QUEEN MONICA: FINAL SEASON
SEHEMU YA 10
Job alifika eneo ambalo
alielekezwa na Mukasha waonane.Gari
kadhaa zilikuwa zimeegeshwa nje ya
kiwanda kikubwa cha mikate.Job
akaichukua tena simu ya silva
akamuandikia ujumbe Mukasha
“Tayari nimefika hapa naziona
gari kadhaa zimeegeshwa .Uko sehemu
gani? Akautuma ujumbe ule na baada
ya muda ujumbe wa majibu ukarejea
“Kuna Toyota harrier rangi nyeusi
imeegeshwa karibu na duka la madawa
niko humo”
Job akaendesha gari taratibu
akaliona gari lile aliloelekezwa na
Mukasha akasimamisha gari nyuma
yake halafu akashuka na bastora yake
ikiwa mkononi akaliendea lile gari la
Mukasha.Alikuwa amevaa kofia
kichwani iliyoufunika uso
wake.Akaufungua mlango wa mbele wa
gari akaingia ndani na kuufunga na bila
kumtazama usoni Mukasha akawasha
gari na kuondoka eneo lile
“Mambo yanakwendaje Silva?
Akauliza Mukasha.
“It’s good to see you again Wilson
Mukasha”
Laiti kama gari lile lingekuwa wazi
Mukasha angeweza kuruka baada ya
kusikia sauti ile.Alitetemeka mikono na
gari likayumba.
“Usiogope Mukasha mimi na wewe
ni marafiki na hatuwezi
kukimbiana.Wanasema milima
haikutani na binadamu hukutana,na
sisi baada ya kupotezana kwa siku
kadhaa hatimaye tumekutana tena”
Akasema Job huku akicheka
kidogo.Mukasha akasimamisha gari
alishindwa kuendesha kwa mstuko
alioupata
“Unahitaji nini toka kwangu wewe
kijana? Lini utaniacha huru na maisha
yangu? Akauliza Mukasha.Job
akatabasamu na kusema
“Geuza gari turudi tulikotoka,
mimi na wewe tuna maongezi ya
muhimu sana leo” akasema
Job.Mukasha akabaki ameduwaa
akimtazama job
“Mukasha endesha gari.!!
Akasema Job na Mukasha akageuza gari
na kurudi walikotopka.Walikwenda
hadi mahala Job alikoacha gari lake
wakashuka na kuingia katika gari la Job
wakaondoka
“What do you want from me ?
Mukasha akauliza
“Usihofu Mukasha sintakuondoa
tena sikio la pili.Safari hii nimekuja
kirafiki.Nahitaji sana kuzungumza na
wewe.Kuna mambo mimi na wewe
tunaweza kukubaliana bila kutumia
nguvu kwa hiyo usiogope” akasema Job
na baada ya mwendo wa kama dakika
kumi hivi akaegesha gari katika klabu
moja ya usiku akamtaka Mukasha
washuke wakaingia klabuni wakatafuta
meza wakakaa.
“Mukasha nafahamu mimi na
wewe hatupikwi chungu kimoja lakini
safari hii sijaja kwa shari.Nahitaji
msaada wako na mimi pia nikusaidie”
akasema Job na kumstua Mukasha
“Unahitaji msaada wangu? Msaada
gani unahitaji? Akauliza
“Nimepata taarifa kwamba dogo
Bill amefariki dunia.Yule pekee ndiye
aliyekuwa anafahamu mahala alipo
mke wangu Monalisa na mwanangu
Millen.Kwa sasa nimekwama na sina
mwanga wowote wa kufahamu familia
yangu ilipo.Nataka unisaidie niweze
kuwafahamu walipo” akasema Job
“Job nilikwisha kueleza toka awali
kwamba sifahamu mahala familia yako
ilipo.Aliyekuwa akifahamu mahala
walipo ni Bill pekee na kama amefariki
hakuna anayejua.Ninachofahamu mimi
ni kwamba Bill alikuwa anatumwa na
mtu mmoja anaitwa Don ambaye sisi
sote hatumfahamu.Aliyekuwa
akimfahamu ni Bill peke yake.”
Akasema Mukasha
“Sikiliza Mukasha,nataka
nikusaidie.Nafahamu sasa hivi
mahusiano yako na rais si mazuri na
uko mafichoni.Nitakusaidia kwanza
kwa makazi ili wewe na familia yako
muwe salama na pili wewe na sisi
tunaweza kuwa shirika moja na
tukafanikiwa kumuondoa Ernest Mkasa
madarakani na wewe ukawa huru.Bila
Ernest kuondoka madarakani na
kushtakiwa kwa mambo maovu
aliyoyafanya utaendelea kuwa
mkimbizi .Kwa hiyo kama una chochote
unachokifahamu kuhusiana na familia
yangu nieleze tafadhali” akasema Job
Maneno yale yakaonekana
kumwingia Mukasha akainama kwa
muda akatafakari kisha akasema
“Una hakika na hayo maneno
unayoyasema? Akauliza Mukasha
‘”Nina uhakika mukasha na ndiyo
maana nikakwambia kwamba safari hii
sijakutafuta kwa ugomvi ila nataka
mimi na wewe tushirikiane” akasema
Job
“Kabla hatujaendelea mbele
nataka kufahamu kuhusiana na Daniel
Swai.Umetumia simu yake kuwasiliana
nami .Where is he? Akauliza
“He’s dead”
“What ?!! he’s dead?
“yes.He’s dead.I killed him”
akasema Job
“He was a traitor na kwangu
msaliti yeyote hana nafasi hivyo
nikamuua.Forget about him.Tujadili
kilichopo mbele yetu sasa hivi”
akasema Job
“Taarifa ambayo Daniel alitaka
kukuuzia ameitoa kwangu kwa hiyo
hakijaharibika kitu ukihitaji taarifa
hiyo utaipata” akasema Job.Mukasha
alionyesha woga mkubwa
“Tell me Mukasha are you going to
help me or not? Akauliza Job.Mukasha
akafikiri kidogo na kusema
“Kuna mtu mmoja anaitwa Abdu
Chizo.Huyu ni rafiki na mtu wa karibu
sana wa Bill.Tukimpata huyu anaweza
akafahamu chochote kuhusiana na mke
wako”
“Anapatikana wapi huyo Abdu
Chizo?
“Huyu kumpata kwa usiku huu si
rahisi kwani ana ulinzi mkali
sana.Nafahamu nyumbani kwake na
tunaweza kwenda asubuhi ila
nitaonana naye mimi peke yangu kwani
hataki watu asiowafahamu nyumbani
kwake” akasema Mukasha
“Hatuwezi kusubiri hadi
asubuhi.Tunakwenda usiku huu”
akasema Job
“Job unapaswa
kunisikiliza.Unahitaji msaada wangu so
let me help you my way.Ukitaka tufanye
unavyotaka wewe katu hatutafanikiwa”
akasema Mukasha.Job akamtazama
kwa muda halafu akasema
“ Fine.We’ll do it your way !! but
tonight”akasema Job
“Haoana Job.Kesho asubuhi.Usiku
huu hakuna anayeruhsiwa kulikaribia
jumba lake” akasema Mukasha.Baada
ya muda Mukasha akasema
“Nitakusaidia kupata taarifa
unazozitaka lakini na mimi lazima
unitimizie kwanza mambo ninayotaka.”
