QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Hatimaye nimefika kwenye foleni ya kusubiri[emoji45] [emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Bado cjapata mbadala Wa hadithi za lege, zina radha kama ya tafrija, au siku ya ndoa, kuna watu wanakaribia ila kwa lege ni mwisho Wa mhunzi
 
SEHEMU YA 11

quick and don’t let anybody know.You are
my only hope.”
Haraka haraka Monica
akaukunja ujumbe ule na kuuweka katika
mfuko wa suruali halafu akatabasamu na
kusema
“ Usijali Marcelo ,kesho nitakuletea
vitu vyote ulivyoagiza ila nataka
nitakapokuja kesho uwe tayari unaongea”
Marcelo akatabasamu .Monica
hakutaka kukaa sana pale hospiali kwani
alihitaji kupata muda wa kujiandaa kwa
safari ya jioni.Akaagana na Marcelo na
kutoka.Mara tu alipotoka nje Julieth dada
wa Marcelo akamfuata.
“ Marcelo alikwambia ana hitaji nini?
Akauliza
“ Kuna baadhi ya vitu
ameniagiza,nitamletea kesho”
“ Jamani kwa nini amekusumbua
namna hii? Nipe mimi hiyo orodha ya
hivyo vitu nikavitafute” akasema Julieth
“ Usijali Julieth nitavitafuta na
kuvileta mwenyewe kesho” akajibu
Monica na kuondoka kuelekea maegesho
akaingia katika gari lake.Akaitoa karatasi
ile yenye ujumbe alioandika Marcelo
akarudia kuusoma na akahisi kijasho
kikimtoka.Akawasha gari na kuondoka
“ Sitaki kuamini eti Dr Marcelo
amepatwa na tatizo la akili hadi akaandika
ujumbe huu.Nina hakika lazima kuna kitu
kinachoendelea.Lazima jambo hili ni la
kweli lakini nani hao wanaotaka kumuua
na kwa nini? Akajiuliza
“ One of them visited me last night”
akakumbuka moja ya sentensi katika
ujumbe ule.
“ Inaonekana Marcelo anawafahamu
watu hao wanaotaka kumuua lakini kwa
nini hawaweki wazi kwa vyombo vya
usalama wawashughulikie? Kwa nini
hataki mtu mwingine yeyote ajue kuhusu
watu hao wanaotaka kumuua? Ninahisi
kuna jambo kubwa linaloendelea hapa na
ndiyo maana hataki kuliweka wazi suala
hili hata kwa ndugu zake.Nadhani suala
hili ni kubwa zaidi ya ninavyofikiria
.Nitafanya nini sasa kumsaidia ?
Nitamuondoaje pale hospitali? Au nikatoe
taarifa polisi? Monica akaendelea kujiuliza
maswali mengi
“ Hapana sitakiwi kuwashirikisha
polisi katika hili.Kama angehitaji msaada
wa jeshi la polisi angenieleza lakini
amesema kwamba hataki mtu mwingine
yeyote afahamu kuhusu suala
hili.Ameniamini mimi peke yangu na
amekiri mimi ndiye tumaini lake.I must
find a way to help him.Najua ni jambo
gumu na la hatari lakini lazima nitafute
namna ya kumsaidia.He’s my friend and I
cant just let him die”
Monica alifika nyumbani kwake na
kuendelea na zoezi la kujiandaa kwa ajili
ya safari.
“ Laiti ningekuwa sijampa uhakika
David kuwa nitakwenda Congo
ningeahirisha safari hii ili nipate muda wa
kushughulikia suala la Marcelo lakini kwa
sasa siwezi tena kuahirisha kwani tayari
ndege iko angani ikija kunichukua.Ngoja
niende
Congo
nitakaporejea
nitalishughulikia suala hili.Naomba
Mungu Marcelo awe salama hadi hapo
nitakapokuwa nimrejea toka Congo”
akawaza Monica
 
SEHEMU YA 12


ege linalotajwa kuwa kubwa kuliko
zote zinazotumiwa na marais wa afrika
linalomilikiwa na rais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo David Zumo tayari
lilikwishatua katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam kwa ajili ya kumchukua
mwanamke mrembo kuliko wote Afrika
,Monica Benedict Mwamsole.
Ilipotimu saa kumi na moja za jioni
,gari ya Monica ikawasili pale
uwanjani.Ndani ya gari alikuwa peke yake
kwani hakutaka watu wafahamu kama
anasafiri .Tayari wazazi wake walikwisha
wasili kitambo na walikuwa wakimsubiri
yeye ili wamuage .Walitumia kama dakika
kumi hivi wakibadilishana hili na lile na
kumpa Baraka zao wakimtakia safari
njema.Monica akaingia katika jengo la
uwanja kwa ajili ya taratibu za safari
.Alipokamilisha taratibu zote akaenda
kuagana na wazazi wake kisha
akaongozana na wahudumu wanne wa
dege hilo waliovalia nadhifu kabisa
kuingia ndegeni

Ama
kweli
David
amedhamiria.Kutuma dege kubwa kama
hili kwa ajili ya tu ya kuja kunichukua
mimi si kitu kidogo.” Akawaza Monica
wakati akipanda ngazi kuingia ndegeni
“ Karibu sana mama Monica” Monica
akasalimiwa na Jean Pierre Muyeye
“ Jean Pierre Muyeye!! Akasema
Monica kwa furaha
Pierre akampeleka Monica katika
sehemu mbalimbali za ndege ile
akamtambulisha kwa marubani na
wahudumu wengine halafu akampeleka
katika chumba maalum cha rais.Saa kumi
na moja na nusu dege likapaa na safari ya
kuelekea Kinshasa ikaanza.Ndani ya
ndege
wahudumu
wachangamfu
walijitahidi kumuhudumia Monica kwa
kila alichokihitaji na kuufanya uso wake
usikauke kwa tabasamu
“ Nimepanda ndege nyingi lakini
sijawahi kupanda ndege nzuri ya kifahari
kama hii.Kweli David ni tajiri
mkubwa.Yeye ni rais pekee Afrika
anayemiliki ndege yake binafsi tena
kubwa kama hii ambayo inafanana kwa
kila kitu na ndege ya rais wa marekani.”
Akawaza Monica na uso wake haukukauka
tabasamu
“ Endapo nitakubali kuolewa na
David ndege hii pia itakuwa ya kwangu na
nitaipanda muda wowote kwenda sehemu
yoyote ninayotaka kwenda.This is
life.Kama alivyonishauri mama misimamo
mingine haina maana sana kitu kikubwa
ni kuangalia moyo na dhamira ya
mtu.David ameonyesha wazi kwamba
ananipenda .Kwa maisha kama haya
mwanamke gani anaweza kukataa ombi la
kuolewa na mtu kama David
Zumo?Nitachekwa hadi na ndege mwitu
nikisema hapana” akawaza Monica akiwa
ndani ya chumba cha kifahari cha David
Zumo ndani ya ndege hii kubwa
 
