QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] mimi tyar nshamaliza

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
QUEEN MONICA
SEASON 6

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Mzee Pantaleo sijafika
ofisini kwako kwa muda mrefu
kidogo.Vipi maendeleo ya huko?
Akauliza rais
“ Maendeleo mazuri
mheshimiwa rais.Kila kitu kiko
sawa na hakuna tatizo lolote”
“ Nafurahi kusikia
hivyo.Kuna kitu nataka
unisaidie.Niletee ile hati ya
muungano nahitaji kuipitia
kuona maendeleo
yake.Nimeelekezwa kuna
teknolojia mpya ya kuweza
kuhifadhi nyaraka mbali mbali
kwa miaka mingi kwa ubora
mkubwa.Niletee niangalie ubora
wake ili nione kama tunaweza
kuhitaji hiyo teknolojia mpya au
tuendelee na hii tuliyonayo sasa”
akasema rais
“ Sawa mheshimiwa rais.”
Akasema mzee Pantaleo na
kuondoka
“ I don’t know if I’m doing
the right thing .Ninachokifanya
ni kitu hatari mno kwa taifa na
endapo hili litafahamika
wananchi watanitafuna nyama
au ninaweza kuozea
gerezani.Hata mimi inaniuma na
sipendi kufanya hivi lakini kipi
bora kuitoa hati ya muungano
au kuiacha nchi iharibiwe na
Alberto’s? Mimi kwa upande
wangu naona ni afadhali nchi
ikavunjika vipande kuliko
kuwaacha Alberto’s watekeleze
mipango yao miovu kwa nchi
yetu.Misuko suko mikubwa
itatokea lakini nitakabiliana
nayo na kama siku moja huko
mbeleni itagundulika hiki
nilichokifanya naamini wapo
watakoniunga mkono kwani
ninafanya haya kwa ajili ya
kuokoa kizazi cha watoto wetu
kisipotee” akawaza Ernest
Mzee Pantaleo akarejea
akiwa na mkoba mdogo mweusi
akaufungua na kutoa ile hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar iliyokuwa na jalada
gumu jekundu.
“ Kuna yeyote aliyeona au
kuifahamu kuwa umeitoa hati
hii? Rais akauliza
“ Hakuna anayefahamu .Ni
mimi pekee”
“ Good.Asifahamu mtu
yeyote.Ngoja niipitie halafu
baadae nitakuita uje uichukue.”
Akasema rais na mzee Pantaleo
akaondoka.
Kwa zaidi ya dakika tano
rais alikuwa ameinamisha
kichwa akitazama hati ile ya
muungano
“ I have to do this” akasema
Rais
“ Tayari nimekamilisha kila
kitu walichokihitaji.Ninaye Tariq
na vile vile Yasmin.Kilichobaki ni
kitu kimoja tu anachokitaka
Yasmin ambacho ni mwanae
Maria” akawaza rais na
kuchukua simu akajaribu
kupiga namba za simu za Austin
na Job lakini simu zao
hazikupatikana.
“ Kuna tatizo gani? Mbona
simu zao leo hazipatikani? Au
wameshambuliwa? Akajiuliza
halafu akachukua simu na
kuzitafuta namba fulani akapiga
“ Hallow mzee shikamoo”
ikasema sauti ya upande wa pili
“ Marahaba Bill.Nipe ripoti
mmefikia wapi kuhusu
Mukasha?
“Mpaka sasa bado
hatujapata taarifa zozote za
kuhusu Mukasha ila bado
tunaendelea kumsaka”
“ Vipi kuhusu Job?
Mlifanikiwa kufahamu mahala
alipo?
“ Hapana mzee.Mpaka sasa
bado hatufahamu”
“ Sawa Bill.Msifanye
chochote kwa sasa hadi hapo
nitakapowajulisha .Ninakaribia
kufahamu mahala aliko ila
ongezeni nguvu katika kumsaka
Mukasha” akasema rais na
kukata simu
“Nilikuwa na wasiwasi labda
yawezekana akina Bill
walifahamu aliko Job na
wakawavamia lakini
hawajafanya hivyo.Kwa nini
basi wote wazime simu?Saa tano
leo natakiwa kumkabidhi
Yasmin hati hii lakini lazima
nimpate Maria pia ili nifanye
mabadilishano na Yasmin.Jana
nilimueleza kwamba nitampa
mwanae endapo atanirejeshea
hati ya muungano.Lakini
kitendo cha akina Austin
kuzima simu wote kwa pamoja
kimenifanya nianze kuwa na
wasi wasi” akawaza rais.
“ Sitakiwi kupoteza muda
kuwawaza hawa jamaa kwani ni
watu ambao ninawamudu na
ninachokisubiri kwako ni
majibu ya kile kipimo cha
vinasaba .Nikipata majibu hayo
nitawafutilia mbali” akawaza na
kutazama saa yake akainuka
akaipakia hati ile ya muungano
katika mkoba na kutoka
akawaagiza walinzi wake
kupunguza magari katika
msafara wake na kubaki na
magari matatu tu na kuwapa
maelekezo wanakoelekea
“Hii ndiyo safari ya mwisho
ya Tanzania.Endapo juhudi za
kuipata tena hati ya muungano
zitagonga mwamba ndio
utakuwa mwisho wa nchi
inayoitwa Tanzania kwani
hakuna uhalali wa kuitwa
Tanzania bila kuwa na hati
inayoonyesha kuwa
Tanganyikana Zanzibar
ziliungana.Kuna wazo
nimelipata .Natakiwa
kumshughulikia mzee
Pantaleo.Endapo mambo
yataharibika huyu mzee
atakuwa wa kwanza kutoa
siri.Nitawelekeza vijana wangu
wamshughulikie haraka sana
kabla ya mchana wa leo”
akawaza rais
ENDELEA…………………………..
 
SEASON 6: SEHEMU YA 1
Ndege aina ya Cessna
Citation Longitude yenye uwezo
wa kubeba watu kumi na mbili
ilikaribia kutua katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Abeid
Amani karume .Marubani
walioendesha ndege hii walifuata
maelekezo waliyopewa na
Yasmin na kuomba kutua kwa
dharura katika uwanja huo
wakidai kugundua hitilafu ya
kiufundi.Yasmin akamfuata
Tariq..
“Sikiliza Tariq,sina lengo
baya na wewe lakini naomba
kitu kimoja.Ndege inakaribia
kutua kisiwani unguja na
ikishatua mimi na wewe
tutashuka na hatutaendelea na
safari yetu.Tutampigia simu
Habib na kumueleza kwamba
ndege yetu imepata hitilafu za
kiufundi na tumelazimika kutua
kwa dharura Unguja hadi hapo
ndege yetu itakapokuwa ndipo
tutakapoendelea na safari
yetu.”Akasema Yasmin.Tariq
akamtazama kwa hasira na
kusema
“ Sikujua kama u mjinga
kiasi hiki Yasmin.Unawezaje
kutusalit wenzako namna
hii?Unafahamu madhara ya hiki
unachotaka kukifanya? Kwa
kweli sikutegemea kabisa kama
ungeweza kufanya ujinga kama
huu.Habib alikuamini sana
lakini umechagua
kumsaliti.Nakuhakikishia lazima
utalipa kwa usaliti huu mkubwa
unaoufanya.” Akasema Tariq
“Tariq tuko karibu kugusa
ardhi naomba ufahamu jambo
moja.Mimi na wewe sote
tumefungwa nchini Tanzania
kwa miaka mingi lakini hawa
watu tunaowatumikia
Alshabaab na IS hawajaonyesha
juhudi zozote za kututoa
kifungoni.Kama isingekuwa rais
ana mipango yake na akafanya
makubaliano na Habib basi
tusingeweza kuliona tena jua
katika maisha yetu.Tungefika
gerezani.Nikiwa gerezani
nimetafakari sana kwa nini
tupate shida hizo zote?
Tunapigana kwa ajili ya
nani?Tumekwisha mwaga damu
za watu wengi wasio na hatia
yoyote lakini nini faida yake?
Hakuna tulichokipata mpaka leo
na maisha yetu yamekuwa kama
ya ndege.Lazima
tubadilike.Binafsi nimeamua
kuachana na IS na kuanza
maisha mapya.Nataka na wewe
ulifikirie suala hilo lakini
tutazungumza zaidi
tutakapotoka nje ya uwanja”
akanyamaza Yasmin baada ya
ndege kugusa ardhi.
“ Tayari ndege imegusa
ardhi.Ikisimama mimi na wewe
tutashuka ,utafuata maelekezo
yangu na utakuwa
salama.usiogope
nitakulinda,lakini ukijaribu kwa
namna yoyote ile kutaka kupiga
kelele au kufanya chochote kile
kwa wanausalama
nitakumaliza.Mimi ni mtu
mbaya sana nadhani umewahi
kusikia sifa zangu kwa hiyo
sitaki mchezo hata
kidogo.Umenielewa Tariq?
Akauliza Yasmin,Tariq akawa
kimya
“Tariq umenielewa ? Uko na
mimi?
“Ndiyo “ akajibu Tariq
“Vizuri.” Akasema Yasmin
na kumfungua Tariq kisha
akawafuata marubani.Tayari
ndege ilikuwa imesimama.
“Baada ya ndege kutua
mimi na mwenzangu tutajifanya
wagonjwa kutokana na mstuko
tulioupata baada ya ndege
kupata hitilafu angani na
mtaomba gari la wagonjwa lije
hapa kutuchukua kutupeleka
hospitali.Baada ya hapo mimi na
ninyi tutakuwa
tumemalizana,mtarejea Dar es
alaam” akasema Yasmin na
kufungua begi lake akatoa kitita
cha shilingi milioni nne
akawapatia wale marubani.
“Hizo ni kwa ajili ya ukimya
wenu.Tusaidieni tutoke nje ya
uwanja huu salama” akasema
Yasmin na marubani
wakatazamana
“ Nini tutamwambia rais?
Maagizo tuliyopewa ni
kuwafikisha Mogadishu”
Akauliza mmoja wa marubani
“Tafuteni namna yoyote ya
kumueleza rais lakini mimi mna
mwenzangu safari yetu imeishia
hapa” akasema Yasmin .Tayari
maafisa na mafundi wa uwanja
wa ndege walikuwa wamefika
katika ndege ile ili kujua tatizo
lililotokea.kabla ya yote
wakaomba kwanza gari la
wagonjwa kwa ajili ya
kuwakimbiza hospitali,abiria
wawili waliokuwamo ndani ya
ndege ile waliopata mstuko
baadaya ndege kupata hitilafu
angani.gari la wagonjwa likafika
haraka sana pale uwanjani tariq
na Yasmin wakaingia na
kuelekea hospitali kwa ajiliya
uchunguzi wa afya.
Walifikishwa hospitali
wakachunguzwa afya zao na
hawakubainika kuwa na tatizo
lolote hivyo wakapewa
mapumziko ya muda kabla ya
kuruhusiwa kuendelea na safari
yao.Wakiwa katika sehemu ya
mapumziko pale
hospitali,Yasmin akampigia
simu Habib kwa kutumia simu
aliyopewa na mmoja wa vijana
wa rais na kumjulisha kwamba
ndege waliyokuwa wamepanda
kuelekea Mogadishu ilipata
hitilafu za kiufundi ikiwa angani
hivyo ikalazimika kutua kwa
dharura mjini
Unguja.Alimfahamisha kuwa
wakati ule walikuwa hospitali
wakichunguzwa afya zao
kutokana na mstuko walioupata
baada ya hitilafu kutokea.Ili
kuhakikisha kama kile
alichokisema Yasmin ni cha
kweli ilimlazimu Habib kufanya
mawasiliano na uongozi wa
uwanja wa ndege wa Abeid
amani Karume ili kupata ukweli
wa jambo lile.Alihakikishiwa
kwamba ni kweli tukio hilo
limetokea na ndege iko pale
uwanjani ikifanyiwa uchunguzi
na pindi uchunguzi ukikamilika
basi ndege itaruhusiwa
kuendelea na safari yake
kuelekea Mogadishu.Habib
akawasiliana tena na Yasmin na
kumtaarifu kuwa kwa namna
yoyote itakavyokuwa ahakikishe
anaitunza sana hati ile ya
muungano.Yasmin
akamhakikishia asiwe na wasi
wasi kila kitu kiko salama.
Walipumzika hapo hospitali
kwa muda wa nusu saa kisha
Yasmin akaomba waruhusiwe
waondoke wawahi uwanja wa
ndege kuendelea na
safari.Waliruhusiwa kuondoka
wakakodisha taksi na
hawakurejea tena uwanja wa
ndege bali walielekea hoteli
Lepatido.Hii ni moja ya hoteli
kubwa na mpya mjini
Unguja.Pale hotelini
walijiandikisha kama mke na
mume na wakapewa chumba
kimoja.Yasmin hakutaka kukaa
mbali na Tariq kwani bado
hakuwa amemuamini moja kwa
moja.
“Hii ni hatua ya kwanza na
imemalizika salama.Bado safari
inaendelea kutafuta kuwa huru
mbali na Alshabaab na IS”
akasema Yasmin na kukaa juu
ya godoro zuri kubwa na
laini.Akakiangalia kile chumba
na kutabasamu
“Nilikosa sana aina hii ya
maisha .Sikutegema kama siku
moja ningeweza tena kuishi
maisha ya namna hii,kulala
katika godoro zuri kama hili”
akasema na kufumba macho na
kumbu kumbu mbali mbali za
maisha yake zikaanza kumjia .
“Yasmin” akaita Tariq na
kumuondoa Yasmin katika
mawazo mazito aliyokuwa nayo.
“ Unasemaje Tariq?
Umeshalifanyia kazi lile wazo
nililokupa? Akauliza Yasmin
lakini Tariq hakumjibu kitu
akabaki anamtazama
“Mbona sura yako
haionyeshi uchangamfu?
Changamka Tariq,huu ni wakati
wetu wa kufurahia maisha.Tuko
huru na Alshabaab na hata
IS.Cheer up!! Akasema Yasmin
“ Yasmin hiki
unachokifanya ni kosa kubwa
sana na kina madhara
makubwa mno kwetu .Tafadhali
naomba ufikirie mara ya pili
kuhusu suala hili” akasema
Tariq
“Tariq sipendi kurudia rudia
kile nilichokisema.Nilikuambi
kwamba utafuata kile
nitakachokueleza.Ninajua
ninachokifanya na sitaki
kufundishwa namna ya kufanya
mambo yangu.Hebu fumbua
macho Tariq .Tumekuwa
tunapambana kwa ajili ya
nini?Kwa miaka mingi
tumekuwa tunaua watu wengi
ambao hawana hatia yoyote
,kwa ajili ya nini au nani? Kuna
faida gani ambayo tumepata
katika mauaji haya
tuliyoyafanya? Hakuna chochote
tunachokipata.Kama
nilivyokueleza tukiwa ndani ya
ndege kwamba tumefungwa
gerezani kwa miaka mingi lakini
wale tunaowatumikia
hawajafanya juhudi zozote za
kututoa magerezani.Kama
isingekuwa ni rais wa Tanzania
ana mipango yake na akafanya
makubaliano na Habib basi
tusingeweza kamwe kutoka
gerezani.Kwa miaka zaidi ya
kumi sijawahi kuliona jua
nimefungwa katika gereza lililo
chini ya bahari lakini wale
tunaowatumikia wameendelea
kuishi maisha yao mazuri bila
kutukumbuka.Swali ambalo
unapaswa kujiuliza ni je bado
kuna sababu ya kuendelea
kuwa sehemu ya hawa watu ?
Kwa upande wangu jibu ni
hapana.Nimekaa gerezani
nimeyatafakari mno maisha
yangu na tayari nimefanya
maamuzi kwamba sitaki tena
kuendelea na IS.Nataka nianze
maisha mapya .Umri wangu
umekwenda na ninataka katika
maisha yangu yaliyobaki niishi
kwa amani na furaha.Hebu
jiangalie kwanza
ulivyo,unaonekana
kituko.Hauna mbele wala
nyuma.Wewe ndiye uliyekuwa
mratibu mkuu wa mashambulio
ya Alshabaab ambayo yameua
watu wengi lakini katika wale
wote uliowaua nini umekipata?
Hakuna chochote zaidi ya
kuchuma dhambi.Tariq
ninakupa nafasi mwisho ya
kubadilika na kama ukishindwa
sintakuwa na namna nyingine
ya kukusaidia.Fikiria sana
kuhusu jambo hilo na leo saa
mbili usiku ninataka
jibu.Endapo utaamua kuendelea
na Alshabaab nitakuacha uende
zako lakini kama ukiamua
kubadilika na kuanza maisha
mapya basi nitakusaidia.”
Akasema Yasmin na Tariq
akabaki kimya.
“Twende tukazunguke
madukani tununue baadhi ya
vitu na mavazi na sisi tuonekane
kama binadamu
wengine.Tutakaporejea tutaingia
katika awamu ya pili ya
mchakato wetu wa kuondoka
Tanzania na kuelekea katika
maisha mapya”akasema Yasmin
wakaondoka kuelekea madukani
kununua baadhi ya vitu
ambavyo wangevihitaji
 