Akasema Mukasha
“Unahitaji nini Mukasha? Akauliza
Job
“Usalama wa famila yangu.Rais
ananitafuta sana hivi sasa na japokuwa
nimejificha lakini siko salama.Nahitaji
familia yangu iende nje ya nchi
kujificha hadi hapo mambo
yatakapokuwa shwari.Nataka unisaidie
kwa hilo tafadhali”akasema Mukasha
“Hilo nitakusaidia lakini si jambo
la haraka kwani linahitaji
mipango.Ninachoweza kukusaidia kwa
sasa ni hifadhi ya familia yako.Wewe na
familia yako mtahamia katika nyumba
yangu na mtakuwa salama pale wakati
mipango mingine ikiendelea.Suala la
kuipeleka familia yako nje ya nchi kwa
wakati huu si suala jepesi na linahitaji
mchakato mrefu na itanilazimu
kuwashirikisha pia wenzangu ili
tulifanye kwa pamoja lakini ili
wenzangu wakubali kukusaidia
unatakiwa utusaidie kitu kimoja”
“Unahitaji niwasaidie kitu
gani?Mukasha akauliza
“Tunataka kukusanya ushahidi wa
kutosha kuhusiana na
Ernest.Tumegundua kwamba ana
mahusiano na haya mashambulio
yaliyotokea jana kwa hiyo tunafanya
uchunguzi ili kupata taarifa na ushahidi
wa kutosha na tumuondoe
madarakani.Wewe umekuwa ni mtu
wake wa karibu,mambo yake mengi
unayafahamu,siri zake nyingi unazijua
unaweza ukatusaidia kufahamu mambo
yake mengi yaliyojificha na sisi
tutakusaidia kwa hilo unalohitaji.Wewe
na familia yako mtakuwa salama na
tukifanikiwa kumuondoa Ernest na
kumfikisha mbele ya sheria wewe
utakuwa ni sehemu ya mchango huo na
hatutakugusa na tutakufanyia mpango
uende kuishi nchi nyingine
ukapumzike.” Akasema Job.
“Nitalifikiria hilo lakini kwa sasa
tuhakikishe kwanza familia yangu
inakuwa salama.Kitu kingine ni
kwamba ili kupata taarifa yoyote toka
kwa Abdu ni lazima niwe na
pesa.Nitakwenda kwake kwa kigezo
kwamba nataka tuzungumze biashara
na nikiwa na fedha ataniamini na
anaweza akanipa taarifa tunayoihitaji”
akasema Mukasha
“Ni kiasi gani unahitaji? Akauliza
Job
“Milioni thelathini zinaweza
kutosha” akasema Mukasha
“Thirty millions?!! Job akashangaa
“Ndiyo si fedha nyingi.Abdu ni
mfanya biashara mkubwa na huwezi
kumwendea ukasema kwamba anataka
mzigo wa laki mbili au tatu.Biashara
zake ni za mamilioni ya fedha.Lengo
hapa ni ili asiwe na mashaka yoyote
kwamba ninachimba taarifa”
“Ni vipi endapo hatakua
anafahamu chochote kuhusiana na mke
wangu? Pesa zetu zitakuwa zimepotea
bure? Akauliza Job
“Job hii ni pata potea.Lazima uwe
tayari kupata au kupoteza.Endapo
anaweza kufahamu chochote itakuwa
sawa kwetu lakini lazima tujiandae
kwamba yawezekana akawa hafahamu
chochote na hapo tutakuwa
tumepoteza.Unatakiwa utafakari na
ufanye maamuzi” akasema Mukasha
“15 millions.Sina zaidi ya hapo”
akasema Job
“Good.So whats next? Mukasha
akauliza
“Kinachofuata kwa sasa mimi na
wewe tunaogozana hadi nyumbani
kwangu,utalala pale na kesho tutaanza
mikakati yetu.Endapo tutafanikiwa
hiyo asubuhi kupata taarifa
ninazohitaji familia yako itahamia
nyumbani kwangu lakini kama
hutafanya juhudi nipate taarifa hizo
you’ll get nothing” akasema Job na
kumtaka Mukasha wainuke
waondoke.Wakaingia garini na
kuondoka
“Ulimwambia Irene adukue simu
ya rais.Nini ulikuwa unahitaji?Job
akamuuliza Mukasha na kumstua sana.
“Umemfahamuje Irene? Akauliza
Mukasha
“Usitake kujua nimemfahamuje
Irene.Just answer my question.Kwa nini
ulimtaka Irene adukue simu ya rais?
Ulikuwa unatafuta nini? Akauliza Job
“Niligundua mpango wa siri wa
kutaka kuniua.Siku ile usiku
uliponikata sikio nilipelekwa hospitali
nikalazwa.Baadae nikafuatwa na Bill
akanieleza kwamba rais amemtuma
anitafute na animalize.Kwa kuwa Bill
alikuwa kijana anayeniheshimu sana
akanisaidia nikatoka haraka pale
hospitali na kwenda
mafichoni,akamueleza Ernest kwamba
nimetoroka.Baada ya kugundua
kwamba rais ananitafuta aniue
nikataka kufahamu mipango yake na
njia pekee ya kufahamau
anachokipanga dhidi yangu ni kwa
kudukua simu yake kujua anaongea na
akina nani na ana mipango
gani.Umefahamuje jambo hili? Akauliza
Mukasha
“Irene aliniambia”
“Amekuambia?Ilikuaje
akakuambia mambo yale ya siri? Do
you know each other? Akauliza
Mukasha .Alishangaa sana
“Ilinimlazimu anieleze ukweli
wote wa kile alichokifanya kwani
ulichomuambia akifanye
kimemsababishia matatizo
makubwa.Hivi sasa hana makazi
anaishi nyumbani kwangu.Usiku huu
nimetoka kuwakomboa wazazi wake
waliokuwa wanashikiliwa mateka.Kuna
jambo aliligundua baada ya kuidukua
simu ya rais na hilo ndilo limemletea
matatizo makubwa ‘
“Oh my God ! what happened to
her? Amegundua jambo gani?Akauliza
Mukasha
“Jambo aliloligundua ni kubwa na
alifanya makosa akamtaarifu Agatha
mke wa rais na hapo ndipo matatizo
yalipoanzia.Agatha na Silvanus
Kiwembe wakawatuma vijana kwenda
kuwateka wazazi wa Irene wakamuua
mtumishi wa ndani na aliyemuokoa
Irene alikuwa Daniel.Ilikuwa bahati
Daniel akamleta kwangu na akanieleza
kilichomsibu.Usiku huu mimi na Daniel
tukaenda kuikoa familia yake na sasa
wako sehemu salama” akasema Job
“Kwa nini ukamuua Daniel wakati
mlikuwa wote katika kuiokoa familia
ya Irene? Akauliza Mukasha
“Daniel alikuwa msaliti na alitaka
kuuza siri zetu kwako na endapo
nisingemuua angeniua mimi.Wasaliti
wote hawana nafasi kwangu” akasema
Job na safari ikaendelea.
