QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 5

Silvanus Kiwembe mkuu wa idara
ya usalama wa taifa aliwasili katika
nyumba moja iliyozungushiwa ukuta
mkubwa uliopakwa rangi
nyeupe.Alipiga honi na kijana mmoja
akatoka,akafungua geti.Yule kijana
akamuongoza Silva wakaenda katika
mojawapo ya vyumba pale na Yule
kijana akabonyeza kengele na mlango
ukafunguka.Silva akatazamana uso kwa
uso na Agatha mkasa.
“ Karibu ndani Silva” akasema
Agatha na Silva akaingia
ndani.Kilikuwa ni chumba kikubwa
chenye nakshi za kupendeza na
kilichosheheni kila kitu.Silva
akakaribishwa sofani
“Agatha vipi hali yako? Akauliza
Silva
“Ninaendelea vizuri kama
unavyoniona.Vipi wewe unaendeleaje?
Akauliza Agatha
“Hata mimi ninaendelea vyema
kukabiliana na majukumu”
“Good to hear that.Kuna chochote
mmepata mpaka sasa kutoka kwa
Irene?Agatha akauliza
“Taarifa niliyonayo wakati
ninakuja huku ni kwamba Irene
amepiga simu na amepewa maelekezo
ya kufuata.Ninasubiri jibu kutoka kwa
vijana kama Irene atatekeleza
maelekezo aliyopewa ama vipi”
akasema Silva
“ Endapo atashindwa kutekeleza
maelekezo aliyopewa hakuna hajaya
kuendelea kuwashikilia wazazi wake
kill them all” akasema Agatha
“Tukiwaua wazazi wake wote
wawili hii inaweza ikamuogopesha
sana Irene na anaweza akajificha
tusimuone tena na taarifa hiyo
aliyonayo tutaikosa” akasema Silva
“Hapana Silva wazazi wake
wakiuawa atachanganyikiwa na
atajitokeza tu hiyo itatupa urahisi sisi
wa kumkamata.”
“Agatha nakushauri tusifanye
hivyo.Wazazi wa Irene wakiuawa
tutampoteza kabisa Irene na
hatutapata taarifa aliyonayo.Tafadhali
nipe nafasi nilishughulikie suala
hili.Mimi na vijana wangu tumejipanga
vizuri sana na ninakuhakikishia
kwamba lazima tumpate Irene na atupe
hiyo taarifa aliyonayo”
“Huyu Irene kama angekuwa yuko
tayari kutupatia hiyo taarifa
angekwisha fanya hivyo lakini mpaka
mida hii hajatokea pamoja na
kuwashikilia wazazi wake .Sina hakika
kama yuko tayari kutupa taarifa
hiyo”akasema Agatha
“Agatha usiwe na wasi wasi.Irene
atafanya kama tunavyotaka na
atatueleza ni wapi ameipata taarifa
hiyo?akasema Silva
“Tuachane na hilo .Kuna jambo
lingine ulisema utanieleza
linalomuhusu Ernest.Nadhani huu ni
wakati muafaka” akasema Agatha
“Ndiyo kuna jambo ambalo
ninataka kukueleza” akasema Silva na
kumsimulia Agatha kila kitu kuhusiana
na Yasmin
“Kwa nini alimuachia huru?
Where is she now? Akauliza Agatha
“Sababu za kumuachia huru
Yasmin mpaka sasa sizifahamu lakini
hivi tuongeavyo Yasmin amekwisha
ondoka nchini anaelekea Congo”
akasema Silva
“Silva nataka kufahamu kitu
kimoja kwa nini Ernest alimuachia
huyo mwanamke halafu baadae
akaanza tena kumsaka tena kwa nguvu
kubwa?
“Swali kama hilo hata mimi
nimewahi kumuuliza rais na hakunipa
jibu lakini inavyoonekana huyo
mwanamke ni mtu muhimu sana
kwake.Nakumbuka aliponituma
kwenda Zanzibar alinitaka nikifanikiwa
kumkamata Yasmin basi nihakikishe
ninaipata bahasha ya khaki ambayo
anayo Yasmin na nihakikishe hakuna
yeyote atakayeifungua zaidi
yake.Inaonekana kuna kitu muhimu
katika hiyo bahasha aliyonayo Yasmin”
“Aliwezaje kutoroka Zanzibar
mlikokuwa mmedhibiti ulinzi na kuja
Dar es salaam? Akauliza Agatha
“Tumegundua Yasmin hayuko
peke yake.Ana watu wanaomsaidia na
ndio waliomsaidia akaweza kutorokla
Zanzibar na kuja Dar es salaam.Kuna
mmoja anaitwa Austin.Huyu amewahi
kufanya kazi katika idara ya usalama
wa taifa .Ninamfahamu huyu jamaa ni
mtu hatari sana.Tunafahamu kwamba
alifariki nchni Somalia katika
mapambano na Alshabaab lakini
nilistuka baada ya kuambiwa kwamba
yuko hai na yuko hapa Dar es salaam
tena anashirikiana na
Yasmin.Nakuhakikishia Agatha kwa
uwezo alionao huyu jamaa itakuwa
vigumu sana kwetu kuweza kumkamta
Yasmin.Ukiacha Austin kuna mwingine
ambaye anashirikiana na Austin.Huyu
anaitwa Monica Benedict mtoto wa
Benedict Mwamsole.”
“ Ninamfahamu sana Benedict
mwamsole na mkewe Janet ni marafiki
zetu wa miaka mingi.Mtoto wao Monica
anashirikiana na Yasmin? Anafahamu
kama Yasmin ni mfuasi wa IS? Agatha
akauliza
“Hakuna anayefahamu kwa nini
Monica anashirikiana na Yasmin”
akasema Silva na kumtazama Agatha
“ You want to tell me something?
Akauliza Agatha
“Agatha kuna jambo nataka
nikufahamishe ambalo sina hakika
kama unalifahamu”
“ Tafadhali niambie” akasema
Agatha
“ Ni kuhusu huyo Monica.Ni mtoto
wa Ernest” akasema Silva.Agatha
akainuka na kusimama akamtazama
Silva kwa hasira
“ Silva mimi na wewe ni marafiki
wa muda mrefu na hatuna
utani.Tafadhali usilete utani hasa
katika wakati kama huu.!! Akasema
Agatha kwa ukali
“Huu si utani Agatha.Hili ni jambo
la kweli kabisa.Monica Benedict ni
mtoto wa rais Ernest” Akasema
Silva.Agatha akaendelea kusimama
akimtazama Silva kwa macho makali
huku akihema mfululizo
“Habari hizi umezipata wapi?
Agatha akauliza
“From president himself”
“ Ernest told you this? Akauliza
“ Ndiyo.Yeye mwenyewe kwa
mdomo wake amenieleza suala hili”
“Do you believe him? Akauliza
Agatha
“ Kwa namna nilivyomuona wakati
ananieleza suala hili.Its true”
“ Oh my God !! kwa nini
hukunitaarifu suala hili toka mapema
Silva?
“Hata mmi mwenyewe
nimelifahamu leo asubuhi aliponiita
ikulu”akasema Silva.Agatha
akaonekana kuchanganyikiwa
“ Inawezekanaje Monica akawa ni
mtoto wa Ernest? Janet alikuwa na
mahusiano na Ernest? Akajiuliza
“ Kama kweli Monica ni mtoto wa
Ernest basi lazima yeye na Agatha
walikuwa na mahusian😵h my gosh
how could I be so fool? Akawaza Agatha
na kuuma meno kwa hasira
“Nilimuheshimu sana Janet kama
rafiki yangu wa kweli na sikutegemea
kabisa kama anaweza akanifanyia kitu
kama hiki kuwa na mahusiano na
Ernest.Kumbe kwa miaka hii yote
tulikuwa tukiishi katika uongo
mkubwa.Ernest ni mume wangu na
sikuwa ni kimuwazia kumfanya kitu
chochote kibaya lakini kwa hiki
nilichokisikia toka kwa Silva lazima
nimfanyie kitu kibaya yeye na huyo
kahaba mwenzake Janet.Kwa nini Janet
akanifanyia hivi? Kwa nini akamuacha
mume wake na kuja kuzaa na mume
wangu? Nitawaonyesha kazi.I’ll destroy
them !! hakuna atakayebaki salama.”
Akawaza Agatha na kumgeukia Silva
“ Silva habari hii uliyonipa ni
habari iliyonistua sana.Naomba
unisthibitishie kama kweli Monica ni
mtoto wa Ernest” akasema Agatha
“ Agatha nina uhakika mkubwa
kwamba Monica ni mtoto wa Ernest
kwa sababu ilimlazimu yeye
mwenyewe anieleze kutokana na kile
kilichokuwa kimetokea jana usiku”
Akasema Silva
“Silva nakupa kazi nataka uende
mbali zaidi ulichunguze suala hili na
upate uhakika kama kweli Monica ni
mtoto wa Ernest.Kama ni kweli nataka
nije na mpango mkubwa wa kulipa
kisasi kwa wote.Kwanza Ernest
mwenyewe na pili kwa Janet .Silva ..”