SEHEMU YA 13


Mr Jing wang Zhu,karibu sana
.Nimefurahi kukutana nawe jioni hii ya
leo” Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania akaanzisha
mazungumzo baada ya kukutana na balozi
wa China nchini Tanzania katika hoteli
yake.Tayari kiza kimekwisha tanda
angani na kwa mujibu wa saa ilionyesha
mida hiyo ilipata saa moja na na dakika
saba za jioni.
“ Mheshimiwa rais hata mimi
nimefurahi sana kukutana nawe jioni ya
leo.Nilikuwa na miadi ya kukutana na
wageni jioni hii lakini baada ya kupata
ujumbe wa kutaka kuonana nawe
imenilazimu kuvunja miadi hiyo na kuja
kukusikiliza.Naamini kuna jambo la
muhimu la kujadili” akasema Jing wang
Zhu
“ Ni kweli mheshimiwa balozi.Kuna
suala la msingi ambalo limenifanya nitake
kuonana nawe jioni ya leo” Ernest
akanyamaza kidogo baada ya sekunde
kadhaa akaendelea
“ Mheshimiwa balozi sitaki nitumie
muda wako mwingi kuelezea kuhusu
mahusiano mazuri ya kindugu baina ya
nchi zetu mbili.Mahusiano yetu
yamekuwa makubwa sana katika Nyanja
zote za kiuchumi na kidiplomasia
.Mahusiano hayo mazuri ndiyo msingi wa
maongezi yetu usiku huu” akasema Ernest.
“ Nakusikliza mheshimiwa rais”
akasema Jing
“ Kuna raia wangu mmoja
anatumikia kifungo cha miaka kumi na
tano katika gereza moja nchini China kwa
kosa la kujaribu kuingiza madawa ya
kulevya nchini China.Ninamuhitaji
msichana huyo na ninataka nimkomboe
kwa hiyo nimekuita jioni hii ili tujadiliane
namna ya kuweza kulifanikisha suala hili”
akasema Ernest.Balozi Jing wang akavua
miwani yake akachukua kitambaa
akafikicha macho na kusema

Mheshmiwa
rais,nadhani
unafahamu sheria za China kuhusu watu
wanaokutwa wakijihusisha na biashara ya
dawa za kulevya zilivyo kali.Serikali ya
China haina masihara katika suala hili na
mfanya biashara wa dawa za kulevya sisi
tunamchukulia kama muuaji na ndiyo
maana wengi wao wanauawa na wengine
kutumikia kifungo kirefu gerezani.Kwa
hiyo mheshimiwa rais suala hilo
unalolihitaji naweza kusema ni gumu
sana kwangu Watu kama hao ni hatari
mno kwa watu wa China na hatuna
huruma nao hata kidogo” akasema Jing
wang Zhu
“ Mheshimiwa balozi,nafahamu
ugumu wa jambo hili na ndiyo maana hapo
awali nilitangulia kuelezea kuhusu
mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi
zetu mbili China na Tanzania.Suala hili
linaweza kumalizwa kirafiki tu bila
kuathiri uhusiano wetu mzuri.Msichana
huyu ninamuhitaji sana arejee Tanzania
na kwa ajili yake niko tayari kufanya
mabadilishano kati yake na raia kumi wa
China waliofungwa hapa nchini.Kuna raia
nane wamefungwa miaka hamsini kila
mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za
serikali ,wengine wawili wamehukumiwa
kunyongwa
kwa
kosa
la
mauaji.Nitawaachia hawa wote kwa ajili ya
kumpata huyo mtanzania mmoja”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais ninaiona nia yako
ya dhati ya kutaka kumkomboa mtu wako
huyo na ndiyo maana uko tayari kuwaacha
watu hao wengi waliohukumiwa hapa
Tanzania.Pamoja na utayari huo lakini
suala hili siwezi kulitolea maamuzi
hapa.Ninaomba
nilichukue
na
niliwasilishe kwa wakuu wangu na
watakachokiamua
nitakujulisha.Ninakuahidi kufanya kila
linalowezekana ili jambo hili lifanikiwe”
akasema balozi Jing wang Zhu
Maongezi kati ya balozi Jing wang
Zhu na rais Ernest Mukasa yaliwapeleka
hadi saa mbili na nusu za usiku kisha
wakaagana balozi akaondoka zake.Baada
ya balozi kuondoka mzee Mukasha
akamfuata rais
“ How did it go mr Mresident?
Akauliza
“ Mambo yamekwenda vizuri
sana.Tumekuwa na mazungumzo mazuri
amelipokea suala langu na ameniomba
nimpe muda awasiliane kwanza na
viongozi wake halafu atanipa jibu.Nina
uhakika mkubwa kwa ombi langu
kukubaliwa kwani mimi na rais wa China
ni marafiki sana.Sasa nahitaji kuzungumza
na mkuu wa magereza.Naomba umruhusu
aje nionane naye tafadhali.” Akasema rais
na kamishna jenerali wa magereza
Elimeleck Akwisa akaingia
 