SEASON 6: SEHEMU YA 2
Vishindo viwili vikubwa
vililitikisa jiji la Dar na kuzua
taharuki kubwa kwa wakazi
wake ambao kwa muda huu wa
jioni wengi walikuwa katika
harakati za kurejea majumbani
kwao baada ya pilika pilika za
kutwa nzima.Moshi mkubwa
mweusi pamoja na vumbi kubwa
vilitanda eneo ulikotokea
mlipuko ule na hivyo kuwafanya
watu wawe na shauku ya
kutaka kufahamu nini
kimetokea .Zilipita dakika tano
baada ya mlipuko kutokea
ving’ora vya magari ya magari ya
polisi na zimamoto vikasikika na
kwa kasi kubwa wakielekea
sehemu ulikotokea mlipuko ule
mkubwa.Bado moshi mzito
uliendelea kutanda eneo
lile.Wananchi walizuiliwa
kulikaribia eneo lile kwa ajili ya
usalama wao.Vikosi viliwekwa
mbali kidogo na eneo lile huku
jitihada za kuuzima moto
ulioendelea kuwaka na kutafuta
manusura zikiendelea.
Wakati jiji la dar likiwa
katika taharuki ile kubwa taarifa
nyingine zikasikika kwamba
jengo la bunge mjini Dodoma
nalo pia limelipuliwa na
hakukuwa na taarifa za awali
zilidai kwamba hakukuwa na
mtu hata mmoja aliyekuwamo
ndani ya jengo lile aliyetoka
hai.Taharuki kubwa ikatanda
nchini.Vyombo vyote vya ulinzi
na usalama vikawekwa katika
tahadhari kubwa .Ofisi na
majengo yote ya umma na
sehemu zile zenye kubeba
mikusanyiko mikubwa ya watu
yakaongezewa ulinzi mkubwa.
Dunia nzima ikaelekeza macho
yake Tanzania na kulaani vikali
mashambulio mawili makubwa
yaliyopelekea vifo vya watu
wengi hasa viongozi .
Hadi ilipofika saa mbili za
usiku bado hakukuwa na taarifa
yoyote iliyotolewa kwa umma
kuhusiana na tukio lile.Vyombo
vya usalama viliwahimiza
wananchi wajitahidi kuwa
watulivu na watapewa taarifa
baadae kuhusiana na tukio
lile.Wananchi waliendelea
kuaswa kuchukua tahadhari
kuepuka mikusanyiko mikubwa
na yeyote mwenye taarifa zozote
zinazoweza kusaidia alitakiwa
kuziwasilisha katika vyombo vya
usalama ili zifanyiwe kazi..
Viongozi wengi wa dunia
waliendelea kumtumia rais wa
Tanzania salamu za rambi rambi
na pole kwa wananchi wa
Tanzania kufuatia
mashambulio yale makubwa
.Wakati dunia nzima ikilaani
mashambulio yale,video
iliyomuonyesha kiongozi mkuu
wa Alshabaab Habib Alzaraq
ilirushwa na kituo kimoja
kikubwa cha runinga kilichopo
huko nchi za kiarabu.katika
video hiyo habib alikiri
Alshabaab kuhusika katika
mashambulio yale mawili
yaliyotokea nchini Tanzania .
“Naitwa Habib
Alzaraq,kiongozi mkuu wa
Alshabaab” ndivyo alivyoanza
katika video hiyo
“Dunia nzima imeelekeza
macho yake nchini Tanzania
kufuatia mashambulio mawili
yaliyotokea jioni ya leo nchini
humo.Nachukua nafasi hii
kuitaarifu dunia kwamba
Alshabaab ndio tuliotelekeza
mashambulio hayo mawili
.Huu ni mwanzo tu wa vita
yetu na Tanzania na
tutaendelea kuishambulia
kila mara hadi pale serikali
ya Tanzania itakapoondoa
wanajeshi wake walioko
katika ardhi ya Somalia
wakilifundisha jeshi la
Somalia .Tumekwisha ionya
mara nyingi serikali ya
Tanzania kuhusiana na
kuwaondoa wanajeshi wake
walioko nchini Somalia
wanaosaidia kulijenga upya
jeshi la Somalia kwa kuwapa
mafunzo lakini wamepuuza
na sasa tumeamua kutumia
nguvu ili kuwashinikiza
kuwaondoa wanajeshi wake
katika ardhi yetu.
Tunatoa nafasi nyingine
kwa seriali ya Tanzania
kuwaondoa haraka sana
wanajeshi wake walioko
nchini Somalia kama
wanataka damu isiendelee
kumwagika.Bila kufanya
hivyo tutaendelea kumwaga
damu ya watanzania kila
uchao hadi pale serikali ya
Tanzania itakapoondoa
wanajeshi wake katika ardhi
yetu.
Kilichotokea leo Tanzania
ni fundisho kwa mataifa
mengine kwamba mzozo wa
Somalia si wa kuingiliwa .Hii
ni vita yetu na mtuachie
wenyewe.Hatutaki taifa lolote
katika ardhi yetu kwa
kisingizio cha kusuluhisha
mgogoro wa Somalia.Yeyote
atakayekanyaga ardhi ya
Somalia na kuisaidia serikali
iliyopo madarakani
tutamuhesabu ni adui yetu na
tutapambana naye bila kujali
ukubwa wala nguvu
zake.Mwisho narudia tena
kuitaka serikali ya Tanzania
na wale wote wenye majeshi
yao Somalia kuyaondoa mara
moja kabla ya damu nyingi
zaidi kumwagika katika nchi
zao”
Ndivyo alivyomaliza Habib
Alzaraq kiongozi mkuu wa
Alshabaab .