Agatha akataka kusema kitu lakini
akanyamaza baada ya simu ya Silva
kuita
“ Mkuu Irene tayari amekwisha
ingia katika gari letu kama
alivyoelekezwa.Tunaelekea eneo la
tukio” akasema mtu aliyempigia simu
Silva
“That’s good.Hakikisheni kwamba
hakuna yeyote anayemfuata na ulinzi
unaimarishwa” akasema Silva
“ Sawa mkuu.Hilo limezingatiwa
sana “
“ Good.Ninakuja huko sasa hivi”
akasema Silva na kukata simu
“ Mambo yanaenda vizuri.Irene
tayari amejileta na hivi sasa vijana
wanampeleka kwenye mahojiano.Mimi
nitaelekea huko mara moja na nikitoka
huko nitakuja hapa”
“Silva tunakwenda wote”
“ Hapana Agatha.Wewe utabaki
hapa.Ni hatari kubwa huko
nje.Unatafutwa sana.” Akasema Silva
“Silva tunakwenda wote.Nataka
Irene anieleze kwa mdomo wake ni
wapi alipata taarifa za hoteli
kulipuliwa.Wait for me outside.I need
to change” akasema Agatha na Silva
akatoka nje
“Nimepatwa na mstuko mkubwa
kwa hiki alichonieleza Silva.Ernest ana
mtoto na amenificha miaka hii yote?
Niliwapoteza watoto wangu kwa ajili ya
mafanikio yetu lakini kumbe
mwenzangu hana wasiwasi kwa sababu
tayari alikuwa na mtoto kwa siri.Ernest
must pay for this.Kitu cha msingi hapa
ni kummaliza huyo mtoto ili sote
tukose.I don’t want to see Ernest
happy.I want him to suffer “ akawaza
Agatha wakati akijiandaa
Baada ya dakika saba Agatha
akatoka chumbani akiwa tayari
amejiandaa .Alikuwa amevaa gauni refu
jeusi na kuofia kubwa nyeusi
iliyoufunika uso wake kiasi cha
kutoweza kutambulika kwa
haraka.Wakaelekea garini na kuanza
safari
“Hapa unapoishi unaamini ni
sehemu salama kwako? Silva akauliza
wakiwa garini
“Ni sehemu salama .Ernest hajui
kama ninaishi hapa.Hakuna
anayefahamu na wala aliyeniona.Siku
ile niliondoka bila ya walinzi wangu
kufahamu chochote.Inaniuma sana kwa
watu wangu wote kuteketea katika
shambulio lile.Nitaendelea kuwalaani
sana hawa Alshabaab kwa ukatili
walioufanya” akasema Agatha na
kuzama mawazoni na mara akageuza
shingo na kumtazama Silva
“ Silva kuna kitu nimekuwa
nakiwaza toka ulipotokea ule
mlipuko.Tumewapoteza wenzetu wengi
katika hoteli ile na hata kule
bungeni.Naweza kusema kwamba
tumebaki wawili tu.Wenzetu wote
wameuawa.Mle ndani ya jengo
kulikuwa na Alberto’s karibu wote
ambao tulikutana pale kwa ajili ya
kuonana na rais”
“Nakumbuka ulinitaarifu
kuhusiana na kikao hicho lakini mimi
sikuweza kuhudhuria kutokana na
kubanwa na majukumu mengine
niliyopewa na rais” akasema Silva
“katika kikao hicho” Agatha
akaendelea
“ Karibu Alberto’s wote
tuilihudhuria kwani Ernest alitutaka
tuwepo wote na mimi peke yangu ndiye
niliyenusurika baada ya kustuliwa na
Irene.Ninachojiuliza ni kwamba kwa
nini mashambulio haya yametokea
katika mahala walipo Alberto pekee?
Pale ndaniya hoteli kulikuwa na kikao
cha Alberto’s na kule bungeni kuna
idadi kubwa ya wabunge wafuasi wa
Alberto’s na mashambulizi haya
yametokea katika sehemu hizo
pekee.Hudhani kama mashambulizi
haya yamewalenga moja kwa moja
Alberto’s? akauliza Agatha
“Hoja yako ina msingi sana Agatha
na inatakiwa ifanyiwe kazi kwa kina
lakini kingine ni kwamba waliotekeleza
mashambulizi hayo ni Alshabaab.Hawa
wanahusiana nini na Alberto’s? Hakuna
mahusiano yoyote kati yetu na hawa
jamaa” akasema Silva
“ Hata mimi hapo ndipo
panaponiumiza kichwa changu
sana.Kuna ulazima wa kulifanyia
uchunguzi mkubwa suala hili ili
kufahamu nini hasa sababu ya
kufanyika kwa mashambulio yale
ambayo yamechukua uhai wa Alberto’s
karibu wote.’ Akasema Agatha
“ Vipi kuhusu makao makuu ya
Alberto’s umewapa taarifa za
kilichotokea? Baba Alberto anasemaje?
“Tayari nimewataarifu lakini
hakuna hatua zozote
walizochukua.Nilichoambiwa ni kutulia
kwa sasa hadi hapo hali ya mambo
itakapokuwa imekaa sawa ndipo
watatoa maelekezo nini kifanyike”
Akasema Agatha
“Inaonyesha hata wao pia
wamekata tamaa” akasema Silva
“Hapana hawawezi kukata tamaa
hata kidogo.Alberto’s hawashindwi na
jambo lolote.Ernest na washirika wake
wasifikiri kwamba wameshinda vita hii
bado kabisa .Ngoja mambo yatulie na
ndipo utakapoijua nguvu ya
Alberto’s.Mambo yetu sisi huwa ni
kimya k imya” akasema Agatha
“Hata hivyo watu wengi
wamepoteza maisha na mtandao wetu
wote umevurugika mno.Itachukua
muda mrefu kutengeneza mtandao
mwingine kama ule.Kila Nyanja
muhimu kulikuwa na Alberto’s”
akasema Silva
“ kama si Yule hayawani Ernest
tayari tungekuwa tumepiga hatua
kubwa sana hivi sasa.Tayari muswada
ungekuwa bungeni hivi sasa.Lakini
ametibua kila kitu .Nikimfikiria sipati
picha ni adhabu gani anastahili Yule
mjinga.lakini kwa vyovyote
itakavyokuwa lazima tuweke mizizi
.Tumeweza katika nchi nyingi na
nyingine ngumu kabisa kuingilika na
hatuwezi kushindwa na nchi kama
Tanzania.Mapambano
yanaendelea.Pamoja na makao makuu
kusema kwamba tusifanye jambo lolote
na tusibiri maelekzo yao lakini
hatuwezi kukaa hivi hivi .lazima tuje na
mpango wa kulipiza kisasi kwa kitu
alichotufanyia rais.Anguko hili kubwa
kwa Alberto’s ni kwa sababu
yake.Kama asingetufanyia usaliti
mkubwa haya yasingetokea.Nataka
tuunganishe nguvu na tuje na mpango
kabambe wa kuweza kumuondoa
Ernest madarakani.Tunatakiwa kuanza
tena kutengeneza mtandao.Baada ya
suala hili la Irene kumalizika tutakaa
na kubuni mpango mkubwa wa
kupambana na Ernest.Safari hii
hataponyoka !! akasema Agatha kwa
hasira.
 
QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 6
Kama Irene alivyokuwa
ameelekezwa ,aliyakuta magari mawili
yameegeshwa karibu na ile
kasino.Akasimamisha gari na kuvuta
pumzi ndefu.
“ Job can you hear me? Akauliza
Irene
“ Yes I rene.We can hear you.”
“ Good.Nimefika hapa na magari
niliyoelekezwa nimeyaona.Ninaelekea
huko sasa.Kabla sijashuka garini kuna
mabadiliko yoyote?mambo yote
yanakwenda sawa? Akauliza Irene
“Hakuna mabadiliko Irene.Kila
kitu kinakwenda sawa” Akasema Job
“Sawa.Mimi nashuka naingia
katika gari nililoelekezwa
kuingia.Ninawategemea sana ninyi”
akasema Irene
“ Usiwe na wasi wasi Irene.Sisi
tuko nyuma yako na tutakulinda “
akasema Job.
Irene akayatazama tena magari
yale.
“ Ee Mungu najiweka katika
mikono yako unilinde na hatari kubwa
inayonikabili.Wawezeshe hawa
wenzangu wanaonifuatilia wafanikiwe
kunikomboa mimi na wazazi wangu”
Irene akafanya maombi mafupi kisha
akashuka garini akatembea haraka na
kwa tahadhari kubwa akaingia katika
gari jekundu kama alivyokuwa
amepewa maelekezo.Mle garini
akawakuta watu watatu.Dakika tano
toka alipoingia garini mlango
ukafunguliwa akaingia tena jamaa
mwingine na Irene akawekwa
katikati.Yule jamaa aliyeingia mwisho
akatoa amri waondoke.
“Tunaelekea wapi? Irene akauliza
“Shut up !! akasema jamaa mmoja
“ Ninahitaji kufahamu mahala
tunakoelekea.Wazazi wangu wako
wapi? Akauliza tena
“ Mrembo usiruhusu tukatumia
nguvu kukufunga huo mdomo
wako.Kaa kimya na ufuate kila kile
utakachoelekezwa” akasema jamaa
mmoja aliyekua pembeni yake.
“ Irene tafadhali endelea kuwa
mtulivu na ufuate kile
watakachokuelekeza.Sisi tuko nyuma
tunakufuatilia” Daniel akamwambia
Irene kupitia kile kifaa kidogo
alichokiweka sikioni.