SEHEMU YA 14


KINSHASA –DRC
Saa mbili na nusu juu ya alama dege
la kifahari aina ya Boeing 747 mali ya rais
David Zumo ikatua katioka uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Kinshasa.Usiku
huu jiji la Kinshasa lilikuwa linang’aa na
kupendeza ukitokea angani.
“ Sikujua kama jiji la Kinshasa
linapendeza hivi ukilitazama kutokea
angani.Hii ni kazi ya David
Zumo.Amelibadilisha mno jiji hili na kuwa
mojawapo ya majiji yanayovutia zaidi
Afrika “ akawaza Monica akilishuhudia jiji
la Kinshasa akiwa ndegeni
Dege lilitua na kusimama,Monica
akawashukuru marubani na wahudumu
kwa kumfikisha salama kisha akaonozana
na Pierre Muyeye kushuka ngazi.
Alipomaliza kushuka ngazi Monica
akapokewa na watoto wawili wadogo
waliomkabidhi maua akainama na
kuwakumbatia akawabusu halafu Muyeye
akamuongoza walikokuwa wamesimama
watu zaidi ya ishirini
“Monica kutana na Pauline Zumo
mke wa rais David Zumo.Hapa Congo
anajulikana kama Malkia.” Muyeye
akamtambulisha
Monica
kwa
Pauline.Nusura
maua
aliyokuwa
ameyashika Monica yamponyoke kwa
mstuko.Hakuwa ametegemea kabisa kama
mke wa David Zumo angeweza kuja
kumpokea pale uwanja wa ndege.Pauline
alikuwa ni mwanamke mrembo na usiku
huu alikuwa aking’aa kwa vito vya
thamani alivyovaa .
“ Monica karibu sana Congo.Karibu
sana Kinshasa.Jisikie nyumbani” akasema
Pauline huku akitabasamu.Monica naye
akatabasamu wakaongea mawili matatu
kila mmoja akimsifia mwenzake kwa
namna alivyopendeza halafu Pauline
akaanza kumtambulisha Monica kwa watu
aliokuwa ameongozana nao pale
uwanjani.Baada ya hapo wakaingia katika
gari la kifahari wakaondoka pale
uwanjani.Ulinzi ulikuwa ni mkali
sana.Ndani ya gari Monica na Pauline
walikuwa wanaongea mambo kadhaa na
kucheka.Kwa muda huu mfupi walitokea
kuzoeana kama watu wanaofahamiana
kwa muda mrefu
Msafara ule uliwasili katika jumba
moja kubwa la kifahari lililowaka taa
nyingi za kupendeza.walinzi wawili
wakafungua milango ya gari lile la kifahari
walimokuwamo
akina
Monica
,wakashuka.Pauline akamuogoza Monica
kuingia ndani ya jumba lile lililokuwa na
uzuri wa kipekee sana.Walikwenda hadi
ghorofa ya pili kulikokuwa na sebule
kubwa iliyosheheni samani za gharama
kubwa
“ Nimeingia katika sebule nyingi
kubwa na nzuri laini sijawahi kuingia
katika sebule nzuri kama hii.Ina uzuri
usioweza kuelezeka.” Akawaza Monica
“ Monica karibu sana hapa ni sehemu
ambayo wageni muhimu wa rais hufikia.Si
sehemu kubwa sana ila tumejaribu
kuifanya iwe ya kupendeza.Ni imani yangu
utapafurahia mahala hapa.” Akasema
Pauline.
“ Wahudumu wapo hapa kwa saa
ishirini na nne na kazi yao ni moja
tu,kukuhudumia.Wapo wapishi ambao
watakupikia
chakula
chochote
ukitakacho,kuna saluni humu ndani na
wapo
wahudumu
maalum
watakaokuremba kwa staili yoyote ile
uitakayo.Ulinzi upo wa kutosha na wa
 
SEHEMU YA 15

uhakika..Monica nimefurahi sana kuonana
nawe ana kwa ana .Narudia tena
kuwapongeza wale waliokutaja kuwa ni
mrembo kuliko wote Afrika
,hawakukosea.Una uzuri wa ajabu sana”
akasema Pauline na wote wakacheka
“ Ahsante Pauline lakini hata wewe
ni mrembo pia” akasema Monica
“ Nakubali mimi ni mzuri lakini
kwako sifiki hata robo.Monica
umebarikiwa uzuri wa kipekee “ akasema
Pauline halafu akamuomba Monica
waongozane kwenda katika chumba cha
chakula
Katika chumba cha chakula
walikuwemo wahudumu waliovalia
nadhifu ,wakiwa wamesimama kwa adabu
tayari kabisa kutoa huduma ya chakula
kwa Pauline na mgeni wake.Monica
akawasalimu wahudumu wale halafu
wakaketi katika meza kubwa yenye viti
kumi na mbili .Vyombo vyote
vilivyotumika kwa chakula vilikuwa vya
dhahabu.Uzuri wa jumba hili ulimsisimua
mno Monica.
“ Kweli huyu ndiye tajiri wa
Afrika.Pamoja na kukulia katika utajiri
lakini sijawahi hata mara moja kula kwa
kutumia sahani au kijiko vyote vya
dhahabu.Haya ni maisha ya kifahari mno.”
Akawaza Monica wakati wakiendelea
kupata chakula
Walipomaliza
kula
Pauline
akampeleka Monica katika chumba
ambacho angelala kilichokuwa katika
ghorofa ya tatu.Kilikuwa ni chumba
kikubwa kilichosheheni samani za
gharama kubwa
“ Monica hiki ni chumba ambacho
utalala.Sifahamu unapendelea vitu gani
katika chumba chako cha kulala lakini
nimejitahidi kukiweka kifanane na hadhi
ya malkia wa afrika.Kama kuna
mapungufu yoyote utanijulisha” akasema
Pauline
“Pauline ahsante sana.Hiki ni
chumba kizuri mno .Nimekipenda sana”
akasema Monica na Pauline akatabasamu
“ Ahante Monica kama umekipenda
.Naomba nikuache upumzike .Kesho saa
nne asubuhi nitakuja kukuchukua
tutakwenda sehemu kupata chakula cha
mchana pamoja na maongezi kidogo”
akasema Pauline halafu akamuelekeza
Monica mambo kadhaa ya mle chumbani
,akaondoka
“ Haya yanayonitokea mbona naona
kama ni ndoto?Mambo yamekuwa tofauti
sana na nilivyotegemea.Nimealikwa na
David Zumo kuhudhuria kongamano la
vijana ambalo alidai linaanza kesho lakini
kesho Pauline amesema kwamba
atanichukua twende mahala tukapate
chakula cha mchana na maongezi
kidogo.Mhh !! haya ngoja nisubiri nione
nini kinachoendelea hapa.hata hivyo
nimempenda Pauline,ni mwanamke
mkarimu sana.kwa namna alivyonipokea
sina hakika kama anafahamu chochote
kuhusu mambo anayotaka kuyafanya
mume wake.Sina hakika kama anafahamu
mume wake anataka kunioa.Baada ya
kuonana na Pauline nadhani
sintakubaliana tena na ombi la
David.Siwezi kuingilia ndoa ya Pauline na
kuiharibu furaha aliyonayo.Sitaki
kuibomoa ndoa yake.Sitaki kumuumiza
.Kwa namna sisi wanawake tulivyo pindi
akigundua kitu anachotaka kukifanya
mume wake urafiki wetu utatoweka na
tutakuwa maadui.Sitaki jambo hilo
initokee.Kama ni utajiri na mali hata
mimi ninaweza kufanya kazi kwa bidii
kwa kutumia vipawa ambavyo Mungu
amenijalia na nikaupata.” Akawaza Monica
baada ya Pauline kuondoka.Mara
akamkumbuka Dr Marcelo
“ Masikini Dr Marcelo sijui
anaendeleaje hivi sasa..Mpaka sasa bado
sijapata njia ya kuweza kumsaidia kumtoa
pale hospitali. Naomba aendelee kuwa
salama hadi hapo nitakaporejea Dar es
salaam ili nitafute namna ya kufanya
kumuokoa dhidi ya watu wanaotaka
kumuua.Najua ni suala la hatari but I’m
too involved now and I must help him”
akawaza huku akijiandaa kwenda kuoga.
 
