QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 23


KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA
YA CONGO
Saa ya dhahabu iliyokuwa
inaning’inia ukutani ilionyesha tayari
imekwisha timu saa mbili na dakika tisa za
asubuhi.Taratibu Monica akatoka
kitandani na kusimama katikati ya
chumba kile kikubwa na kutabasamu
.Alivutiwa mno na uzuri wa chumba kile.
“ Jana sikukichunguza vizuri chumba
hiki ..mhh ni chumba chenye uzuri wa
ajabu kabisa.” Akaenda dirishani akafunua
pazia na kuchungulia nje
‘” Wow !! akajikuta akitamka baada
ya kuishuhudia mandhari ya aina yake
kulizunguka jumba lile
“ This house is amazing.Kuna uzuri
wa kipekee kabisa mahala hapa.Panavutia
na unaweza kutamani uishi hapa maisha
yako yote” akawaza na kuvaa nguo zake za
mazoezi akatoka mle chumbani
,akasalimiana na wafanyakazi wa ndani
halafu akaelekea katika chumba cha
mazoezi.Kisha maliza mazoezi akarejea
chumbani akaoga na akiwa katika
kujiandaa kengele ya mlangoni ikalia
akaenda kuufungua mlango akakutana na
mwanadada mrembo aliyejitambulisha
kama mpambaji wake mkuu,akamtaka
waongozane hadi katika saluni
iliyokuwamo ndani ya hilo jengo ambako
Monica akarembwa vilivyo.
Kisha maliza kujiandaa akaenda
katika chumba cha chakula akapata
kifungua kinywa halafu akarejea tena
chumbani kumsubiri Pauline ambaye
alimuahidi kuwa angefika kumchukua
.Wakati akimsubiri Pauline Monica
akatumia simu iliyokuwao mle chumani
kuwapigia simu wazazi wake
akawahakikishia kwamba anaendelea
vizuri na wasiwe na wasiwasi.Kisha maliza
kuwasiliana na wazazi wake akapata wazo
“ Natamani nijue hali ya Dr
Marcelo.Mtu pekee ambaye anaweza
akanipa habari za Marcelo ni Daniel “
akawaza na haraka haraka akaziandika
namba za simu za Daniel kwani
alizifahamu kwa kichwa akampigia.
“ Hallow” ikasikika sauti ya Daniel
upande wa pili wa simu
“ Daniel its me Monica”
“ Monica!! How are you? Umenipigia
kwa namba hi...” akasema Daniel lakini
Monica akamkatisha kabla hajaendelea
zaidi
“Daniel nimekupigia kutaka
kufahamu jambo moja tu.Ni kuhusiana na
Dr Marcelo.Anaendeleaje?
“ Nimetoka kumtazama leo asubuhi
anandelea vizuri lakini bado hajaanza
kuzungumza.Bado anatumia maadishi
kuwasiliana.Amekuulizia nikamdanganya
kuwa umepata dharura nje ya Dar es
salaama na akasema nikukumbushe
kuhusu ombi lake.Hizi ni namba za Congo
 