SEASON 6: SEHEMU YA 3
Taarifa za mashambulio yale
mawili yaliyotokea dar es salaam
na Dodoma ziliwastua na
kuwachanganya sana Austin na
wenzake.Walisimamisha kazi
zote wakakaa sebuleni
wakifuatilia matangazo ya moja
kwa moja katika runinga
kuhusiana na tukio lile la
kustusha sana.
“ Najaribu kutakakari
kuhusiana na matukio haya
mawili.Ukitazama m uda
yaliyotokea unakaribiana sana
na hii inanipa picha kwamba
yawezekana mshambuliaji
anaweza kuwa mmoja.Dah ! hili
ni shambulio kubwa sana
ambalo halijawahi kutokea
katika historia ya Tanzania na
afrika mashariki kwa ujumla.”
Akasema Austin
Wakati wakiendelea kujadili
juu ya tukio lile mara wakapata
taarifa kuwa katika kituo kimoja
cha runinga cha nje ya nchi
kulionyeshwa video ya kamanda
mkuu wa Alshabaab akijtapa
kuhusika katika mashambulio
yale.Kwa kutumia simu yake ya
mkononi Amarach akaitafuta
video ile na kusikia kile
alichokisema Habib.
“Alshabaab !!! akasema
Austin kwa mshangao
“ Alshabaab ndio
waliohusika na mashambulio
haya? Akazidi kushangaa
“Mbona umestuka Austin
kusikia ni Alshabaa ndio
waliofanya shambulio hili?
Akauliza Job
“ Hainiingii akilini job.Kwa
nini iwe sasa ? Kwa nini
washambulie leo? Vikosi vya
wanajeshi wa Tanzania walioko
nchini Somalia kwa ajili ya
kulifundisha jeshi la Somalia
vina wanajeshi wasiozidi
hamsini na wako nchini Somalia
kwa miaka kadhaa sasa kwa
nini kwa muda huo wote
wasishambulie Tanzania hadi
leo hii? Kingine kinachonifanya
niwe na mashaka ni kwamba
nchi zilizojitolea kujenga upya
jeshi la Somalia si Tanzania
pekee bali kuna Afrika
kusini,Angola na Misri lakini
kwa nini wachague kushambulia
Tanzania pekee? Ndugu zangu
hili jambo linanipa ugumu
kidogo.” Akasema Austin na
kuitazama tena video ile ya
Habib
“ Kwa mujibu wa maelezo ya
huyu anayejiita Habib Alzaraq
kiongozi wa Alshabaab
yawezekana wameamua kuanza
na Tanzania ili kuzifanya nchi
nyingine zenye majeshi yake
nchini Somalia kuyaondoa
kabla nazo hazijashambuliwa.”
Akasema Amarachi
“ Mawazo yako yanaweza
kuwa sahihi Amarachi lakini
kwa upande wangu bado akili
yangu inakataa kabisa
kukubaliana na hiki
walichokifanya
Alshabaab.Wanajeshi wa
Tanzania walioko Somalia ni
wachache sana ukilinganisha na
ukubwa wa mashambulio
waliyoyafanya.Kikosi cha
wanajeshi wasiozisdi hamsini
hakiwezi kusababisha ukalipua
hoteli ile yenye watu wengi
wakiwamo wageni toka mataifa
mbali mbali na kama haitoshi
kulipua pia ukumbi wa bunge
na kwa mujibu wa taarifa za
awali hakuna mbunge ambaye
anasemekana kutoka hai.Hata
hivyo tusubiri taarifa kamili
itakapotolewa kuhusiana na
mashambulio haya na hapo
tutapata mwanga zaidi”
akasema Austin na kuendelea
kutazama matukio katika
runinga ambapo juhudi za
kuuzima moto na kuwatafuta
manusura wa mashambulio yale
mawili ya Dar es salaama na
Dodoma zilikuwa zinaendelea.
“Hawa jamaa wameitikisa
nchi na hiki walichokifanya ni
uchokozi na wanastahili
kuadhibiwa vikali sana.”
Akasema Job.
“ Kuna kitu kinanijia akilini
lakini sina hakika kama
kinaweza kuwa na mahusiano
na hiki kilichotokea leo.Yasmin
aliniambia kwamba rais alifanya
makubaliano na Alshabaab na
moja kati ya makubaliano yao ni
yeye kuachiwa huru.Nini hasa
kilichopelekea rais afanye
makubaliano na Alshabaab hadi
akaamua kumuachia huru mtu
hatari kama Yasmin. Rais wa
nchi unawezaje kuwa na
mawasiliano au hata kufanya
makubaliano na magaidi? Au
walibadilishana wafungwa na
ndiyo maana akamuachia
Yasmin?.”akajiuliza
“Austin !! akaita Amarachi
na kumtoa Austin katika
mawazo mengi
“ Tunaendelea na jambo
gani kwa sasa? Baada ya tuko
hili naona kila kitu
kimesimama.Are we going to
watch this all night? Akauliza
Amarachi
“ We have lots to do lakini
hiki kilichotokea kwa kweli
kimestua kila mtu.Kuna
wabunge zaidi ya mia tatu na
themanini ndani ya bunge lile
na hatujui ni wangapi walikuwa
ndani ya ukumbi wa bunge leo
jioni wakati shambulio hilo
likitokea nina amini ni zaidi ya
mia tatu.Hatujui ni wageni
wangapi waliokuwamo ndani ya
hoteli ile wakati inalipuliwa.Huu
ni msiba mkubwa sana kwa
taifa na maisha ya watu wengi
yamekatishwa kikatili.Hata
hivyo tunaweza kuendelea na
majukumu yetu huku
tukifuatilia kwa karibu
kinachojiri.Kilichokuwa mezani
kilikuwa ni majibu ya kipimo
cha vinasaba ambayo tayari
tunayo mkononi.Rais alidai
kwamba asionyeshwe mtu
mwingine majibu hao isipokuwa
yeye pekee lakini kwa hili
lililotokea leo sina hakika kama
atakuwa na nafasi hata ya
kufuatilia suala hili.Mimi
ushauri wangu tufungue
bahasha hii na tuangalie
kilichomo ndani.Marcelo ni
daktari na atatuambia
kilichoandikwa humu kwani
lugha ya kitabibu huwa ngumu
kidogo kuielewa” Akasema
Austin na kuichukua bahasha
ile yenye majibu ya vipimo vya
vinasaba na kuifungua kisha
akampa Marcelo akaanza
kuipitia.Wakati Marcelo akiipitia
barua ile kukatokea habari
mchepuko katika runinga.
“Habari za wakati huu
watazamani wetu.Tunaendelea
kuwaleteeni habari mbali
kuhusiana na mashambulio ya
bomu katika hoteli jijini dar es
salaam na Dodoma katika jengo
la bunge,mashambulio
yaliyosababisha vifo vya watu
wengi ambao mpaka sasa bado
haijajulikana idadi kamili ya
vifo.Wakati vikosi vya u okoaji
vikiendelea na juhudi za
kuwatafuta manusura wa
mashambulio hayo ,kuna taarifa
zinazoendelea kusambaa katika
mtandao ya kijamii kwamba rais
wa Tanzania ni miongoni mwa
watu waliokuwamo katika hoteli
iliyoshambuliwa na magaidi
lakini taarifa tuliyoipata hivi
punde kutoka kwa waandishi
wetu walioko katika eneo la
tukio ni kwamba rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania ndugu Ernest Mkasa
alikuwa akienda katika hoteli
hiyo kuhudhuria shughuliya
uchangishaji fedha kwa ajili ya
mradi wa kuwawezesha akina
mama wajasiriamali ,hafla
iliyoandaliwa na mke wa
rais.Kwa mujibu wa taarifa ya
msemaji wa ikulu ni kwamba
shambulio hilo lilitokea wakati
msafara wa rais ukiwa
umebakia mita chache sana
kufika katika hoteli hiyo lakini
walinzi wa rais waliwahi
kumnusuru rais mara tu
shambulio lilipotokea na
kumuondosha eneo la tukio na
msemaji wa ikulu amethibitisha
kwamba rais ni mzima na hana
tatizo lolote .Tunawaomba
wananchi mzipuuzie taarifa
zisizo rasmi zinazoendelea
kusambaa katika mitandao ya
kijamii kuhusiana na matukio
haya.Tutaendelea kuwaleteeni
taarifa za kile kinachoendelea
kadiri tutakavyokuwa
tunazipata.”
Austihn na wenzake
wakatazamana.
“ Inawezekana Alshabaab
walikuwa wanamlenga rais?
Akauliza Amarachi
“Inavyoonekana walikuwa
na lengo hilo na walikusudia
kumuua rais kwani mlipuko
umetokea mita chache kabla ya
rais kuwasili katika jengo
hilo.Inawezekana waliwahi kabla
rais hajaingia katika hoteli hiyo
kwani wangechelewa kidogo na
kusubiri hadi rais aingie hotelini
hivi sasa tungekuwa
tunazungumza mambo
mengine.” Akasema Job
Austin aliyekuwa
ameinamisha kichwa akiwaza
akainua kichwa akamtazama
Marcelo
“ Marcelo tueleze
kilichoandikwa katika karatasi
hizo” akasema
Marcelo ambaye tayari
alikwishayapitia majibu yale
akasema
“Ndani ya report hii kuna
barua iliyoeleza kwa ufupi
kuhusiana na matokeo ya
vipimo na mwisho wa barua hii
wamesema kwamba kutokana
na uchunguzi walioufanya
asilimia 99.9999 inaonyesha
kwamba mlengwa ni baba wa
mtoto.Kwa hiyo Rasmi Monica ni
mtoto wa rais Ernest Mkasa.”
Akasema Marcelo na wote
wakawa kimya kisha Austin
akasema
“ Hizi ni taarifa nzuri kwa
rais lakini zimekuja kwa wakati
mbaya ambao anakabiliwa na
jambo zito .Kitu cha msingi kwa
sasa ni kuiweka taarifa
hiipembeni na kuendelea na
mambo mengine.Tunamsubiri
Yasmin apige simu kama
tulivyokubaliana lakini mpaka
sasa bado hajapiga.Hata hivyo
kuna jambo moja ambalo
linaniumiza mno kichwa na
ambalo nataka kuwashirikisha
na ninyi” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea.
“ Tulikuwa wote wakati
nazungumza na Yasmin na
alisema kwamba aliachiwa huru
kutokana na makubaliano kati
ya rais na Alshabaab.Mpaka
sasa bado haijaniingia akilini
iweje rais wa nchi afanye
makubaliano na magaidi? Ni
makubaliano gani hayo hadi
akaamua kumuachia huru
Yasmin ambaye amefungwa
mahala pa siri kwa miaka zaidi
ya kumi? Sitaki kuunganisha
moja kwa moja hiki kilichotokea
leo na haya mahusiano ya rais
na Alshabaab lakini kuna hisia
zinakuja kwamba kuna jambo
limejificha hapa na endapo
kama tukimpata Yasmin
angeweza kutueleza ni kitu gani
kinachoendelea kati ya rais na
Alshabaab.Nimejiuliza labda
kulikuwa na mabadilishano ya
wafungwa lakini kama ingekuwa
hivyo vipo vyombo husika
ambavyo vingeshughulikia suala
hili lakini hapa anaonekana rais
mwenyewe ndiye
amelishughulikia jambo hili na
hadi akadiriki kutaka
kutuzunguka ili amchukue
Maria na kumkabidhi kwa
mama yake.Jamani hebu
jaribuni kupanua akili zenu na
tuliangalie hili suala kwa
mapana yake.” Akasema Austin.
“ Hata mimi ninaona kitu
Fulani katika hoja ya
Austin.Huyu Yasmin Esfahani
alikamatwa na kufungwa
mahala pa siri akiwa katika
jitihada za kukipanua kikundi
cha IS katika ukanda wa afrika
mashariki.Lazima rais
anafahamu kabisa kwamba
Yasmin ni mfuasi wa IS ambalo
ni kundi hatari kabisa la kigaidi
duniani kwa sasa lakini pamoja
na kufahamu huko bado
akaamua kumuachia
huru.Kama haitoshi akakusudia
kumuachia huru pia Maria
mtoto wa Yasmin akiwa
anafahau kabisa kwamba
tunamshikilia kwa mahojiano
baada ya kutaka kumuua
Austin.Yote hayo ameyaweka
pembeni lakini lengo lake ni
moja tu kutaka mpango wake
wa kumuachia Yasmin
ukamilike.Hapa kweli kuna
jambo ” Akasema Amarachi
“ Kwa kawaida mimi
hupenda kulitazama jambo
lolote ninalolitilia shaka kwa
mapana yake.Muda mfupi
uliopita tumetoka kutazama
habari inayosema kwamba
shambulio lilitokea wakati rais
akiwa mita chache toka hoteli
hiyo.Inawezekana labda
mlengwa wa shambulio la Dar
alikuwa ni mheshimiwa rais.Kwa
mtazamo wa kawaida unaweza
kuamini hivyo lakini mimi bado
nina mashaka.Kwanza mke wa
rais alikuwa ni mfuasi wa
Alberto’s ambao tayari rais
amewaasi na kama kungekuwa
na hafla h iyo ya kuchangisha
fedha aliyoiandaa mke wa rais
basi lazima kungekuwa na
Alberto’s wengi sehemu hiyo na
rais asingeweza kwenda kwani si
mwenzao tena na wana
uhasama mkubwa.Swali la
kujiuliza rais alikwenda
kutafuta nini katika hoteli hiyo?
Jambo lingine ni kwamba kwa
mujibu wa Yasmin,rais na hawa
jamaa waliojitangaza kuhusika
katika msahambulio yote mawili
ni watu wanaofahamiana na
wamefikia hadi hatua ya
kufanya makubaliano na
akamuachia huru mtu hatari
kwa usalama wa taifa na Afrika
mashariki ambaye ni Yasmin
Esfahani.Iweje watu hao hao
watake kumuua rafiki yao? Je
kuna makubaliano amekiuka?
Kama shambulio la dar es
salaam lilimlenga rais,lile
shambulio la Dodoma ambako
idadi kubwa ya wabunge
inasemekena wamepoteza
maisha mlengwa ni nani?
Akauliza Austin
“ Austin unanifurahisha
sana kwa namna
unavyochambua mambo na
hata mimi unanifanya nianze
kupata picha Fulani ya kile
unachokisema.Kwa mtazamo
huo ulioutoa ni wazi hapa kuna
jambo limejificha.Tukio hili
halijatokea kwa bahati mbaya
.Lazima limepangwa.Kama
ulivyosema awali kwamba kwa
nini Alshabaab washambulie
sasa wakati wanajeshi wa
Tanzania wako Somalia kwa
miaka kadhaa ? Hapa lazima
kuna sababu nyingine na si hiyo
ya kuitaka Tanzania iondoe
wanajeshi wake
Somalia.Tukifanikiwa kumpata
Yasmin tutafahamu mambo
mengi” akasema Job
“ Ni kweli Job,kama
tungeweza kumpata Yasmin
tungefahamu kuhusu uhusiano
wa rais na Alshabaab.Mwenendo
wa rais umebadilika na ananipa
shaka sana.Ni Jana tu ambapo
tumefahamu kuhusu
makubaliano yake na Alshabaab
na leo haohao Alshabaab
wanafanya mashambulio
makubwa na kumwaga damu
nyingi.” Akasema Austin
“Kwa hiyo unashauri nini
kifanyike Austin? Akauliza
Amarachi
“ Tusubiri kwanza taarifa
rasmi ya tukio hili itoke halafu
tutajua nini cha kufanya,lakini
rais ni mtu ambaye tunapaswa
kumuwekea alama ya
kiulizo.Kuna maswali ambayo
anahitaji kutupatia majawabu
yake.Najua kwa sasa inaweza
kuwa vigumu kuonana naye au
hata kuwasiliana naye kutokana
na hili lililotokea lakini ripoti hii
ya kipimo cha vinasaba
itamfanya atutafute .Kwa sasa
tupumzikeni na tuendeleeni
kufuatilia tukio hili kwa karibu
.” akasema Austin na kuwaacha
wenzake sebuleni akaelekea
chumbani kupumzika.
SEASON 6: SEHEMU YA 4
Yasmin Esfahani na Tariq
walikuwa katika chumba cha
hoteli walimofikia wakifuatilia
habari za kile kilichotokea jijini
Dar es salaam na Dodoma jioni
ya siku hiyo.Walikuwa
wanatazama chaneli moja
inayotangaza kwa lugha ya
kiarabu. Yasmin alikuwa
ameketi katika zuria
laini,pembeni yake kukiwa na
chupa kubwa ya mvinyo .Tariq
yeye alikuwa sofani akiwa na
pakiti la sigara akivuta moja
baada ya nyingine.Mara katika
chaneli ile kukaonyeshwa video
ya Habib akitangaza Alshabaab
kuhusika katika mashambulio
yale mawili yaliyotokea
Tanzania. Video ile ilimstua
sana Tariq
“ Kumbe ni Alshabaab ndio
waliotekeleza mashambulio haya
!! akasema kwa mshangao.
“Kwa miaka kadhaa
sijamuona Habib.Nimestuka
sana nilipomuona .Hajabadilika
na hata sura yake bado ina lile
tabasamu lake la kikatili.”
Akasema Tariq huku akiwasha
sigara nyingine na kuvuta kwa
fujo
“Umeshuhudia Alshabaab
walichokifanya leo.Mamia ya
watu wasio na hatia wamepoteza
uhai .Faida gani inayopatikana
kwa kuua watu wengi hivi wasio
na hatia ? Ndani ya hoteli ile
kulikuwa pia na watoto wadogo
hao wamekosa nini? Kwa hiki
tunachokishuhudia bado kuna
sababu ya kuendelea kuwa
wafuasi wa makundi haya? Bado
unatamani kuendelea kuua
watu wasio na hatia? Huu ni
unyama uliopitiliza.!!! Akasema
Yasmin.Tariq akapuliza moshi
mwingi hewani na kusema
“ Yasmin kuna jambo
ambalo limekuwa linaniumiza
kichwa changu toka jana
ambalo naomba unisaidie
kupata jibu lake kama
unalifahamu.”
“Uliza” akajibu Yasmin
“ Rais alinifuata gerezani
akaniambia kwamba anataka
kuniachia huru lakini atafanya
hivyo iwapo nitamsaidia kupata
mawasiliano ya
Habib.Nilishangaa sana kwa rais
wa nchi kutaka kuwasiliana na
kamanda mkuu wa Alshabaab.
Kwa kuwa nilikwisha choka
kukaa gerezani nilimsaidia rais
na akafanikiwa kuzungumza na
Habib .Sikujua waliongea
nini,hadi jana usiku nilipotolewa
gerezani nikaambiw akwmaba
niko huru na kukabidhiwa kwa
vijana wale walionileta katika ile
nyumba tuliyolala.Wewe
umekuwa unazungumza na rais
kwa muda mwingi na katika
maongezi yenu nimesikia
kwamba kuna makubaliano
yamefanyika kati ya rais na
Alshabaab.Nataka kufahamu
wamekubaliana nini?Nijibu
tafadhali kama unafahamu
chochote” akasema Tariq
“ Tariq ,hata mimi kama
ilivyokuwa kwako rais alinifuata
gerezani akaniambia kwamba
amekuja kuniachia
huru.Nilimuuliza kwa nini
anataka kuniachia huru
akasema kwamba amefanya
makubaliano na Habib na moja
kati ya makubaliano yao ni mimi
kuachiwa huru.Nilishangaa
sana kwani sikuwa
nikimfahamu huyo Habib ni
nani hadi pale aliponitajia
kwamba ni kiongozi wa
Alshabaab.Baada ya kutoka pale
gerezani akanipeleka katika ile
nyumba tuliyolala na
nikafanikiwa kuzungumza na
Habib kwa mara ya kwanza ,
akaniambia kwamba yeye
hanifahamu lakini ameelekezwa
na IS kwamba moja kati ya
makubaliano yake na rais ni
mimi kuachiwa huru.Kitu cha
pili ambacho walikitaka ni hati
ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar hii ambayo tunayo
hapa.” Akamimina pombe katika
glasi akanywa halafu akatikisa
kichwa na kusema
“ Nilifanikiwa kuzungumza
na viongozi wangu wa IS
wakaniambia kwamba rais wa
Tanzania anataka Alshabaab
wamfanyie kazi Fulani nchini
kwake na Alshabaab
wakawasiliana na IS ambao
walitoa masharti hayo
mawili.Endapo Alshabaab
wangefanikisha kupatikana kwa
vitu hivyo viwili basi IS
wangewalipa pesa nyingi na vile
vile wangeunganisha nguvu na
kuanzisha mapambano ili
kuhakikisha wanaiangusha
serikali ya Somalia kitu
ambacho Alshabaab wamekuwa
wakikitafuta kwa miaka
mingi.Kwa sasa IS ni kikundi
cha kigaidi chenye nguvu kubwa
duniani.Alshabaab
walikubaliana na matakwa hayo
ya IS na wakampa masharti rais
wa Tanzania akakubali.Kuhusu
makubaliano ya rais wa
Tanzania na Alshabaab mimi
siyafahamu lakini yawezekana
walikubaliana kuhusu
mashambulio haya ya leo kwani
si mara moja rais wa nchi
kutumia vikundi vya kigaidi
katika kufanikisha mambo yao
Fulani Fulani na inawezekana
kabisa katika mashambulio
haya mawili yaliyotokea leo hii
hata rais wa Tanzania anaweza
kuwa anahusika japokuwa sina
uhakika na hilo ” akasema
Yasmin .Kama madirisha ya
chumba kile yasingekuwa wazi
chumba chote kingejaa moshi
kutokana na sigara mfululizo
alizokuwa anavuta Tariq.
“ Maelezo yako yamenipa
picha kamili ,kweli nilikuwa
gizani na sikujua chochote
kinachoendelea.Bado kuna kitu
kimoja nahitaji kukifahamu.IS
wanaitaka hati ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kwa
kusudi gani? Akauliza
Tariq.Ilimchukua Yasmin zaidi
ya dakika mbili kujibu.
“Baada ya kupata upinzani
mkubwa katika nchini nyingi za
mashariki ya kati ,ulaya na
Amerika Is wameamua
kuwekeza na kuliimarisha zaidi
kundi lao barani Afrika,hivyo
wakanituma mimi nije afrika
mashariki kuweka sawa
mipango ya kuanzisha kwa tawi
la IS katika ukanda huu.Kwa
muda wa miaka kumi na nne
nimeishi katika sehemu mbali
mbali za afrika mashariki
nikifanya uchunguzi na mipango
ya kueneza kundi la IS na
namna tutakvyoweza kufanya
kazi.Pamoja na kuzunguka
sehemu mbali mbali za afrika
mashariki makao yangu makuu
yalikuwa Dar es salaam
Tanzania ambako nilifanikiwa
kumpata mwanaume mmoja
aliyekuwa anajishughulisha na
biashara ya dawa za kulevya
nikazaa naye mtoto
mmoja.Huyu alinisaidia sana
bila yeye kufahamu mimi ni
nani.Baadae nikakamatwa na
kufungwa gerezani .” akatulia
kidogo akamimina pombe katika
glasi na kunywa .
“ Niliyakosa sana maisha
kama haya .Nilikuwa na kiu ya
mvinyo huu ” akasema Yasmin
na kunywa tena pombe nyingine
halafu akaendelea.
“Katika uchunguzi wangu
niligundua kwamba IS
tungekuwa na mafaniko
makubwa na tungeweza kufanya
kazi zetu kwa uhuru zaidi iwapo
tungefanikiwa kukimiliki kisiwa
cha Pemba.Tungefanikiwa
kukipata kisiwa hiki tungeweza
kulitawala eneo la bahari na
hata eneo zima la afrika
mashariki.Niliwasilisha
mapendekezo hayo kwa wakuu
wangu wakakubaliana nayo
lakini tatizo likawa ni namna ya
kuweza kukipata kisiwa hicho
kwani kiko ndani ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania .Kitu
pekee ambacho kingepelekea IS
wakitwae kisiwa cha pemba ni
kwanza kuuvunja muungano
kati ya Tanganyika na Zanzibar
halafu visiwa vya Unguja na
Pemba kila kimoja kiwe
huru.Wakati nakamatwa
tulikuwa katika kutafuta namna
ya kulifanikisha hilo yaani
kuuvunja muungano wa
Tanganyika na Zanzibar na
mpaka sasa bado mawazo yangu
wanaendelea kuyafanyia kazi
kwa kutumia mbinu mbali mbali
za kutaka kuuvunja muungano
huu lakini bado hawajafanikiwa
na ilipojitokeza fursa kama hii
wameamua kuitumia vyema
.Kujibu swali lako IS wanaitaka
hatiya muungano wa
Tanganyikan a Zanzibar kwa
lengo la kuuvunja muungano ili
wakitwae kisiwa cha Pemba..”
Akasema Yasmin na kukawa
kimya.
Yasmin aliendelea kunywa
mvinyo huku Tariq akiendelea
kuvuta sigara kwa fujo huku
akimtazama Yasmin halafu
akatabasamu.
“ Yasmin sikuwa
nikikufahamu na wala sijawahi
kukusikia hadi nilipokutana
nawe jana katika ile nyumba
tuliyolala.Nilipokuona mwanzo
nilikuona kama mwanamke wa
kawaida lakini kwa haya
uliyonieleza na kwa mambo
niliyoshuhudia ukiyafanya leo
hadi tukafanikiwa kutoka
salama katika uwanja ule wa
ndege nimekuogopa.Mimi
nilikuwa mratibu mkuu wa
mashambulio yote ya Alshabaab
lakini nakiri mbele yako kuwa
sina akili za haraka haraka
kama ulizonazo .Ningekuwa
peke yangu nisingeweza kutoka
ndani ya ule uwanja” akatulia
akavuta sigara yake na kusema
“ Kuna jambo ambalo
sikuwa nimekueleza.Nikiwa na
Alshabab niliratibu
mashambulio mengi tu ambayo
yalipelekea vifo vya watu wengi
na kwa taarifa yako ninatafutwa
sana na serikali za Kenya na
Somalia kutokana na kuratibu
mashambulio mengi
yaliyopoteza maisha ya watu
wengi.Toka jana nilipoambiwa
kwamba tumeandaliwa ndege ya
kutupeleka Mogadishu nilikuwa
na mawazo mengi sana ni jinsi
gani nitakavyoweza kushuka
Mogadishu bila kukamatwa?
Japokuwa ni miaka mingi
imepita lakini uhakika wa
kuvuka salama pale uwanjani
ulikuwa mdogo sana. Mawazo
niliyokuwa nayo yalikuwa ni
kuiteka ndege ile kabla ya
kufika Mogadishu na kuibadili
muelekeo ili tupelekwe sehemu
nyingine jambo ambalo
ulilifanya wewe na ninashukuru
na wewe kuwa na wazo kama
langu.Sijui lengo la Habib ni nini
aliposema kwamba tupelekwe
Mogadishu wakati anafahamu
fika kwamba serikali ya Somalia
wananitafuta .Kwa hiyo kitendo
ulichokifanya cha kubadili
uelekeo wa ndege kimenisaidia
sana ni kama vile ulikuwa
katika akiliyangu.Napenda
kukuhakikishia kwamba niko
tayari kufanya kazi nawe
.Maneno uliyonieleza tukiwa