KINSHASA – DRC
“Thank you Austin.Sijawahi kuhisi
raha ya kufanya mapenzi kama usiku
wa leo.Sijui nikupe zawadi gani kwa
furaha niliyonayo ya kukutana na
mwanaume kama wewe
unayeyafahamu mapenzi kiasi
hiki.Maria alikosea sana alipotaka
kukuua.Mwanaume kama wewe
unapaswa kulindwa kwa gharama
yoyote” akasema Amarachi wakiwa
wamelala katika zuria baada ya
kuanguka toka kitandani kutokana na
kipute kuwa kikali sana.Austin
akamtazama Amarachi aliyekuwa
mtupu akahisi mwili bado
unamsisimka.Akatabasamu na kusema
“Amarachi kilichotokea hapa
chumbani kitabaki hapa hapa
chiumbani.Hatakiwi kufahamu mtu
mwingine yeyote na wala hatupaswi
kuendelea” akasema Austin
“Austin vyovyote utakavyoamua
ila ukweli utabaki pale pale kwamba
sijawahi kukutana na mwanaume kama
wewe.Nilitekwa na Boko haramu
nikiwa bado mwanafunzi na
kilichokuwa kinafanyika kule msituni
si mapenzi bali ni ubakaji ila leo
nimefanikiwa kufanya mapenzi ila
Austin nina ombi moja kwako”
Akasema Amarachi
“Unataka nini Amarachi?
“Kama mambo haya yatamalizika
na wote tukawa salama naomba
tutafute nafasi walau siku kadhaa mimi
na wewe tuende mahala
tukapumzike.Please dont say no”
akasema Amarachi na Austin
akatabasamu akamvuta Amarachi
kifuani pake akambusu na kusema
“Amarachi sitaki nikuahidi kitu
ambacho siwezi kukitekeleza.Pindi
masuala haya yakimalizika nitapotea
na kwenda kuanza maisha yangu
mapya mbali.I want to try again but far
from here kwa hiyo siwezi kukuahidi
kwamba ninaweza kupata nafasi ya
kupumzika na wewe”akasema Austin
“Austin you’ll go with me!!.Kokote
utakakokwenda I’ll be with you.You
cant live me behind.Ninahisi
amani,salama na furaha nikiwa karibu
nawe kwa hiyo ulipo nami nipo.Potelea
mbali utakavyofikiri kuhusu mimi
lakini siwezi kukubali ukaniacha.Take
me wherever you go.I’ll be your
maid,your slave your
everything”akasema Amarachi.
“Sijawahi kukutana na mwanamke
aliyenitamkia maneno mazito kama
haya.Amarachi nashindwa nikujibu nini
lakini ukweli ni huo kwamba you’ll
never be happy with me,you’ll never
have a normal life and you’ll never be
safe kwa hiyo nakuomba Amarachi
jitahidi kuendelea na maisha yako
nchini Tanzania .You are very happy
there” akasema Austin
“Ndiyo nina furaha lakini
nitakuwa na furaha zaidi endapo
nitakuwa karibu yako.Austin hakuna
neno unaloweza kulitamka likanibadili
mawazo.Tayari nimekwisha fanya
maamuzi.Niko tayari kwa chochote iwe
ni shida iwe ni raha niko tayari kwa
yote lakini lengo langu ni moja tu kuwa
karibu nawe” akasema Amarachi
.Wakatazama kwa muda Amarachi
akauliza
“Do you still love her? Akauliza
Amarachi
“Nani?
“Maria”
“I loved her with all my heart na
siwezi kusema kwamba tayari
nimekwisha mtoa moyoni mwangu
kabisa kwani hili jambo litachukua
muda.Mimi na yeye tulifikia hatua
kubwa sana but I have to let her
go.Hata kama bado ninampenda lakini
mimi na yeye hatuwezi kuwa pamoja
tena.It’s over” akasema Austin
“Amarachi tulale sasa na tujiandae
kwa siku ya kesho.” Akasema Austin
“Austin japo kwa usiku wa leo
naomba nikilaze kichwa changu katika
kifua chako” akasema Amarachi.Austin
akambusu Amarachi ambaye alikilaza
kichwa chake katika kifua cha Austin
taratibu machozi ya moto yakaanza
kukiloanisha kifua cha Austin
“Amarachi unalia nini? Akauliza
Austin
“It’s nothing.Let’s sleep” akasema
Amarachi
“kwa miaka mingi nimekuwa na
ndoto ya kumpata mwanaume mwenye
kunifaa na sasa nimempata Austin
lakini hayuko tayari kuwa na mimi
kwani ameumizwa sana na mahusiano
yake yaliyopita.What am I going to do?
akajiuliza
“Siwezi kumkosa Austin.Huyu ni
mwanaume wangu na ninaamini
kukutana kwetu hakukuwa kwa
makosa.Lazima nihakikishe ninafanya
kila juhudi kumpata.He must be
mine.I’m a fighter na sijawahi kukata
tamaa katika jambo lolote lile na siwezi
kushindwa kupambana kwa ajili ya
Austin.Sintojali kama kuna hatari au
vipi lakini lazima nihakikishe mwisho
wa sakata hili niwe nimempata Austin”
Akawaza Amarachi
“Monica aliwahi kuniambia siku
moja kwamba kuna kitu anakiona kati
yangu na Amarachi.Alinisistiza kwamba
nifanye kila ninaloweza kuwa na
Amarachi kwani ndiye mwanamke
anayenifaa.Naweza kukiri kwamba
alikuwa sahihi.Kweli kuna kitu kipo
kati yetu na leo hii nimethibitisha
hilo.Tulipofanya mapenzi kuna kitu
nimekiona.Nimejisikia hali ya tofauti
ambayo haijawahi kunitokea hapo
kabla.Ninatamani hiki ninachokihisi
kingekuwa kweli lakini siwezi kuingia
katika mahusiano na Amarachi
japokuwa ni mwanamke mwenye sifa
zote na anaonekana tayari ananipenda
japokuwa hajaniambia ila vitendo tu
vinanipa picha kwamba
ananipenda.Sitaki kumuingiza mtoto
mzuri kama huyu katika dunia yangu
na kumfanya aishi maisha ya taabu
yasiyo na furaha.Watu kama mimi
hatuna maisha ya kawaida yenye
furaha.Nimejaribu hilo nikashindwa na
sitaki kumuingiza Amarachi katika
matatizo.Ameteseka sana msituni na
anastahili mwanaume ambaye atampa
furaha anayoitaka na si mimi.Nitajaribu
kuendelea kumuelewesha”akawaza
Austin huku akizichezea nywele za
Amarachi
“Laiti ningekuwa na maisha ya
kawaida naamini Amarachi angenifaa
sana lakini sina maisha ya kawaida
kama wenzangu.Maisha yangu
yamekuwa hivi hivi kutwa kucha mikiki
mikiki.Kama ilishindikana kwa Maria
haitawezekana kwa mwanamke
mwingine tena” Austin akajawa na
mawazo mengi sana kuhusiana na
mustakabali mzima wa maisha yake
.Alikumbuka maisha yake ya nyuma
yalivyokuwa na alipo sasa na taratibu
akahisi kijiusingizi kikimnyemelea
akaanza kusinzia
DAR ES SALAAM - TANZANIA
Kumepambazuka tena
Tanzania.Tayari mitaa na barabara
zilijaa watu alfajiri hii wakiwahi katika
majukumu ya kujitafutia mkate wa kila
siku.Bendera bado ziliendelea kupepea
nusu mlingoti kutokana na siba mzito
uliolIkikumba taifa.Ikulu Dar es salaam
Ernest mkasa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania alidamka
mapema sana akijiandaa kwa ajili ya
safari yakuelekEa Dodoma ambako
miili ya viongozi wote waliopoteza
maisha katika mashambulio
yaliyotokea katika miji ya Dar es
salama na Dodoma itaagwa kitaifa na
kuzikwa.Kitu cha kwanza alichoamua
kukifanya rais asubuhi na mapema ni
kwenda hospitali kutazama hali ya
Agatha mke wake.