Baada ya mwendo wa dakika
ishirini hivi jamaa aliyekuwa amekaa
pembeni ya kiti cha dereva akatoa amri
kwamba Irene afungwe kitambaa
usoni.Zoezi hilo likafanyika kwa haraka
sana na safari ikaendelea.Irene hakujua
tena ni wapi wanaelekea.Dakika kama
kumi baadae gari ikasimama milango
ikafunguliwa akashushwa akafungwa
pingu mikononi na kupelekwa sehemu
yenye giza nene.Akasikia milango
inafungwa.
“Hawa jamaa wamenileta wapi?
Akawaza Irene na mara akasikia sauti
ya Job kupitia kile kifaa cha sikioni
“Irene tayari wamekuondoa
kitambaa usoni? Unaweza kuona kitu
chochote karibu yako?
‘ Hapana siwezi kuona chochote na
wala sifahamu niko wapi.Bado
nimemfungwa kitambaa usoni .Ninyi
mko wapi?akauliza Irene kwa sauti
ndogo
“ Irene tunakusikia kwa taabu
sana.Hata hivyo tunaendelea
kukufuatilia.Hatuko mbali sana na
mahala ulipo” Akasema Job
“Tablet yetu inatuonyesha
kwamba si umbali mrefu toka hapa
ndipo alipo Irene.Tutaacha gari hapa na
kutembea kwa miguu.” Akasema Job
“Ninalifahamu eneo hili .Mita
chache kutoka hapa kuna bustani ya
wanyama.Kuna wanyama wanafugwa
hapa na wengine ni wakali.Tunapaswa
kuwa makini sana.” Akasema Daniel
“ Hakuna cha kutuogopesha.Hata
aje Simba tutapambana naye” akasema
Job na wakashuka garini wakaanza
kutembea kwa tahadhari na taratibu
mwangaza wa taa zilizotoka katika
nyumba za jirani na eneo lile ukaanza
kupungua wakakutana na kiza.Lilikuwa
ni eneo lenye miti na vichaka vingi.
“ Job ,wait for me here I want to
make a phone call.It’s important”
akasema Daniel
“Fanya haraka” akasema Job.
Daniel akasogea mbali na pale
alipokuwa amesimama Job aliyekuwa
makini akiangaza huku na huku.Eneo
lile hakukuwa na mwangaza mkali na
kulikuwa na ukimya mkubwa.Ni sauti
za wadudu na vyura zilizokuwa
zinasikika .
Kabla hajapiga simu akakitoa kile
kifaa cha mawasiliano sikioni
akakitupa mbali halafu akazitafuta
namba Fulani katika simu yake
akapiga.
“ Hallow mzee Mukasha” akasema
Daniel na kumstua Job ambaye
alimsikia kupitia kifaa kifaa cha
mawasiliano alichokivaa
sikioni.Alistuka mno aliposikia Daniel
akilitamka jina la Mukasha.
“ What ?!! Daniel anamfahamu
Mukasha?Akajiuliza.hakuweza kusikia
upande wa pili wa simu bali aliweza
kusikia kile alichokizungumza Daniel.
“ Mzee nimekupigia kukutaarifu
kuna jambo kubwa nimelipata.Niko
katika operesheni Fulani na
nitakapoimaliza nitakuja kuonana
naewqe usiku huu nikueleze .Ni jambo
zito ambalo unaweza ukalitumia na
likakufaa lakini andaa pesa ya
kutosha.” Akasema Daniel
Job alihisi mwili unaingiwa na
baridi ya ghafla kwa maneno yale
aliyoyazungumza Daniel
“ Siamini hiki nilichokisikia.Daniel
ana mawasiliano na Mukasha? Mbona
nilimuuliza akadai kwamba
hamfahamu? Ama kweli ninaamini
Mungu yuko nasi katika operesheni hii
kwani amemmleta Daniel kwetu
makusudi kabisa ili atuonyeshe namna
watu walivyo wasaliti wa nchi
hii.Unaweza ukadhani mambo haya ni
filamu lakini ni kitu cha kweli kabisa
kinatokea” akawaza Job.Daniel
akarejea
“Tunaweza kuendelea na safari”
akasema Daniel na mara katika kile
kifaa alichokjuwa nacho sikioni Job
akasikia Irene akiamriwa asimame .
“ Wanamuhamisha” akasema Job
huku akitazama kile kifaa walichokuwa
wanakitumia kutazama mwenendo wa
Irene
“ Tunatakiwa tufanye haraka
kabla hawajaanza kumtesa.” Akasema
Daniel.
Walipita katika vichaka na
hatimaye wakaruka uzio na kuingia
ndani ya bustani ya wanyama.Kulikuwa
na vibanda vya chuma walimowekwa
wanyama mbali mbali.Huku
wakiendelea kufuata maelekezo ya
kutoka katika kile kifaa walitembea
kwa tahadhari ili wasionekane.
“Kifaa chetu kinatuonyesha
kwamba Ireen yuko maeneo haya”
akasema Job na kutoa kiona mbali
akaanza kuangaza katika eneo lile na
mara ukatokea mwangaza wa gari
wakajificha katika kichaka cha
maua.Gari lile likapita kwa kasi
likifuata bara bara yenye majani mengi.
“Gari lile linakwenda wapi?
Akauliza Job
“ We need to follow that
car.Hakuna shughuli zozote
zinazoendelea hapa za kutazama
wanyama usiku huu.Kuna kitu
wanakifuata waliomo katika gari lile”
aksema Job na kutazama tena kile kifaa
ambacho walikuwa wanakitazama
kufuatilia mwenendo wa Irene
“Bado Irene yuko pale pale
hajahamishwa” akasema Job na kisha
wakachunguza usalama na kuanza
kutambaa na mabanda ya wanyama
wakielekea upande ule ilikoenda ile
gari nyeupe aina ya range rover.Eneo
lilikuwa kimya sana na mara wakaliona
jengo lilionekana kama ofisi.Nje ya
jengo lile kulikuwa na magari matatu
yameegeshwa.Wakalitambua gari moja
wapo ni lile lililowapita muda mfupi
uliopita.Baada ya kuchunguza zaidi
wakagundua kuna watu wawili
walikuwa pale nje wakizunguka
zunguka kulinda usalama.
“ Utapita upande ule liliko gari
jekundu mimi nitatokea upande huu
liliko lile gari jeupe.Tuwastukize wale
jamaa ambao wanaonekana kuzama
katika mazungumzo” akasema Job na
Daniel akanyata akavuka barabara na
kutokea upande wa pili huku Job akiwa
tayari ameziweka sawa bastora zake
kukabiliana lolote ambalo lingeweza
kujitokeza.Baada ya Daniel kuvuka
salama barabara Job naye akaanza
kujongea mahala liliko lile gari jeupe.
 
QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 7
Hatimaye dege la kifahari au kasri
linalopaa la rais David Zumo liliwasili
salama katika uwanja wa ndege
mkubwa wa kijeshi wa King David
airbase.Rais David Zumo tayari
alikwisha pata taarifa za kile
kilichotokea nchini Tanzania kupitia
kwa balozi wa Tanzania nchini Congo
DRC.Jitihada za rais Ernest Mkasa
kuwasiliana na David Zumo hazikuzaa
matunda ikamlazimu amtumie balozi
wa Tanzania ambaye alijitahidi na
kufanikiwa kumpata David Zumo
simuni akamueleza kile kilichotokea na
ikamlazimu David kuwasiliana na
Ernesr wakaongea na kisha David
akatoa maelekezo ndege yake ikatue
katika uwanja wa ndege wa kijeshi.
“Tumetua katika uwnaja
mwingine .Huu si uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kinshasa”akasema
Monica alipochungulia nje baada ya
ndege kusimama.
“Ninaona wanajeshi wengi
wakiranda randa hapa na kuna baadhi
ya ndege na helkopta za
jeshi.Inaonekana huu ni uwanja wa
kijeshi.Kwa nini wametuleta hapa?
Akauliza Austin.wakati wakiendelea
kujadiliana kuhusiana na kwa nini
wameenda kutua pale katia uwanja wa
kijeshi mlango wa chumba
walimokuwamo ukafunguliwa na
akaingia Pierre Muyeye akiwa
ameongozana na wanajeshi tisa.Pierre
Muyeye akawatambulisha akina Austin
kwa kikosi k ile cha wanajeshi halafu
akasema
“Tumetua salama katika uwanja
wa ndege wa kijeshi wa King David air
base.Kutoka hapa tutaelekea mahala
kulikoandaliwa kwa ajili yenu.Lakini
kuna maelekezo kidogo kamanda
atayatoa.” Akasema Muyeye na
kumkaribisha kamanda Yule wa kile
kikosi
“Utaratibu wa kuondoka hapa
utakuwa hivi, kuna gari maalum,
aliloandaliwa Monica.Atakuwa peke
yake garini na atatangulia kuondoka
hapa baada ya hapo watafuata wazazi
wa Monica, nao kuna mahala
kumeandaliwa kwa ajili yao.Mwisho
wengine wote mtakaobaki mtaondoka
pamoja kuelekea mahala
kulikoandaliwa kwa ajili yenu.Msihofu
hizi nitaratibu za kawaida kwa ajili ya
wegeni wetu.Tuna wageni wengi sana
wanakuja kwa hiyo lazima tuhakikishe
wageni wetu wanakuwa salama”
akasema Yule kamanda
aliyejitambulisha kuwa anaitwa Henry
nzamibona.