ndegeni kuhusiana na
kuendelea na ushirika na
mitandao yetu ya zamani
nimeyatafakari sana na
nimefanya maamuzi hata mimi
ya kuachana na maisha kama
yale na kuanza maisha
mapya.Kwa hiyo Yasmin kama
una mpango wowote ulionao wa
kuanza maisha mapya naomba
unishirikishe na mimi tafadhali”
akasema Tariq.Yasmin akageuka
akamtazama Tariq usoni kisha
akauliza
“ Una hakika na maamuzi
yako?
“ Ndiyo Yasmin.Nahitaji
kupotea na kwenda kuanza
maisha mapya mbali kabisa na
Alshabaab.Kauli yako
imenifanya nitafakari sana
maisha yangu ndani ya
Alshabaab na faida
nilizozipata.Mpaka sasa sijaona
faida yoyote niliyopata kwa
kulitumikia kundi hili .Nimeua
watu wengi lakini hakuna kitu
cha maana nilichopata sina mke
,sina mtoto sina familia .Nataka
nianze upya. Usiniache tafadhali
kama una mipango yoyote
mizuri ya kuanza maisha mapya
mbali na hapa.” Akasema Tariq
“ Sawa nimekusikia
.Nitakusaidia kama kweli una
nia ya dhati” akasema Yasmin
na kuendelea kunywa mvinyo.
“Ninatakiwa kuwa makini
sana na huyu
jamaa.Ninafahamu namna ya
kuwasoma watu huyu si mtu
mzuri hata kidogo.Nikimtazama
machoni hamaanishi kile
anachokisema.Najua ana lengo
lake lingine lakini hapa kwangu
hawezi kufanya lolote.” Akawaza
Yasmin
“ Yasmin”akaita Tariq na
Yasmin akageuka akamtazama.
“ Habib alikuwa na
mategemeo leo saa kumi na
moja tungefika Mogadishu lakini
mpaka sasa hatujatokea na
hatuna mawasiliano naye
yoyote.Nini kitatokea iwapo
mpaka kesho asubuhi hatakuwa
ametuona ?
“ Ni wazi atafanya
mawasiliano na rais wa
Tanzania kumuuliza nini
kimetokea na hapo ndipo msako
wa kututafuta
utakapoanza.Kesho asubuhi
tunarejea Dar es salaam.”
“ Dar es salaam? !! akauliza
Tariq kwa mshangao
“ Ndiyo tunarejea Dar es
slaam” akajibu Yasmin bila wasi
wasi wowote
“ Tunakwenda kutafuta nini
Dar es salaam? Kule ni hatari
sana kwetu.Kama ulivyosema
mwenyewe kwamba lazima
Habib atawasiliana na rais wa
Tanzania na atamfahamisha
kwamba hatujafika Mogadishu
na tutaanza kutafutwa kila
kona.Kwa sasa tuko mbali na
Dar es salaam kwa nini tusianze
safari yetu na kutokomea mbali
bila kwenda kutafuta hatari
tena? Yasmin maisha ya mateso
niliyokaa gerezani yananitosha
sitaki tena maisha kama yale na
ndiyo maana nimeanua kuanza
maisha mapya.Tafadhali
nakuomba ufikirie upya mpango
wako huo wa kurejea tena Dar
es salaam” akasema
Tariq.Yasmin akanywa mvinyo
kidogo na kusema
“ Kesho tunarejea Dar es
salaam.Kuna kazi ambayo
sijaikamilisha .Natakiwa kwenda
kumchukua mwanangu ambaye
yuko Dar es alaam na safari ya
kuelekea katika maisha mapya
itaanzia hapo.Siwezi kuondoka
bila mwanangu Shamim.kama
uko kitu kimoja na mimi
tutaongozana wote kurejea Dar
es salaam.Tuko pamoja?
Akauliza.Tariq akatumia muda
kidogo kutafakari na kusema
“ Sawa tutaenda huko Dar
es salaam” akasema Tariq huku
akiwasha sigara nyingine.
“ Sipati picha Habib
atakuwa katika hali gani muda
huu .Atakuwa na hasira
zisizomithilika.Ninamfahamu
Yule jamaa ni mkatili sana na
ana roho ya kinyama .Endapo
atagundua kwamba
tumemzunguka na kumfanyia
mchezo huu sijui nini kitatokea
.Atatusaka kwa maisha yake
yote yaliyobaki na akitupata
kitakachofuata ni kutuua.Siwezi
kumsaliti Habib kiasi hiki,lazima
nitafute namna ya kufanya na
kuichukua hii hati
nikamkabidhi Habib.Huyu
mwanamke hawezi kunishinda
kwani tayari nimekwisha
muweka upande wangu na
tayari ananiamini
.Ninachotakiwa kabla ya kesho
asubuhi niwe nimemmaliza
kisha niondoke na hati hii.Kabla
ya yote natakiwa kutafuta nafasi
ya kuzungumza na Habib au
mtu mwingine yeyote katika
Alshabaab nimfahamishe kile
kinachoendelea.pamoja na
kukaa gerezani muda mrefu
lakini siwezi kulisaliti kundi
langu hata kidogo.Nimejiunga
na Alshabaab nikiwa kijana
mdogo sana wa miaka kumi na
nne na nitakufa mtiifu kwa
Alshabaab.”akawaza Tariq na
kukohoa kidogo kisha akaita
“Yasmin”
Yasmin akageuka
akamtazama
“Kwa miaka kadhaa
tumekuwa kifungoni lakini
baada ya kutoka kifungoni bado
tunaendelea kujificha
ndani.Japo kwa mara moja kwa
nini tusitoke tukaenda sehemu
kupoteza mawazo na kutuliza
akili zetu.Tumepitia mambo
mengi sana hadi tumefika hapa
kwa hiyo si vibaya endapo
tukatoka kidogo.Hakuna
anayetufahamu hapa Zanzibar
kwa hiyo tuko huru kwenda
sehemu mbali mbali za
burudani.Ninahisi kuboreka
sana hapa ndani” akasema
Tariq.Yasmin akatabasamu na
kusema
“ Mimi si mwendaji wa
sehemu za burudani na zaidi ya
yote sijaboreka hapa ndani na
ninajisikia furaha
sana.Niliyakosa sana maisha
haya nilipokuwa gerezani.”
Akasema Yasmin na kuinuka
akamfuata Tariq akaketi
pembeni yake.
“ Kitu gani hasa
ulichokikosa ulipokuwa
gerezani? Akauliza Yasmin.Tariq
akatabasamu na kusema
“ Nilikosa vingi lakini
kikubwa nilichokikosa ni
kushuhudia milipuko ya
mabomu niliyoyatega.Mimi ndiye
niliyekuwa mratibu wa
mashambulio yote ya Alshabaab
na nilisikia raha sana kuona
shambulio nililoliratibu
linafanikiwa” akasema Tariq
“ Hicho peke ndicho
kinachokupa furaha katika
maisha yako? Ukiacha milipuko
ya mabomu hakuna kingine
ambacho kinakupa furaha
katika maisha ? Hakuna
wanawake huko katika kambi
zenu wa kuwastarehesha?
“ Wanawake? Akauliza Tariq
“ Ndiyo”
“ Wanawake wapo lakini
mimi starehe yangu si
wanawake bali ni milipuko kama
nilivyokueleza.Wanawake nakaa
nao mbali kabisa na ndiyo
maana mpaka sasa sina mke
wala mtoto” akasema Tariq na
kuwasha sigara nyingine.Yasmin
akamshika bega na kusema
“ Ni vipi endapo
nitakwambia kwamba kitu
nilichokikosa sana nikiwa
gerezani ni mwanaume wa
kufanya naye mapenzi?
Akasema Yasmin huku
akitabasamu.Tariq akastuka.
‘”Mbona umestuka Tariq?
Hicho ndicho kitu nilichokikosa
mno nikiwa gerezani.Ninapenda
sana kufanya mapenzi.Ni
starehe yangu kubwa na kwa
usiku wa leo kwa kuwa niko
nawe humu chumbani utanikata
kiu yangu ya miaka mingi.Kwa
hiyo hatutakwenda kokote
nataka tufanye mapenzi usiku
kucha kufidia miaka yote
ambayo nilikuwa gerezani.”
Akasema Yasmin huku
akimshika shika Tariq maeneo
nyeti.
“ Yasmin subiri
kwanza.Mimi si mpenzi wa
mambo hayo.Japokuwa nimekaa
gerezani kwa miaka mingi lakini
bado sina hamu ya kufanya
mapenzi.” Akasema Tariq lakini
Yasmin hakusikia chochote
kwani tayari mashetani
yalikwisha mpanda.Akavua
gauni alilolivaa na kubakiwa na
nguo za ndani.Pamoja na kukaa
miaka mingi gerezani lakini
bado mwili wa Yasmin ulikuwa
mwororo na wenye
kung’aa.Tariq akahisi mwili
unamchemka baada ya
kuushuhudia mwili ule mwororo
.Yasmin akaendelea na utundu
wake akaifungua suruali ya
Tariq na kwa kutumia mdomo
na ulimi wake akafanya utundu
mkubwa pale ikulu kiasi cha
kumfanya Tariq atoe
miguno.Ghafla kama mbogo
majeruhi Tariq akavua fulana
aliyoivaa akaitupa chini
akamuinua Yasmin na kumbeba
mikononi.Tariq alikuwa ni pande
la mtu mwenye nguvu
nyingi.Hakuwa na subira
akakianzisha kipute.Yasmin
alitoa ukele kufurahia kipute
kile na gwaride alilochezeshwa
na Tariq.Kilikuwa ni kipute hasa
kilichochukua dakika arobain
.Hadi wote wanamaliza vitu
vilikuwa vimetawanyika hovyo
mle chumbani kwani kutokana
na ugumu wa mpangano ule
mechi ilichezwa kila mahali .
Wote wawili walikuwa
wanahema kama wakimbiaji wa
mbio ndefu.
“ Sikutegemea kama una
uwezo mkubwa kiasi
hiki.Ahsante kwa kunikata kiu
japo bado nitahitaji zaidi na
zaidi usiku wa leo” akasema
Yasmin
“ Mapenzi si starehe yangu
lakini nikiamua kufanya nina
uwezo mkubwa sana na
ninaweza kufanya kwa muda
mrefu” akasema Tariq.
Yasmin akainuka
akachukua taulo akaingia
bafuni kujimwagia maji
“ Hii ndiyo nafasi niliyokuwa
naitafuta” akawaza Tariq
akainuka kitandani akajifunga
taulo halafu akanyata hadi
katika begi la Yasmin
akalifungua na kuitafuta simu
.Alipoipata akanyata hadi katika
mlango wa bafu akasikia maji
yakimwagia,Yasmin aliendelea
kuoga.Haraka haraka akaiwasha
halafu akaziandika namba
Fulani katika simu ile akapiga
na kuiweka sikioni ili kusikia
kama inaita taratibu
akaufungua mlango akatoka nje
.Akazungumza na mtu fulani
haraka haraka kwa kiarabu
halafu akakata simu na
kufungua mlango taratibu
kurejea ndani.Alipata mstuko
mkubwa pale alipojikuta
akitazamana na Yasmin
aliyekuwa mtupu akichuruzika
maji mwili huku akiwa
amemnyooshea bastora.
“ Ingia ndani taratibu kama
ulivyotoka” akasema
Yasmin.Tariq akaingia ndani na
kuufunga mlango akaamriwa
apige magoti .Ghafla kikatokea
kitu ambacho Yasmin hakuwa
amekitegemea.Tariq aliruka
mzima mzima na kumvaa
Yasmin wote wakaanguka
chini.Bastora ya Yasmin
ikamponyoka na kuanguka
pembeni.Tariq akampiga Yasmin
ngumi nzito sana na kunyoosha
mkono ili kuichukua bastora ile
lakini Yasmin tarai alikwisha
msoma na hakutawa tayari
kumpa nafasi hiyo.Akamchoma
kidole cha jicho.Tariq
akapandisha hasira na kuanza
kumvurumishia Yasmin
makonde mazito.Yasmin
akaishika stuli iliyokuwa
pembeni na kumpiga nayo Tariq
kichwani akaanguka
chini.Akainuka haraka haraka
na kumpiga teke zito maeneo ya
korodani na kumfanya Tariq
agugumie kwa maumivu makali
aliyoyapata.Kama hiyo haitoshi
akauchukua stuli ile na
kumbamiza nayo mara mbili
kichwani.Tariq akaanza kutokwa
na damu kichwani.Yasmin
akaiokota bastora yake na
kumuelekezea
“ Nani ulikuwa unaongea
naye? Nieleze ukweli ama sivyo
sintakuacha hai” akasema
Yasmin
Tariq hakusema chchote
aliendelea kugugumia maumivu
“ Tariq hii ni mara ya
mwisho nieleze nani uliyempigia
simu? Akauliza lakini Tariq
hakumjbu.Akaiokota simu
akatazama namba aliyopiga
Tariq lakini tayari ilikuwa
imefutwa.
“ Nilifahamu toka awali
lengo lako na nilikuwa
nakusubiri ufanye
ulivyofanya.Ulisema hutaki tena
kushirikiana na Alshabaab ili
nikuamini na mwisho wa siku
uweze kuchukua hati hii na
uondoke nayo.Mimi ni mtu
mwingine Tariq huwezi
kunizunguka hata mara moja na
kwa hili ulilolifanya
sintakusamehe.” Akasema
Yasmin
“ Unadhani utafanikiwa
malengo yako? Usijidanganye
Yasmin hakuna chochote
utakachofanikiwa.Hutafanikiwa
kundoka salama hapa Zanzibar
na hautakwenda
kokote.Jisalimishe kwa Habib
na umrejeshee kilicho mali
yake.Usipofanya hivyo hata
mwanao hautamuona tena .Hivi
tunavyoongea vikosi vyote vya
ulinzi tayari vina taarifa zako
muda wowote toka sasa
utakamatwa” akasema Tariq na
kuzidi kumpandisha hasira
Yasmn na kwa kutumia bastora
ile iliyofungwa kiwambo cha
sauti akammiminia Tariq risasi
kichwani.
“ Yasmin Esfahani huwa
hazungukwi hata mara
moja.Hukujua unacheza na mtu
wa aina gani” akasema Yasmin
kwa hasira.Tariq hakuwa na
uhai.Akamvuta na kumpeleka
bafuni na kuufunga
mlango.Akavaa haraka na
kujitazama katika kioo.
“Lazima niondoke hapa
haraka iwezekanavyo.Natakiwa
kwenda Dar es salaam
kumchukua Shamin ” Akawaza.
SEASON 6: SEHEMU YA 5
Imetimu saa tatu na dakika
ishirini katika makao makuu ya
Alshabaab hali ikiwa ya
ukimya.Ulinzi ulikuwa mkali
kama ilivyo kawaida yake.Mpaka
mida hii hakukuwa na taarifa
zozote kuhusiana na walipo
Tariq na Yasmin ambao
walitegemewa wangewasili
Mogadishu mida ya jioni baada
ya ndege yao kusemekana
kupata hitilafu angani na
kulazimika kutua kwa dharura
kisiwani Unguja.
Habib Alzaraq alirejea
kutoka kuswali,akauliza kama
kuna taarifa zozote kuhusiana
na akina Tariq lakini hadi muda
huo hakukuwa na taarifa zozote
zilizopatikana .Akamuagiza mtu
wake anayehusika na masuala
ya mawasiliano afanye
mawasiliano na uwanja wa
ndege wa Zanzibar kufahamu
kama ndege ile waliyokuwa
wanasafiria akina Tariq iliyotua
kwa dharura pale Zanzibar
kama imekwishaondoka pale
uwanjani au bado inaendelea na
matengenezo.Mawasiliano
yalifanyika na taarifa
iliyopatikana ni kwamba baada
ya kufanyiwa uchunguzi katika
injini yake ndege ile ilifanikiwa
kuruka na kurejea Dare s
salaam.Habib akapewa taarifa
hizo na zikamstua
“ Dar es salaam ? akauliza
Habib kwa mshangao.
“ Ndiyo mkuu.Nimetaarifiwa
kwamba ndege ilifanyiwa
uchunguzi na kisha
ikaruhusiwa kuondoka na
ikarejea Dar es salaam.”
“Yasmin na Tariq
walikuwemo ndani ya hiyo ndege
iliporejea Dar es salaam?
Akauliza Habib
“ Nimepewa jibu la jumla
kwamba ndege hiyo imerejea
Dar es salaam,hawakufafanua
kama akina Tariq nao
walikuwemo ndani yake”
akasema Yule msaidizi wake wa
masuala ya mawasiliano.Habib
akajaribu kupiga zile namba za
simu ambazo Yasmin alimpigia
mara ya mwisho akiwa hospitali
lakini hazikuwa zikipatikana.
“ Naanza kuingiwa na wasi
wasi kwamba yawezekana kuna
mchezo unataka kuchezwa
hapa.Kwa nini ndege irejee Dar
es salaam wakati ilitakiwa
iendelee na safari kuelekea
Mogadishu? Watu wa kutoka IS
watawasili usiku huu kwa ajili
ya kufanya makabidhiano ya ile
hati ya muungano ambayo
tayari Yasmin na tariq
wamekwishakabidhiwa.Nitawael
eza nini? Akajiuliza Habib kisha
akazitafuta namba za simu za
rais akapiga.Sura yake ilikuwa
imejikunja kwa hasira.Simu
iliita bila kupokewa akapiga tena
na safari hii ikapokewa.
“ Hallo Habib niko kwenye
kikao kizito sana kuhusiana na
mambo yaliyotokea hapa nchini
leo.Naomba niwasiliane nawe
baada ya kama saa moja hivi”
akasema rais kwa sauti ndogo.
“Sina muda wa kusubiri rais
nataka tuongee sasa hivi.Kama
ni muhimu wewe kuwepo katika
kikao hicho simamisha kikao
uzungumze nami kwanza.”
Akasema Habib kwa ukali.Rais
akatazama pande zote kama
kuna mtu karibu kisha akauliza
“ Unasemaje Habib?
“ Sikiliza rais,sihitaji ugomvi
na wewe wala vita na nchi
yako.Tulikubaliana vizuri na
nimeifanya kazi yako kama
ulivyotaka.Nataka unipatie
Tariq,Yasmin na ile hati kama
tulivyokubaliana kama si hivyo
utatufahamu sisi ni nani !!
akasema Habib kwa ukali
“ Mbona sikuelewi Habib?
Nilitoa ndege kwa ajili ya
kuwapeleka Tariq na Yasmin
Mogadishu.Hawapo hapa
nchini,tayari wamekwisha
ondoka.”
“Hawajafika
Mogadishu.Niliwasiliana na
Yasmin jioni ya leo walitua kwa
dharura katika uwanja wa ndege
wa Zanzibar kutokana na
hitilafu katika ndege .Mpaka
usiku huu hakuna taarifa zozote
kuwahusu wao.Tumefuatilia
uwanja wa ndege wa Zanzibar
tumetaarifiwa kwamba ndege ile
baada ya kufanyiwa uchunguzi
imepaa na kurejea Dar es
salaa.Mheshimiwa rais naamini
huu ni mchezo
unatuchezea.Nilikuonya hapo
awali kwamba usijaribu kufanya
mchezo wowote wa kihuni na
sisi lakini unaonekana
kulipuuza onyo hilo na unataka
kutuzunguka.Tumeifanya kazi
yako na sisi tunahitaji haki
yetu” akasema habib.
“ Habib naomba unisikilize
vizuri.Mimi sifahamu chochote
kuhusiana na suala hilo.Nilitoa
ndege ambayo ni nzima kabisa
na haina hitilafu yoyote
nashangaa kusikia kwamba
walitua Zanzibar kwa
matengenezo.Kinachonishangaz
a sijataarifiwa chochote
kuhusiana na jambo hilo
nikiamini kwamba mpaka muda
huu tayari Yasmin na Tariq
watakua wamekwisha fika
hapo.Hizi unazonipa ni taarifa
ngeni kabisa.Naomba unipe
muda nilifuatilie suala hili.”
Akasema rais
“ Ninakupa mpaka kesho
saa mbili asubuhi tuwe
tumepata kila kile tulichokuwa
tumekubaliana .Kama
hatutakuwa tumepata haki yetu
nakuhakikishia damu hii
iliyomwagika leo itaendelea
kumwagika kila uchao hapo
Tanzania.” akasema Habib na
kukata simu.Ernest Mkasa
akahisi mwili kuloa jasho.
“ Nini kimetokea? Ni kweli
ndege waliyopanda akina Tariq
ilipata hitilafu na kutua
Zanzibar kwa dharura? Mbona
sijataarifiwa jambo hili?
Akajiuliza.
“ Hili sasa ni suala jipya
ambalo natakiwa
kulishughulikia kwa haraka.
Tariq na Yasmin wako wapi?
Akajiuliza rais.
“ Au huu ni mpango wa
Yasmin ili anirudishie hati ile ya
muungano kwa lengo la
kumpata mwanae? Nahisi hivyo
kwani aliniahidi kufanya kila
atakachoweza ili kumpata
mwanae.Kama huu ni mpango
wake kwa nini basi hajanitaarifu
chochote? Hata hivyo natakiwa
kuanza maandalizi ya
kuhakikisha ninampata Maria
haraka iwezekanavyo ili ikitokea
Yasmin akamuhitaji basi tayari
niwe naye.” Akawaza rais na
kumpigia simu mmoja wa vijana
wake aliyempa jukumu la
kuhakikisha kwamba Yasmin na
Tariq wanaondoka nchini
akamtaka afuatilie suala lile
kama lina ukweli wowote na
amjulishe ndani ya muda
mfupi,halafu akarejea katika
ukumbi wa mikutano
Baada ya kuongea na
rais,Habib akawakusanya
makamanda wake kwa ajili ya
kikao cha dharura kujadili
kilichotokea.Kabla ya kikao
kuanza,Aziz mmoja wa wasaidizi
wake anayemuamini sana
akatokea akiwa anahema na
ilionekana alikuwa anakimbia
“ Samahani nimechelewa
mkuu nilikwenda kuswali lakini
hata hivyo nimekuja na habari
ya muhimu sana”
“ Habari gani Aziz? Akauliza
Habib
“ Nimezungumza na Tariq.”
“ Tariq? Amekupigia simu?
“ Ndiyo mzee.Tariq
amenipigia simu nikiwa njiani
kuja hapa.”
“ Yuko wapi? Nini kimetokea
hadi wakashindwa kufika hapa
kama tulivyokuwa tumepanga?
Akauliza Habib
“Kuna tatizo
limetokea.Amenieleza kwa ufupi
sana kwani alitumia simu ya
Yasmin bila yeye
kufahamu.Tariq anasema
kwamba ndege waliyokuwa
wanaitumia haikupata hitilafu
yoyote bali Yasmin
aliwalazimisha marubani
kubadili muelekeo na kutua
Zanzibar kwa kisingizo cha
hitilafu katika injini.Anasema
kwamba Yasmin amebadilika na
ana mpango wa kutokomea
kusikojulikana na hati ya
muungano.Ameniambia kwamba
tufanye haraka tumuwahi
Yasmin wako Hotel Lepatido”
akasema Aziz na wote
wakamtazama Habib kusikia
atasema nini
“ Niliwakatalia IS kwamba
siwezi kumpa nyaraka kubwa ile
ya hati ya muuungano mtu
nisiyemfahamu vizuri lakini
wakakataa na kudai kwamba
Yasmin hana matatizo ni mtu
wao lakini kumbe hisia zangu
zilikuwa za kweli.Huu ni
mgogoro mwingine kati yetu na
IS.Nilifanya kosa kubwa sana
kumuamini Yasmin badala ya
mtu wangu Tariq.” Akawaza
Habib na kuchukua simu
akampigia rais Ernest ambaye
licha ya kuwa katika kikao kizito
na wakuu wa vyombo vyote vya
usalam wakijadili mashambulio
yale yaliyotokea alilazimika
kutoka nje ya ukumbi wa
mikutano baada ya kuiona
namba ya Habib
“ Habib nilikuomba unipe
muda nilifuatilie suala
lako.Vijana wangu bado
hawajanipa taarifa zozote mpaka
sasa.Nitakujulisha nikipata
taarifa zozote toka kwao”
akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais
nimepata taarifa sasa hivi nini
kimetokea.Tariq amemmpigia
simu mmoja wa wasaidizi wangu
na akamweleza kwamba ndege
waliyopanda haikuwa na hitilafu
yoyote bali ni Yasmin ndiye
aliyewatishia marubani kwa
bastora na kuwataka wabadili
uelekeo waelekee
Zanzibar.Yasmn amefanya
usaliti mkubwa na sasa anataka
kutoroka na hati ile
uliyompatia.Kwa mujibu wa
Tariq mpaka sasa bado wako
Hotel Lepatido
walikofikia.Mheshimiwa rais
nakuomba fanya kila unaloweza
uweze kumdhibiti Yasmin na
niweze kuipata hiyo hati usiku
wa leo na umkabidhi
Tariq.Tuma vikosi vya polisi sasa
hivi vilizingire jengo la hoteli
hiyo walimo na Yasmini
akamatwe haraka sana.Tayari
nimekupa taarifa zote na
ukishindwa kufanikisha
kukamatwa Yasmin nitaamini
kwamba wewe na Yasmin mko
kitu kimoja.Nitakupigia tena
baada ya robo saa kujua
maendeleo” akasema Habib na
kukata simu.Rais
akachanganyikiwa.
“ Ninaamini Yasmin
amefanya hivi alivyofanya
kutokana na yale makubaliano
yetu kwamba akinirejeshea hati
na mimi nitampatia mwanae.Ni
juu yangu sasa kuchagua
kwamba ninataka hati au
ugomvi na Alshabaab? Akawaza
na kumuita mkuu wa majeshi
Jenerali lameck Msuba
akamueleza kuhusiana na
jambo lile
“ Mheshimiwa rais hii ni
nafasi imepatikana ambayo
hatupaswi
kuichezea.Tunatakiwa kufanya
kila tunaloweza kumdhibiti
Yasmin na kuichukua hati
yetu.Usiogope vitisho kutoka
kwa Alshabaab kwani hawawezi
kufanya chochote.Tutapambana
nao” akasema lameck
“ Kwa hiyo unanishauri nini
Lameck?
“ Ushauri hapa ni kutuma
kikosi maalum toka usalama wa
taifa kwenda hotelini hapo
kuwadhibiti akina Tariq na
Yasmin.Hawatakiwi kwenda
askari au wanajeshi .Watu wale
wanapaswa kukamatwa kimya
kimya na kurejeshwa mahala
walikokuwa wamefungwa ”
akasema Lameck na rais
akamuita Silvanus Kiwembe
mkurugenzi wa idara ya
usalama wa taifa ambaye naye
alikuwemo katika kikao kile.
“ Silva nimekuita hapa kuna
jambo nataka lifanyike kwa
haraka na ambalo ni muhimu
mno.Yasmin Esfahani pamoja
na mtu mwenzake anaitwa Tariq
wako katika hoteli moja inaitwa
Lepatido kisiwani Zanzibar
.Nataka haraka sana tuma
kikosi cha vijana hodari kumi au
zaidi waende hotelini hapo usiku
huu na wahakikishe
wanawakamata watu hao wawili
na warejeshwe kule
gerezani.Kuna bahasha anayo
Yasmin ambayo nataka
ichukuliwe na isifunguliwe na
mtu yeyote kuona kilichomo
ndani bali iletwe kwangu moja
kwa moja.Kwa umuhimu wa
suala hili nataka wewe
mwenyewe uwepo katika kikosi
hicho ili kila kitu kiende
sawa.No mistake.Nawahitaji
Tariq na Yasmin wakiwa hai.”
Akasema rais na Silvanus
akaondoka kwenda kutekeleza
maagizo yale ya rais..Baada ya
Silva kuondoka ,rais
akamgeukia Jenerali Lameck
“Lameck nataka njia zote za
kuingilia na kutokea Zanzibar
zifungwe kwa muda ili kuzuia
Yasmin asiweze kupata nafasi ya
kutoroka.Viwanja vyote vya
ndege visiruhusu ndege yoyote
kutoka na hata bandari zote
zisiruhusu mtu yeyote kutoka
hadi hapo tutakapofanikiwa
kumpata Yasmin.” Akasema
Rais
 