SEHEMU YA 16


DAR ES SALAAM – TANZANIA
Inakaribia saa tano za usiku,bado
rais Ernest Mkasa alikuwa hotelini akiwa
na mazungumzo na Kamishna Jenerali wa
Magereza .Walikuwa na maongezi ya kina
sana.Wakiwa bado katika maongezi
akaingia Mukasha na kumnong’oneza rais
jambo na kutoka
“ Kamishna nimepata dharura
kidogo nalazimika kwenda sehemu
Fulani.Nakushukuru sana kwa kufika na
kwa kunielewa.Nitawasiliana nawe tena
muda wowote nitakapopata jibu toka kwa
balozi wa China.Naomba nikukumbushe
kuwa mambo haya tuliyoyazungumza ni
ya siri kubwa na jitahidi asifahamu mtu
mwingine yeyote.”
“ Mheshimiwa rais usiwe na wasi
wasi kabisa ,mambo yote yatafanyika kwa
siri sana na hakuna yeyote
atakayejua.Mheshimiwa rais ahsante sana
naomba sasa niende ili nikupe muda wa
kuendelea na majukumu mengine.”
Akasema mkuu wa magereza na
kusimama akampa mkono rais
wakaagana.Baada ya mkuu wa magereza
kuondoka Ernest akamuita mlinzi wake
mkuu
“ Evans kuna sehemu nataka kwenda
usiku huu lakini sihitaji kwenda na
msafara au walinzi zaidi yako kwani sitaki
kufahamika.Ninataka nitumie gari la
kawaida ambalo si rahisi kwa mtu yeyote
kuhisi
kuwa
rais
anaweza
akalitumia.Najua taratibu haziko hivyo
lakini ninalotaka kufanya ni la muhimu
mno”
“ Sawa mheshimiwa rais naomba
unipe dakika kumi nifanye maandalizi”
akasema Evans na kutoka.Ernest akaingia
chumba cha kulala akafungua kabati na
kuchagua mavazi ya kuvaa .Alichagua
suruari ya jeans ya bluu na shati zuri
halafu akavaa koti jeusi ,kofia na miwani
myeusi.Shingoni akavaa mkufu mkubwa
wa dhahabu.Mwisho kabisa akaweka
ndevu za bandia kidevuni na haikuwa
rahisi kumtambua kuwa ni rais Ernest
Mkasa.Akajitazama katika kioo na
kutabasamu
“Kwa muonekano huu hata mke
wangu hawezi kunitambua.” Akawaza
Ernest halafu akampigia simu Mukasha
akamtaarifu kuwa yuko tayari.Baada ya
dakika mbili Mukasha na Evans wakaingia
mle chumbani
“ Mzee tayari kila kitu kimekamilika
na tunaweza kuondoka.Tutapita upande
huu wa nyuma na kwenda hadi katika
maegesho ya VIP 2.Hakuna mtu yeyote
upande ule atakayekutambua “ akasema
Evans
“ Evans sitaki gari zaidi ya mbili”
akasema Ernest “
“ Ndiyo mzee kuna gari mbili tu.Moja
utapanda wewe na mzee Mukasaha na
nyingine nitakuwepo mimi na walinzi
wengine wawili.Mheshimiwa rais pamoja
na kwamba safari hii ni ya kibinafsi lakini
lazima uwe na ulizi wa kutosha kwa hiyo
tutakuwa walinzi watatu”
“ Sawa Evans.Tunaweza kuondoka”
akasema Ernest na kumgeukia Mukasaha
“ Tutawahi kabla ya ndege haijatua?
“ Ndiyo mzee.Ndege itatua baada ya
dakika ishirini toka sasa kwa hiyo
tutawahi.Usiku huu magari yamepungua
sana
barabarani”
akasema
Mukasha.Walitoka ndani ya kile chumba
wakapita upande wa nyuma hadi mahala
zilikoegeshwa gari mbili .Evans
akamfungulia rais mlango katika gari la
nyuma akaingia pamoja na Mukasha
halafu yeye na walinzi wawili wakaingia
katika gari la mbele wakaondoka pale
hotelini.Mukasha ndiye aliyekuwa
akiendesha gari lile alimopanda rais
“ Kila kitu tayari kimekaa sawa
kilichobaki kwa sasa ni kusubiri jibu la
 
