaidi”
“ Usihofu Julieth uliza”
“ Dr Marcelo ni kaka yangu ,mimi na
yeye baba yetu mmoja lakini mama zetu ni
tofauti.Marcelo ni mtoto wa pekee kwa
mama yake na mimi kwa mama yangu
niko peke yangu pia.Maisha ya Marcelo
naweza kusema kwamba yametawaliwa
na usiri mkuwa.Kuna mamo mengi
tusiyoyajua kuhusu yeye.Kwa sasa hali
yake inazidi kuwa tete na kuna wasi wasi
yawezekana akapoteza maisha kwa
mujibu wa daktari alienieleza leo kwamba
hali yake si nzuri .Toka alipopata matatizo
haya umekuwa ukifika hapa hospitali
mara kwa mara kumjulia hali na
 
SEHEMU YA 111


unaonekana kuguswa sana .Naomba
kuuliza wewe na Marcelo mna mahusiano
yoyote? Au kwa lugha nyepesi ninyi ni
wapenzi? Akauliza Julieth na kumfanya
Monica atoe kicheko kidogo
“ Usinielewe vibaya Monica
nimeuliza hivyo kwa makusudi ili hata
likitokea la kutokea basi tujue marehemu
ameacha mchumba au hata kama kuna
mtoto”
“ Hilo ni suala zuri na la muhimu
sana julieth lakini mimi na Dr Marcelo
hatuna mahusiano yoyote ya
kimapenzi.Sisi ni marafiki wa kawaida
.Nimefahamiana naye hivi karibuni na
aliyetukutanisha ni Daniel ambaye
amekuwa rafiki yangu wa muda mrefu
toka tukiwa wadogo.Kwa muda huu mfupi
tuliofahamiana tumekuwa marafiki
wakubwa na mtu yeyote angeweza
kudhani labda sisi ni marafiki wakubwa
wa muda mrefu au hata wapenzi.”
Akasema Monica.
“ Ahsante kwa majibu hayo
Monica.Hata mimi nilihisi labda
yawezekana mkawa ni wapenzi.kaka
yangu ana bahati sana ya kupata marafiki
wazuri lakini mpaka leo hii hatujawahi
kumfahamu mpenzi wake” akasema
Julieth
“ kwa hiyo Marcelo hajawahi kuwa
na mpenzi? Akauliza Monica
“ Sisi kama ndugu zake hatulifahamu
hilo kwani amekuwa msiri sana kuhusiana
na kuweka wazi mahusiano yake”
akasema Julieth
“ Poor Marcelo.Mungu amsaidie
apone na aendelee na maisha yake.He’s a
good person.Watu waliofanya kitendo hiki
tayari wamekwisha fahamika na
kukamatwa? Akauliza Monica
“ Hapana bado hawajafahamika ila
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi
kuwabaini na kuwatia nguvuni.” Akajibu
Juliet
“ Ninasali sana kumuomba Mungu ili
watu hawa waliofanya ukatili huu
wapatikane na kufikishwa mbele ya
sheria.Kinachoniumiza zaidi mchana wa
siku ile ya tukio nilikutana naye kuna
jambo alikuja kunieleza.Niliingiwa na hofu
kuhusiana na usalama wake nikamuomba
aje akae nyumbani kwangu kwa muda
hadi hapo masuala yake yatakapopatiwa
ufumbuzi lakini akakataa na jioni ya siku
hiyo akapigwa risasi.Inaniuma sana na
ndiyo maana siachi kuja kila siku kumjulia
hali” akasema Monica na machozi
yakamtoka
“ Pole Monica .Hili ni tukio
linalotuumiza sote na tuzidi kumuomea
Marcelo apone” akasema Julieth .Baada ya
dakika tano daktari akatoka na
kuwataarifu kuwa hali ya Marcelo
inaendelea vizuri akawatoa hofu na
kuwataka warejee nyumbani
Baada ya kutoka hospitali Monica
akaelekea moja kwa moja nyumbani
kwake.Alisalimiana na wafanyakazi wake
pale nyumbani halafu akaenda chumbani
kwake
“Kichwa changu ni kama vile
kinabebeshwa mzigo mzito zaidi ya uwezo
wake.Ninawaza hadi nahisi kufika
mwisho wa uwezo wangu wa kufikiri.Huku
kuna suala la David Zumo na huku kuna
suala la Marcelo.Yote haya yananich......”
akastuliwa toka mawazoni na mlio wa
simu akaitoa katika pochi akatazama
mpigaji.Zilikuwa
ni
namba
ngeni.Akazitazama vizuri na kugundua
 