Mkuu haiwezekani kwa kuwa mm ndiye nilianzisha huu uzi lazima niumalize nimeacha kwanza wenye vifront front na wajuzi zaidi wamalize kupiga kelele zao then nibwage mzigo wote mwanzo mwisho.kwa kuwa wao wapo kwenye folen wanasubili season 7 wakati mm ninayo mkononi hapa..wacha wakishauziwa season 7 mm nakuja kumaliza
Unacholalamika ni nini hasa? Kuna mtu amekuzuia kuiweka humu.
 
Mkuu lege ahsante sana

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Season 7 tayari???

Sent from my GT-N7105 using JamiiForums mobile app
 
SEASON 6: SEHEMU YA 6

Sauti ya muziki laini wa ala
ilisikika kwa mbali ndani ya
chumba kikubwa kilichokuwa
na mwaga hafifu. Monica
Benedict alikuwa amejilaza
sofani akionekana kuwa na
mawazo mengi.Katika meza
ndogo kulikuwa na sahani ya
chakula lakini hakuwa na hamu
ya kula chochote siku hii.Akiwa
bado katika mawazo mengi simu
yake ikaita akainuka kwa uvivu
na kuichukua akakuta ni
namba za nje ya nchi.
“Huyu lazima atakuwa
David “ akawaza na
kuipokea.
“ Hallow” akasema
“ Hallow malaika wangu”
ikasema sauti ya David
Zumo
“ David habari yako mpenzi?
“ Nzuri mpenzi
wangu.Habari za usiku
huu? Umeshindaje leo?
“ Nimeshinda salama
David.Pole na mihangaiko
ya siku”
“ Ahsante
Monica.Tunaendelea vyema
na taratibu za mazishi.”
Akasema David
“ Tayari mmekwisha panga
tarehe ya mazishi?
“ Ndiyo .Tayari tumepanga
.Mwili utaondoka kesho
kuelekea Kinshasa na kesho
kutwa tutampumzisha
Pauline.Nimeona hakuna
sababu ya kuweka msiba huu
kwa muda mrefu wakati kuna
mambo mengi yananikabili.Kwa
hiyo kesho jioni nitatuma ndege
kuja kuwachukua na kuwaleta
Congo wewe na wazazi wako ili
kuhudhuria mazishi ya Pauline
hapo kesho kutwa.Natumai
wazazi tayari wanafahamu
kuhusu suala hili na
wataungana nawe”
“ Ndiyo David .Tayari
nimekwisha wajulisha na
tutakuwa nao siku hiyo ya
mazishi.”
“ Nashukuru sana.Jambo
lingine ninalotaka kukwambia
usiku huu ni kwamba
nimewasiliana na ujumbe
nilioutuma kuja kuonana na
wazzzi wako na wamenieleza kila
kitu na ninachukua nafasi hii
kukushukuru sana wewe na
wazazi wako kwa kuupokea
ujumbe wangu na kufanya nao
mazungumzo yenye afya na
kuanzisha rasmi mchakato wa
ndoa yetu.Yale yote
yaliyoelekezwa nitayafanyia kazi
na ndani ya muda mfupi ujao
baada ya mazishi ya Pauline
nitautuma tena ujumbe wangu
uje kwa ajili ya kukamilisha
mambo yaliyoagizwa.”akasema
David
“ David wazazi na ndugu
zangu pia wamefurahi sana kwa
kuonyesha nia yako ya dhati ya
kutaka
Kufunga ndoa na mimi.Pamoja
na hayo kuna jambo nataka
kushauri.Kwa nini masuala
haya yasiahirishwe kwa muda ili
makovu ya kifo cha Pauline
yapone ?.”
“ Monica mpenzi wangu
nimekwisha kueleza kuhusu
suala hili kwamba hakuna
yeyote ambaye anaweza kuzuia
mipango yetu.Pauline amefariki
na hatarudi tena na sisi
tuliobaki maisha yanaendelea
kwa hiyo hakuna kitu
kitakachosimama.Mipango yote
itakwenda kama
tulivyopanga.Usiogope watu
kusema hiyo ni jadi ya
wanadamu lazima wataongea tu
lakini maneno yao haya athari
zozote kwetu.Sababu nyingine ni
kwamba muda si mrefu toka
sasa jamhuri ya kidemokrasia
ya Congo itakuwa nchi ya
kifalme na mimi ndiye
nitakayetawazwa kuwa mfalme
wa kwanza wa Congo kwa hiyo
kabla ya kutawazwa mfalme
lazima kwanza niwe na
mke.Wiki ijayo wananchi
watapiga kura ya maoni ili
kukubali nchi yao iwe ya
kifalme.Wewe ndiye
utakayekuwa malkia wa kwanza
wa Congo kwa hiyo mpenzi
wangu naomba sana kusiwe na
kikwazo chochote katika
mapenzi yetu.Naomab kila kitu
kiende kwa haraka .Nina hamu
sana ya kuishi na wewe”
akasema David
“ Ahsante nimekuelewa
David. Nashukuru kwa upendo
wako mkubwa kwangu.”
“ Hata mimi nakushukuru
sana kwa kukubali kuwa mpenzi
wangu.Ninajiona ni mwanaume
mwenye bahati kubwa .”
akasema David na uso wa
Monica ukajenga tabasamu
kubwa.Ukimya mfupi ukapita
kisha Monica akasema
“ David kuna jambo nataka
nikushirikishe.Ni la muhimu
sana kati yangu nawe” akasema
Monica
“ Nishirikishe
Monica.Usiogope kunishirikisha
kitu chochote ambacho unaona
kina manufaa kwetu.Hata kama
ni jambo gumu kiasi gani
naomba unishirikishe” akasema
David.
“ Ni kwamba….” Akasema
Monica na kusita
“ Nitakueleza tukionana ana
kwa ana.Huu si wakati wake”
akasema Monica
“ Sawa
Monica.Utanishirikisha ukiwa
tayari.Kabla sijasahau nimesikia
kumetokea shambulio la kigaidi
leo jijini Dare s salaam.Poleni
sana .”
“ Ahsante sana mpenzi.Ni
shambulio kubwa na bay asana
ambalo limepoteza maisha ya
watu wengi wakiwamo viongozi.
Alshabaab wanadai kuhusika na
shambulio hili .Ni watu makatili
mno hawa.” Akasema Monica.
“ Hiki kilichotokea leo
kinanifanya nikuone kama
hauko salama.Niruhusu mpenzi
wangu nikuwekee ulinzi imara
na madhubuti.Nataka uwe
salama” akasema David
“ Niko salama David
usihofu.Pamoja na shambulio
hili lakini bado Tanzania ni nchi
salama .Kwa muda huu kabla ya
kuingia katika ikulu ya
Kinshasa naomba niutumie
kuwa huru kuishi bila ulinzi
wowte ila pale nitakapokuwa
tayari mke wako sintakataa
ulinzi” akasema Monica
“ Sawa Monica.Natamani
sana kuendelea kuzungumza
nawe usiku mzima lakini kuna
majukumu mengine
yananikabili.Kwa heri kwa sasa
nitawasiliana nawe tena kesho
ila mjiandae kesho jioni ndege
yangu itakuja kuwachukua”
akasema David
“ Ahsante David.Sauti yako
imenifanya walau nijisikie
faraja kubwa na nitalala usingizi
mzuri sana.Uwe na usiku
mwema mpenzi” akasema
Monica na David akakata simu
“ Kadiri siku zinavyokwenda
najikuta nikizidi kumpenda
David.Ninavyojihisi sasa
kuhusu yeye ni tofauti na
nilivyokuwa nikijihisi pale
mwanzo kabla sijamfahamu
vizuri.Nilitaka kumueleza
kuhusiana na hiki
kilichonitokea cha kutoziona
siku zangu lakini
nimeshindwa.Hata hivyo lazima
nimueleze angali mapema ili
afahamu kinachoendelea ili
kama ikithibitika nina ujauzito
kusiwe na mgogoro wowote kati
yetu.Baada ya shughuli za
msiba kumalizika lazima
nitafute nafasi nizungumze naye
nimueleze kuhusu suala hili.”
Akawaza Monica na mara
akakumbuka kitu
“ Jana marcelo alinipigia
simu na kunitaka tuonane na
nikamuahdi tungeonana leo
.Nimesahau kabisa kama
nilimuahdi kumtafuta
leo.Nimefurahi sana kusikia
kwamba yuko huru.Nadhani
baada ya maombi yangu kwa
rais akaamua kumuacha awe
huru .Vipi kuhusu wale
wanaomtafuta kumuua tayari
wamekamatwa? Usalama wa
Marcelo ni pale tu wale
waliokuwa wanataka kumuua
watakapokamatwa.Ningepata
nafasi ya kuonana naye
tungezungumza mengi .Hata
hivyo napaswa sana
kumshukuru Austin kwa
msaada wake wa kuniunganisha
na rais.” Akawaza na
kumkumbuka Austin
“ Siku yangu imekuwa
mbaya sana hadi nimesahau
kumkumbuka Austin.Najua
amejihisi vibaya kwa siku nzima
kupita bila kumjulia hali.Siwezi
kulala bila kujua maendeleo
yake.Ngoja nimpigie simu”
Monica akainuka na
kuchukua simu akazitafuta
namba za Austin akampigia.
“ Hallow queen Monica”
akasema Austin baada ya
kupokea simu ya Monica
“ Am I a Queen ? Akauliza
Monica huku akicheka
“You are queen of
Africa.Arent you? Akauliza
Austin.
“ Ofcourse I am” akajibu
Austin na wote wakacheka.
“ Vipi hali yako Monica?
Akauliza Austin
“ Ninaendelea vyema ila
samahani sana kwa kutokujulia
hali toka asubuhi.Unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri.Leo
nimeshinda salama nina nguvu
za kutosha” akajibu Austin
“ Nafurahi kusikia
hivyo.Nikipata nafasi kesho
nitakuja
kukutembelea.Amarachi naye
anaendeleaje?
“ Anaendelea vyema”
“Mpe salamu
zangu.Nimempenda
sana.Nakushauri Austin kama
bado hauna mchumba basi Yule
anakufaa sana.”akasema Monica
na kuangua kicheko
“ Yule ni rafiki yangu
mkubwa na siwezi kuwa na
mahusiano naye hata
kidogo”akajibu Austin
“ Hakuna ubaya wowote
Austin wa kuubadili urafiki
kuwa uchumba.Nimekushauri
hivyo kwa sababu
nimemchunguza yeye alivyo na
wewe mnaendana sana.Lifanyie
kazi hilo Austin.Au tayari unaye
mchumba?
“ C’mon Monica mbona
umenikalia kooni mimi kuhusu
suala la mahusiano? Vipi
kuhusu wewe una mpango gani?
Mbona mpaka sasa bado uko
mwenyewe? Akauliza Austin
“ Nani kakwambia niko
mwenyewe Austin? Akauliza
Monica
“ Toka tumefahamiana
hujanieleza chochote kama upo
katika mahusiano nikajua
hauna mtu” akasema Austin na
Monica akacheka kidogo
“ Malkia wa Afrika
nitakosaje mfalme ? Au
unatafuta nafasi Austin?
Akauliza Monica na wote
wakacheka
“ Ukweli ni kwamba ,mimi
ninaye mtu wangu na ambaye
ikimpendeza Mungu nitafunga
naye ndoa miezi michache
ijayo.”
“ Ouh kumbe tayari
umepiga hatua kubwa namna
hiyo,hongera sana Monica.Ana
bahati sana mwanaume huyo
aliyepata nafasi hiyo
adimu.Ningebahatika kumjua
ningempa hongera zake na
ningemuonya asithubutu
kukutoa chozi ama sivyo atajibu
kwangu” akasema Austin na
kumfanya Monica acheke.
“ Hawezi kunitoa chozi ni
mtu mwenye mapenzi ya kweli
na mimi na tunapendana”
“ Nafurahi kusikia
hivyo.Naweza kumfahamu ni
nani? Akauliza Austin huku
akitabasamu
“ mhh ! Austin itoshe tu
kufahamu kuwa nina mchumba
na ninatarajia kufunga naye
ndoa.Utamjua hapo baadae
muda ukifika” akajibu Monica
“Sawa Monica .Kuna jambo
alinieleza Amaarchi jana
kwamba ulipata msiba.Pole
sana”
“ Alikwambia?
“ Ndiyo alinieleza.”
“ Ni kweli.Tukiwa garini
wakati ananirejesha nyumbani
jana asubuhi ,nilipata taarifa za
msiba wa rafiki yangu mke wa
rais wa Congo anaitwa Pauline
Zumo”
“ Pole sana .Sikujua kama
unafahamiana na familia ya
David Zumo”
“ Ninafahamiana nao”
akasema Monica halafu
akanyamaza kidogo na kusema
“ Austin” akaita Monica
“ Kuna jambo nataka
nikwambie kwani
nisipokwambia leo huenda
ukalisikia na hautajisikia vibaya
kwa nini sikukueleza
kabla.”akasema Monica ukimya
mfupi ukapita akasema
“ David Zumo ndiye mpenzi
wangu ambaye ninatarajia
kufunga naye ndoa miezi
michache ijayo”
Kauli ile ikamstua sana
Austin.
“ David Zumo rais wa
Congo? Akauliza Austin kwa
mshangao
“ Ndiyo.Mbona
umeshangaa? Siwezi kuwa na
mahusiano na David Zumo?
Akauliza Monica
“ Si hivyo Monica.Unajua
David Zumo ni jina kubwa hapa
Afrika na duniani kwa
ujumla.Kulisikia tu jina hili
unastuka. Monica u mwanamke
mwenye nyota ya ajabu
sana.David Zumo amevuka
mabara na kati ya mamilioni ya
wanawake wote duniani
amekuchagua wewe.Hongera
sana” akasema Austin.
“Ahsante. Nadhani sasa kiu
yako ya kumfahamu mtu wangu
imekwisha .”akasema Monica
hukuakicheka
“ Imekwisha na
ninashukuru sana” akajibu
Austin huku akicheka
“Hata hivyo kuna jambo
nataka niliweke sawa .Uhusiano
wangu na David hata mke wake
aliuridhia kwani hakuwa na
mategemeo ya kupona kutokana
na ugonjwa uliokuwa
ukimsumbua.Kwa hiyo usifikiri
kwamba niliingilia ndoa ya mtu”
akasema Monica na kucheka.
“Austin nimefurahi sana
kuzungumza nawe usiku huu
.Naomba sasa nikuache
upumzike .Kwa siku kadhaa
tunaweza tusionane kwani
kesho nina safari ya kuelekea
Congo kwenye msiba wa Pauline
ambaye anatarajiwa kuzikwa
kesho kutwa.Nitakaa huko kwa
siku kama mbili hivi kisha
nitarejea.Nataka nitakaporejea
nikute tayari umepona.”
Akasema Monica wakaagana
“ David Zumo ni kidume
.Anastahili kuwa na malaika
kama huyu.Kwa uzuri wa
Monica anastahili kuwa na mtu
kama David. Sasa nimepata
picha inawezekana ni Monica
ndiye aliyemuomba David Zumo
aongee na rais Ernest ili
amsaidie Marcelo.Nilijiuliza sana
David Zumo amefahamiana vipi
na Marcelo,kumbe ni kwa
sababu ya Monic………….”
Mara simu ya Austin ikaita
na kumtoa mawazoni.Zilikuwa
ni namba ngeni
kabisa.Akaipokea
“ Hallow” akasema
“ hallow unazungumza na
Yasmin Esfahani hapa”ikasema
sauti ya Yasmin upande wa pili
“Hallo Yasmin.” Akasema
Austin
“Nikumbushe jina lako
uliniambia unaitwa
nani?akauliza Yasmin
“ Naitwa Austin”
“ Austin unakumbuka
tulichokubaliana ?Shamim yuko
salama?
“ Shamim yuko salama
usijali.Uko wapi?
“ Naomba kwanza
nizungumze na Shamim halafu
mimi nawewe tutazungumza.”
Akasema Yasmin .Austin
aliyekuwa chumbani amejilaza
akainuka akaelekea sebuleni na
kuwachukua Amarachi na Job
wakaelekea katika chumba cha
Maria.Mlango ukafunguliwa
akaingia na kumpa simu Maria
azungumze na mama
yake.Walizungumza kwa dakika
tano ,Austin akachukua simu
“ Nadhani umeridhika
kwamba mwanao anaendelea
vizuri sasa niambie kile
unachotaka kuniambia”
akasema Austin
“ Kwa sasa niko Zanzibar,
nahitaji haraka sana usafiri wa
kuja Dar es salaam.Niko hoteli
Lepatido.Fanya unavyoweza
niweze kuondoka hapa haraka
niko katika hatari
kubwa.Alshabaab wanafahamu
niko hapa na
wananitafuta.Nahitaji msaada
wa haraka” akasema Yasmin.
“ Yasmin naomba unipe
dakika kadhaa nitakupa jibu “
akasema Austin na kukata simu
akawageukia wenzake
“ Yasmin yuko
Zanzibar.Yuko katika hatari na
anahitaji msaada wa kuja Dar es
salaam haraka
iwezekanavyo.Alshabaab tayari
wanafahamu mahala alipo na
wanamtafuta.Tunatakiwa
tutafute namna ya kufanya
kuweza kumuondoa pale haraka
sana.Mkumbuke kwamba huyu
ni mtu wa muhimu mno na ana
mambo mengi tunayohitaji
kuyafahamu .Naombeni msaada
wa mawazo nini tufanye?
Akauliza Austin.Ukimya mfupi
ukatanda na baada ya tafakari
Amarachi akasema
“ Kitu cha kwanza ambacho
nakiona kifanyike ni kumtaarifu
Yasmin atoke katika hoteli hiyo
haraka sana ,aelekee sehemu
ambayo hataweza kuonekana
wakati sisi tukiendelea na
mchakato wa kutafuta namna
ya kwenda kumchukua kule
Zanzibar”
“ Hilo ni wazo zuri.Mtaarifu
kwanza atoke hapo hotelini
haraka sana kwani Alshabaab
tayari wana ushirika na rais na
wanaweza wakamtumia rais
kutuma vikosi vya polisi haraka
kwenda kumdhibiti.” Akashauri
Job na bila kupoteza muda
Austin akachukua simu na
kumpigia Yasmin.
“ Yasmin nisikilize
vizuri.Nimejadiliana na wenzagu
hapa na kitu cha kwanzaa
ambacho tumeona kifanyike ni
wewe kuondoka haraka sana
hapo hotelini.Nikatapo simu hii
chukua kila kilicho chako
ondoka hapo haraka na uelekee
sehemu ambayo utaona ni
salama na hautaweza
kugundulika kirahisi.Simu yako
izime kabisa na uiwashe pale tu
unapoona kuna ulazima.Mimi
na wenzagu tunatafuta namna
ya kufika huko kwa haraka kuja
kukuchukua.” Akasema Austin.
“ Sawa Austin.Nitafuata
maelekezo yako.Tafadhali
fanyeni haraka” akasema
Yasmin na kukata simu.
“ Hatua ya kwanza
tayari.Kinachofuata sasa ni
namna tutakavyoweza kufika
Zanzibar kwa haraka.Tunahitaji
usafiri wa haraka wa
kutufikisha huko .Endapo
Alshabaab wataomba msaada
kwa rais ,naamini njia zote za
kuingilia na kutokea Zanzibar
zitakuwa katika ulinzi mkali
mno ili kuzuia Yasmin asiweze
kutoka na hii inaashiria
kwamba kutakuwa na
mapambano na hatuogopi
kupambana ili kumpata Yasmin.
Endapo tutapata boti ya
mwendo kasi tutatumia si chini
ya dakika arobaini na tano
kufika Zanzibar.Muda huo ni
mrefu kwa hiyo tutahitaji ndege
au helkopta ili tufike huko kwa
haraka zaidi na kumchukua
Yasmin.”
“ Uko sahihi Austin lakini
swali linakuja tutaipataje hiyo
ndege? Kutokana na tukio
lililotokea leo hakuna ndege
yoyote inayoruhusiwa kutua au
kuruka angani zaidi ya helkopta
za jeshi na polisi.Hatutaweza
kufanikiwa katika hili labda
tutafute usafiri wa boti.”
Akashauri Job
“ Boti itatuchukua muda
mrefu na hatuna huo muda wa
kusubiri.” Akasema Austin na
kuinama kwa muda akatafakari
halafu akainua kichwa na
kumtazama Amarachi.
“Ulimpeleka Monica
nyumbani kwake,unaweza
kupakumbuka? Akauliza Austin
“ Ndiyo ninapakumbuka “
“ Good.Tunakwenda huko
sasa hivi.”
“ Tunakwenda kufanya nini
? akauliza Job
“ Kutafuta namna ya kufika
Zanzibar kwa haraka na salama
zaidi.Job andaa silaha ulizo
nazo hapa ndani na tujiandae
kuelekea Zanzibar” akasema
Austin
“Tunakwendaje huko
Zanzibar Austin? Mbona
hutuweki wazi? Akauliza Job
“Job hatuna muda wa
maneno mengi.Tukiendelea
kupoteza muda hapa
tutampoteza Yasmin.Fuata
maelekezo yangu” akasema
Austin na Job akamuomba
Amarachi akamsaidie kubeba
silaha.Baada ya Job na
Amarachi kuondoka Austin
akachukua simu na kumpigia
rais.Simu ikaita marta ya
kwanza haikupokelewa,akapiga
tena
“ C’mon pick up the phone”
akasema Austin kwa sauti
ndogo na safari hii ikapokelewa
“ Austin niko katika kikao
kizito sana kuhusiana na
mambo yaliyotokea
leo.Tunaweza kuzungumza
baadae tafadhali” akasema rais
“ Mzee naomba dakika moja
tu .Kuna jambo la muhimu sana
nataka nikueleze”
“ Haya sema haraka”
“ Tumepata majibu ya kile
kipimo na kutokana na mambo
yaliyotokea leo itakuwa vigumu
kwa sisi kuonana nawe hivi kwa
hiyo nimeamua kuifungua
bahasha ile kwa niaba yako na
kusoma kilichomo ndani”
“ sawa kabisa.Majibu
