SEHEMU YA 4
unayemuhitaji katika maisha yako lakini
unachopaswa kuangalia ni moyo wake na
dhamira yake ya dhati ya kutaka
kukuoa.Monica mimi kama mama yako
nakushauri nafasi hii usiikatae.Wanawake
wenzako nafasi kama hizi wanaziota
ndotoni.Kwa hiyo Monica nakushauri
ulipokee ombi la David kwa mikono miwili
kwani ni jambo lenye faida nyingi kubwa
kwako na kwetu pia kama familia na hata
nchi kwa ujumla.Ukiolewa na David
utakuwa mke wa bilionea mkubwa
duniani,utakuwa mtu mkubwa na mwenye
nguvu,utafanya mambo mengi yale
ambayo umekuwa ukiota kuyafanya
,utatimiza ndoto zako zote.Dakika
utakayotamka neno nakubali basi maisha
yako yatabadilika .Ukiolewa na David
utaumiliki utajiri wake wote,utafungua
viwanda vikubwa hapa nchini na utaleta
ajira kwa maelfu ya vijana .Kwa kuwa
lengo lako la muda mrefu ni kuisaidia
jamii masikini na yenye uhitaji basi hii
ndiyo
fursa
unayotakiwa
kuitumia.Inawezekana Mungu anataka
kukutumia ili uwasaidie watu wake wenye
uhitaji kwa hiyo isikie sauti yake ndani
mwako na ukubali ombi la David.Mimi
kama mama yako,kama rafiki yako,kama
msiri wako,sina maneno mengine mazuri
zaidi ya kukushawishi kuhusu suala
hili,nimekueleza mengi ,ni juu yako sasa
kupima na kufanya maamuzi sahihi.”
Akasema bi Janet akachukua glasi ya maji
akanywa Monica naye akachukua pakiti
lake la biskuti akatoa moja na
kutafuna,kila mmoja alionekana kuwaza
lake.Mwishowe Monica akauvunja ukimya
“Mama nimekusikiliza kwa makini
na nimefurahi pia kusikia japo kwa ufupi
kuhusu historia yenu wewe na baba.Kwa
ufupi ni kwamba usiku wa leo sikuweza
kupata usingizi kutokana na mawazo
mengi niliyokuwa nayo na kubwa zaidi
ilikuwa ni suala hili .Baada ya tafakari ya
kina nimeamua kulipa nafasi jambo hili”
“ Wow ! that’s good my princess”
akasema bi janet
“Kuamua kulipa nafasi suala ili si
kukubali ombi la David bali nataka nipate
wasaa wa kutosha kutafakari,kumfahamu
David ni mtu wa aina gani na mwisho nitoe
maamuzi.Nina
msimamo
wangu
kuhusiana na mwanaume wa maisha
yangu na sibabaishwi na jina au utajiri wa
mtu na hata nilipotajiwa kuhusu David
Zumo sikustuka sana kwa sababu
ninaufuata moyo wangu hata hivyo
nimeona hakuna sababu ya kutoa
maamuzi ya haraka kuhusu suala hili
kwani inawezekana David akawa ni mtu
mzuri wa kunifaa .Naombeni mnipe muda
wa kutosha ,nataka nijenge kwanza
mahusiano mazuri na David na baadae
nitatoa jibu langu.Kwa hiyo mama jioni ya
leo ninakwenda Congo nimealikwa na
David kutoa mada katika kongamano la
umoja wa vijana wa Congo.”
“Usinitanie Monica.Mara hii David
amekwisha kupa mwaliko?? Bi Janet
akapatwa na mshangao
“Ndiyo mama,leo nakwenda
Congo.David amenipigia simu asubuhi na
kuniomba niende na nimekubali
japokuwa najua anataka kutumia kigezo
hicho kutengeneza ukaribu na mimi.Hicho
ndicho kitu ambacho ninakitaka hata
mimi kuwa karibu naye ili nimfahamu
vizuri.”
“Monica mwanangu Mungu
anakuongoza na ndiyo maana mambo