Monica akaagana na akina Austin
kwa ahadi ya kukutana tena baadae
usiku ule au asubuhi kutegemea na
ratiba yake itakavyokuwa.Akaongozana
na wanajeshi watatu wakashuka
ndegeni na kuelekea katika gari la
kifahari sana akafunguliwa mlango
akaingia na kisha gari lile likaondoaka
pale uwanjani huku likisindikizwa na
magari mengine ya kijeshi.Baada ya
Monica kuondoka wazazi wake
wakashuka ndegeni wakaingia katika
gari na kuondoka halafu ikafuata zamu
ya akina Austin.Wote kwa pamoja
wakaingia katika basi dogo la kijeshi
wakaondoka wakisindikizwa na magari
kadhaa ya jeshi yaliyosheheni
wanajeshi wenye silaha.Ulikuwa ni
ulinzi mkali sana
“ Austin” Amarachi akamuita
Austin kwa sauti ya kunong’ona
“ Mbona sielewi elewi
kinachoendelea hapa? Kwanza kwa nini
tumekuja hapa katika uwanja wa ndege
wa kijeshi? Pili kwa nini
wakatugawanya makundi? Tatu kwa
nini tuko katika ulinzi mkali kiasi hiki.
Tazama wanajeshi walivyotuzingira
mbele na nyuma.Unadhani hii ni hali ya
kawaida? Akauliza Amarachi
“ Usihofu Amarachi.Hakuna
chochote kibaya.wamefanya hivi ili
kufuata itifaki .Monica ni mpenzi na
mke mtarajiwa wa David Zumo kwa
hiyo ana haki ya kupewa nafasi ya
kwanza na umuhimu mkubwa kabla ya
sisi wengine.Unaona hata wazazi wake
nao hawajruhusiwa kuambatana
naye.Haya ni mambo ya kawaida wala
yasikupe homa.Mpaka hapa tulipofika
hakuna chochote kibaya
kitakachotutokea.Kama litatokea lolote
Monica yupo atalitatua.Yule ni malkia
mtarajiwa wa Congo na ana nguvu sana
.Akisema lolote litakuwa” akasema
Austin huku
akitabasamu.Hakuonekana kuwa na
wasi wasi wowote
Safari ya dakika ishirini hivi
iliwafikisha katika nyumba moja ya
ghorofa.Wakashuka na kuongozwa
kuelekea ghorofani .Wanawake
wakatengwa katika chumba kimoja na
wanaume ambao ni Austin na Boaz
katika chumba kingine.Kila chumba
kilikuwa na ulinzi mkali wa wanajeshi.
“ Austin kuna nini kinaendelea?
Mbona tumetenganishwa halafu
tunalindwa namna hii? Akauliza Boaz
wakiwa chumbani.Austin hakumjibu
kitu.
“Amarachi alikuwa sahihi.Kuna
kitu hapa kinaendelea si bure” akawaza
Austin na kuchungulia dirishani.
“ Tuko katika kambi ya jeshi.kwa
nini tumeletwa hapa? Naanza kuhisi
inawezekana kabisa tayari taarifa zetu
zimekwisha fika kwa serikali ya
Congo.Kuna uwezekano tayari
tumezuiliwa.Nitavuta subira kuona
kama Monica atafanya chochote na
endapo hakuna chochote
kitakachokuwa kimefanyika baada ya
masaa matatu nitajua mwenyewe nini
cha kufanya.Lazima nihakikishe
ninakamlisha opresheni hii na Yasmin
anaondoka salama na sisi tunaipata
hati ya muungano.” Akawaza Austin
Gari alimopanda Monica liliwasili
katika jumba moja
kubwa.Akafunguliwa mlango akashuka
na kusalimiana na wanadada warembo
waliovalia nadhifu kabisa na kujipanga
mstari.Akaongozwa na mwanamke
mmoja aliyempokea pale akapelekwa
sebuleni.
‘ karibu sana Kinshasa Monica”
akasema Yule mama kwa adabu
‘ Ahsante sana” akajibu Monica na
kuhudumiwa kinywaji.
“ Monica hapa ndipo mahala
utakapoishi kwa muda wote
utakaokuwepo Kinshasa.Kuna
wahudumu kumi na mbili hmu ndani
kwa ajili ya kazi moja tu ya
kukuhudumia kwa saa ishirini na
nne.Nimezungumza na rais muda mfupi
uliopita yuko njiani anakuja hapa
kuonana nawe.” Akasema Yule
mwanamama .Monica akapelekwa
katika chumba cha kulala ili apumzike
wakati akimsubiri rais.
“ Natamani sana kuzungumza na
akina Austin nijue kama wamepewa
huduma nzuri huko walikopelekwa.Vile
vile nataka kufahamu walipo wazazi
lakini sina wasi wasi nafahamu David
atakuwa amewaandalia sehemu nzuri
kama alivyoniandalia mimi.Huyu
mwanaume ananipenda kupita
maelezo.Ingekuwa ni kule kwetu
wangesema ninatumia dawa
kumchanganya lakini hakuna dawa ni
yeye mwenyewe amechanganyikiwa tu
na mimi.Hata mimi tayari nimeanza
kumpenda japokuwa si muda mrefu
tuliofahamiana lakini kwa muda huu
mfupi nimegundua ni mwanaume
anayenijali na anaonekana ana
mapenzi ya kweli.Hata marehemu
Pauline alinihakikishia hilo kwamba
David ni mwanaume bora kabisa”
akawaza Monica akavua nguo na
kuingia bafuni kuoga .Akiwa bafuni
akasikia mlango wa chumba chake
ukifunguliwa.Akajifunga taulo haraka
haraka ili akaangalie ni nani aliyeingia
na alipotoka tu akajikuta akatazama na
David Zumo ambaye uso wake ulijaa
tabasamu huku akiwa ameipanua
mikono yake tayari kabisa
kumkumbatia Monica
“Hallow malaika wangu.Karibu
tena Kinshasa.Nina furaha ya ajabu
sana kukuona tena japokuwa nipo
katika majonzi lakini kuiona tu sura
yako nimepata faraja kubwa sana”
akasema David na kumkumbatia
Monica kwa nguvu
“Pole sana mpenzi.Hii ni mitihani
tu ya maisha .Mungu akupe nguvu ya
kuhimili wakati huu mgumu” akasema
Monica
“ Ahsante sana malaika wangu”
akasema David na kumbusu.Mara taulo
alilokuwa amejifunga Monica
likaanguka kwani lilikuwa
limelegea.Wote wawili wakajikuta
wakitazamana.Mwili wa David
ulisisimka mno baada ya kumshuhudia
Monica akiwa mtupu.Akameza
mate.Monica akataka kuinama aliokote
taulo lile lakini David akamzuia na
badala yake akainama yeye akaliokota
na kumuomba Monica ageuke
akamfunga lile taulo na kuanza
kupitisha mikono yake taratibu katika
kifua cha Monica kilichobeba matiti
madogo yaliyojaa.Monica akatoa
mguno baada ya kuguswa kifuani
,aakanza kuhema haraka haraka.David
ikulu tayari kulikuwa kumechachamaa
.Monica akageuka na ni kama vile
alikuwa anaisubiri sana nafasi hiyo
akamkubatia David na kumpiga busu
ambalo lilikuwa ni kama taa ya kijani
kwa David.Haraka haraka akalivua koti
na kulitupa chini akamkumbatia
Monica akambusu mfululizo na kuanza
kunyonyana ndimi.Wote wawili
mashetani yalikwisha amka na kila
mmoja alianza kufanya jitihada ya
kuyatuliza.Wakati mikono ya David
ikiendelea na zoezi la usaili katika
mwili wa Monica,taratibu mikono laini
ya Monika ikafungua suruali ya David
ikaanguka chini ,akaanza kuipapasa
ikulu iliyokuwa imekasirika
vilivyo.Kitendo kile cha kuichezea ikulu
ya David kikamfanya aongeze manjonjo
na mwisho akashindwa kuvumilia
akamuinua Monica akamtupa kitandani
na mtanange ukaanza.
Kilikuwa ni kipute kizito
kilichodumu kwa muda wa nusu
saa.Kila mmoja alikuwa hoi .David
akamkumbatia Monica na kumpa busu
zito
“Ahsante sana Monica.Pauline
ameondoka lakini imekuja zawadi
kubwa badala yake .Ahsante sana
Monica kwa kuja katika maisha yangu”
akasema David
“Nashukuru sana David.Pole tena
kwa msiba huu mkubwa.Binafsi
nimeguswa mno kwa msiba
huu.Pauline alikua ni mtu mzuri
mwenye moyo wa huruma na upendo
wa ajabu.Nimefahamiana naye kwa
siku chache tu lakini ni kama vile
tumejua miaka mingi.Ameondoka bado
mapema sana ” akasema Monica
“ Ni kweli Monica hayo
uyasemayo.Mimi na Pauline tumeishi
miaka mingi na tumeishi kwa furaha
kubwa .Nina huzuni kubwa ambayo
siwezi kuielezea ila kama wasemavyo
kila kitu hutokea kwa sababu.Tuzidi
kumuombea apumzike kwa amini.”
Akasema David halafu wakatazama
kwa sekunde kadhaa akasema
“ Pole na safari Monica.”