“Nashangaa asubuhi hii ninajikuta
nina hamu ya kwenda kumuona
Agatha.That woman is a
witch.Sikupanga kabisa kwena
kumtazama hospitali shetani yule
lakini ngoja nikamtazame nijue
maendeleo yake.Ngoja nijiweke karibu
yake na pengine anaweza kuwa na
jambo la muhimu la kunieleza.Nataka
nifahamu ni namna gani alinusurika
katika shambulio lile? Nitapata taarifa
hizo endapo nitajiweka karibu naye na
kuonyesha kumjali” akawaza Ernest.
Akiwa njiani kuelekea hospitali
akapata taarifa toka kwa mkuu wa
polisi kwamba imeokotwa maiti ya
mkuu wa idara ya usalama wa taifa
Silvanus Kiwembe katika bustani ya
wanyama iliyoko nje kidogo ya jiji la
Dar es salaam.Taarifa hiyo ilisema
kwamba Silvanus aliuwa kwa kupigwa
risasi zaidi ya nane.Sambamba naye
walikuwepo watu wengine kadhaa
waliokutwa wamekufa kwa kupigwa
risasi na mmoja kati ya watu
waliokwisha tambulika ni Daniel Swai
mtoto wa mfanyabiashara
mkubwa.Rais alitaarifiwa kwamba mtu
mmoja aliyejitambulisha kama daktari
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa
mahojiano baada ya kukutwa eneo la
tukio akiwa amefungwa miguu na
mikono na kujazwa matambara
mdomoni.Jeshi la polisi pia
linawashikilia walinzi wa bustani hiyo
kwa ajili ya kusaidia katika uchunguzi.
Hizi zilikuwa ni taarifa mbaya kwa
rais Ernest asubuhi hii ambazo
zilimstua mno
“Nani kamuua Silva? Alikwenda
kufanya nini katika bustani ya
wanyama usiku ? akajiuliza.
“Japokuwa alikuwa ni mfuasi wa
Alberto’s lakini alikuwa ni mtu
niliyemuhitaji sana hasa kwa kipindi
hiki ili kusafisha hali ya mambo.Nani
nitampata ambaye atakuwa upande
wangu na kutii maelekezo yangu?
Akajiuliza
“Nimeumizwa sana na taarifa hizi
za kumpoteza Silva.Sijui nani nitampata
anayeweza kuziba nafasi yake kwa
haraka.Laiti nisingekuwa nimemuweka
Austin katika orodha ya maadui zangu
ningemteua awe mkuu wa idara ya
usalama wa taifa kwani anafaa sana
lakini mambo yamekwisha
haribika.Ngoja nimpigie simu David
Zumo nijue kama alifanikiwa
kuwakamata na kuwaweka kizuizini
Austin na wenzake” akawaza Ernest na
kuchukua simu akampigia David Zumo
“Habari za asubuhi mheshimiwa
rais Ernest” akasema David Zumo
baada ya kupokea simu
“Huku kwema kabisa sijui huko
kwenu” akasema Ernest
“Huku kwema tumeamka salama.”
“David samahani kwa usumbufu
asubuhi hii.Nimekupigia simu
kufahamu kuhusu ule msaada
niliokuomba jana.Je ulifanikiwa
kuwatia kizuizini wale watu? Akauliza
Ernest
“Ernest naomba suala hilo
tulizingumze baadae kidogo kwani kwa
sasa niko katika maandalizi ya mazishi
ya mke wangu .Nitafute baadae jioni ili
tuzungume kwa kirefu zaidi suala hili”
akasema David
“Mheshimiwa rais nafahamu leo ni
siku ngumu sana kwako na hata
kwangu pia kuna mazishi ya kitaifa kwa
wale watu waliouawa katika
mashambulio yale mawili.Ninataka tu
kufahamu kama tayari umewatia
ngvuni ili niwe na cha kuwaambia
watanzania hapo baadae
nitakapohutubia katika mazishi ya
kitaifa.” Akasema Ernest.David Zumo
akabaki kimya.
“David tafadhali nahitaji
kufahamu hilo tu halafu tutazungumza
jioni sote tutakapokuwa
tumetulia.Tafadhali ni muhimu sana
“akasema Ernest
“Wale watu hawako kizuizini”
akasema David
“ What ?!! hawako kizuizini? Kwa
nini David wakati nilikutaarifu kwamba
watu wale ni hatari na wanahusika
katika mashambulizi yaliyotokea
katika miji ya Dar es salaam na
Dodoma?Kwa nini umewaachia huru?
Akauliza Ernest kwa sauti ya ukali
“Sikiliza Ernest.Watu wale
nimewashikilia kama ulivyoniomba
lakini nililazimika kuwahoji mimi
mwenyewe na baadae nikajiridhisha
kwamba watu wale hawakuwa hatari
na wala hawakuhusika katika
mashambulio yale ya Dar es salaam
wala Dodoma.Ninadhani taarifa
ulizopewa na watu wako wa usalama
hazikuwa sahihi.Wasisitize watafute
watu sahihi na si wale hawahusiki
kabisa “
“My God!! Akasema Ernest
“Wako wapi hivi sasa?akauliza
“Kwa hivi sasa siwezi kufahamu
wako wapi kwani waliomba ruhusa ya
kuendelea na sfari na nikawaruhusu
waendelee na safari yao na sijui
wameelekea wapi ” akasema David
Zumo
“David umefanya kosa kubwa sana
kuwaachia wale jamaa ambao sisi
tunafahamu na tunamini kwamba ni
watu hatari sana kwa usalama wa nchi
yetu na wanahusika katika
mashambulizi yale ya mabomu.Naomba
nikuache kwa sasa ila nitakupigia simu
baadae jioni tuongee zaidi.Naomba
ufahamu kwamba sijafurahishwa na
kitendo ulichokifanya kwani
umeshindwa kumsaidia rafiki yako
wakati ana shida.Kwa heri kwa sasa”
akasema Ernest na kukata simu kwa
hasira
“Oh my God !! mambo gani haya
yananitokea? Mbona siku imeanza
vibaya namna hii? Kwa nini David
anifanyie hivi wakati nilimuomba na
tukakubaliana vizuri kabisa na
akaahidi kuwakamata akina Austin.I’m
confused.Sielewi nitafanya nini
kuwapata tena.They are gone.Hati ya
muungano imekwenda na Tanzania
imekwenda.!! Akawaza
“Zote hizi ni jitihada za
Austin.Anamtumia sana Monica na
ndiyo maana wamefanikiwa hadi
kumrubuni David Zumo.Je ni kweli
amewafanyia mahojiano kama
anavyodai? Kama amewafanyia
mahojiano ni wazi lazima watamueleza
ukweli na David akiufahamau ukweli
itakuwa mbaya sana kwa upande
wangu.Nitafanya nini kuliweka sawa
jambo hili? Akawaza
“Hakuna nman ninatavyoweza
kuliweka sawa suala hili bila kuipata
hati ya mungano.Suala hili tayari
limevuka mipaka na linahitaji hatua za
haraka sana kabla halijasambaa na
kuniletea mimi matatizo
makubwa.Ninaheshimika na marais wa
nchi zote za Afrika na endapo
watagundua kwamba nimehusika
katika kupanga mashambulizi yale sijui
nitaiweka wapi sura yangu.Lazima
nichukue hatua za haraka sana kwani
nikiliacha suala hili litanishinda na kila
nilichokifanya kitakuwa hakina
maana.” Akaendelea kuwaza rais
“Nilimlaumu bure Jenerali Lameck
kwa mpango wake wa kutaka kuilipua
ndege ile kabla haijavuka mpaka wa
Tanzania lakini ulikuwa ni mpango
mzuri.Ni bora ndege ile ingelipuliwa
angani na kuwaua wote waliokuwamo
mle ndani .Sioni tena faida ya Monica
kwani ni kwa sababu yake haya yote
yametokea.Austin amegundua udhaifu
wangu uko kwa Monica na anamtumia
kama fimbo ya kunichapia.Nikiendelea
na udhaifu huu nitajikuta pabaya
sana.Kuanzia sasa Monica naye
ninamjumuisha katika orodha ya wale
watu wangu wa hatari kwa kuwa
amechagua mwenyewe kujiunga na
akina Austin.Hali ilikofika si kuzuri na
siwezi tena kukubali Monica atumike
kunibomoa.Nitambomoa yeye kabla
lengo lake na wenzake halijatimia”
“Mzee tumefika” ilikuwa ni sauti
ya mlinzi wake aliyemtaarifu rais
kwamba tayari wamefika
hospitali.Kutokana na mwazo mengi
aliyokuwa nayo hakukumbuka kama
walikuwa wamewasili
hospitali.Alishuka na kuingia katika
chumba alicholazwa mke wake.