yanasemaje? Akauliza Rais
huku moyo ukimwenda mbio
“ Majibu yanaonyesha
kwamba kwa asilimia 99.9999
wewe ni baba wa
Monica.Mheshimiwa rais pamoja
na mambo mazito
yanayokukabili hivi sasa,hii ni
moja ya habari inayoweza kidogo
kukupa ahueni katika kipindi
hiki kigumu.Usiwe na shaka
tena Monica ni mwanao.”
Akasema Austin
“ Austin sijui niseme nini
kwa hili uliloniambia lakini nina
maneno mawili ya kusema
.Ahsante sana . Bila wewe hili
lisingewezekana.Ninaamini
baada ya misuko suko hii
kumalizika basi tutakaa na
kuzungumza kwa
kirefu.Nifikishie salamu zangu
za shukrani kwa wenzako wote.”
Akasema rais
“ Ahsante mzee” akasema
Austin
“ Kuna lingine unalohitaji
Austin? Akauliza rais
“ Ni hilo tu mzee nililotaka
kukufahamisha.Tutaongeza
zaidi mambo yatakapotulia”
“ Ahsante Austin” akasema
rais na kukata simu.
Job na Amarachi wakarejea
na sanduku la chuma lenye
silaha mbali mbali .Kila mmoja
akachukua bastora mbili halafu
Marcelo akaitwa
“ Marcelo tumepata safari ya
dharura tunaelekea
Zanzibar.Sote watatu
tunaondoka na wewe utabaki
hapa ukisubiri
turejee.Hatutachukua muda
mrefu ndani ya saa mbili
tutarejea.Tafadhali usimfungulie
mlango mtu yeyote
Yule.Tunakuachia bastora
utakayoitumia endapo kuna mtu
yeyote atathubutu kuingia
ndani.” Akasema Austin na
kuwatazama akina Job
“ Wote mko tayari?
“ Ndiyo Austin” akasema
Amarachi kisha wakaelekea
garini. Amarachi akashika
usukani wakaondoka .
“ Ndugu zangu naomba
niwaweke wazi,tunakwenda
katika mapambano na lolote
linaweza kutokea huko kwa hiyo
kila moja awe mlinzi wa
mwenzake.Nawakumbusha tu
kwamba Yasmin ni mtu muhimu
mno kwetu .Kupitia kwake
tutafahamu mambo mengi
kuhusiana na rais na
Alshabaab.Vile vile alisema
kwamba anacho kitu kikubwa
cha thamani ambacho
atatupatia ili tumpatie Maria
kwa hiyo kufa au kupona lazima
Yasmin apatikane” Akasema
Austin.
“ Endapo tukifanikiwa
kumpata Yasmin na akakupa
hicho kitu cha thamani
anachokisema,utakuwa tayari
kumuacha yeye na Maria
waende zao? Akauliza
Job.Austin akachukua sekunde
kadhaa kutafakari na kujibu
“ Itategemea na kitu
tutakachokipata toka
kwake.Endapo tutapata taarifa
ya maana basi nitamuacha yeye
na mwanae waende lakini bado
ni mapema sana kusema
chochote kuhusu suala hilo.”
Akasema Austin.
“ Austin hali yako bado
haijakaa sawa sawa,tafadhali
ujizuie sana kuingia katika
mapambano endapo yatatokea
,tuache mimi na Amarachi
tupambane ikitokea rabsha
yoyote” akasema Job na Austin
akatabasamu
“ Ni kweli hali yangu bado
haijakaa sawa sawa lakini sina
budi kuongeza nguvu katika
mapambano.We must fight
together” akasema Austin
Jiji la dare s salaam
halikuwa na zile pilika pilika
zake za usiku ,na hii
ilisababishwa na kile
kilichokuwa kimetokea
jioni.Watu walikuwa wachache
sana barabarani usiku huu na
hata magari yalipungua mno.Hii
iliwasaidia sana akina Austin
kuchukua muda mfupi kufika
nyumbani kwa Monica.
“ Ni pale kwenye lile
ghorofa” akasema Amarachi
wakiwa mita kadhaa kabla ya
kufika nyumbani kwa Monica
“ Mbona amechagua kuja
kuishi nje ya mji namna hii?
Akauliza Job na hakuna
aliyemjibu.Austin akachukua
simu na kumpigia Monica
“ Austin” akasema Monica
baada ya kupokea simu
“ Monica samahani kwa
kukusumbua usiku huu”
“ Usijali Austin.Kuna tatizo
gani?
“ Monica nimekuja kwako
kuna jambo la dharura nataka
tuongee”
“Acha kunitania Austin.”
Akasema Monica
“ Sikutanii Monica.Ni kweli
nimekuja hapa kwako.Niko mita
kadhaa toka geti lako” akasema
Austin
“ Umefahamuje nyumbani
kwangu? Akauliza Monica
“ Niko na Amarachi ambaye
anapafahamu kwako” akajibu
Austin.Monica akavuta pumzi
ndefu na kuuliza
“ Kuna tatizo gani Austin?
Akauliza Monica
“ Tayari nimefika hapa
getini.” Akasema Austin na
kukata simu.Gari lilisimama nje
ya geti la Monica na walinzi
wakawafuata.
“ habari zenu” Austin
akawasalimu
“ Nzuri .Mna shida gani?
“ Tunahitaji kuonana na
Monica”
“ Madam amepumzika na
huwa akiingia ndani hatoki
tena.Mnatakiwa mje kesho”
Mara mlango mdogo wa geti
akatokea Monica.Alishangaa
sana .
“Austin !! akasema kwa
mshangao na kuwaamuru
walinzi wafungue geti Amarachi
akaingiza gari ndani
“ Sikuamini kama kweli
umekuja kwangu.Karibu sana”
akasema Monica na
kuwakaribisha akina Austin
sebuleni
“ Ahsante Monica” akajibu
Austin
“ Monica samahani kwa
kukuvamia ghafla usiku huu
lakini kuna tatizo limenifanya
nije kwako kutafuta
msaada.Kwanza kabla ya yote
naomba nikutambulishe kwa
huyu mwenzangu ambaye bado
hujamfahamu,anaitwa Job
Israel.Ni rafik yangu mkubwa”
akasema
“ Hi Monica” akasema Job
na kuinuka akampa Monica
mkono
“ Austin kuna tatizo gani?
Nikusaidie nini?umenistua
mno.Sikutegemea kukuona
hapa kwangu mida hii” Akauliza
Monica kwa wasi wasi.
“ Numepata dharura nataka
kwenda Zanzibar sasa hivi na
ninahitaji usafiri wa haraka
sana wa kuelekea huko
.Kutokana na tukio lililotokea
leo imekuwa vigumu sana
kupata ndege ya haraka ya
kunifikisha huko mimi na
wenzangu kwa hiyo niko hapa
kutafuta msaada wako”
akasema Austin na Monica
akashangaa
“ Austin
sijakuelewa.Unataka
nikusaidiaje? Mbona mimi sina
usafiri wowote wa kukufikisha
huko Zanzibar kwa haraka?
Akauliza Monica
“ Nitakupa namba ya simu
ya rais utampigia na kumuomba
akusaidie upate usafiri wa
haraka wa kwenda
Zanzibar.Mueleze kwamba
umepata dharura na unahitaji
kwenda huko haraka
iwezekanavyo.Mweleze kwamba
unahitaji usafiri wa haraka
kama ndege” akasema Austin na
Monica akamtazama kwa
mshangao mkubwa hakujua
ajibu nini
“ Monica fanya hivyo
nilivyokueleza tafadhali.Nisaidie
katika hilo” akasema Austin
“ Austin unanishangaza
sana.Sina mazoea wala ukaribu
na rais nitaanzaje kumueleza
mambo kama hayo? Na vipi
iwapo atafahamu kama
ninamdanganya? Akauliza
Monica
“ Fanya nilivyokueleza
Monica na rais atakubali bila
wasiwasi.Usimueleze kitu
chochote kuhusu kuonana na
mimi na akikuuliza
utaambatana na nani kwenda
huko Zanzibar mwambie
utakwenda na walinzi wako”
akasema Austin.Bado Monica
alionyesha kusita
“ Monica please.I real need
your help .” akasema
Austin.Kwa shingo upande
Monica akaenda chumbani
akachukua simu yake na
kurejea sebuleni,akapewa
namba za rais akapiga.
“ Simu haipokelewi”
akasema Monica
“ Piga tena” akasema
Austin.
“ Austin kuna tatizo gani?
I’m scared” akasema Monica
“ Tutaongea baadae lakini
piga tena hiyo simu” akajibu
Austin.Monica akapiga tena ile
simu ikaita lakini
haikupokelewa.
“ Austin simu haipokelewi”
akasema Monica
“ Endeleea kupiga hadi
apokee” akasema Austin na
Monica akapiga tena .Safari hii
simu ikapokelewa
“ hallow” ikasema sauti ya
upande wa pli ambayo Monica
akaitambua ilikuwa ya rais
“ Shikamoo mzee.Samahani
ni mimi Monica”
“ Monica !!! akasema rais
kwa mshangao.
“Ndiyo mzee.Samahani sana
kwa usumbufu usiku huu.”
“ Bila samahani
Monica.Nimefurahi kusikia sauti
yako.Vipi hali yako? Akauliza
rais aliyeongea kwa furaha sana
kana kwamba hakuna tatizo
lolote kubwa lililotokea nchini
“ Ninaendelea vizuri mzee.”
“ Monica nimefurahi mno
kwa kunipigia simu”
“ Nashukuru kusikia hivyo
mheshimiwa rais.” Akasema
Monica halafu akasita.Austin
akamfanyia ishara aseme kile
alichomuelekeza.
“Mzee samahani..”akasema
Monica
“ Bila samahani Monica.”
“ Nimelazimika kukupigia
simu usiku huu kuomba
msaada wako.Kwanza naomba
ufahamu kwamba nilichukua
namba zako hizi kwa Austin ili
niwasiliane nawe kuhusiana na
lile suala tuliloongea juzi”
akasema Monica
“ Lile suala ninalifanyia kazi
Monica.Lini unataka kwenda
kumuona Marcelo? Akauliza rais
“ Mzee leo sitaki kuongelea
hilo suala bali nina tatizo lingine
ambalo nahitaji sana msaada
wako kwani kwa wakati huu
sina mwingine ninayeweza
kumkimbilia kuomba msaada
zaidi yako.Nimejaribu kutafuta
msaada sehemu mbali mbali
nimekosa na nikaamua kuja
kwako .”
“ Sema shida yako Monica
na nikutatulie haraka sana”
akasema rais.Monica akavuta
pumzi ndefu na kusema
“ Shida yangu nataka usafiri
wa haraka wa kunifikisha
Zanzibar ndani ya muda mfupio
ujao.Kuna mtu ambaye nahitaji
sana kuonana naye kwa haraka
na kurejea tena Dar es salaam”
akasema Monica
“ Unataka kwenda
Zanzibar?!! Rais akashangaa
“ Ndiyo mheshimiwa rais
“ Usiku huu?
“ Ndiyo mzee” akajibu
Monica.Rais akasikika akivuta
pumzi ndefu kisha akasema
“ Kuna nini huko Zanzibar?
Huwezi kusubiri hadi kesho
asubuhi ili nikutafutie usafiri wa
haraka uende na kurudi?
“ Mheshimiwa rais nahitaji
kufika Zanzibar ndani ya muda
mfupi ujao lakini nimejaribu kila
namna ya kuweza kupata usafiri
nimekosa ndiyo maana
nimekupigia wewe ili
unisaidie.Naomba sana
mheshimiwa rais ni muhimu
mno”
“ Kuna nini hasa
kinachokupeleka huko usiku
huu? Unaweza ukanieleza
tafadhali ?
“ Kuna mdau nakwenda
kuonana naye usiku huu
ambaye ataondoka Zanzibar
ndani ya dakika hamsini
zijazo.Huyu ni mtu muhimu
sana katika shughuli zangu za
kujitolea kwa jamii.Nikimkosa
mambo yangu mengi
yatakawama.Isitoshe kesho
alfajiri na mapema nitaondoka
kueleka Congo kwa ajili ya
kuhudhuria mazishi ya mke wa
David Zumo Mzee kwa hiyo
nahitaji kwenda Zanzibar na
kurejea usiku huu.Nahitaji sana
msaada wako.Ukishindwa wewe
basi mambo yangu mengi
yatakwama” akasema
Monica.Kimya cha sekunde
kadhaa kikapita halafu rais
akasema
“ Kuna jambo kubwa
limetokea hapa nchini leo hii na
ninatumai tayari umelisikia na
ndiyo maana njia zote za kuingia
na kutoka zimefungwa lakini
hata hivyo
nitakusaidia.Nitakupatia ndege
maalum itakupeleka Zanzibar
na kukusubiri hadi
utakapomaliza mazungumzo
yako na huyo jamaa kisha
itakurudisha.Nawatuma vijana
wangu wawasiliane nawe
utawaelekeza mahala ulipo ili
waje wakuchukue wakupeleke
uwanja wa ndege haraka ndani
ya muda mfupi ujao”
“ Ahsante sana mheshimiwa
rais”
“ Monica nimefurahi sana
umepiga simu.Siku nyingine
ukiwa na shida yoyote muda
wowote usisite kunipigia simu
na nitakusaidia” akasema
Ernest na kukata simu.
“ It’s done” akasema Monica
“ Ahsante sana
Monica.Umefanya jambo kubwa
mno.Sasa kajiandae tunaondoka
wote kwenda Zanzibar.”
“ Mnaondoka na mimi?
Akauliza Monica
“ Ndiyo Monica
.Tunakwenda wote
Zanzibar.Hatuwezi kwenda bila
wewe” akasema Austin
“ Austin hapana,siwezi
kwenda Zanzibar.Tayari
nimekwisha watafutia usafiri
hivyo siwezi kwenda Zanzibar”
“ Naomba tafadhali
uongozane nasi Monica.Bado
tunahitaji sana msaada wako
hata huko Zanzibar”
“ msaada wangu tena? Kuna
nini kinaendelea Austin?
“ Nitakueleza hapo baadae
lakini kwa sasa naomba
ukajiandae” akasema Austin na
simu ya Monica
ikaita.Akaipokea na kuongea na
mpigaji .Alikuwa ni mtu
aliyepewa maelekezo na rais .
“ Tayari rais amekwisha
tuma watu kuja kunichukua
.Twendeni niwapeleke mahala
nilikowaelekeza tukutane.Watu
hao hawanifahamu kwa hiyo
Amarachi utajifanya ni Monica
na mtakwenda salama na
kurudi bila tatizo lolote”
“ Monica please.Naomba
ukubali kuongozana nasi.Bado
tunahitaji sana msaada wako ”
akasema Austin
“ Austin natamani sana
kukusaidieni na tayari
nimefanya hivyo ila suala la
kwenda Zanzibar hilo
mtanisamehe.Sintakwenda
huko.” Akasema Monica
akionekana kutokubadili
msimamo wake.Austin akakuna
kichwa kisha akasema
“ Ni vipi iwapo mimi na
wewe tukafanya makubaliano?
“ makubaliano?
“ Ndiyo.Tufanye
makubalianao kwamba twende
wote Zanzibar halafu
tutakaporejea nitakueleza jambo
kubwa ambalo hulifahamu
linalokuhusu wewe” akasema
Austin na Monica akashangaa
“ Jambo kubwa
linalonihusu mimi? Akasema na
kucheka kidogo
“ Austin unanifanya
nicheke.Hatuna muda mrefu
toka tumefahamiana na
haufahamu chochote kuhusu
mimi” akasema Monica
“ Monica ninakufahamu
vizuri kuliko unavyojifahamu
mwenyewe.Kama unataka
kufahamu hicho kitu
ninachokwambia twende wote
Zanzibar na tumkirejea
nitakueleza kila kitu.” Akasema
Austin.Monica akafikiri kidogo
kisha akasema
“Fine .Nitakwenda nanyi
Zanzibar lakini ni kwa sababu
ninakuamini Austin.Isingekuwa
hivyo nisingekubali kabisa
kufanya hivyo.wait for me here”
akasema Monica na kuelekea
chumbani kwake akavaa haraka
haraka na kurejea sebuleni
akawachukua akina Austin
wakaondoka.
Muda mfupi baada ya
kutoka nyumbani kwa
Monica,simu ya Austin ikaita
.Zilikuwa ni namba ngeni
kabisa.Akapokea
“ hallow” akasema
“ Austin ni mimi
Shamim.Umefikia
wapi?Umefanikiwa kupata
usafiri ?
“ Ndiyo Shamim.Muda
mfupi ujao nitakuwa tayari
nimefika Zanzibar.Umekwisha
toka pale hotelini?
“ Ndiyo nimetoka niko
katika klabu moja hapa
nimetumia simu ya jamaa
Fulani ambao ninawanunulia
pombe .Simu yangu nimeizima
na kuitupa.Ukifika piga namba
hizi.” Akasema Shamim.
“ Sawa Shamim.Chukua
tahadhari’ akasema Austin na
kukata simu
“ Austin simuelewi
kabisa,mbona amebadilika
namna hii usiku huu? Si Yule
Austin niliyemfahamau siku
chache zilizopita ambaye uso
wake umejaa tabasamu.leo hii
hacheki na hata hawa wenzake
wote wamenuna
hawacheki.Kuna nini
kinaendelea? Ee Mungu nisaidie
huko niendako nisijui nini
kinakwenda kutokea” akawaza
Monica
Waliwasili mahala ambako
Monica alipanga kukutana na
watu waliotumwa na rais
kumpeleka uwanja wa
ndege.Akamuelekeza Amarachi
aegeshe gari .Karibu na pale
walipoegesha kulikuwa na gari
limeegeshwa.
“ Monica ukiulizwa na watu
hao sisi ni akina nani sema ni
walinzi wako” akasema Austin
kisha wakashuka.Mlango wa
gari moja kati ya yale mawili
ukafunguliwa wakashuka jamaa
wawili mmoja mfupi mnene na
mwingine mfupi mrefu wastani
wakawafuata akina Monica.
Zanzibar ? Akauliza mmoja
wao
“ Ndiyo” akajibu Austin
“ Tumepewa maelekezo ya
mtu mmoja tu kumpeleka
Zanzibar anaitwa Monica.Ninyi
wengine mtaishia hapa”
akasema yule jamaa
“ Hawa ni walinzi wangu na
ninaambatana nao kila sehemu
niendako” akasema Monica
“ Haya ni maelekezo ya rais
kwamba ni wewe tu
unayekwenda Zanzibar na hawa
wengine watakusubiri hadi
utakaporudi.Jukumu la ulinzi
tutalichukua sisi hadi
utakaporudi kisha
tutakukabidhi kwa walinzi
wako” akasema Yule jamaa
mrefu mwembamba.
“ Monica tafadhali naomba
tusipoteze muda .Ndege iko
tayari inatusubiri.Ingia garini
tuondoke” akasema jamaa mfupi
na mara kikatokea kitendo cha
ghafla ambacho wale jamaa wala
Monica hawakukitarajia.Austin
alichomoa bastora na kumlenga
yule jamaa mfupi,kufumba na
kufumbua Job na Amarachi nao
wakatoa bastora zao.
“ Kwa kuwa mmekuwa
kiburi kuanzia sasa mtafuata
maelekezo nitakayowapa”
akasema Austin na kumtaka
Amarachi awasachi wale jamaa
na kuchukua silaha zao.Monica
akabaki katika mshangao
mkubwa. Hakuamini kile
alichokiona .Alihisi miguu
kuishiwa nguvu.
“ Get in the car” akaamuru
Austin wakaingia garini na
mmoja wale jamaa akawasha
gari wakaondoka kuelekea
uwanja wa ndege.
“ Mungu wangu naomba
unisaidie niweze kurejea
nyumbani salama.Sikutegemea
kama Austin anaweza akafanya
kitu kama kile.Ni nani huyu
Austin? Ni mpelelezi? Ni
usalama wa taifa ? Najuta
kujenga urafiki na watu
nisiowafahamu.Leo ni mwisho
kupapatikia watu na sasa sijui
ninapelekwa wapi.Sielewi kama
ninapelekwa kuuawa au vipi.Ee
Mungu nisaidie nirejee salama”
akawaza Monica
Safari ilikuwa ya kimya
kimya hadi walipofika uwanja
wa ndege wa Julius
Nyerere,wakasimamishwa getini
kwa ajili ya ukaguzi.Jamaa
aliyekuwa anaendesha akageuka
akamtazama Austin aliyekuwa
amekaa kiti cha pembeni.
“ Ukifanya jambo lolote la
kijinga tutawaua wote!!!
Akasema kwa sauti ndogo.Yule
jamaa akashusha kioo na kutoa
kitambulisho chake akajieleza
kwamba mle garini kuna wageni
wa rais ambao wanatakiwa
kupelekwa Zanzibar mara
moja.Wakaruhusiwa kupita
wakaelekea katika maegesho ya
watu maalum wakaegesha
gari.Wale walinzi wawili
wakafungwa miguu na mikono
wakafungwa vitambaa usoni na
kuwekewa matambara mdomoni
.Austin akamfanyia ishara Job
ambaye aliwapa kipigo
wakapoteza fahamu kisha
wakawaacha mle ndani ya gari
na kulifunga wakaondoka na
funguo.Wakatembea kuelekea
ilipo ndege wakaingia na safari
ya kueleka Zanzibar ikaanza.
Austin akamfuata Monica
ambaye sura yake ilionyesha
woga mkubwa na kukaa kiti cha
pembeni yake
“ Austin ,what’s going on?
Who are you? Akauliza kwa wasi
wasi
“ I’m sorry ,I didn’t want
that to happen infront of you”
akasema Austin.Monica
akamtazama kisha akauliza
“ Who are you? You are not
that Austin I know” akasema
Monica
“ Nitakueleza kila kitu
baadae baada ya kurejea Dar es
salaam ila nakuomba usiwe na
hofu yoyote.Mimi na wenzangu
tutakulinda na utakuwa salama”
akasema Austin
 