SEHEMU YA 17


kutoka China ili mchakato wa
mabadilishano uweze kufanyika mara
moja” Ernest akamueleza Mukasha
wakiwa garini
“ That’s good Mr President” akajibu
Mukasha na safari ikaendelea kimya
kimya.Waliwasili uwanja wa ndege dakika
nne kabla ya muda wa ndege waliyoisubiri
kuwasili.
“ Tumewahi mheshimiwa rais.Ndege
inatagemewa kuwasili ndani ya dakika
chache zijazo” akasema Mukasha
Hatimaye ndege waliyokuwa
wanaisubiri ikawasili katika muda ule ule
uliopangwa.Hii ilikuwa ni ndege maalum
ya rais yenye kasi ya aina yake iliyotumwa
na rais kwenda Afrika ya kusini
kumchukua Austin January na kumleta
Dare s salaam.Tayari Mukasha na mlinzi
mmoja walikwisha ingia ndani ya uwanja
kwa ajili ya kumpokea Austin.Mlango
ukafunguliwa na Austina akiwa
ameambatana na wanausalama wawili
waliotumwa kumfuata Afrika ya kusini
wakashuka na kupokewa na Mukasha
halafu akamuongoza kutoka nje ya uwanja
moja kwa moja hadi katika gari alimo rais
akamfungulia Austin mlango na kumtaka
aingie.Mizigo ya Austin ikaingizwa katika
gari la walinzi na bila kupoteza hata
dakika moja wakaondoka pale uwanjani.
“ Hallow Austin “ akasema Ernest na
kuivua kofia aliyokuwa ameivaa,akatoa
miwani na zile ndevu za bandia
“ Mr President !! Austin
akashangaa.Alipoingia mle garini hakuwa
amemtazama vizuri mtu aliyekuwa
amekaa pembeni yake na wala
hawakusalimiana.
“ Pole na safari Austin,Karibu tena
Tanzani”
“ Mr President what are you doing
here? Samahani sikujua kama ni
wewe.Umebadilika sana” akasema Austin
“ Nimefanya hivi ili niweze kuja
kukupokea mimi mwenyewe na
nihakikishe kama kweli umefika
Tanzania.Wewe ni mtu muhimu sana”
“ Ahsante mheshimiwa rais”
akasema Austin na kugeuza shingo
kutazama nje .Alionekana kutokuhitaji
maongezi.
“ Nimefurahi Austin amefika
salama.Anaonekana ni kijana mahiri
sana.Hana maongezi mengi.Anaonekana ni
mtu wa kazi tu.Huyu atanifaa sana
kunifanyia kazi zangu za siri.Nitafanya kila
niwezalo kuhakikisha haondoki tena
Tanzania ili nimuajiri kwa ajili ya kazi
zangu.Nimesoma faili lake,amepata
mafunzo ya hali ya juu sana ya ujasusi
.Amepata
mafunzo
nchini
Israel,Marekani,China
na
hata
japan.Amepata pia mafunzo nchini Iran na
Iraq kuhusiana na mitandao ya kigaidi na
namna wanavyofanya kazi zao.Amefanya
pia mafunzo ya kupambana na magaidi
akiwa na vikosi vya Marekani nchini
Afghanistani na ameiva sana katika
kupambana na magaidi.Anazifahamu
mbinu nyingi wanazotumia magaidi na
ndiyo maana aliweza hata kufahamu
mahala walikofichwa Watanzania
waliotekwa na kundi la Alshabaab nchini
Somalia na akakiongoza kikosi maalum
kwenda kuwakomboa.Taifa linapaswa
kujivunia kuwa na mtu kama huyu lakini
nashangaa kwa nini alitaka kuuawa?
Inawezekana aligusa maslahi ya watu
Fulani na ndiyo maana akaonekana ni mtu
mbaya na hivyo akatakiwa afe.Suala lake
 
SEHEMU YA 18


ni kubwa na ndiyo maana limefanywa
siri.” Akawaza Ernest na kugeuza shingo
akamtazama Austin
“ Anaonekana bado ana hasira na
Tanzania na kama isingekuwa mdogo
wake katu asingekubali kuja .Kijana huyu
ni hazina kubwa kwa taifa hili na
nitamlinda.Anatakiwa kulindwa kama
mboni ya jicho.” Akaendelea kuwaza
Ernest.Safari ikaendelea kimya kimya
Walifika Mikinda iliko nyumba ya
Ernest ambako ndiko Austin
atakapoishi.Ni nyumba nzuri ya ghorofa
mbili iliyozungukwa na ukuta mrefu imara
.Milango ya gari ikafunguliwa Ernest na
Austin wakashuka
“ Karibu ndani Austin” Ernest
akamkaribisha ndani Austin.
“ Austin hapa ndipo utakapoishi.Hii
ni nyumba yangu na miezi michache
iliyopita alikuwa akiishi balozi wa
Denmark hapa nchini.Ni nyumba kubwa
ya ghorofa mbili.Ina mfumo wa kisasa wa
ulinzi .Nitaongeza vile vile walinzi watatu
wa kukulinda.Kesho asubuhi watakuja
wafanyaazi wawili mmoja kwa ajili ya
kukupikia na mwingine kwa ajili ya kazi
nyingine za ndani kufua n.k.Hapo nje kuna
gari tatu za kisasa ambazo
utazitumia.Kama kuna chochote kingine
utakachokihitaji utanijulisha.” Akasema
Ernest.Ukapita ukimya mfupi Ernest
akasema
“ Kama hutajali naomba
nikuzungushe katika sehemu mbali mbali
za jumba hili uzifahamu”
Walizunguka sehemu mbali mbali za
jumba lile na sehemu ya mwisho ikawa
katika chumba cha kulala.Kilikuwa ni
chumba kizuri kikubwa kilichochukua
sehemu kubwa ya ghorofa ya pili.Mle
chumbani wakaketi katika sofa nzuri
nyeupe
“ Austin umeiona nyumba
imekuridhisha? Naomba uwe muwazi
kama haijakuridhisha nieleze ili
nikutafutie nyumba nyingine mimi nina
nyumba nyingi.” Akasema Ernest na kutoa
mkebe katika koti akaufungua na kutoa
sigara kubwa akaiweka mdomoni halafu
akatoa nyingine na kutaka kumpa Austin
“ Cigar ?... akamuuliza Austin endapo
angehitaji
“ No thanks.” Akajibu Austin.Ernest
akawasha sigara yake na kuvuta mikupuo
kadhaa
“ Mzee kuna mambo mawili ambayo
nataka niyaweke wazi kwako” akasema
Austin
“ Karibu” akasema Ernest
“ Kwanza nataka mifumo yote ya
usalama katika nyumba hii itolewe, na
wala sihitaji mtu yeyote wa
kunilinda.Nitaweka mifumo yangu
mwenyewe ninayoiamini.Sihitaji pia
mfanyakazi , kazi zote nitafanya
mwenyewe.Jambo la pili nataka kufahamu
kuhusu mchakato wa kuachiwa huru dada
yangu umefikia wapi.Sintoifanya kazi yako
yoyote hadi hapo nitakapohakikisha kweli
dada yangu ameachiwa huru.” Akasema
Austin.Ernest akavuta mkupuo mkubwa
na kupuliza moshi mwingi hewani na
kusema
“ Tukianzia na suala hilo la pili,tayari
mchakato umekwisha anza na uko katika
hatua nzuri.Tayari nimekwisha zungumza
na mamlaka za China na ninachosubiri ni
jibu toka kwao muda wowote kwa hiyo
usiwe na wasi wasi Austin niamini na kila
 
