QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Twende season 2, hii tumeshameza yote, BTW asante kwa kuufanya usiku kuwa mzuri. Ubarikiwe sana. Tunaamini utaifanya Jumapili ya leo iwe ya kipekee, maana story inazidi kuwa tamu.
 
QUEEN MONICA SEASON YA 2

SEHEMU YA 1

ILIPOISHIA SEASON 1
“ Mheshimiwa rais kwa hili ulilolifanya
hujanitendea haki hata kidogo.Ulipaswa
kunitaarifu kwanza ili nithibitishe ushiriki
wangu kabla ya kuutangazia umma.”
Akasema Monica akanyamaza na
kuendelea
“ Hata hivyo,tayari umenifunga
mikono na siwezi tena kusema
hapana.Nitahudhuria kongamano hilo”
“ Ahsante sana Monica.Nashukuru
mno.Hii ni heshima kubwa umenipa”
“ Lini linafanyika kongamano hilo?
Akauliza Monica
“ Linaanza kesho.Kwa hiyo jioni ya
leo nitatuma ndege yangu binafsi kuja
kukuchukua hapo Dar es salaam” akasema
David Zumo.Ukimya ukatanda tena baada
ya muda Monica akasema
“Sawa David”
“Ahsante Monica.Nitawasiliana nawe
baadae mchana wa leo” akasema David na
kukata simu
“Dah ! Kweli David amedhamiria
kufanya kila awezalo kutafuta ukaribu na
mimi.Amenibana katika kona na
nisingeweza kusema hapana.Hili ni jaribu
kubwa na taratibu najiona kama vile
ninaelekea kuanguka.Ninapoisikia sauti
ya David nahisi kutetemeka kwa
ndani.Nahisi amefanya hili makusudi
kabisa ili apate nafasi ya kuwa na
mimi.Lakini hata hivyo hii ni nafasi yangu
pia ya kumsoma na kumfahamu vizuri ni
mtu wa aina gani hasa.Ngoja niende Congo
kwa sababu naona kuna nguvu kubwa
inanitaka niende kuonana na David “
akawaza na kuoga akajiandaa akatoka
kuelekea ofisini kwake.Njiani bado kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi na hata
alipofika ofisini kwake alishindwa
kufanya kazi yoyote.Kikubwa alichokuwa
anakiwaza ni safari ya kwenda Congo.
ENDELEA SEASON 2.......................
“Any word from Monica? Akauliza
mzee benedict akiwa mezani na mkewe
wakipata kifungua kinywa
“Sijawasiliana
naye
toka
asubuhi.Nimeambiwa kwamba aliamka
alfajiri akaondoka.Nahisi aliwahi hospitali
kumjulia hali Yule rafiki yake aliyepigwa
risasi” akajibu Jane
“Ulivyomuona unadhani anaweza
kukubali kuolewa na David Zumo?
Akauliza mzee Ben
“ Siwezi kujua anawaza nini na
atatoa jibu gani lakini nakuhakikishia
nitafanya kila niwezalo na lazima Monica
atakubali kuolewa na David ila Ben...”
Janet akasita kidogo.Ben akamkazia
macho
“Makubaliano yetu yabaki vile vile
kama
tulivyokualiana
.Monica
hatalifahamu suala hili katika maisha yake
yote na familia yetu itabaki na
amani.Monica will remain your daughter
forever” akasema Jane.
“Mimi sina tatizo kabisa katika hilo
lakini wasi wasi wangu ni kwako kama
utaweza kuitunza siri hii na hutamueleza
Ernest kama Monica ni mwanae.”
Janet akatabasamu na kusema
“Naomba uniamini Ben.Siwezi
kwenda kinyume na makubaliano
yetu.Sintomueleza chochote.Hii itabaki ni
 