SEHEMU YA 112



hazikuwa ni namba za Tanzania.Akasita
kidogo halafu akaipokea
“ Hallow’ akasema kwa wasi wasi
kidogo
“ Hallow Monica.David Zumo
ninaongea hapa.Habari za asubuhi.? Vipi
maendeleo yako?
Monica akastuka sana baada ya
kuisikia sauti ile ya David
“ Hallow mheshimiwa rais” akasema
kwa sauti yenye kukwama kwama
“ Monica nimefurahi sana kuisikia
tena sauti yako nzuri.Vipi maendeleo
yako?
“ Ninaendelea vizuri mheshimiwa
rais”
“ Nafurahi kusikia hivyo,ila
nakuomba unite David inatosha sana”
“Sawa mhe....oh samahani David..”
akasema Monica na wote wakacheka
“Monica utanisamehe kwa kukupigia
asubuhi hii naamini hukuwa umerajia
simu toka kwangu.Lengo kubwa ni kutaka
kujua maendeleo yako na pili
kukufahamisa kwamba mimi ni mlezi wa
umoja wa vijana wa Congo.Umoja huu
lengo lake kubwa ni kuwajenga vijana
kifikra watambue wajibu wao kwa taifa na
kwa jamii.Kila mwaka wanachama wa
umoja huu hufanya kongamano kubwa na
kujadili mambo mbali mbali na
changamoto zinazowazunguka kama
vijana.Mwaka huu kongamano hilo
linafanyika hapa Kinshasa na mimi kama
mlezi wao nimealikwa kulizindua.Monica
kuna jambo ambalo sikuwa nimelipanga
hapo kabla lakini baada ya kukutana nawe
nimeona kuna ulazima wa wewe kuwa
mmoja wa watoa mada katika kongamano
hilo.Mchango wako utawasaidia vijana
wengi wa kike na wa kiume kujitambua
wao ni akina nani na wafanye nini ili
watimize malengo yao ya maisha.Kwa hiyo
Monica napenda nitumie nafasi hii
kukukaribisha rasmi katika kongamano la
tisa la umoja wa vijana wa Congo.Uwepo
wako utawapa hamasa vijana wengi.”
Akasema David
“ David nimefurahi kwa mwaliko huo
lakini nashindwa nikujibu nini kwani
imekuwa ni ghafla mno na sijajiandaa
kabisa kwa jambo hil..” Monica
hakumaliza sentensi David akasema
“Monica tafadhali naomba usiseme
hapana.Nafahamu nilipaswa kukutaarifu
toka mapema kuhusiana na suala hili
lakini sikuwa na mawazo hayo.Baada ya
kuondoka Tanzania nimetafakari na
kuona kuna umuhimu mkubwa sana wewe
kuhudhuria katika kongamano hilo.Tayari
nimekwisha wataarifu viongozi wa umoja
huo kwamba na wewe utakuwepo na
vijana wametangaziwa na kwa taaarifa
nilizozipata ni kwamba vijana
wamehamasika mno kuihudhuria katika
kongamano baada ya kusikia uwepo
wako.Kwa hiyo Monica nakuomba
tafadhali usiniangushe.Naomba ukubali
mwaliko huu rasmi toka kwangu”
akasema David.Ukimya mfupi ukapita
.Monica akatafakari kasha akasema
“ Mheshimiwa rais kwa hili
ulilolifanya hujanitendea haki hata
kidogo.Ulipaswa kunitaarifu kwanza ili
nithibitishe ushiriki wangu kabla ya
kuutangazia umma.” Akasema Monica
akanyamaza na kuendelea
“ Hata hivyo,tayari umenifunga
mikono na siwezi tena kusema
hapana.Nitahudhuria kongamano hilo”
“ Ahsante sana Monica.Nashukuru
mno.Hii ni heshima kubwa umenipa”
“ Lini linafanyika kongamano hilo?
Akauliza Monica
“ Linaanza kesho.Kwa hiyo jioni ya
leo nitatuma ndege yangu binafsi kuja
kukuchukua hapo Dar es salaam” akasema
David Zumo.Ukimya ukatanda tena baada
ya muda Monica akasema
“Sawa David”
“Ahsante Monica.Nitawasiliana nawe
baadae mchana wa leo” akasema David na
kukata simu
“Dah ! Kweli David amedhamiria
kufanya kila awezalo kutafuta ukaribu na
mimi.Amenibana katika kona na
nisingeweza kusema hapana.Hili ni jaribu
kubwa na taratibu najiona kama vile
ninaelekea kuanguka.Ninapoisikia sauti
ya David nahisi kutetemeka kwa
ndani.Nahisi amefanya hili makusudi
kabisa ili apate nafasi ya kuwa na
mimi.Lakini hata hivyo hii ni nafasi yangu
pia ya kumsoma na kumfahamu vizuri ni
mtu wa aina gani hasa.Ngoja niende Congo
kwa sababu naona kuna nguvu kubwa
inanitaka niende kuonana na David “
akawaza na kuoga akajiandaa akatoka
kuelekea ofisini kwake.Njiani bado kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi na hata
alipofika ofisini kwake alishindwa
kufanya kazi yoyote.Kikubwa alichokuwa
anakiwaza ni safari ya kwenda Congo.


NINI KITATOKEA MONICA AKIWA
CONGO? ATAKUBALI KUOLEWA NA DAVID
ZUMO?
AUSTIN JANUARY ATAKUBALI
KUREJEA TANZANIA?
NANI KAMPIGA RISASI DR MARCELO
NA KWA NINI ?


[HASHTAG]#USIKOSE[/HASHTAG] KUENDELEA NA SIMULIZI
HII KATIKA SEASON 2#
 
Back
Top Bottom