“Vipi Agatha unaendeleaje? Ernest
akamsalimu mkewe
“Ninaeendelea vizuri.Vipi wewe
unaendeleaje?Mbona naona kama
hauko katika hali yako ya kawaida?
Akauliza Agatha lakini Ernest
hakumjibu kitu
“Una tatizo gani Ernest? Tafadhali
nieleze nifahamu pengine ninaweza
kukusaidia hata kimawazo” akasema
Agatha.Ernest akawatoa nje walinzi
akabaki peke yake na Agatha.
“Silva na watu wengine kadhaa
wamekutwa wamekufa katika bustani
ya wanyama nje ya jiji” Ernest
akamwambia Agatha
“Umapata wapi taarifa hizo?
Akauliza Agatha
“Nimepigiwa simu asubuhi hii na
mkuu wa polisi.Hizi nitaarifa mbaya
sana ambazo sikuwa
nimezitegemea.Ninajiuliza Silva
alikwenda kutafuta nini kule katika
bustani ya wanyama usiku? Nani
kamuua? Nimechanganyikiwa Agatha”
akasema Ernest
“Ernest nimeambiwa na
madaktari kwamba jioni ya leo
ninaweza kuruhusiwa kurejea
nyumbani.Nikitoka nitakuja kukusaidia
katika wakati huu mgumu ulio
nao.Unahitaji mtu wa kukusaidia na
ninakuomba unipe nafasi
nikusaidie.Nafahamu mimi na wewe
tuna tofauti zetu lakini naomba
tuziweke tofauti pembeni kwa sasa na
tuunganishe nguvu.Ernest mimi ni mke
wako na unapaswa kuniamini kuliko
mtu mwingine yeyote.Kuna mambo
mengi yanayoendelea hivi sasa ambayo
huyajui.Kuna mambo ninayafahamu
ambayo ni ya hatari kwako.Nipe nafasi
nikusaidie na kwa pamoja tuweze
kulimaliza suala hili linaloendelea”
akasema Agatha
“Agatha nashukuru kwa kujali
matatizo niliyonayo lakini its hard to
trust you again.Mambo uliyonifanyia
yananifanya nishindwe kukuamini
tena. Usijali ninao watu wa kutosha wa
kulishughulia suala hili.Wewe
unapaswa upumzike” Akasema rais
Ernest na kumtazama Agatha aliyetaka
kusema kitu lakini kabla hajatamka
akamuwahi
“Leo ni mazishiya kitaifa ya wale
wote waliouawa katika mashambulio
yale kwa hiyo muda mfupi ujao
nitaelekea Dodoma na baada ya
shughuli ya kuaga miili ya wabunge na
viongozi mbali mbali nitaelekea
Zanzibar kwa ajili ya kuongoza mazishi
ya makamu wa rais.Nitakuwa na siku
ndefu sana.Utakapo ruhusiwa kutoka
hospitali utaenda moja kwa moja ikulu
na utanisubiri hadi nirudi” akasema
Ernest
“ Ahsnate sana Ernest kwa kuja
kunitembelea.Kuna jambo moja nataka
nikuombe.Kuwa makini sana na watu
unaofanya nao kazi.Kuna watu
wanakuzunguka” akasema Agatha na
kumstua Ernest
“ Kwa nini unasema hivyo Agatha?
“Kuna jambo kubwa
tutazungumza jioni ukirejea”akasema
Agatha na Ernest akaondoka kurejea
ikulu
“Kuna kitu kikubwa Agatha
anakifahamu na ili kukijua natakiwa
kuendelea kujiweka karibu
yake.Ameniomba nimuamini na
kumshirikisha katika mambo yangu
lakini siwezi kufaya hivyo hata
kidogo.Yule mwanamke ni shetani na
hafai kabisa kuwa na ushirika naye
wowote.Ninajifanya kuwa karibu naye
na kumjali ili nifahamu kile ambacho
anakifahamu kuhusiana na shambulio
lile na alinusurika vipi? Nikifahamu
hayo nitamuondoa haraka
sana.Hatakiwi kuendelea kuwa hai yule
mwanamke” akawaza Ernest
“Ernest kabadilika
sana.Nitajiweka karibu nami kujifanya
nimebadilika ili aweze kuniamini tena
na baada ya kuniamini nitaanza awamu
ya pili ya kuotesha upya mbegu ya
Alberto’s hapa Tanzania kwani mimi
ndiye niliyepewa jukumu hilo” akawaza
Agatha na kuyakumbuka maneno ya
Alberto mkuu aliyomwambia
alipompigia simu usiku wa jana.
“Usiku kucha nimekuwa
ninalifikiria jambo lile alilonieleza baba
Alberto mkuu jana.Kuwa kiongozi wa
Alberto’s si jambo dogo na hasa kwa
nchi yenye changamoto nyingi kama hii
lakini sina namna ya kufanya kwani
tayari nimekwisha muhakikishia
Alberto mkuu kwamba nitaifanya kazi
aliyonipa.Kwa sasa ngoja njiweke
karibu na Ernest ili kulifanikisha jambo
hili” akaendelea kuwaza
Ernest Mkasa alifika ikulu na mtu
wa kwanza kuonana naye alikuwa
Jenerali Lameck Msuba ambaye aliwahi
sana kufika.Kama kawaida yao
wakaenda katika chumba cha maongezi
ya faragha
“Lameck kuna habari yoyote mpya
umeipata? Akauliza rais
“ Hakuna habari yoyte mpya .Sijui
kwako”
“Ninazo habari kadhaa .Kwanza
Agatha amepatikana”
“ Amepatikana ? Alikuwa wapi?
“ Bado hatujazungumza ila
amejeruhiwa mguu kwa risasi na
amelazwa hospitali.Nimetoka
kumtazama asubuhi hii anaendelea
vyema.Baadae jioni nitapata nafasi ya
kuzungumza naye ili nifahamu
alinusurikaje katika shambulo
lile,alikuwa wapi na ani kamshambulia
jana”akasema Rais Ernest
“Do you trust her mr President?