‘ Ahsante sana mpenzi”
“Monica kwanza samahani sana
kwa kwenda kushukia katika uwanja
wa ndege wa kijeshi.Malkia wa Congo
hupaswi kushukia kule japokuwa ni
sehemu yenye usalama mkubwa.Nataka
inkuhakikishie kwamba jambo hili
halitajirudia tena” akasema David
“ Usijali David” akasema
Monica.David akavuta pumzi ndefu na
kumtazama Monica kwa makini kisha
akasema
“ Wakati ndege ikiwa angani
nilipokea simu toka kwa balozi wa
Tanzania hapa Congo akinitaarifu
kwamba rais Ernest Mkasa anahitaji
kuzungumza nami kuna suala la
muhimu sana.Kutokana na shughuli
nyingi za maandalizi ya kesho sikuweza
kuwa na simu hivyo mheshimiwa rais
akanipigia mara kadhaa na
kunikosa.Nilimpigia rais Ernest
akanieleza jambo lililonikstua
kidogo.Aliniambia kwamba katika
ndege ulikuwa umeambatana na watu
ambao ni hatari kwa usalama wa
Tanzania.Kilichoniogopesha zaidi ni
pale aliposema kwamba watu hao
wanahusika na mashambulio
yaliyotokea jana jijini Dar es salaam na
Dodoma.Nilistuka sana kusikia malkia
wa Congo ana mahusiano na watu
hatari kama hao ikanilazimu niombe
rais anifafanulie zaidi na ndipi
akanieleza kwamba hauna mahusiano
yoyote na watu hao bali una urafiki na
mtummoja anitwa Austin ambaye ndiye
mwenye mahusiano na hao watu.Baada
ya maelezo ya rais ikanilazimu
kuelekeza ndege ikatue katika uwanja
wa ndege wa jeshi na wale wote ambao
nimeombwa na rais niwashikilie na
kuwarejesha Tanzania hivi sasa
wanashikiliwa na jeshi na nitafanya
mipango warejeshwe Tanzania haraka
wakajibu tuhuma zinazowakabili”
Akasema David Zumo.Monica
akapatwa na mstuko mkubwa akalitupa
shuka alilokuwa amejifunika akainuka
na kumtazama David Zumo kwa
mshangao
“Umesema nini? Akauliza
“ Nadhani umenisikia vizuri
Monica.Ulikuwa unasafiri na watu
hatari sana bila ya wewe kufahamu
kama ni watu hatari na wanahusika
katika mashambulio yaliyotokea jana
jinii Dar es slaam na kuua watu wengi
na wengi wao wakiwa viongozi wa
kitaifa.Usihofu tena Monica uko salama
na watu wale hawataweza kufanikisha
lengo lao la kutoroka kukimbia maovu
waliyoyafanya.Siku nyingine
usiwaamini sana marafiki zako.Si wote
ni wazuri.Kama huyu anayeitwa Austin
ambaye umemuamini sana na
akakutumia ili kuweza kuwatorosha
watu hao hatari.Tuachane na hayo
tuongelee masuala yetu” akasema
David Zumo
“Hapana David tuendelee na suala
hilo.Naomba unisikilize vizuri ”
Akasema Monica
“Aliyekupa taarifa hizo
amekudanganya na yote aliyokuelekza
ni uongo mkubwa.Nataka sasa hivi wale
wenzanguwote Austin na wenzake
waondolewe katika kizuizi na waletwe
hapa mara moja” akasema Monica kwa
sauti isiyoonyesha masihara
“Monica tafadhali usikasirike kwa
hiki nilichokifanya.Nimefanya kwa ajili
ya usalama wako wewe mwenyewe na
kwa usalama wa nchi yako.Nafahamu ni
vigumu kuamini haya ninayokwambia
hasa kutokana na namna
unavyomuamni huyo rafiki yako Austin
lakini naomba ufahamu kwamba huyo
si rafiki mzuri hata kidogo.Ni mtu
mbaya sana.Angekuwa ni rafiki wa
kweli asingeweza kukuweka katika
hatari yote hii.Kesho wote wanarudi
Tanzania” akasema David
“ Hakuna yeyote atakayerudishwa
Tanzania.David naomba uniamini.Yote
uliyoelezwa na rais ni uongo mtupu
.Nina fahamu kila kitu kinachoendelea
na ndiyo maana nakuomba uwaachie
marafiki zangu haraka sana kwani
hawana kosa lolote na David nataka
marafiki zangu wote waje hapa katika
nyumba hii mara moja” akasema
Monica.David akazidi kushangaa
“ Monic….!! David akataka kusema
kitu lakini Monica akamzuia
“ David hatutaongea chochote bila
ya marafiki zangu kuja hapa mara
moja.Ukjitaka amani iwepo kati yagu
nawe naomba uwatoe marafiki zangu
kizuizini haraka sana!! Akasema
Monica kwa ukali.Ni mara ya kwanza
toka wamefahamiana David alimuona
Monica akiwa amekasirika namna
ile.Kwa muda wa sekunde kadhaa
wakabaki wanatazama
“David unaniamini? Akauliza
Monica
“ Asilimia mia moja” akajibu David
“ Kama unaniamini kiasi hicho
naomba uwatoe Austin na wenzake
kizuizini na uwalete hapa .Hawana kosa
lolote.Watakapofika hapa nitakueleza
kila kitu.Kuna masuala makubwa
ambayo tutakueleza.Naomba sana
David” akasema Monica na kama ilivyo
kawaida yake macho yake tayari yaliloa
machozi.David akamfuata
akamkumbatia na kumfuta machozi
“Basi usilie malaika
wangu.Nilikuahidi kwamba niko tayari
kufanya jambo lolote lile.Hata kama ni
kupindisha sheria kwa ajili yako
nitafanya hivyo.Nitawatoa rafiki zako
kizuizini na wote watakuja hapa”
akasema David Zumo na kuchukua
simu akapiga akaongea kwa dakika tatu
halafu akamgeukia Monica
“Rafki zako watakuja hapa muda
si mrefu sana.Samahani sana
nimekutoa machozi mpenzi
wangu.Niumeumia kukuona malaika
kama wewe unadondosha
machozi.Naomba unisamehempenzi
wangu.Nilifanya kosa kubwa kufanya
haya niliyoyafanya bila ya
kukushirikisha kwanza wewe” akasema
David alyekuwa amempigia magoti
Monica
“ Siku nyingine kama kuna suala
lianihusu mimi naomba usilitolee
maamuzi hadi kwanza uwasiliane na
mimi.Watu wale uliowaweka kizuizini
ni watu wangu wa muhimu sana na
nilipo mimi nataka nao wawepo”
akasema Monica
“ Wanakuja sasa hivi .Tayari
wamekwisha tolewa kizuizini.”
Akasema David huku akiendelea
kumfuta machozi Monica
Ilimchukua Davidi zaidi ya dakika
kumi kumbembeleza Monica halafu
wakabusiana na tabasamu la Monica
likarejea tena usoni pake.David
akashusha pumzi
“Nilitaka kukoroga mambo
hapa.Sijui kwa nini nilimsikiliza Ernest
na kufanya maamuzi bila ya
kumshiriisha Monica.” Akawaza David
“ Wazazi wangu nao wako wapi?
Nao walikua kizuizini? Akauliza Monica
“ Hapana .Wako katika kasri zuri
wametulia hivi sasa.Wale ni wazazi
wako na ni wazazi wangu pia kwa hiyo
ninawajali sana.Usihofu chochote
kuhusu wao” akasema David
“Ahsante kwa hilo” akasema
Monica
Waliingia bafuni wakaoga kwa
pamoja halafu wakawa na mazungumzo
kuhusiana na shughuli za mazishi
zinazotarajia kufanyika kesho na mara
mlango ukagongwa.Alikuwa ni mlinzi
wa rais aliyemtaarifu kwamba wale
wageni wake wamewasili.Uso wa
Monica ukaonyesha tabasamu kubwa
kwa taarifa ile wakashuka yeye na rais
kwenda kuwapokea akina Austin
“ Karibuni sana ” David Zumo
akawakaribisha akina Austin.Monica
akawatambulisha akina Austin kwa rais
David Zumo halafu wote wakajumuika
kwa chakula cha usiku na baadae
Austin ,Amarachi ,Monica na rais
wakaenda juu ya ghorofa lile kwa ajili
ya maogezi.Akina Yasmin wakapewa
vyumba vya kupumzika.