SEHEMU YA 24

umekw......” akasema Daniel lakini kabla
hajamaliza Monica akasema

Niko
Kinshasa.Kumbuka
nilikueleza kwamba nimepata safari ya
dharura kwa hiyo niko hapa Kinshasa
nitarejea kesho au kesho kutwa” akasema
Monica akaagana na Daniel akakata simu
“ Hili suala la Marcelo mbona linazidi
kuniumiza kichwa ? Kama ameendelea
kukumbusha kuhusu ombi lake la
kunitaka nimsaidie ,basi ni kweli kuna
watu wanaotaka kumuua.How am I going
to help him? Akajiuliza
“ I must find a way to hep him as
quick as possible.Siwezi kuach.....” Monica
akaondolewa mawazoni na mlio wa
kengele ya mlangoni.Akaenda kuufungua
na kukutaa na sura inayong’aa yenye
tabasamu ya Pauline Zumo
“ Monica” akasema Pauline kwa
furaha.
“ Pauline karibu sana,nimestuka
nikadhani ninatazamana na malaika “
akasema
Monica
na
wote
wakacheka.Pauline alipendeza mno.Alivaa
suti nzuri nyeupe iliyomkaa vyema na bila
kusahau vito vya thamani .Baada ya
maongezi machache Pauline akamtaka
Monica amfuate wakatoka nje ya jumba
lile na kuelekea moja kwa moja sehemu
kulikokuwa na helkopta ya rangi nyeupe
wakaingia
na
helkopta
ikapaa.Walilitazama jiji la Kinshasa
kutokea angani na kuufanya uso wa
Monica usikaukiwe tabasamu.Helkopta ile
ilitua katika uwanja mzuri wenye nyasi za
kijani za kuvutia uliokuwa pembeni ya
hoteli moja kubwa.Mlango ukafunguliwa
Monica na Pauline wakashuka
Pauline akamuongoza Monica hadi
katika meza iliyokuwa kandoni mwa mto
mdogo uliopita pemeni ya hoteli hiyo
kubwa.Bata wazuri weupe walikuwa
majini wakiogeleza na kuifanya mandhari
ya eneo lile kuwa ya kuvutia mno.Haraka
haraka wahudumu wakafika na kuanza
kuwahudumia.Pauline akawataka walinzi
wake wasogee mbali na kuwaacha peke
yao
“ Monica mahala hapa panaitwa
hoteli Patrice.Ni hoteli inayomilikiwa na
rafiki yangu.Mimi hupenda sana kuja hapa
mara moja kila juma kupunga upepo .Hii
ni hoteli inayosifika nchini Congo kwa
kuwa na madhari nzuri ya kuvutia.”
Akasema Pauline.
“ Kweli Pauline hii ni sehemu nzuri
na hata mimi nimepapenda” akasema
Monica.Pauline akainua glasi ya maji
akanywa na kusema
“ Monica nimekuleta hapa nje ya jiji
kwa ajili ya maongezi ya muhimu mno”
akasema Pauline na kumfanya Monica
ahisi baridi kwa ndani,alianza kuingiwa na
woga.
“ nahisi atakuwa amegundua kitu
anachotaka kukifanya mumewe na
anataka kunikanya,nilifaya kosa kubwa
kukubali ombi la David la kuja Congo.I’m
so stupid! Akawaza Monica na macho yake
yalionyesha wasiwasi mkubwa alionao
“ Kama nilivyojitambulisha kwako
jana naitwa Pauline Zumo mke wa David
Zumo rais wa Congo.Historia yangu na
David ni ndefu na tuna miaka 12 sasa
katika ndoa yetu.Tulifunga ndoa tukiwa
bado vijana sana.Baba yangu na baba yake
David ni marafiki wakubwa na urafiki huo
ndio uliopelekea hata mimi na David
tukawa marafiki wakubwa ,urafiki
uliotupeleka hadi katika ndoa.Baba yake
 