SEHEMU YA 2

siri yetu mimi na wewe pekee” akasema
Janet akamtazama Ben usoni na kuuliza
“Are you still angry with him?
“Nani?
“Ernest”
Ben akanywa chai akaweka kikombe
chini na kumtazama mke wake kwa
makini kwa sekunde kadhaa halafu
akasema
“No ! I’m not”
“Good.Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Jane
“Ninyi ni marafiki mmetoka mbali na
hamtakiwi kugombana katika umri
huu.Makosa yamekwisha fanyika na
hatutakiwi kuangalia mambo ya
nyuma.Tuelekeze nguvu zetu katika
mambo makubwa ya msingi yaliyoko
mbele yetu .” akasema Janet
“ Hicho ndicho kikubwa
tunachopaswa kukifanya” akasema Ben na
kuinuka
“Naelekea ofisini kama utapata
taarifa zozote toka kwa Monica
utanijulisha”
“Sawa Darling” akajibu Janet,Ben
akaondoka
“Mwanamke muongo mkubwa
huyu.Bado anakutana kwa siri na
Ernest.Nina uhakika lazima atamueleza
ukweli kuhusiana na Monica.Ernest
akifahamu kama Monica ni mwanae
atafanya kila awezalo kumchukua na hilo
ndilo jambo ambalo sitaki litokee.Monica
ataendelea kuwa mwanangu daima.”
Akawaza Ben
Muda mfupi baada ya benedict
kuondoka,mkewe Janet naye akaondoka
na moja kwa moja akaelekea ofisini kwa
Monica
“Naomba Monica akubali ombi la
David ili amani iwepo ndani mwetu kwani
bila kufanya hivyo hili bomu litalipuka na
kutujeruhi sote.Lazima nifanye kila
ninaloweza kuhakikisha Monica anakubali
kuolewa na David.Mimi mwenyewe ndiye
niliyechafua hali ya hewa kwa hiyo lazima
nifanye jitihada za kuisafisha.” Akawaza
Janet akiwa njiani kuelekea ofisini kwa
Monica
Aliwasili ofisini kwa Monica na
kumkuta akiwa amejiegemeza kitini
hakuwa na hamu ya kufanya kazi.Mezani
kulikuwa na pakiti la biskuti
“ mama karibu sana” akasema
Monica na kumkaribisha mama yake
ofisini kwake
“Ahante Monica.Samahani kwa kuja
bila taarifa”
“Usijali mama karibu sana ni muda
mrefu hujafika hapa ofisini kwangu”
akasema Monica.Bi Janet akalishika lile
pakiti la biskuti na kumtazama mwanae
“Nakufahamu
vizuri
Monica.Unapenda kutumia biskuti hizi
pale unapokuwa na mawazo mengi.Pole
sana nina imani ni kuhusu lile suala
tulilokueleza jana.” Akasema Bi Janet
“ Ni kweli mama kichwa changu
kimejawa mawazo mengi.Suala lile
linaninyima amani kabisa.” Akasema
Monica
“ Pole Monica lakini suala hilo hilo
ndilo limenileta hapa kwako .Nataka
tuzungumze kama mama na
mwana.Nataka niwe muwazi kwako na
wewe ufunguke kwangu.It’s a serious talk
between you and me” akasema
Janet.Monica akamtazama halafu
akainuka na kusema
“Twende bustanini”
 
SEHEMU YA 3


Walitoka ofisini wakaelekea
bustanini.Ilikuwa ni bustani nzuri
iliyotengenzwa kwa ustadi mkubwa
“Monica wewe ni mwanangu”
akaanzisha maongezi bi Janet
“Nimekukuza
mimi
na
ninakufahamu vizuri kuliko mtu
mwingine yeyote.Ninafahamu msimamo
wako kuhusiana na masuala ya mahusiano
na ninafahamu unahitaji mwanaume wa
namna gani.Ni jambo zuri kuwa na mpenzi
Yule mwenye sifa unazozitaka lakini
Monica mambo yamebadilika sana zama
hizi.Nafahamu wapo wanaume wengi tu
wanakupenda kwa dhati ya mioyo yao
lakini wengi wamekosa sifa unazozitaka”
akanyamaza na baada ya sekunde kadhaa
akaendelea
“Mwanangu kama nilivyokueleza
awali kwamba maisha yamebadilika sana
siku hizi na hivyo kutufanya tusiegemee
sana katika masuala ya vigezo au sifa bali
tunachoangalia kikubwa ni moyo wa mtu
na nia ya dhati .Ukisema usubiri mtu
mwenye vigezo unavyotaka utasubiri sana
na usimpate.Nikupe mfano wangu mimi
,baba yangu alikuwa ni tajiri mkubwa na
niliishi maisha ya kitajiri mno,nilisoma
shule nzuri na nilikuwa na ndoto nyingi
kubwa za kutimiza maishani lakini kila
kitu kilibadilika pale nilipokutana na baba
yako” akanyamaza kidogo kisha
akaendelea
“ndoto yangu ilikuwa ni kumpata
mwanaume tajiri,mzuri wa sura,mwenye
elimu ya kutosha .Nilitaka mwanaume
mwenye kufanana na hali yangu na
msimamo
wangu
haukuyumba.Niliwakataa vijana wengi
toka familia kubwa walionitaka
kimapenzi lakini msimamo wangu
ulitetereka pale nilipokutana na baba
yako.Hakuwa akitoka katika familia
kubwa yenye uwezo na alikuwa anasoma
shule ya kawaida .Nilikutana naye wakati
shule zetu zilipokutana katika bonanza la
michezo.Alivutiwa nami na bila kujali
utofauti wa hali zetu za kimaisha kwa
ujasiri mkubwa alinipenda akanifuata
akanitongoza.Nilishangazwa mno na
ujasiri wake nikajikuta nikimpenda.Ni
hicho tu kimoja kiichonivutia kwake na
kunifanya nilegeze msimamo wangu na
kuingia katika mapenzi kwa mara ya
kwanza na katika mapenzi hayo kwa
bahati mbaya nikapata ujauzito
nikatakiwa na familia yangu nikaitoe
mimba hiyo lakini nilikataa.Baba yangu
akanitaka nichague maisha mazuri
aliyoniandalia au Benedict nami kwa
ujasiri nikamchagua baba yako na
nikafukuzwa nyumbani.Ndoto zangu za
maisha nilizokuwa nazo zikaishia hapo
lakini angalia mahala niliko hivi
sasa,nimetimiza kila kile nilichokuwa
nakihitaji.Sijawahi kuwaelezeni historia
hii lakini nimeona nikueleze leo ili
ufahamu namna maisha yanavyoweza
kubadilika” Bi Janet akanyamaza na kwa
mbali sura ya Monica ikaonyesha
tabasamu
“That’s a very interesting
story.Sikufahamu historia yenu “ akasema
Monica
“Ni safari ndefu na haikuwa rahisi
lakini tumesimama imara na hadi sasa
tumekuwa wazee.Huu ni mfano nimekupa
kukufundisha kwamba usiiache nafasi hii
iliyojitokeza.Ni nadra sana kwa nafasi
kama hizi kutokea zama hizi.Inawezekana
David hana vigezo vya mwanaume
 
