SEHEMU YA 32
DAR ES SALAAM - TANZANIA
Inakariabia saa mbili na nusu jijini
Dar es salaam rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Ernest mkasa
yupo katika chumba chake maalum ndani
ya hoteli hii anayoimiliki .
“Mukasha nadhani ni muda
muafaka sasa wa kwenda kuonana na
Austine”Ernest akamweleza Mukasha
aliyekuwa naye mle chumbani
wakijadiliana mambo kadhaa,akainuka na
kurejea katika chumba cha kulala na kama
alivyofanya siku iliyotangulia akabadili
muonekano wake.akajitazama na
kutabasamu.
“ Austin amenifanya nikumbuke
mbali sana enzi za ujana wangu.Nimepitia
mambo mengi sana na siamini eti leo hii
mimi ni rais a jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Kweli maisha yana maajabu
.Najikubali kwa historia ya maisha yangu
sikuwa na vigezo vya kuniwezesha
kushika nafasi kubwa na nyeti kama hii
.I’m a monster,lakini tazama nilipo
sasa,niko katika ofisi kubwa kuliko zote
nchini.Kweli hakuna kisichowezekana
chini ya jua” akawaza Ernest na kutoka
mle chumbani na kama ilivyokuwa usiku
uliopita akaongozana na Mukasha na
Evans mlinzi wake wakazunguka upande
wa nyuma ambako kuna njia ya siri ya
kupita wakaingia katika magari na
kuondoka.
Waliwasili katika nyumba anayoishi
Austin.Evans akashuka na kubonyeza
kengele ya getini baada ya dakika tatu geti
likafunguliwa na gari zile mbili zikaingia
ndani.Rais akafunguliwa mlango akashuka
“ Hallow Austine” akasema Ernest
“ Karibu sana mheshimiwa rais”
akasema Austin na kugeuka akaanza
kupiga hatua kuelekea ndani.Mukasha
,Evans na wale walinzi wengine wawili
wakaambatana
nao.Mara
Austin
akageuka.
“ Namuhitaji rais peke yake humu
ndani.Wengine mtasubiri nje”
“ Hilo halitawezekana kaka.Huyu ni
rais wa nchi na jukumu letu ni kumlinda
katika sehemu anayokwenda .Hatuwezi
kumuacha peke yake hata sekunde moja.”
Akasema Evans.Austin akamuelekezea
macho Ernest
“ You want to talk to me ? Waambie
watu wako wabaki nje “ Austin
akamwambia Ernets ambaye aliwataka
walinzi wabaki nje akaingia ndani na
Austin
“ Karibu mheshimiwa rais” akasema
Austin na kumkaribisha rais sofani
“ Ahsante Austin lakini hukupaswa
kufanya vile,wale ni walinzi wangu
walioapa kuyatoa maisha yao kunilinda
,wanastahili heshima”
“ I’m sorry mr President ,that’s how I
work.I don’t trust people so easily.Ukitaka
kufanya kazi na mimi lazima ukubali tabia
zangu”
“ Sawa hakuna tatizo.Umeshindaje
leo?