SEHEMU YA 19


kitu kitakwenda vizuri.Kuhusu usalama
hilo ni jukumu langu kukulinda kwani
ndiye niliyekuleta hapa.Maadui zako bado
wapo na wakifahamu kuwa upo hai na
umerudi Tanzania watasuka mipango ya
kutaka kukuangamiza tena .Sitaki jambo
hilo litokee na ndiyo maana ninataka
kuimarisha ulinzi kila mahala
ulipo.Niruhusu nitumie nguvu niliyo nayo
kukulinda Austin”

Ahsante
mheshimiwa
rais,sijamaanisha kuutoa mfumo huu wa
usalama hapa ndani basi nikae bila
kujilinda la hasha ,nitaweka mfumo wangu
wa ulinzi ninaouamini zaidi” akasema
Austin
“ sawa Austin uko huru kufanya
chochote utakachojiskia kufanya lakini
usisite kuomba msaada wowote
utakaohitaji muda wowote” akasema
Ernest
“ Ahsante mheshimiwa rais.Kwa sasa
mimi na wewe nadhani hatuna chochote
cha kuongea .Tutazungumza pale dada
yangu atakapokuwa ametoka gerezani
.Naomba nikutakie usiku mwema
mheshimiwa rais” akasema Austin na
kuinuka akampa mkono Ernest wakatoka
mle chumbani wakashuka chini.Ernest
akawachukua watu wake wakaondoka

mambo
yamekwendaje
mheshimiwa rais? Akauliza Mukasha
“ Mambo bado.Mchakato wa kumtoa
gerezani mdogo wake ukikamilika ndipo
tunaweza kuzungumza lakini kwa sasa
amekataa tusizungumze chochote.”
Akasema Ernest na kuegemea kiti
“ Toka nimekuwa rais nimekuwa
karibu sana na hawa watu wa usalama wa
taifa lakini sijawahi kukutana na mtu
kama Austin.Nitahakikisha haondoki
Tanzania ” akawaza Ernest
“ Im back again.Back to Tanzania”
akawaza Austin akiwa amekaa kibarazani
akitazama mataa ya jiji la Dar es salaam
“ Niliapa kutokurudi tena Tanzania
lakini nimevunja kiapo changu na
nimerejea tena.Sina namna nyingine ya
kufanya kumsaidia dada yangu atoke
gerezani zaidi ya kukubali kuifanya kazi
ya rais.Masikini Linda kwa nini aliamua
kujiingiza katika biashara hizo haramu
wakati alikuwa na utajiri mkubwa ambao
ungemuwezeha kuendesha maisha yake
kwa miaka mingi bila hata kufanya kazi?
Lakini yote haya yamesababishwa na mimi
kutokuwepo.laiti kama ningekuwepo
karibu naye asingejiingiza katika mambo
kama haya.Lazima nifanye kila lililo ndani
ya uwezo wangu kumsaidia.Siwezi
kujilaumu sana kwa sababu sikuwa na
namna nyingine ya kufanya kwa wakati
ule zaidi ya kutoweka.Nisingeweza
kurejea Tanzania na wala nisingeweza
kumueleza Linda mahala nilipo kwa ajili
ya usalama wake.Angefahamu mahala
nilipo ningemuweka katika hatari kubwa.”
Akawaza Austin
“ Akifanikiwa kutoka gerezani sitaki
arejee tena Tanzania.Nataka akaishi mbali
ambako ataanza maisha mapya
.Nitamsaidia kuanzisha biashara kubwa na
ataishi maisha mazuri.Nikimaliza kazi ya
rais nitaondoka na sintarejea tena
Tanzania na nitafanya mipango ya
kuungana na dada yangu tena.” Akawaza
Austin na kumbu kumbu nyingi zikaanza
kumjia kichwani
“ I loved this country with all my
heart lakini kwa sasa ninaichukia
.Ninaichukia Tanzania kwa sababu ya
 