Akauliza Lameck
“I don’t.Nimejiweka karibu naye
kwa sasa ili kufahamu hadithi yake
aliokoka vipi katika shambulio
lile?Baada ya kuisikia hadithi yake
tutatafuta namna ya kummaliza kwani
ni mtu hatari sana kwetu.Jioni ya leo
naamini atanieleza kila kitu na mimi
nitakujulisha atakachoniambia.”
Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Jambo la pili ni kifo cha Silvanusi
Kiwembe.”
“Nimezipata taarifa hizi za kifocha
Silva nimestuka sana” akasema Lameck
“Hata mimi nimestuka
sana.Najiuliza imetokeaje? Alikwenda
kutafuta nini kule katika bustani ya
wanyama usiku? Nani kamuua na kwa
nini? Ninajiuliza maswali mfululizo
toka nilipopata taarifa hizi na sijapata
jibu.Kuna watu kadhaa tayari
wanashikiliwa na pengine
watakapohojiwa kuna kitu
kitapatikana.Lakini hili ni pigo kubwa
kwetu kwani alikuwa ni kiungo
muhimu sana .Alifanya kila kazi
aliyopewa bila kuhoji.Sijui tutampata
wapi mtu kama yule wa kushika nafasi
yake” Akasema Ernest
“Kweli ni pigo kubwa mheshimiwa
rais.Waliofanya jambo hilo la kinyama
lazima wapatikane haraka sana”
akasema Lameck
“Tukiachana na suala hilo la Silva
ambalo jeshi la polisi
wanalishughulikia ,kuna jambo lingine
ambalo limeifanya siku hii ianze vibaya
sana.”akasema rais na kunyamaza
akamtazama Lameck
“Ulikuwa sahihi kutaka kuilipua
ile ndege ya David Zumo.Ni afadhali
ndege ingelipuliwa na wote wakauawa
kuliko hiki kilichtokea.”
“Nini kimetokea mheshimiwa
rais?
“ David Zumo amewaachia akina
Austin na Yasmin wameenda zao”
“That’s not true!! Akasema
Lameck kwa mshangao
“Its true.Nimezungumza naye
asubuhi na amenieleza kwamba eti
aliwahoji na akaona hawana kosa lolote
akaamua kuwaachia wakaondoka zao
na hajui wameelekea wapi.Lameck hili
ni pigo lingine kubwa kwetu.Nilikuwa
na mategemeo makubwa kwa David
Zumo atawazuia akina Yasmin na
nilitegemea labda leo tungeweza
kuirejesha hati ya muungano lakini
imekuwa tofauti.Matumaini hayo
hayapo tena na sina hakika kama
tutafanikiwa kuipata tena hiyo hati
kwani hatujui sehemu ya kumtafutia
Yasmin.Ametuzidi akili.Ninajilaumu
sana kwa kupuuza ushauri wako na
kuziondoa zile ndege jana na yote haya
yamesababishwa na mapenzi makubwa
niliyonayo kwa Monica.Austin
ameugundua udhaifu wangu kuwa ni
Monica na anamtumia kufanikisha
mipango yake”akasema rais
“Hata mimi nimechanganyikiwa
mheshimiwa rais na sielewi tutafanya
nini kuwapata tena kama tayari
wamevuka Congo.Lakini kama
ulivyosema kwamba haya yote
yamesababishwa na Monica na
inawezakena hata Monica ndiye
aliyemshawishi David Zumo awaachie
huru akina Yasmin.Amefanya jambo
baya sana”
“Kwa hapa tulipofika imenilazimu
kufanya maamuzi magumu.Kushindwa
kwetu kumesababishwa na Monica kwa
hiyo naye anaingia katika orodha ya
watu hatari kwetu.Sintojali kama ni
mwanangu ama vipi lakini kuanzia sasa
hataonewa huruma hata kidogo na
kama tutalazimika kuua na yeye akiwa
miongoni mwa watu tunaotaka kuwaua
hakuna huruma ni kumuondoa
tu.Siwezi kujiharibia mwenyewe
sababu ya kumtetea mwanangu ambaye
hata hafahamu kama mimi ni baba yake
” akasema Ernest
“Lakini mheshimiwa rais
nilikutaarifu jambo hili mapema sana
na laiti kama ungelipa uzito unaostahili
tusingefika hapa tuipofika.”akasema
Lameck
“Uko sahihi Lameck.Ninajilaumu
sana kwa ujinga nilioufanya.Kwa sasa
inabid tuje na mikakati mipya namna
ya kufanya ila kuna jambo ninataka
kulifanya”akasema
“Ni jambo gani mzee?
“David Zumo anadai kwamba
amewahoji akina Yasmin na akagundua
kwamba hawana kosa na wala
hawahusiki kwa namna yoyote katika
mashambulio yale kwa hiyo
akawaachia huru.Nina wasi wasi
watakuwa wamemueleza David kila
kitu wanachokifahamu na hii itakuwa
mbaya zaidi kwetu.Nina wasi wasi sana
kwa namna David alivyokuwa
akizungumza kuna jambo tayari
amekwisha ambiwa kwa hiyo kuna kitu
kimoja tu ninakifikiria kifanyike”
“Ni kitu gani mzee? akauliza
Jenerali Lameck
“ Nataka kumuondoa David
madarakani”
Chumbani kukawa kimya
wakabaki wanatazamana.Baada ya
muda Lameck akauliza
“Utamuondoa madarakani kwa
kivpi mzee?
“Tutaiangusha serikali yake”
Jenerali Lameck akafikiri kwa
muda halafu akasema
“Mheshimiwa rais jambo hilo
ulilolitamka ni jambo zito sana na
utekelezaji wake si rahisi.David Zumo
ni rais mwenye ulinzi mkali mno.Licha
ya………….”
“Lameck bado tunao muda wa
kulijadili suala hili.Nimeona nikueleze
mapema ili kwa siku nzima ya leo
ufikirie njia mbali mbali tunazoweza
kufanya ili kumuondoa David
madarakani na jioni ya leo
tutakapokutana basi tutalijadili kwa
kirefu zaidi” akasema Ernest
‘Mheshimiwa rais lakini
ninakushauri jambo moja.Usifikirie
tafadhali kuanzisha mgogoro mwingine
mkubwa kwa kuiangusha serikali ya
David Zumo.Utaiingiza nchi katika
matatizo makubwa kuzidi hata haya
tuliyonayo sasa.Tutafute njia nyingine
ya kuweka sawa mambo yetu na kama
nchi inakwenda kugawanyika let it be
lakini si kuingia katika mgogoro na
David Zumo.Nakuomba sana mzee
lifikirie hilo jambo” akasema Jenerali
Lameck
“Lameck ushauri wako ni mzurio
lakini kwa hapa ilipofika hakuna
namna zaidi ya kumuondoa David
Zumo madarakani.Tutajadili baadae
jioni.Kwa sasa tujiandae na safari ya
kuelekea Dodoma” akasema rais na
wakatoka katika kile chumba.
“David Zumo lazima nimuondoe
madarakani.Pamoja na hili alilolifanya
la kuwaachia huru akina Yasmin lakini
sitaki kabisa awe na ukaribu na
mwanangu Monica ambaye tayari
amempa mimba kwa hiyo lazima
nihakikishe ninampoteza.Sitaki damu
yangu ichanganyike na ya David
Zumo….” Akawaza rais Ernest na
kusimama kidogo baada ya simu yake
kuita.Akatazama mpigaji akastuka na
kuipokea.