SEASON 6: SEHEMU YA 7

Kikosi cha watu nane
kikiongozwa na mkuu wa idara
ya usalama wa taifa Silvanus
Kiwembe kiliwasili kisiwani
Unguja kwa kutumia ndege ya
jeshi.Tayari gari nne zilikwisha
andaliwa kwa ajili yao na mara
tu waliposhuka katika helkopta
wakaingia katika magari yale na
kuondoka tayari kabisa kuifanya
kazi iliyowapeleka.
Hotel Lepatido ni moja ya
hoteli kubwa yenye hadhi ya
nyota tano inayomilikiwa na
mwekezaji raia wa Italia.Ni hoteli
inayosifika kwa kuwa na
huduma nzuri na hivyo kuifanya
iwe maarufu na kufikiwa na
wageni wengi wanaotoka mataifa
mbali mbali.
Silvanus na vijana wake
walifika Lepatido hotel
wakashuka na kujitambulisha
kwa uongozi wa hoteli na
kuwaeleza dhumuni
lililowapeleka pale.Meneja wa
hoteli akaongozana nao hadi
katika chumba walichokuwa
wamepanga akina Yasmin
.Akagonga lakini
hakujibiwa.Akakinyonga kitasa
mlango ulikuwa
umefungwa.Akachukua kadi ya
akiba akaufungua mlango
wakaingia ndani.Chumba
kilikuwa kitupu na damu
ilitapakaa kila mahali. Silva
akawaelekeza vijana wake
wachukue tahadhari .Walipekua
taratibu na kwa tahadhari
kubwa na mmoja wao
alipofungua mpango wa bafu
akashuhudia mtu mmoja
ameuawa akiwa amechakazwa
risasi kichwani.Walikagua kila
sehemu lakini Yasmin
hakupatikana..Silva akampigia
simu rais.
“Silva nipe ripoti ya huko?
Mmekwisha fika?
“ Ndiyo mheshimiwa
rais.Tumetumia muda mfupi
kufika hapa na tayari tuko eneo
la tukio”
“Good.Nipe ripoti
mmefanikiwa kuwapata yasmin
na Tariq?
“Tumekuta kuna mtu
mmoja ameuawa ambaye
naamini atakuwa ni Tariq lakini
Yasmin hayupo ametoweka.”
“ Oh my God !!! akasema
Rais
“ Hakuna chochoe
mlichokipata? hakuna bahasha
yoyote mmeikuta humo ndani?
Akauliza Rais
“ Hakuna kitu chochote
tumekikuta humu ndani .”
Rais akavuta pumzi ndefu
na kusema
“ Yasmin bado hajatoka
Zanzibar.Yuko hapo hapo na
anatakiwa atafutwe kwa udi na
uvumba usiku huu apatikane.Ni
mwanamke hatari sana .Silva
washirikishe polisi pia katika
suala hili ili wasaidie katika
kumtafuta Yasmin na
kuhakikisha anapatikana
.Ifanyike doria kubwa kila
sehemu ,katika hoteli
zote,kumbi zote za starehe
kukaguliwe na muhakikishe
Yasmin anapatikana.Hakuna
ndege wala meli kuingia au
kutoka hadi hapo Yasmin
atakapokuwa amepatikana”
akasema Rais
“ Sawa mzee nitafanya
hivyo” akajibu Silvanus.
“ Silva kabla sijasahau kuna
ndege itatua katika uwanja wa
Zanzibar ndani yake yuko
msichana mmoja anaitwa
Monica.Huyu ana kibali
changu.Ana shughuli yake ya
muhimu hapo Zanzibar usiku
huu na akishaimaliza ataondoka
mara moja.Kuna walinzi wawili
ameambatana nao naomba
aongezewe ulinzi ,apatiwe gari
na akimaliza shughuli zake
arudishwe katika ndege arejee
Dar es salaam.Hilo nalo ni la
muhimu sana na ulipe uzito
mkubwa pia” akasema rais na
kukata simu.
“ Mambo yanazidi kuwa
magumu.Yasmin kaenda wapi?
Mategemeo ya kuipata hati ya
muungano yanaanza kuwa
madogo.Ni vipi endapo Yasmin
hatapatikana? Akajiuliza
“ Lazima apatikane.Nina
uhakika bado yupo Zanzibar na
hajatoka nje ya kisiwa kile”
akawaza rais na kurejea
ukumbini kuendelea na kikao
na wenzake huku akijitahidi
kuficha wasiwasi mkubwa
aliokuwa nao
 