SEHEMU YA 25


David alikuwa mwanasiasa na mfanya
biashara tajiri ambaye alimshawishi David
aingie katika siasa na kwa bahati nzuri
watu wa Congo wakavutiwa naye na
wakamchagua awe rais.Amefanya mambo
mengi makubwa kiasi cha kuwafanya raia
wa Congo wamtake awe kiongozi wao wa
maisha.” Pauline akatabasamu baada ya
sekunde kadhaa akaendelea.
“ Mimi na David tuna maisha mazuri
ya furaha lakini kuna jambo moja ambalo
kwa miaka mingi sasa limekuwa
linatunyima usingizi na kama
tusingekuwa na mapenzi ya dhati toka
mioyoni mwetu basi ndoa yetu ingekwisha
sambarataika lakini penzi letu lina mizizi
imara na ndiyo maana kila uchao penzi
letu linachanua “ Akanyamaza akainua
glasi yake ya maji akanywa halafu
akaendelea
“ Mimi na David tunalo tatizo letu la
ndani ambalo hatujawahi kumueleza mtu
yeyote na leo nitakueleza kwa mara ya
kwanza.Toka tumeoana hadi leo hii
hatujabahatika kupata mtoto na hatuna
mategemeo ya kupata mtoto kwani sina
uwezo wa kubeba mimba.Kizazi changu
kiliondolewa ili kunusuru maisha yangu”
Pauline akainama na sura yake
ikabadilika akaonyesha namna jambo lile
linavyomuumiza.Monica
akamuonea
huruma sana.Pauline akaendelea
“ Jambo hili limekuwa linaniumiza
mno japokuwa kila dakika uso wangu
unatabasamu na watu wananiona ni
mwanamke mwenye furaha lakini ndani
nina mauivu ambayo hakuna anayeweza
kujua uchungu wake zaidi ya Mungu
pekee.Tuna mali nyingi mno,ni matajiri
namba moja Afrika lakini huwezi kuamini
kila usiku ninapopanda kitandani
hufumba macho na kumuomba Mungu
anichukue ili nisiione kesho na kuzidi
kuteseka.Sina hamu na kuishi tena
.Nimekwisha kata tamaa” akasema na
machozi yakamtoka.Akachukua kitambaa
akafuta machozi na kuendelea
“ Yapata miaka mitatu sasa imepita
nilifanya maamuzi .Nilimruhusu David aoe
mke wa pili.Nilimtaka afanye hivyo ili
tuweze kupata mtoto,mrithi wa utajiri
wetu huu mkubwa.David hakuwa tayari
kwa hilo hadi hivi juzi baada ya kutoka
katika mkutano Dar es salaama
aliponifuata na kunieleza kwamba
amekubali ombi langu na tayari ameona
mwanamke anayeweza kutufaa.Kwangu
hizo zilikuwa ni taarifa njema sana na
nikataka kumfahamu mwanamke huyo
ambaye amebadili msimamo wa David na
ndipo aliponieleza kwamba ni
wewe.Nilijikuta na mimi nikivutiwa nawe
sana na nikataka nikufahamu zaidi na
David akakuomba uje kwa ajili ya
kuhudhuria kongamano la vijana.Kwa
ufupi utatusamehe sana Monica kwani
hakuna Kongamano hilo alilokueleza
David bali hili lilikuwa ni wazo langu kwa
lengo la kutaka kukuona.Kwa hiyo Monica
karibu sana Congo.Tunafurahi na tunaona
fahari kubwa kuwa na mgeni kama wewe”.
akanyamaza Pauline akamimina maji
katika glass akanywa kidogo na
kumgeukia Monica.
“Monica huna haja ya kunieleza
wewe ni nani kwani tayari nimekwisha
fanya uchunguzi wangu na kufahamu kila
kitu kuhusu wewe na nimetokea
kukupenda sana.Sote tunakupenda.David
alinieleza kuwa hakuweza kukutamkia
wazi wazi kuhusu azma yake ya kutaka
 
Duh ! Duh !
Nilikua nikijizui sana kucomment lakini kumbe ni kama nilikua najaribu kuzuia mdomo kuongea.

Mkuu lege wewe ni muungwana sana maana kama ningekua mimi kwa jinsi raia hapa walivokua wanakusimanga japo ulikua ukijitahid sana kuleta muendelezo kila upatapo wasaa ningekua nishawabwaga..thanx in advance kwa busara na ukarimu wako wa kutoa burudani bila malipo maana ni adimu sana kupata huduma za mfano huo
 
Monica umezingua sana ole wako Marcelo afe yani amekupa taarifa ume ignore umeenda congo
 
Naona Monica kashakubal ndoa na raisi hapo kikwazo kitakua Mzee Ernest huyu hawez kubali binti yake aolewe na kibabu
 
Mgogoro mwingine unaanza katika familia ya Rais Ernest naona mkewe nae anaanza udukuzi hii stori ni tamu haina mfano
 
Dah!aiseee..yan naisoma hii story kwa hisia kali mnoo..mpk najiona mimi ndo km austin vile[emoji16][emoji16]
 
Kweli mambo ni matamtam. Asante sana LEGE , we jamaa ni wa pekee sana. Na uendelee kuwa hivyo hivyo, usiwe kama wale. Najua usiposhusha mzigo unakuwa umekosa time tu. Pamoja na madongo ya baadhi ya wasomaji wasiyo wavumilivu lakini hujawahi kuvunjika moyo au kukasirika. Una busara ya hali juu mno. Much respect. Keep it up Bro!!
 
Back
Top Bottom