‘Hallow naomba unipe dakika tatu
nitakupigia” akasema rais na kuikata
ile simu
“Mambo yameanza.Habib anataka
kunieleza nini? akawaza
Alistuka sana kwa simu ile ya
Habib asubuhi ile.Haraka haraka
akaelekea chumbani kwake
“Habib Amenistua sana.Najua
atauliza kuhusu akina Yasmin na mimi
sina jibu la kumpa” akawaza na kuvuta
pumzi ndefu
“Ngoja nimpigie nisikie
anachokitaka” akawaza na kumpigia
Habib
“Mheshmiwa rais habari za
asubuhi”akasema habib
“Habari za asubuhi nzuri ”akajibu
rais
“Mheshimiwa rais nimekupigia si
kwa kutaka taarifa za Yasmin au hati ya
muungano kwani najua ni uhuni
umenifanyia na hauko tayari kuitoa
hati hiyo.Nimekubali kushindwa katika
hilo lakini kuna jambo nataka
nikueleze.Kuna mtu anakuja Tanzania
leo hii anaitwa Bashar bin
Abdulsalaam.Anakuja na ujumbe
mzito.Mpokee na uupokee ujumbe
anaokuja nao uufanyie kazi.Endapo
utaupuuza nchi ya Tanzania itaingia
katika vilio visivyokwisha.Kila nyumba
Tanzania italia machozi kwani
tutafanya mashambulio karibu kila siku
katika sehemu mbali mbali.Uwezo huo
tunao na wewe unalifahamu hilo na
tayari tumekwisha anza maandalizi na
hadi hivi nikwambiavyo Alshabaab
wako Tanzania na wanasubiri amri
yangu tu ili kutekeleza mashambulizi
kwa hiyo usitake tuiharibu
Tanzania.Fuata maelekezo katika
ujumbe utakaopewa na Bashar ili nchi
yako iwe salama” akasema Habib
“Habib tafadhali usijaribu
kunitisha.Unafahamu kabisa mimi
sipendi vitisho na jeshi langu linaweza
likawashambulia na kuwasambaratisha
kabisa kwa hiyo msithubutu kufanya
shambulio lolote katika ardhi ya
Tanzania!!
“Mheshimiwa rais nadhani
unatusikia tu na bado haujatufahamu
vyema.Ngoja nikuonyeshe kidogo tu
nguvu yetu.Nitakupigia tena baada ya
dakika kumi” akasema Habib
“Habib!! Habib !! akaita Ernest
lakini tayari simu ilikwisha katwa.
“Huyo mtu anayetumwa kwangu
anataka nini? Ni vipi endapo atakuwa
ametumwa kuja kuchukua hati ya
muungano? Ni vipi kama vitisho vya
Habib vikawa vya kweli na wakafanya
mashambulio mfululizo hapa Tanzania
na kuharibu hali ya amani na utulivu?
Akajiuliza
“Ninajuta kuwashirikisha watu
kama hawa katika mipango
yangu.Sikujua kama mambo yangefika
hapa yalipofika.Niliupuuza ushauri wa
Lameck aliyenisihi nisithubutu
kuwashirikisha Alshabaab kwani
madhara yake ni makubwa…”
Ghafla kikasikika kishindo
kikubwa cha mlipuko.Mlango wa
chumba cha rais ukapigwa na
makomando wanaomlinda rais
wakaingia na kumchukua rais
wakamkimbiza katika nyumba ya siri
inayotumika endapo kutatokea
mashambulizi yoyote katika jengo la
ikulu.Ernest Mkasa alikuwa
anatetemeka kutoka na ukubwa wa
kishindo kile
“Nini kimetokea? Akauliza.walinzi
wake hawakumjibu kitu kwani hata
wao pia hawakufahamu nini hasa
kilichotokea.
“Jamani niambieni nini
kimetokea? Akauliza tena lakini
hakujibiwa hadi alipofikishwa katika
nyumba ya siri iliyo chini ya jengo la
ikulu mahala ambako panaaminika ni
salama zaidi.Ernest
alichanganyikiwa.Baada ya dakika tano
akafahamishwa kwamba kumetokea
mlipuko unaosadikiwa ni bomu katika
soko la samaki la kimataifa lililo karibu
na ikulu.Taarifa hiyo ilisema kwamba
mlipuko huo ulioua watu kadhaa
ulitokea baada ya watu moja lililobeba
mlipuko kulikaribia gari lililokuwa
limebeba samaki na kuzingirwa na
watu wengi waliokuwa wananunua
samai hao.
“Oh my God !!! akasema rais
akajiinamia na kushika kichwa na mara
simu yake ikaita.Akatazama mpigaji
alikuwa Habib.Akawaomba watu wote
watoke mle katika chumba na
wamuache peke yake aongee na
simu.Aliitazama simu ile ikiita na
kukatika ikaanza kuita tena akaipokea
“Mheshimiwa rais nadhani tayari
umepata salamu zangu.Nimetaka
nikuonyeshe uwezo wetu .Kama
tumeweza kufanya shambulio karibu
kabisa na ikulu yako hatuwezi
kushindwa kushambulia sehemu
nyingine yoyote kwa hiyo tafadhali
sana usicheze na sisi.Mashambulio
kama haya yataendelea kutokea
sehemu mbalimbali za nchi yako na
mamia kwa mamia ya watanzania
watapoteza maisha kila uchao endapo
hautakuwa tayari kufanya kile
tunachokuamuru .Tafadhali mpokee
mjumbe anayetumwa kwako na
umsikie alichotumwa” akasema Habib
na kukata simu.Uso wa Ernest mkasa
uliloa jasho.
KINSHASA - DRC
Mlango wa chumba walimolala
akina Austin ukagongwa na
kuwastua.Tayari kumekucha.Austin
akajiinua kitandani na kwenda
kuufungua mlango akakutana na sura
iliyojaa tabasamu pana ya Monica
“Goodmorning .can I come in?
akasema Monica huku akicheka
kidogo.Austin akamkaribisha ndani.
“Mhh !! kulikuwa na shughuli pevu
humu ndani jana usiku” Akawaza
Monica baada ya kuona namna vitu
vilivyokuwa vimeparaganyika mle
chumbani .Amarachi akaamka baada ya
kusikia sauti ya Monica
“Monica;’akasema Amarachi
akionekana kuwa bado na usingizi
mzito.
“Goodmorning
Amarachi.Umelalaje?Are you
comfortable? Akauliza Monica
‘We’re fine.Ahsante sana kwa kila
kitu Monica” Akasema Austin
“Nimekuja kuwajulisha kuwa leo
ni mazishi ya Pauline Zumo mke wa
David Zumo kwa hiyo
nitahudhuria.Litakuja gari kunichukua
baadae saa tatu za asubuhi kuelekea
mahala shughuli za mazishi
zitakapofanyika.Nadhani ninyi
mtaendelea kupumzika hapa .Jioni
David atakuja na tutalizungmza lile
suala letu.Hapa kuna wahudmu wengi
watawahudumia kila kitu
mnachokihitaji na ninawaomba
mjisikie nyumbani.You guys have been
through a lot so its your time to enjoy”
akasema Monica
“Monica ahsante sana na
tunakuombea kwa Mungu azidi
kukubariki.Hili ulilolianya ni jambo
kubwa kwa nchi yako” Akasema Austin
“Ahsante.Uliwasiliana na Job?
Akauliza Monica
“Hapana ninataka kuwasiliana
naye asubuhi hii kujua kama
wamefanikiwa kuwakomboa wazazi wa
Irene.” Akasema Austin.Monica akatoka
huku akimkonyeza Amarachi
aliyekuwa amekaa kitandani na wote
wawili wakatabasamu.