SEHEMU YA 20


watu wachache walioiuza nchi hii na
kuitumbukiza katika mambo machafu ya
laana .Kwa mfano hivi sasa kuna mswaada
unaotaka kuwasilishwa bungeni ambao
unataka kutambua haki za wapenzi wa
jinsia moja na utoaji mimba.Haya ni
mambo ambayo yanalipeleka taifa hili
katika laana na inaniumiza kwa sababu
watu waliopewa dhamana ya kuiongoza
nchi hii wamewageuka wale waliowapa
dhamana ya kuwaongoza.Nilikuwa
kikwazo kwao na walitaka kunitoa uhai
lakini wakashindwa.Wao ndio sababu ya
mdogo wangu Linda kujitumbukiza katika
biashara haramu.Kama nisingeikimbia
nchi kwa sababu yao mdogo wangu
angeendelea kuishi maisha mazuri .I’m
back again and I must fight them with all
the strength I have.Nahisi ni kama vile
Mungu amenirudisha nyumbani ili nije
niiokoe nchi yangu.Safari hii watakimbia
wao wakajifiche na si mimi
tena.Nitawanyima usingizi na nitahaikisha
ninawafagia mmoja baada ya mwingine.”
Akawaza Austin na kukumbuka kitu
“ Nimemkumbuka mpenzi wangu
Maria,alilia
machozi
mengi
nilipomwambia kwamba ninakuja
Tanzania.Maria ananipenda kwa dhati na
amekuwa nguzo kubwa katika maisha
yangu.Natakiwa kuwasiliana naye
kumjulisha kuwa tayari nimekwisha fika
Dar es salaam.” Austin akaingia ndani
akafungua begi lake dogo akatoa
kompyuta akawasha na kumpigia simu
Maria mchumba wake kwa kupitia
mtandao wa Skype
“ Hallow Austin my love” akasema
Maria.Austin akatabasamu baada ya
kuiona sura ya Maria
“ Maria sijui umenipa nini mpenzi
wangu kwani kila ninapoiona sura yako
akili yangu inahama.Unaendeleaje
malaika wangu?
“ Ninaendelea vizuri Austin.Muda si
mrefu nimemaliza kikao na Alnoor na
kesho au kesho kutwa tutasaini mkataba
.Nimechoka kukaa hapa Dubai.Wiki ya
tatu sasa niko mbali nawe.Tukishasaini
mkataba nitaondoka haraka sana”
“ Good job Maria.Najua haikuwa kazi
rahisi kumshawishi Alnoor akubali
kufanya biashara nasi.Mimi tayari
nimekwisha wasili Dar es salaam muda si
mrefu”
“ Ahsante kama umefika salama
mpenzi wangu.Mimi nitakapomaliza
mambo ya huku kesho au kesho kutwa
nitakuja moja kwa moja Dar es salaam.Ni
muda mrefu sijafika Dar “ akasema Maria
huku akitabasamu na kuzichezea nywele
zake ndefu.
“ Maria my love nakuomba sana
malaika wangu usije Dar es
salaam.Ukitoka Dubai nenda moja kwa
moja nyumbani Afrika kusini mimi
nitakapomaliza tu kazi iliyonileta huku
basi nitaondoka haraka sana kurejea
huko.Narudia tena kukuomba Maria
tafadhali usije Dar es salaam.”
Maria akacheka kidogo na kusema
“ Mbona una wasiwasi hivyo? Austin
wiki hizi tatu nilizoishi mbali nawe
nimejihisi kama mfu.Nimejihisi kama ....oh
no!! Nashindwa hata kukueleza how I
feel.Siwezi kuvumilia zaidi ya hapa.Kwa
hiyo Austin nitakapomaliza tu mambo
yangu huku Dubai nitapanda ndege na
kuja Tanzania and please don’t say
 
SEHEMU YA 21



no.Hakuna mjadala katika hilo” akasema
Maria.
“ Maria tafadhali mpenzi wangu
nakupenda sana zaidi ya kitu chochote
duniani,nakuomba usije Dar .Kama
ujuavyo kwamba huku si sehemu salama
kwangu lakini nimekuja tu kwa sababu ya
lile suala la dada yangu kwa hiyo siwezi
kuhatarisha maisha yako kwa kukuruhusu
uje huku Dar es salaam.Nisubiri Afrika
kusini sintakawia kurudi” akasema Austin

Austin
hakuna
kitu
utakachonieleza kitakachonizuia nisije
Dar.Hapo ni nyumbani kwetu na ninaweza
kuja muda wowote nikitaka lakini nijapo
safari hii ni kwa ajili ya kukufuata wewe
tu.Siogopi hayo masuala ya usalama kwani
najua utanilinda.Kwa hiyo Austin nitakuja
Dar es salaam au labda kuna sababu
nyingine iliyokupeleka huko tofauti na
hilo suala la ndugu yako na hautaki mimi
nifahamu .Au umepata mwanamke huko?
Au umerudia zile kazi zako? Akauliza
Maria
“ Maria ondoa mawazo
hayo.Kilichonileta huku ni suala la mdogo
wangu ambaye amejiingiza katika
madawa ya kulevya na hakuna jambo
lingine.Siwezi kurudia zile kazi zangu
tena.Nimekwisha
achana
nazo
kabisa.Kuhusu mwanamke mwingine
ondoa wasi wasi katika hilo ,wewe ni
pekee nikupendaye katika dunia
hii.Thamani yako kwangu ni kubwa kuliko
hata kontena lenye madini ya almasi.Kwa
hiyo hakuna mwigine anayeweza kuwa na
thamani ya juu kukushinda wewe”
akasema Austin na kumfanya Maria
atabasamu
“ Mungu amekujalia ulimi wenye
kutamka maneno matamu ambayo
hunifikisha mbingu ya saba.Basi ngoja
nikuache upumzike kwani tayari
nimekwisha hisi kuanza kuchafuka huku
chini kutokana na msisimko ninaoupata
kwa kuongea nawe.Nitakutaarifu kesho
kama tutakuwa tumesaini mkataba na
Alnoor ili ujue siku nitakayokuja Dar .One
more thing kesho nataka unipe namba ya
simu unayotumia ukiwa Dar.I love you
baby” akasema Maria na kufunika
kompyuta yake.Austin akashika kichwa
“ Maria anataka kuja Dar es
salaam.Nilimdanganya kuwa ninakuja
kushughuilikia suala la mdogo wangu
anayetumia madawa ya kulevya
.Nisingeweza kumueleza kuwa nimeitwa
na rais kuna kazi anataka nimfanyie kwani
nilikwisha kula kiapo cha kuachana na
kazi hizi na endapo atakuja Dar lazima
ataufahamu ukweli.What am I going to do?
akajiuliza
“ Akiufahamu ukweli ataumia sana
kwani hii ni mara ya kwanza
ninamdanganya hataniamini tena.Maria
nampenda sana na na sitaki kumuumiza
lakini lazima nifanye kazi ya rais kwa ajili
ya kumsaidia mdogo wangu.Mimi nadhani
sina namna nyingine ya kufanya zaidi ya
kumueleza ukweli potelea mbali kama
ataumia lakini sina namna nyingine ya
kumsaidia mdogo wangu zaidi ya kufanya
kazi ya rais.” akawaza Austin
 