“Austin na Amarachi karibuni
sana Kinshasa.Nimefurahi kukutana
nanyi.Nadhani tayari Monica
amekwisha waeleza kuhusu mimi na
yeye kwa hiyo Marafiki wa Monica ni
wangu pia hivyo kwa mara nyingine
tena nawakaribisha Kinshasa karibuni
sana na mjisikie nyumbani” Akasema
David Zumo
“ Ahsante mheshimiwa
rais.Tunashukuru kwa makaribisho
mazuri tuliyopata na tayari tunajihis
tuko nyumbani” akasema Austin
“Napenda vile vile kuchukua
nafasi hii kuwataka radhi kwa kile
kilichotokea usiku huu pindi tu
mlipowasili.Kilichotokea ni makosa
yangu kwani nilipewa taarifa ambazo
sikuzifanyia uchunguzi wa kutosha na
hivyo nikaelekeza ndege ikatue katika
uwanja wa kijeshi na kisha
mkashikiliwa.Nilipewa taarifa na rais
wa Tanzania kwamba katika ndege
yangu ambayo niilituma Dar es salaam
kumchukua Monica na familia yake
kuja kuhudhuria mazishi ya mke wangu
hapo kesho kuna watu hatari ambao
wanahusika na msahambulio
yaliyotokea jana katika miji ya Dar es
salaam na Dodoma.Nilistuka sana na
nikajiuliza maswali mengi kuhusiana
na jambo hilo.Ninamfahamu Monica na
nikashangaa sana kusikia anahusiana
na watu hao hatari hivyo nikaelekeza
kwamba ndege iende moja kwa moja
katika uwanja wa jeshi na Monica na
wazazi wake wapelekwe mahala
walikoandaliwa ila wale wengine wote
alioambatana nao wakazuiliwe katika
kambi ya jeshi.Namshukuru Monica
ambae amenifumbua macho na
kunieleza kwamba kile nilichoelezwa si
kitu cha kweli hata kidogo.Amesema
kwamba kuna jambo linaloendelea
kubwa na ninadhani ninahitaji
kulifahamu kwani rais wa nchi yenu
aliniwekea msisitizo sana kwamba
ninyi ni hatari mno.” Akasema
David.Austin na Monica wakatazamana
kisha akasema
“Mheshimiwa rais kama Monica
alivyokutambulisha ninaitwa Austin
January .Nimewahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi ya taifa na kwa sasa
ninaishi nchini afrika ya kusini
.Nililazimika kuikimbia nchi yangu
kutokana na mambo
yaliyonitokea.Nilinusurika kuuawa
nikiwa katika operesheni nchini
Somalia na waliotaka kuniua ni
wenzangu tuliokuwa nao katika
operesheni hiyo na huo ulikuwa ni
mpango wa watu ndani ya serikali
ambao niligundua kuhusu mpango wao
muovu.Boaz ambaye nimeambatana
naye ndiye aliyenikomboa toka kwa
Alshabaab kwa kulipa kiasi kikubwa
cha fedha na niakenda kuishi na familia
yake afrika kusini hadi hivi majuzi
nilipoitwa na rais kumfanyia kazi
binafsi.Mimi ndiye niliyemtoa Marcelo
hospitali Yule rafiki yake Monica
aliyekuwa katika hatari ya kuuawa na
Monica akakuomba umsaidie”
“ Ni wewe !! akasema David huku
akitabasamu
“ Ndiyo ni mimi.Hiyo ilikuwa ni
mojawapo kati ya kazi mbili alizonipa
rais nizifanye.Wakati nikiendelea
kuifanya kazi ya pili aliyonipa nilipatwa
na matatizo nikapigwa risasi na
msichana ambaye alikuwa mpenzi
wangu.Mimi na rais tulikuwa na
operesheni ya pamopa ya kuwaondoa
Alberto’s nchini Tanzania ambao tayari
walikwisha weka mzizi yao na ndio
waliokuwa wakiiongoza nchi.”
“ Alberto’s? akauliza David
“ Ndiyo mheshimiwa rais.Nadhani
tayari unawafahamu ni akina nani na
lengo lao ni nini” akasema Austin
“ Ninawafahamu watu hawa lakini
mimi katika nchi yangu wameshindwa
kuingia kwani hatuhitaji tamaduni za
kigeni na wala hawawezi kuniwekea
vikwazo vyovyote vya kiuchumi
kunilazimisha kujiunga nao.Sisi Congo
ni taifa linalojitosheleza kiuchumi na
hatutegemei misaada toka kwa mataifa
ya kigeni kama mataifa mengi ya Afrika
yanavyofanya na ndiyo maana inakuwa
rahisi kwao kukubaliana na masharti
ya Alberto’s kwa kuogopa kunyimwa
misaada.Kwa mambo yaliyokuwa
yanaendelea Tanzania na hasa kutaka
kuupeleka ule muswada bungeni wa
kutaka kutambua haki za watu wa
mapenzi ya jinsia moja na utoaji mimba
niliamini hizo zilikuwa ni jitihada za
Alberto’s.” akasema David
“ Rais Ernest Mkasa aliwekwa
madarakani na hawa jamaa na yuko
pale kama picha tu kwani nchi
inaongozwa na Alberto’s na yeye ni
mtekelezaji wa maagizo na maelekezo
yao.Nilimfumbua macho rais na
kumtaka tupambane na Alberto’s na
tukaanza mikakati ya kuwaondoa
.Kabla hatujaanza operesheni yetu ya
kuwaondoa Alberto’s nchini Tanzania
mimi na wenzangu ambaye ni huyu
Amarachi na mwingine ambaye
amebaki Tanzania anaitwa Job
tuligunuda kuwa kuna mwanamke
mmoja aliyekuw amefungwa nchini
tanzania mahala pa siri ambaye ni
mfuasi wa mtandao wa kigaidi wa IS
anaitwa Yasmin Esfahani.Nilimuuliza
rais kuhusiana na mwanamke huyu
akasema kwamba hana taarifa zake
zozote lakini baadae tukagundua
kwamba rais alikuwana anatudanganya
kwani alikuwa anamfahamu na
alimuachia huru kutokana na
makubaliano aliyoyafanya na
Alshabaab”
“ Alshabaab ?!! David Zumo
akashangaa
“ Ndiyo.Rais Ernest alikuwa na
makubaliano na Alshabaab na katika
makubaliano hayo Alshabaab walitaka
huyo mwanamke Yasmin pamoja na
mtu mwingine aliyejulikana kama
Tariq waachiwe huru “
“ Hebu subiri kidogo
Austin.Unasema kwamba rais Ernest
ana mawasilaino na kikundi cha
Alshabaab? Kama ana mawasiliano nao
na hadi wamefikia hatua ya kuweka
makubaliano kwa nini wakafanya
mashambulio yale makubwa na kuua
watu wengi? David Zumo akauliza
“ Hata sisi tumejiuliza sana swali
hilo lakini bado tunaendelea
kuchunguza ili tufahamu iweje
Alshabaab washambulie Tanzania
wakati wana mawasiliano na rais?
Tulifanikiwa kumpata Yasmin ambaye
aliachiwa huru na ndipo tukafahamu
jambo jingine kubwa .” Austin
akanyamaza akamtazama David Zumo
kisha akaendelea
“Katika makubaliano kati ya rais
na Alshabaab kuna vitu viwili
walikubaliana.Kwanza ni kuwaachia
hao watu wawili ambao ni Yasmin na
Tariq na pili walihitaji wapewe hati ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar”
“ Wametaka wapewe hati ya
muungano wa Tanganyikana
Zanzibar?!! David naye akashangaa
“Ndiyo.Walihitaji wapatiwe hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.Hati hiyo alipewa Yasmin ili
akaikabidhi kwa viongozi wake wa IS
kwani ndio waliokuwa wanaitafuta hati
hiyo na wakawatumia Alshabaab
kuipata”
“ IS wanaitaka hati ya muungano
wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu
gani? Akauliza David
“ Lengo kuu la IS ni kujitanua zaidi
upande huu wa afrika mashariki na
wanataka kukipata kisiwa cha Pemba
kwani katika uchunguzi wao
wamegundua kwamba wanaweza
kustawi zaidi iwapo wataweka makazi
yao katika kisiwa cha Pemba kwa hiyo
ili kukipata wanalazimika kwanza
kuuvunja muungano kwani Pemba iko
ndani ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania na baada ya muungano
kuvunjika itakuwa rahisi kwao
kuvitenganisha visiwa vya Unguja na
Pemba na kisha watakimiliki kisiwa
cha Pemba .Hiyo ndiyo sababu yao kuu
ya kutaka hati ya muungano.” Akasema
Austin
“Haya ni mambo makubwa sana.Je
hati hiyo imekwisha tolewa ?
akaulizaDavid Zumo
“ Tayari Ernest amekwishaitoa
hati hiyo na alikabidhiwa Yasmin ili
akawakabidhi viongozi wake lakini
hakwenda Mogadishu kama
alivyotakiwa bali alilazimsha ndege
waliyopanda ikatua Zanzibar na
akarejea Dar es salaam kwani sisi
tulikuwa tunamshikilia mtoto wake
ambaye ndiye yule binti aliyenipiga
risasi.Yasmin anayo hati ya muugano
na yuko tayari kutupatia hati hiyo
endapo tutamtimizia masharti kadhaa
aliyoyataka” akasema Austin
“ Ni masharti gani hayo
anayoyataka Yasmin? David akauliza
“ Yasmin hataki tena kuwa mfuasi
wa IS anataka aanze maisha mapya
sehemu ya mbali ambako hataweza
kugundulika na IS.Anataka
tulifanikishe hilo na ndipo atuonyeshe
mahala ilipo hati ya muungano.Kwa
upande wetu sisi suala hilo ni gumu
sana kulifanikusha kutokana na hali
inayoendelea Tanzania kwa sasa na
hasa baada ya rais kuanza kutusaka
baada ya kugundua kwamba
tumekwisha fahamu mipango yake.