SEASON 6: SEHEMU YA 8
Ndege walimopanda akina
Austin ikatua salama katika
uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Abeid Aman karume
Zanzibar uliokuwa ukilindwa
kwa ulinzi mkali .Mlango
ukafunguliwa na Austin akawa
wa kwanza kushuka
.Akasalimiana na jamaa wawili
ambao walijitambulisha kuwa
wametoka idara ya usalama wa
taifa na wametumwa pale kwa
ajili ya kumchukua Monica
kumpeleka sehemu anakotaka
kwenda.
“ Ahsanteni lakini hakuna
haja kwani tayari sisi walinzi
wake tupo.Tunachohitaji ni gari
tu” akasema Austin
“ Sisi tunatekeleza amri ya
mkuu wetu ambayo imetoka
kwa rais.Kwa hiyo tunaomba
mtuache tufanye kazi
zetu.Monica atakapotoka
Zanzibar atakuwa wa kwenu
lakini jukumu lote la ulinzi wa
Monica kwa hapa ni la kwetu
sisi” akasema mmoja wa wale
jamaa akaingia ndegeni na
kumtaka Monica ashuke
wakaongozana hadi katika gari
wakaondoka.
“ Tunaelekea wapi? Akauliza
mmoja wa wale jamaa.Monica
akamtazama Austin ambaye
naye hakujua mahala alipo
Yasmin.Akaomba gari lisimame
akashuka akaenda kupiga
simu.Akashusha pumzi baada
ya simu kupokelewa.
“ Austin” akaita Yasmin
baada ya kupokea simu
“ Yasmin tayari niko
Zanzibar.Nielekeze mahala
uliko” akasema Austin na
Yasmin akamuelekeza kisha
akarejea garini na kumtaka
dereva awapeleke Ibo night
club.Safari ilikuwa ya kimya
kimya hadi walipofika katika
klabu ile ambayo Austin
alielekeza.
“ Mimi nitaingia ndani
.Monica stay in the car”
akasema Austin aliyekuwa
ameketi nyuma kabisa na
wakati akishuka akampa Job
ishara fulani .
Mara tu aliposhuka Job na
Amarachi waliokaa viti vya kati
kati wakapeana ishara na kwa
kasi ya umeme wakawavamia
wale walinzi wawili waliokuwa
viti vya mbele na kuwapiga
kabali hadi wakahakikisha
wamepoteza fahamu. Amarachi
akakalia usukani.Monica
aliogopa sana.Hakuota kama
siku moja atayashuhudia
mambo kama yale yakifanyika
mbele yake.Moyoni alizidi kusali
na kumuomba Mungu amlinde
na amrejeshe Dar es salaam
salama.
Austin aliingia katika ile
klabu na kumpigia simu Yasmin
akamuelekeza mahala alipo na
baada ya muda Yasmin
akatokea akiwa na begi
lake.Wakatazamana kisha
Austin akampa ishara amfuate.
Amarachi alimuona Austin
akija akiwa ameongozana na
mwanamke mmoja nyuma yake
akashusha kioo na kumfanyia
ishara akae mbele.Yasmin
akafunguliwa mlango akaingia
kiti cha kati kati na gari
ikaondoka kurejea uwanja wa
ndege.Ni tukio lililochukua
muda mfupi sana.
 
SEASON 6: SEHEMU YA 9
Askari wawili waliokuwa
doria uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar
es salaam walisikia kishindo
kama mtu akigonga gari toka
katika mojawapo ya magari
yaliyokuwa yameegeshwa eneo
la maegesho ya watu
maalum.Kwa tahadhari kubwa
wakasogelea magari yale ili
kujua kishindo kile kilitokana
na nini. Baada ya kuchungulia
katika gari ambalo kishindo kile
cha kugonga kilikuwa kinatoka
waliona kuna watu wawili
wamefungwa miguu na mikono
na kufungwa vitambaa
usoni.Haraka haraka wakatoa
taarifa na askari zaidi
wakaongezeka,wakalizingira gari
lile ambalo milango yake yote
ilikuwa imefungwa.Wakavunja
dirisha na kuufungua
mlango.Wakawatoa watu wale
wawili na kuwapatia huduma ya
kwanza .Mmoja hali yake
haikuwa nzuri wakamuwahisha
hospitali haraka .Mwingine
ambaye aliweza kuzungumza
akawaeleza
kilichotokea.Akawasimulia
mkasa mzima namna
walivyofanyiwa na watu
aliowataja kama walinzi wa
Monica.Taarifa ya tukio lile
ikamfikia rais ikulu na kumstua
sana.Akahitaji kuzungumza na
Yule mlinzi ambaye yeye na
mwenzake walipewa kazi ya
kuhakikisha Monica anafika
Zanzibar na kurudi salama
Rais alipewa taarifa ya
mkasa mzima ulivyotokea
akastuka sana bna kulazimika
kumpigia simu Silva.
“ Silva mpaka sasa kuna
ripoti yoyote kuhusiana na
Yasmin?akauliza rais
“ bado hakuna taarifa
yoyote mzee.Tunashirikiana na
jeshi la polisi lakini mpaka sasa
bado hakuna fununu za mahala
aliko Yasmin.Ninaanza kuwa na
wasi wasi yawezekana tayari
ametoroka”
“ Hapana hawezi
kutoroka.Lazima yuko hapo
hapo Zanzibar.Endeleeni na
msako lazima mpaka asubuhi
muhakikishe amepatikana.Njia
zote za kuingilia na kutokea
Zanzibar zimefungwa kwa hiyo
endeleeni kumtafuta” akasema
“ Sawa mzee.” Akajibu Silva
“ Vipi kuhusu Yule binti
niliyekwambia anakuja
Zanzibar,umemuwekea ulinzi wa
kutosha?
“ Ndiyo mzee niliweka vijana
wawili kwa ajili ya kumlinda
lakini kuna kitu cha
kushangaza kimetokea.”
“ Kumetokea nini? Akauliza
rais kwa wasiwasi
“ Muda mfupi uliopita
nimepewa taarifa na maafisa wa
uwanja wa ndege kwamba
waliingiwa na wasi wasi baada
ya kuliona gari walilokuwa
wanalitumia vijana wangu
kukaa pale uwanjani kwa muda
mrefu ikawalazimu kulifuatilia
kujua kwa nini hawaondoki na
walipochungulia ndani
wakawakuta vijana wangu
hawana fahamu.Hatujui nini
kimewapata hivi sasa
wamekimbizwa hospitali kwa
ajili ya huduma ya kwanza .”
“ Monica tayari ameondoka
hapo Zanzibar? Akauliza rais
“ Ndiyo.Tayari ndege
aliyokuja nayo imekwisha
ondoka kurejea Dar es salaam”
akasema Silva na rais akavuta
pumzi ndefu
“ Ahsante Silva kwa taarifa
hizo naomba ukipata taarifa
zozote kuhusiana na msako wa
Yasmin unitaarifu mara moja”
akasema na kukata simu
“ Haya ni mambo gani
yanatokea? Mbona sielewi nini
kinaendelea? Watu niliowapa
maelekezo kwa ajili ya
kumpeleka Monica Zanzibar
wamekutwa garini wamefungwa
na kwa mujibu wa maelezo yao
ni kwamba wamefungwa na
walinzi wa Monica.Kama
haitoshi vijana wa usalama wa
taifa waliowekwa na Silva kwa
ajili ya kumsaidia Monica kule
Zanzibar wamekutwa pia garini
hawana fahamu.Nini maana ya
matukio haya yote mawili?Kwa
nini walinzi hawa wote
wapotezwe fahamu? Kuna nini
ambacho Monica na walinzi
wake wanakificha? Akajiuliza
Rais na kumuita Jenerali
Lameck Msuba akampa taarifa
zile alizopata.
“ Mheshimwia rais hapa
lazima kuna kitu ambacho hawa
jamaa wanakificha .Hata kama
Monica ana walinzi wake
hakukuwa na sababu yoyote ya
kuwapoteza fahamu walinzi wale
uliowatoa kwa nia njema ya
kumsindikiza na kuhakikisha
anakuwa salama .Lazima kuna
kitu ambacho endapo
wangeongozana na walinzi wale
basi kingegundulika na ndiyo
maana wakawapoteza fahamu”
akasema Lameck
“ Monica ni msichana
ambaye hata ukimtazama
haonekani kama ana mambo ya
kuficha ficha imetokeaje leo
akafanya hivi? Akauliza rais
“ Umeniambia kwamba
wako angani wanarejea Dar es
salaam? Akauliza Lameck
“ Ndiyo wako angani
wanarejea.” Akasema rais
“ Basi inabidi tuwazuie
uwanja wa ndege ili tujue ni kitu
gani hicho wanachokificha.
Tayari kuna vikosi viko pale
uwanjani vinapiga doria kwa
hiyo tuviweke katika tahadhari
na pindi tu wakitua basi
wakamatwe tuwahoji tujue nini
hasa wanaficha?Mheshimiwa
rais vijana wale uliowatuma
wanatoka usalama wa taifa na
ni vijana wenye mafunzo ya hali
ya juu,Lazima hao walinzi wa
Monica wawe ni watu hatari.Hili
ni suala la kulishughulikia kwa
haraka sana” akasema lameck
“ Wazo lako ni zuri sana
Lameck lakini sitaki ndaniya
ndege hiyo yupo Monca ambaye
sitaki aguswe au apewe
kashkashi zozote.Sitaki
kumuudhi” akasema
rais.Lameck akashangazwa na
kauli ile ya rais akamtazama
kwa muda na kusema
“ Mheshimiwa rais huyu
Monica anaonekana ni mtu
muhimu sana kwako mpaka
ukadiriki kumpatia ndege
maalum na walinzi wa
kumpeleka Zanzibar na hata
wazo la kumkatamata yeye na
wenzake linakupa mashaka
sana.Ana uhusiano wowote na
wewe? Akauliza Lameck.Rais
akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Lameck kwa kuwa wewe ni
mshirika wangu nitakueleza
lakini naomba hii iwe ni siri
yako.Monica ni mwanangu”
“ Mwanao? !! Lameck
akashangaa
“ Ndiyo ni
mwanangu.Nilizaa na
mwanamke Fulani enzi za ujana
wangu” akasema rais
“ Nimeelewa .Basi Monica
hataguswa lakini hao walinzi
wake lazima tuwahoji kwa nini
wakawapoteza fahamu walinzi
uliotuma wamlinde Monica?
Kuna jambo linafichwa hapa
mheshimiwa rais na lazima
tulifahamu.Hili si suala la
kupuuzia hata kidogo
mheshimiwa rais.Kitu cha
kujiuliza wamekwenda kufanya
nini Zanzibar usiku huu?
Akauliza Lameck.Rais
aliinamisha kichwa akawaza
halafu akasema
“ Lameck hakuna
kuwazuia.Let them go”
“ Sawa mheshimiwa rais”
akasema Lameck halafu
wakaingia ndani kuendelea na
kikao.
Wakati kikao kikiendelea
Jenerali Lameck msuba aliinuka
akaelekea maliwatoni na akiwa
kule akatoa simu na kutoa
maelekezo kwa kamanda wa
vikosi vilivyokuwa vinalinda
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kwamba Monica na
wenzake mara tu watakapotua
wakamatwe wahojiwe .Aliweka
msisitizo kwamba wanatakwia
wachukue tahadhari kubwa
wakati wa kuwakamata na
kuwahoji kwani wanaonekana ni
watu hatari.Baada ya agizo lile
la mkuu wa majeshi,vikosi
vilivyokuwa uwanjani
vikajipanga tayari kuwakabili
akina Austin mara tu
watakapotua kwani walitaarifiwa
ndege ilikaribia sana kufika Dar
es salaam.

SEASON 6: SEHEMU YA 10
Ndege waliyopanda Austin
na wenzake ilianza kutua katika
uwaja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere ikitokea
Zanzibar.Kabla haijagusa ardhi
Austin akagundua kitu ambacho
hakikuwa cha
kawaida.Kulikuwa na idadi
kubwa ya askari na wanajeshi
na mara tu ndege ilipogusa
ardhi gari mbili zilizojaza
wanajeshi zikaanza kuwafuata.
“ Guys something is wrong
here !! akasema na kuchomoa
bastora yake akawafuata
marubani na kuwalizimisha
warudishe ndege
angani.Walionekana kupingana
naye akalazimika kumpiga
rubani mmoja risasi ya bega
.Mwenzake akaogopa na
kuipaisha ndege ikarejea tena
angani.
“ Tunakwenda wapi?
Akauliza Yule rubani.
“ Tutazunguka angani hadi
tutakapopata uwanja wa karibu
wa kutua.Ni uwanja upi
tunaweza kutua kwa haraka
usiku huu”
“ Sina mafuta ya kutosha
katika ndege na endapo
tukiendelea kuzunguka hewani
ndege itaishiwa mafuta na
itaanguka.Sote tutakufa.”
“ Kama unajua hauna
mafuta ya kutosha then do
something!!akafoka Austin na
mara Yasmin akatokea
“ Austin kuna nini
kinaendelea ? Mbona tumerejea
tena angani? Akauliza
“ Nimegundua kuna idadi
kubwa ya wanajeshi pale
uwanjani na kama tungetua
tungekamatwa.Tayari taarifa
zetu zimekwisha wafikia”
“ Kwa hiyo tunakwenda
wapi? Akauliza Yasmin
“ Bado sijapata jibu wapi
tuelekee na rubani anadai
kwamba ndege haina mafuta ya
kutosha.Hatuwezi kwenda
umbali mrefu.Nina wasiwasi
kama wametukosa kule
uwanjani watatuma ndege ya
jeshi itufuatilie angani na kujua
tunakoelekea” akasema Austin
na mara akastuka.
“Hii ni aina gani ya ndege?
Akauliza Austin
“ Hii ni Dassault Falcon7x”
akasema Rubani na Austin
akanyamaza kidogo kwa
sekunde kadhaa na kisha
akasema
“ Kwa ndege kama hii ya
Falcon 7x inahitaji barabara ya
mita 630 kuweza kutua.Tayari
nimepata wazo.Tunaweza kutua
katika daraja la Nyerere.Usiku
huu hakuna magari mengi.”
Akasema Austin na
kumuelekeza rubani aelekeze
ndege katika daraja la Nyerere
ambalo liliweza kuonekana kwa
urahisi kutokea angani
kutokana na kuwaka taa
nyingi.Austin akawafuata akina
Job
“ Guys hatuna ujanja
tena.Ndege haina mafuta ya
kutosha kutuwezesha kwenda
mbali kwa hiyo nimeona ni
vyema endapo tutatua katika
daraja la Nyerere.Usiku huu
hakuna magari mengi kwa hiyo
nawaomba mjiandae kwa lolote
litakalotokea” akasema Austin
“ Austin are you sure we’ll
land safely? Akauliza Amarachi
kwa wasiwasi mkubwa
“ I don’t know but we must
pray ! Soon as the plane lands
we’ll get out quicly and
disappear.” Akasema Austin na
kumfuata Monica
“ Monica I’m sorry
.Utanisamehe sana kwa
kukuingiza katika hatari kama
hii .Nakuomba ondoa hofu na
tutatua salama.” Akasema
Austin na kurejea tena kwa
rubani akashangaa kumkuta
Yasmin akiwa amekaa katika
kiti cha rubani msaidizi
akimsaidia rubani.Rubani
aliyepigwa risasi na Austin
alikuwa amelazwa chini akivuja
damu.Austin na Yasmin wote
walimsaidia rubani na kisha
ndege ikakaa tayari kwa kutua
katika daraja la Nyerere.
“ Ee Mungu tusaidie tutue
salama” akaomba Austin wakati
ndege ikishuka chini.Kama
alivyokuwa ametabiri,hakukuwa
na magari usiku huu katika
daraja hili.Ndege ikagusa sakafu
ya daraja na kuyumba lakini
kwa uhodari wa rubani ikakaa
sawa na huku ikipunguza
mwendo taratibu na mwisho
ikasimama.Kila mmoja akavuta
pumzi baada ya ndege
kusimama.Austin akamshukuru
rubani na kumtaka afanye
haraka kumpeleka mwenzake
hospitali.Wote wakashuka
haraka ndegeni kwani watu
tayari walikwisha anza kukimbia
kuifuata ndege ile.Haraka
haraka wakaingia katika njia ya
watembea kwa miguu.Taarifa za
ndege kutua katika daraja la
Nyerere zilisambaa kwa kasi
kubwa na watu waliokuwa
maeneoya karibu na daraja lile
walikuwa wanakimbia kuelekea
kule ndege ilikotua. Vyombo vya
usalama havikubaki nyuma
,kwa haraka vikafika katikaeneo
lile ili kuhakikisha kuna kuwa
na usalama wa kutosha..
Watu waliokuwa wakielekea
kule ilikotua ndege waliwasaidia
sana akina Austin kupotea na
hakuna aliyeweza
kuwatambua.Walitembea hadi
walipokuta kituo cha taksi
wakakodisha na kuwapeleka
hadi walipoacha gari lao
wakaingia na kuondoka.
“ Take me home.I don’t want
to be near you anymore!!
Akasema Monica kwa
hasira.Macho yake yalikuwa
mekundu
“ Monica there is something
I need to tell you” akasema
Austin
“ I don’t want to hear
anything from you.Just take me
home” akasema Monica huku
machozi yakimtoka.Mwili
ulikuwa unamtetemeka.Mambo
aliyoyaona yalimuogopesha mno
“ Monica I promised to tell
you something very important
about you.Please Monica it’s
important” akasema Austin
“ I’ve said No!..I don’t want
to see you again,I don’t want to
hear anything from you.I don’t
want you near me ever
again.Just take me home!!!!
Akasema Monica kwa ukali
“ Austin,le’t just take here
home.” Akasema Amarachi
“ Fine” akasema Austin na
kumtaka Amarachi aliyekuwa
akiendesha gari waelekee
nyumbani kwa Monica.Safari
ilikuwa ya kimya kimya hadi
walipofika nyumbani kwa
Monica akashuka.Austin naye
akashuka
“ Monica thank you so
much.Bila wewe tusingef…….”
“ Save your breath Austin!!!
Akasema Monica kwa sauti kali
“ Austin kumbuka maneno
niliyokwambia.I don’t want to
see you ever again.You don’t
deserve to be friend with me.!!!!
akasema Monica na kuelekea
ndani kwake kwa hasira.Astin
na wenzake wakaondoka
 
Back
Top Bottom