SEHEMU YA 22

Simu iliyopigwa na balozi wa China
nchni Tanzania ilimkuta rais Ernest Mkasa
tayari amekwisha amka kitambo na
alikuwa anajiandaa kwenda katika
mazoezi ya asubuhi kama kawaida
yake.Ilipata saa kumi na mbili na dakika
tatu za asubuhi.
“ Hallow mheshimiwa balozi”
akasema Ernest baada ya kupokea simu
“ Habari za asubuhi mheshimiwa
rais”
“ habari nzuri mheshimiwa
balozi.Nadhani una habari nzuri za kunipa
asubuhi hii” akasema Ernest
“ Ndiyo meshimiwa rais.Ninazo
taarifa nzuri asubuhi ya leo.Nimetaarifiwa
muda mfupi uliopita na msaidizi wa rais
kuwa kutokana na urafiki mzuri baina ya
China na Tnzania,rais amekubali ombi
lako kwa hiyo tutafanya mabadilishano ya
wafungwa.Kwa hiyo mheshimiwa rais saa
tano kamili leo kwa saa za hapa Tanzania
mfungwa Linda atakabidhiwa kwa ubalozi
wa Tanzania nchini China na kwa taratibu
za mabadilishano zilivyo muda huo huo
wafungwa wa China watakabidhiwa kwa
ubalozi wa China hapa Tanzania.Natumai
tumeelewana meshimiwa rais”
“ Nashukuru sana mheshimiwa
balozi.Siwezi elezea furaha yangu kwa
jambo hili kufanikiwa.Makabidhiano
yatafanyika kama kawaida katika muda
huo.Mheshimiwa
balozi
narudia
kukushukuru tena.Ahante sana” akasema
Ernest na kukata simu.
“Sasa kazi yangu inakwenda
kufanyika kwani Austin hakuwa tayari
kufanya chochote
hadi
pale
atakapohakikisha mdogo wake ametoka
gerezani.” Akawaza Ernest huku
akizitafuta namba za simu za Mukasha na
kumpigia
“ Habari zaa asubuhi mheshimiwa
rais” akasema Mukasha baada ya kupokea
simu
“ Habari nzuri Mukasha.Nimepokea
simu muda si mrefu kutoka kwa balozi wa
China anasema ule mpango umefanikiwa
kwa hiyo saa tano kamili leo kwa saa za
Tanzania mabadilishano yatafanyika
katika balozi zetu.Kwa hiyo lishghulikie
suala hili”
“ Hizo ni taarifa njema sana
mheshimiwa rais.Nitamtaarifu mkuu wa
magereza suala hili ili mchakato uanze
mara moja” akasema Mukasha .
“ Sawa Mukasha,shughulikia suala
hilo na tutawasiliana baadae’ akasema
Ernest na kukata simu akatoka mle
chumbani akasalimiana na walinzi wake
akaelekea katika mazoezi.Mara tu
alipotoka mle chumbani,bi Agatha Mkasa
mke wa Ernest akaichukua simu na
kupekua akaipata namba ya simu ya mtu
aliyekuwa anaongea na rais muda mfupi
uliopita
“ Jing wang Zhu??...akajiuliza
“ Balozi wa China na Ernest wana
mpango gani unaoendelea? Nimemsikia
Ernest akiongelea kuhusu makabidhiano
yatakayofanyika leo,wanakabidhiana kitu
gani? Nahisi kuna jambo Ernest ananificha
kwani nimegundua kwa siku za karibuni
amebadilika ghafla .Ni wazi kuna jambo
linaloendelea chini kwa chini na hataki
kunitaarifu.Nimemuona hata usiku
anakuwa macho muda mwingi ,lazima
kuna kitu kinamsumbua” akawaza
“ Ili nifahamu kinachoendelea lazima
nimchunguze Mukasha kwani ndiye
aliyetumwa kuhakikisha makabidhiano
hayo yanafanyika”
i Agatha akairudisha simu mezani
na haraka akaichukua simu yake
akazitafuta namba Fulani akapiga
“ Hallow “ akasema Agatha baada ya
simu yake kupokelewa upande wa
pili.Baada ya salamu Agatha akasema
“ Muhsin nimekupigia asubuhi hii
kuna jambo nataka nikueleze.Kwa siku
kadhaa nimeona mabadiliko kwa Ernest
nikahisi kuna kitu kinamsumbua.Leo
asubuhi nimemsikia akizungumza na
balozi wa China hapa nchini na walikuwa
wanazungumiza
kuhusu
makabidhiano.Sifahamu ni makabidhiano
gani hayo ila ninaamini kuna kitu
kinachoendelea kati ya Ernest na balozi
wa China.Kuna chochote unachokifahamu
kuhusu Ernest na balozi wa China?
“ Mhh !! hapana sifahamu chochote
.Rais hajanieleza jambo lolote” akajibu
Muhsin.
“Damn you Muhsin,you are a vice
president and its your job to know
everything that’s going on.Tunakutegemea
sana wewe kujua kila kinachoendelea
katika ofisi ya rais.Be smart Muhsin.Find
out whats going on.Kwa kukusaidia kujua
kinachoendelea ni kwamba tuma vijana
wamchunguze Mukasha kwani ndiye
aliyekabidhiwa
kazi
hiyo
aisimamie.Kupitia kwake kuna kitu
tunaweza kukigundua” akasema Bi Agatha
“ Agatha ahsante kwa taarifa
nitaifanyia kazi” akajibu Muhsin
Abdulkareem masoud makamu wa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania na
kukata simu
 
Back
Top Bottom