Nililazimika kumuomba msaada
Monica na na ndiye aliyetusaidia
kuweza kumtorosha Yasmin nchini
Tanzania.Kwa hiyo mheshimiwa rais
alichokueleza rais Ernest si kitu cha
kweli hata kidogo.Ukweli ndio huo
niliokueleza na tumekuja kwako
kutaka msaada.” Akasema Austin.David
Zumo akawatazama kwa sekunde
kadhaa halafu akasema
“ Nimestushsa sana na mambo
haya uliyonieleza Austin.Lakini
kinachonisikitisha zaidi ni kitendo cha
kumshirikisha Monica katika suala hili
kwani tayari naye ameingia katika
hatari.Rais tayari amemjumuisha
katika orodha ya watu anaowatafuta
ambao ni hatari kwake.” Akasema
David Zumo
“Hapana mheshimiwa rais.Monica
hayuko katika hatari .Rais anamfahamu
vyema yeye na wazazi wake na ni
familia marafiki kwa hiyo hawezi
kumfanya kitu chochote.Hata
tulipofuatwa na zile ndege ni yeye
aliyempigia simu rais na kumuomba
msaada na haikuchukua dakika tano
ndege zile zikaondoka.Nakutoa wasi
wasi mheshimiwa rais kuhusu Monica
hatakuwa katika hatari yoyote”
akasema Austin
“Ahsante kwa kunitoa hofu hata
hivyo itanilazimu kumuwekea ulinzi
kuhakikisha kwamba anakuwa
salama.Umesema pia mmekuja kwangu
mnahitaji masaada.Ni msaada upi
mnaouhitaji? Akauliza rais David
“ Tunataka Yasmin atafutiwe
mahala pa kwenda kuishi yeye na
familia yake ambako IS hawataweza
kumgundua .Anahitaji wapatiwe majina
mapya na pasi mpya za
kusafiria,nyumba nzuri huko mahala
watakakoenda kuishi na tatu biashara
ya kuweza kuwaingizia kipato na
kuwawezesha kuendesha maisha yao”
Akasema Austin.David Zumo
akainamisha kichwa kidogo
akatafakari.Austin akamtazama Monica
na kumfanyia ishara aongee na David
“David” akaita Monica na David
akainua kichwa haraka akamtazama
“Ninaomba utusaidie suala hilo
alilokueleza Austin.” Akasema Monica
na David akaonekana kuendelea
kutafakari kisha akasema
“ Monica suala hili si rahisi kama
mnavyolichukulia.Huyo mtu
mnayeomba nimsaidie anahusiaa na
mtandao wa kigaidi na sehemu yoyote
utakayomuombea hifadhi wakigundua
kwamba ni mfuasi wa mtandao wa
kigaidi hawatakubali na hata mmi
nitaanza kutiliwa shaka kwamba
ninahusiana na magaidi.” Akasema
David
‘ David nafahamu hili ni suala
gumu kwako lakini nakuomba
unisaidie.Hunisaidii tu mimi na
wenzagu hawa bali unasaidia nchi
yangu pia.Usiponisaidia katika hili nchi
yangu itagawanyika vipande vipande
jambo ambalo mimi na wenzangu
hatutaki litokee.Tafadhali nakuomba
David sintakuomba tena suala lingine”
akasema Monica na kwa mbali macho
yake yakaonekana kuanza kuloa
machozi.David akasema
“Kesho mke wangu anazikwa kwa
hiyo sintakuwa na nafasi.Naombeni
tulijadili suala hili kesho kutwa baada
ya mazishi ya mke wangu
kumalizika.Nitawasaidia kwani
Tanzania ni nyumbani kwetu
pia.Wakati nchi yetu ikiwa katika vita
ya wenyewe kwa wenyewe nchi ya
Tanzania ilikuwa ni nyumbani kwa
wananchi wa Congo hivyo Tanzania si
tu nchi jirani au rafiki bali ni ndugu wa
damu kwa hiyo nitafanya kila
linalowezekana kuhakikisha nchi ya
Tanzania haiingii katika matatizo
yoyote.Baada ya shughuli za mazishi
kumalizika mimi na ninyi tutakaa
pamoja na kulimaliza suala hili”
akasema David
“ Tunashukuru sana mheshimiwa
rais kwa msaada wako huu mkubwa
kwa nchi yetu.”akasema Austin .David
Zumo akaagana nao kwa ajili ya
kuelekea katika shughuli nyingine.
“ Ahsante David” akasema Monica
wakati akimsindikiza David kuelekea
katika gari lake
“ Monica nilikuahidi kufanya kila
kitu kwa ajili yako kwa hiyo
nilichokifanya ni wajibu wangu.Hata
hivyo Tanzania ni nyumbani kwetu pia
kwa hiyo siwezi kukubali kuona kuna
tatizo kubwa kama hili lazima nitoe
msaada kwani ndiko anakotoka malkia
wa Congo” akasema David na kumbusu
Monica.Walichukua dakika kadhaa nje
ya gari la David wakiongea na kisha
wakaagana David akaingia garini na
kuondoka Monica akarejea ndani
“ Monica ahsante sana .Bila wewe
suala hili katu lisingefanikiwa.Hata
David Zumo aliogopa kutusaidia na bila
wewe kumshawishi tungekwama.”
Akasema Austin
“ Msijali Austin.Ulikuwa ni wajibu
wangu kumshawishi akubali.Nilistuka
aliponiambia kwamba mmewekwa
kizuizini kutokana na maelezo
aliyopewa na rais Ernest.Hili jambo
sasa limekwisha vuka mipaka ya nchi
na linawezekana likawa kubwa zaidi na
kufika mbali.Ni vipi kama Ernest
akigundua kwamba David hajalifanyia
kazi agizo lale la kuwakamata na
kuwarudisheni nchini Tanzania?
Akauliza Monica
“ Ni wazi utaibuka mgogoro kati
yao lakini kwa wakati huo tayari
tutakuwa tumekwisha ipata hati yetu
ya muungano na nchi itakuwa salama.”
Akasema Austin
“ Nini kitafuata baada ya kuipata
hati ya muungano? Amarachi akauliza
“Kitakachofuata ni kutafuta
ushahidi wa kuweza kumtoa rais Ernest
madarakani na kumfikisha mbele ya
sheria kwa mauaji aliyoyafanya.Kwa
rekodi hii aliyotupa Irene ni wazi rais
anahusika katika mashambulio yale
lakini lazima kwanza tuwe na ushahidi
wa kutosha kumtia hatiani.Rekodi hii
pekee haiwezi kutosha kutumika kama
ushahidi.Katika rekodi hii kuna mtu
mwingine ambaye anasikika ambaye ni
Jenereali Lameck msuba.Huyu
nilimpendekeza mimi kwa rais kwani
ninamfahamu vyema lakini naye
amegeuka na kuanza ushirika na
rais.Tunatakiwa kuwachunguza hawa
wawili na toka kwao tutaufahamu
mtandao wao na tutafahamu mambo
mengi na kisha kusanya ushahidi wa
kutosha tutawafikisha mbele ya sheria”
akasema Austin
“ Hili halitakuwa suala rahisi”
Akasema Amarachi
“ Ni kweli halitakuwa suala rahisi
lakini tutapambana na nina uhakika
tutashinda.Mungu yuko upande
wetu”akasema Austin
“ Mmewasiliana na Job kujua
wamefikia wapi kuhusiana na ile kazi
uliyomuachia aifanye na Daniel?
Akauliza Monica
“ Job tutawasiliana naye
kesho.Tutakuwa na muda mzuri wa
kutosha.Kwa sasa ni wakati wa kwenda
kupumzika.Siku imekuwa ndefu sana.”
Akasema Austin
“ Tunawaacha akina Yasmin peke
yao? Akauliza Amarachi
‘ Ulinzi wa hapa si wa kitoto.Ni
sehemu yenye ulinzi mkali sana sana na
wanaolinda hapa ni wanajeshi. Palipo
na malkia wa Congo lazima pawe na
ulinzi mkali sana” akasema Austin na
wote wakaangua kicheko
“ By the way guys kuna vyumba
vingi hapa,mngependa kulala katika
chumba kimoja au kila mtu na chumba
chake? AkaulizaMonica.
“Chumba kimoja tu
kinatosha”akasema Austin na
kumtazama Amarachi na wote
wakatabasamu.Monica akawapeleka
katika chumba kikubwa
kilichojitosheleza kila kitu.
“Kuna wahudumu humu ndani
kwa saa ishirini na nne.Muda wowote
mkihitaji huduma yoyote kuna simu
mezani mtapiga na mtahudumiwa.”
Akasema Monica na kuagana na akina
Austin akaelekea chumbani kwake.
Austin akaketi kitandani na
Amarachi akaketi katika sofa.
“Sikujua kama pale tulikopelekwa
baada ya kutolewa uwanja wa ndege
tulikuwa kizuizini” akasema Amarachi
“Mimi nilihisi hivyo tayari na
nilikuwa natafuta namna ya kuweza
kutoka pale.Nisingekubali mpango
wetu ushindikane.Ningefanya kila
linalowezekana hadi tungefanikiwa
kutoka pale.” Akasema Austin
“David anampenda sana Monica
na anaonekana yuko tayari kumfanyia
jambo lolote.” Akasema Amarachi
“ Hiyo ni faida kwetu kwani
kupitia kwa Monica tumefanikisha
operesheni zetu.Bila Monica
tusingefanikiwa kumtoa salama Yasmin
Dar es salaam .Ni kwa sababu yake
David amekubali kutusaidia kwa hiyo
uhakika wa kuipata hati ya muungano
ni mkubwa.Monica anapaswa
kushukuriwa sana” akasema Austin na
Amarachi akaonekana kuzama katika
mawazo
“ Unawaza nini Amarachi?
Unaogopa kulala nami chumba kimoja?
Akauliza Austin.Amarachi akaangua
kicheko
“ Hilo si suala la kuniogopesha
mimi hata kidogo kwani kipi sijakiona?
Akauliza Amarachi .
“ Nimeuona upendo wa kweli kwa
David Zumo ambaye yuko tayari
kuingia katika mgogoro na rais
mwenzake kwa sababu ya Monica.Laiti
na mimi siku moja ningepata
mwanaume mwenye kunipenda kama
David anavyompenda
Monica.Umeyaonaje mapenzi yao?