SEHEMU YA 4

unayemuhitaji katika maisha yako lakini
unachopaswa kuangalia ni moyo wake na
dhamira yake ya dhati ya kutaka
kukuoa.Monica mimi kama mama yako
nakushauri nafasi hii usiikatae.Wanawake
wenzako nafasi kama hizi wanaziota
ndotoni.Kwa hiyo Monica nakushauri
ulipokee ombi la David kwa mikono miwili
kwani ni jambo lenye faida nyingi kubwa
kwako na kwetu pia kama familia na hata
nchi kwa ujumla.Ukiolewa na David
utakuwa mke wa bilionea mkubwa
duniani,utakuwa mtu mkubwa na mwenye
nguvu,utafanya mambo mengi yale
ambayo umekuwa ukiota kuyafanya
,utatimiza ndoto zako zote.Dakika
utakayotamka neno nakubali basi maisha
yako yatabadilika .Ukiolewa na David
utaumiliki utajiri wake wote,utafungua
viwanda vikubwa hapa nchini na utaleta
ajira kwa maelfu ya vijana .Kwa kuwa
lengo lako la muda mrefu ni kuisaidia
jamii masikini na yenye uhitaji basi hii
ndiyo
fursa
unayotakiwa
kuitumia.Inawezekana Mungu anataka
kukutumia ili uwasaidie watu wake wenye
uhitaji kwa hiyo isikie sauti yake ndani
mwako na ukubali ombi la David.Mimi
kama mama yako,kama rafiki yako,kama
msiri wako,sina maneno mengine mazuri
zaidi ya kukushawishi kuhusu suala
hili,nimekueleza mengi ,ni juu yako sasa
kupima na kufanya maamuzi sahihi.”
Akasema bi Janet akachukua glasi ya maji
akanywa Monica naye akachukua pakiti
lake la biskuti akatoa moja na
kutafuna,kila mmoja alionekana kuwaza
lake.Mwishowe Monica akauvunja ukimya
“Mama nimekusikiliza kwa makini
na nimefurahi pia kusikia japo kwa ufupi
kuhusu historia yenu wewe na baba.Kwa
ufupi ni kwamba usiku wa leo sikuweza
kupata usingizi kutokana na mawazo
mengi niliyokuwa nayo na kubwa zaidi
ilikuwa ni suala hili .Baada ya tafakari ya
kina nimeamua kulipa nafasi jambo hili”
“ Wow ! that’s good my princess”
akasema bi janet
“Kuamua kulipa nafasi suala ili si
kukubali ombi la David bali nataka nipate
wasaa wa kutosha kutafakari,kumfahamu
David ni mtu wa aina gani na mwisho nitoe
maamuzi.Nina
msimamo
wangu
kuhusiana na mwanaume wa maisha
yangu na sibabaishwi na jina au utajiri wa
mtu na hata nilipotajiwa kuhusu David
Zumo sikustuka sana kwa sababu
ninaufuata moyo wangu hata hivyo
nimeona hakuna sababu ya kutoa
maamuzi ya haraka kuhusu suala hili
kwani inawezekana David akawa ni mtu
mzuri wa kunifaa .Naombeni mnipe muda
wa kutosha ,nataka nijenge kwanza
mahusiano mazuri na David na baadae
nitatoa jibu langu.Kwa hiyo mama jioni ya
leo ninakwenda Congo nimealikwa na
David kutoa mada katika kongamano la
umoja wa vijana wa Congo.”
“Usinitanie Monica.Mara hii David
amekwisha kupa mwaliko?? Bi Janet
akapatwa na mshangao
“Ndiyo mama,leo nakwenda
Congo.David amenipigia simu asubuhi na
kuniomba niende na nimekubali
japokuwa najua anataka kutumia kigezo
hicho kutengeneza ukaribu na mimi.Hicho
ndicho kitu ambacho ninakitaka hata
mimi kuwa karibu naye ili nimfahamu
vizuri.”
“Monica mwanangu Mungu
anakuongoza na ndiyo maana mambo
 
Back
Top Bottom