Akauliza Amarachi
“ Ni wazi wanapendana kwa
dhati.Kwani Amarachi hauna mpenzi?
Akauliza Austin
“ Hapana sina” akajibu Amarachi
“ What about Job? Mimi nilidhani
ni mpenzi wako kwa namna
mnavyojaliana” akasema Austin na
Amarachi akaangua kicheko kikubwa
“Mimi na Job ni marafiki wa
karibu sana na hatuna mahusiano
yoyote.Job ni zaidi ya ndugu yangu
kwani yeye ndiye aliyenileta hapa
Tanzania.Baada ya kuachiwa toka
msituni tulikokuwa tunashikiliwa na
wanamgambo wa Boko Haram
,nilikutana na unyanyapaa mkubwa
sana nchini kwangu Nigeria.Msituni
nilipata mateso makubwa kwani
tulikuwa tunabakwa karibu kila siku na
nikapata mtoto nilipoachiwa nilirudi
nyumbani na mwanangu lakini baadae
akauawa kwa kisingizio kwamba ni
damu ya boko haramu.Mimi mwenyewe
nilinusurika kuuawa mara nyingi na
kilichonisaidia ni kuwa na uwezo
mkubwa wa kujilinda niliojifunza
nikiwa msituni. Kaka yangu
anafahamiana na Job hivyo akamuomba
anifanyie mpango niweze kuja kuishi
Tanzania mahala ambakohakuna
anayenifahamu.Job alikubali na
akanisaida nikaja Tanzania na kuanza
maisha yangu hapa.Haikuwa rahisi
mwanzoni lakini Job alihakikisha
kwamba ninayabadili maisha yangu na
kuanza maisha mapya.Amefanya kazi
kubwa kuniondoa katika maisha yale
niliyokuwa tayari nimeyazoea ya uboko
haramu.Kwa mambo aliyonifanyia
ndiyo sababu ya mimi na yeye kuwa na
ukaribu mkubwa.Hata hivyo Job ni
zaidi ya ndugu na ni mtu wa muhimu
mno katika maisha yangu kwa hiyo
hatuwezi kuwa na mahusiano ya
kimapenzi” Akasema Amarachi
“Pole sana kwa masahibu yote
yaliyokupata.Hata hivyo mnapendeza
sana mkiwa pamoja” akasema Austin
na wote wakacheka.
“Acha uitani Austin.Mimi na Job ni
kweli tunaweza kuonekana tunaendana
sana lakini hatuwezi kuwa wapenzi.Job
ni kama kaka yangu na lazima awe
karibu na mimi kuhakikisha kwamba
ninakuwa salama siku zote” akasema
Amarachi
“Ni mwanaume wa aina gani
unayemuhitaji katika maisha yako?
Akauliza Austin
“Sitazami sura wala hali yake ya
kiuchumi bali nataka mwanaume
ambaye atakuwa na mapenzi ya dhati
kwangu kama David anavyompenda
Monica.Nataka mwanaume ambaye
atakuwa tayari kujitoa kwa ajili yangu”
akasema Amarachi.Austin akamtazama
na kusema
“Baada ya mambo yote
yaliyokutokea katika maisha yako,are
you ready to open your heart and love
again? Akauliza
“Austin umeniuliza swali ambalo
hata mimi nimekuwa najiuliza mara
kwa mara kwamba je iwapo atatokea
mwanaume ambaye nijampenda je niko
tayari kuufungua tena moyo wangu na
kupenda tena? Picha za mambo yale
yaliyonitokea msituni bado zinanijia
mara kwa mara.Ninakumbuka
nilivyokuwa ninabakwa na wakati
mwingine na zaidi ya mtu mmoja.Moyo
wangu unaumia bado lakini lazima
maisha yaendelee.Siwezi kuwachukia
wanaume wote na siwezi kuweka agano
kwamba sintopenda tena kwani si
wanaume wote wabaya na wala si wote
ni boko haram.Endapo nitampata Yule
mwanaume mwenye mapenzi ya kweli
basi nitaufungua moyo wangu kwa ajili
yake” akasema Amarachi
“I wish I could be that
man”akasema Austin kwa sautio ndogo
ambayo iliweza kumfikia Amarachi.
“ Umesemaje Austin? Amarachi
akauliza
“Oh ! forget what I said.Kuna
nyakati ulimi unajikuta umetamka
jambo biula kuwasiliana kwanza na
ubongo” akasema Austin
“Kuna kitu umekisema
nimekisikia.Unaweza kurudia kile
ulichokitamka? Amarachi akasisitiza
“Nilisema I wish I could be that
guy” Akasema Austin
“Why you wish?Ukitaka iwe
haitakuwa? Akauliza Amarachi
“Amarachi wewe ni mwanamke
wa kipekee kabisa ambaye nimewahi
kukutana naye katika maisha
yangu.Unastahili mwanaume ambaye ni
bora na ambaye hatakutoa chozi kwani
tayari umekwisha lia vya
kutosha.Nakuhakikishia kwamba
mwanaume ambaye atakupata wewe
atakuwa na bahati sana.Ninatamani
endapo ningekuwamimi lakini sina sifa
za kuwa na wewe.Siwezi kuwa na
maisha ya kawaida.Nlijaribu
nimeshindwa.Maisha yangu hadi siku
ninaingia kaburini yatakuwa ni
kukimbizana na risasi kama hivi.Laiti
kama nisingekuwa katika kazi hizi
nakuapia ningefanya kila niwezalo
mpaka ungekuwa wangu” akasema
Austin na kucheka kidogo
“Austin you are so sweet” akasema
Amarachi
“Lakini Austin kwa nini uliingia
katika kazi hizi? Mwanaume kama
wewe hukupaswa kabisa kufanya kazi
kama hizi za hatari.Unastahili kuwa na
familia yako.Unafikiria nini kuhusu
kuachana na kazi hizi na kuanza maisha
ya familia? Akauliza Amarachi
“Uliniuoliza swali kama hili
tukiwa ndegeni na nikakujibu ila kwa
kuongezea pale nilipojibu kwa sasa
familia yangu ni wananchi wa Tanzania
ambao ninawapigania kwa hiyo siwezi
kuachana na kazi hii.Nitaendelea
kupambana kwa ajili ya familia yangu
hadi mwisho wangu.Sina mpango wa
kupenda tena kwani nilijaribu na
nimeumizwa vibaya sana.I don’t believe
in love anymore” akasema Austin
“Austin usiseme hivyo
tafadhali.Kuumizwa na mwanamke
mmoja si kwamba wote ni wabaya
.Bado wako wanawake wazuri wenye
mapenzi ya kweli.Ninaamini kabisa
yuko mwanamke ambaye ameumbwa
kwa ajili yako.Ukimpata huyo maisha
yako yatakuwa na amani na furaha
kubwa.Tafadhali usikate tamaa
Austin.Kuna maisha mazuri
yanakusubiri” akasema Amarachi
“Maisha mazuri labda nikiondoka
hapa duniani lakini nikiwa bado
ninaishi maisha yangu yatakuwa kama
hivi.” Akasema Austin.
“Amarachi ni wakati wa
kupumzika sasa.Siku imekuwa
ndefu.Wewe utalala kitandani na mimi
nitalala sofani” akasema Austin
“Austin tutalala wote
kitandani.Unaogopa kulala nami
kitandani?Amarachi akauliza
“Haitakuwa jambo la busara
tukilala wote kitandani.Usihofu hakuna
tatizo lolote .Lala kitandani na mimi
nitalala hapa sofani.I’ll be fine”akasema
Austin.Amarachi akasimama na
kumuendea
“Unaogopa nini Austin?Kuna kitu
gani ambacho hujakiona?
“Amar…..”
“Shhhh !! don’t say anything
Austin.This is our night.Tumepitia
mambo mengi na usiku wa leo lazima
na sisi tujipumzishe.let’s make love
tonight.Najua utashangaa sana kwa
mwanamke kuomba tufanye mapenzi
lakini sina namna.Nahitaji sana usiku
wa leo kufanya mapenzi na wewe
Austin.Naamini hata wewe ulikuwa
unasubiri sana fursa kama hii ijitokeze
na ndiyo maana ulichagua tulale katika
chumba kimoja.Ulijua kabisa kuna kitu
kama hiki kitafanyika and you wanted
it so let’s do it.Tuuache ulimwengu na
madhira yake kwa muda na tujipe
raha.Look we’re both lonely na nafasi
kama hizi zinapojitokeza tunapaswa
kuzitumia kikamilifu.Austin I’m on fire
right now please help me unless …”
akasema Amarachi na kumtazama
Austin
“Unless what ? akauliza Austin
“kama huna uwezo wa
kumridhisha mwanamke” akasema
Amarachi
“You think so?
“Prove to me that you are a real
man and take me to the moon...!!
akasema Amarachi hku akiivua nguo
yake ya juu na kuitupa chini .Austin
akasisimkwa mwili baada ya kukiona
kifua chenye kutamanisha cha
Amarachi.
“Kwa vile umeataka mwenyewe
ngoja nikuonyeshe shughuli
leo.Japokuwa bado ninaumwa lakini
nitakufundisha adabu” akawaza Austin
na kuanza harakati zake za kumdhibiti
Amarachi ambaye alionekana ni kama
amepatwa na uchizi wa ghafla.Austin
alimmiliki vilivyo na baada ya muda wa
kupasha joto hatimaye wakaingia
katika ulingo na kipute kuanza.
 
Back
Top Bottom