“Good morning Amarachi”
akasema Austin baada ya Monica
kutoka
“Goodmorning
Austin.Unajisikiaje?
“Ninajisikia vizuri sijui wewe”
“Hata mimi najisikia vizuri
mno.Sijawahi kuamka nikiwa najisikia
vizuri kiasi hiki.Thank you for the last
night.Ni wewe uliyesababisha niwe na
usiku mzuri ambao sijawahi kuupata
katika maisha yangu’ akasema
Amarachi.Austin akatabasamu na
kusema
“Wake up Amarachi.Ni muda wa
kujiandaa kuikabili siku”
“Austin bado ni mapema
mno.Please come to bed.Hatuendi
kokote leo hii.Let’s enjoy the morning”
akasema Amarachi
“Nahitaji kuwasiliana na Job kujua
kinachoendelea Dar es salaam”
Akasema Austin na kwenda katika
meza ya simu akaziandika namba za
simu za Job akapiga.
“Hallow” akasema Job baada ya
kupokea simu
“Hallow Job ,Austin hapa
ninaongea”
“Austin. Mambo yanakwendaje
huko ? Mko salama kabisa? Akauliza
Job
‘Tuko salama Job .Tulifika salama
japokuwa tulipata misuko suko
njiani.Jamaa waligundua kwamba
tumepanda ndege ya David Zumo na
zikatumwa ndege vita kutufuata na
zilikuwa tayari kutushambulia
ikamlazimu Monica ampigie simu rais
na kumfahamisha kwamba tunataka
kushambuliwa na ndipo ndege zile
zikaondoka.Kama haitoshi rais
akawasiliana na David Zumo
akamuomba atuweke kizuizini pindi
tukiwasili Kinshasa.Ndege ilitua katika
uwanja wa kijeshi na tukachukuliwa
tukapelekwa kizuizini katika kambi ya
jeshi.Tunamshukuru Monica kwani
alitusaidia na tukafanikiwa kutolewa
tukazungumza na David Zumo
tukamueleza ukweli wote,ametuelewa
na ameahidi kutusaidia.Hapa tulipo
tupo katika jengo moja kubwa lenye
ulinzi mkali na siku ya leo tutashinda
hapa hadi jioni kusubiri kuongea na
David Zumo.Tutakutaarifu kila
kitakachokuwa kinajiri huku.Vipi huko
Dar es salaam kuna habari gani?
akauliza Austin
“Huku tumepiga hatua.Jana
tumefanikiwa kuwakomboa wazazi wa
Irene na nimewaleta hapa nyumbani
kwa ajili ya usalama wao.”
“Safi sana.Mlifanikiwa
kuwafahamu ni akina nani waliokuwa
wamewateka wazazi wa Irene? Austin
akauliza
“Alikuwa ni Agatha mke wa rais
pamoja na Silvanus Kiwembe mkuu wa
idara ya usalama wa taifa.Walihitaji
kufahamu Irene alifahamuje kuhusu
lile shambulio? Tulifanikiwa
kuwakomboa wazazi wa Irene lakini
kuna mambo yalitokea.Silvanus
Kiwembe mkuu wa idara ya usalama
wa taifa alifariki,Agatha akafanikiwa
kutoroka.Daniel pia amefariki dunia.I
killed him!!
‘You killed him? Austin
akashangaa
“ Yes I did.Daniel ni mtu mbaya
sana na sikupata nafasi ya kukueleza
sifa zake.Ni wakala wa mashirika ya
kijasusi na amekuwa akijipatia fedha
nyingi kwa kuuza taarifa mbali mbali za
siri na nilimgundua akiwasiliana na
Mukasha akimueleza kwamba anazo
taarifa nyeti anataka kumuuzia”
“dah ! akasema Austin
“One more thing” akasema Job
‘Jana usiku nimefanikiwa
kumnasa tena Mukasha kwa kutumia
simu ya Daniel.Yuko tayari kutusaidia
kupata taarifa na ushahidi wa kuweza
kumuondoa Ernest madarakani lakini
ameomba ulinzi kwa familia yake.Yuko
hapa kwangu na ninawasubiri ninyi
mrejee kutoka Kinshasa ili tujadili kwa
upana zaidi hili suala lake na tuona
atatusaidia vipi”
“Mukasha again? Austin akauliza
‘Ndiyo Austin.Kwa sasa yeye na
Ernest si marafiki tena na amekuwa
kama mkimbizi na tunaweza kutumia
fursa hiyo kupata taarifa muhimu
kuhusu Ernest zinazoweza
kutusaidia.Kumbuka huyu ni mtu wake
wa karibu na anafahamu mambo yake
mengi” akasema Job
“Job una hakika umemchukua
tena Mukasha kwa sababu hiyo
uliyoieleza au kuna sababu nyingine
binafsi? Akauliza Austin
“Both.Austin katika yale
mashambulio ya juzi,Yule jamaa dogo
Bill ambaye alikuwa na taarifa za
kuhusu mahala aliko mke wangu ni
miongoni mwa waliofariki kwa hiyo ni
Mukasha pekee anayeweza kunisaidia
kupata walau mwanga mahala aliko
mke wangu.Asubuhi ya leo atanipeleka
kwa mtu mmoja ambaye ni rafiki
mkubwa wa Bill na tunategemea
tunaweza kupata taarifa kuhusu
mahala aliko mke wangu.Utanisamehe
kwa kuongeza kazi nyingine lakini sina
namna lazima niitumie fursa hii
kumtafuta mwanangu Millen”Akasema
Job.Austin akafikiri kidogo na kusema
“Sawa Job.Endelea na hiyo
operesheni na endapo kutakuwa na
tatizo lolote usisite kunijulisha kupitia
namba hii ya simu niliyotumia
kukupigia.Chukua tahadhari kubwa”
akasema Austin halafu wakaagana.
“Akina Job walifanikiwa
kuwakomba wazazi wa Irene jana
usiku” Austin akamwambia Amarachi
“Austin uliniahidi kuniweka wazi
kuhusiana na suala la Irene.Ana
matatizo gani? Amarachi
akauliza.Austin akaketi karibu yake
akamsimulia kila kitu kuhusu Irene.
“Siamini kama rais amefika
mahala hapa.Kumbe mashambulio yale
yote ni mipango yake!!!Austin damu za
watu wasio na hati zimepotea na
tunapaswa kufanya kila tuwezalo
kuhakikisha rais Ernest anafikishwa
mbele ya sheria.!!
“Ni kweli Amarachi.Lazima yeye
na washirika wake wafike mbele ya
sheria” akasema Austin
“Lakini kwa nini aamue kuua watu
wengi kiasi hiki? Akauliza Amarachi
“Swali kama hilo hata mimi
nimekuwa nikijiuliza mara nyingi na
kuna kitu ninakihisi.Endapo yeye ndiye
kweli anahusika katika mashambulio
yale basi dhumuni lake kubwa ni
kuwaangamiza Alberto’s kwani
ukitazama kwa haraka haraka
utagundua kwamba waliokuwamo
ndani ya hoteli ile iliyoshambuliwa Dar
es salaam wengi ni Alberto’s.Ukiacha
Dar kule Dodoma bungeni kuna idadi
kubwa ya Alberto’s na ninahisi aliamua
kulilipua jengo la bunge ili kuwaondoa
kabisa Alberto’s.Yawezekana lengo lake
llikuwa jema na zuri la kuwaondoa
Alberto’s Tanzania lakini hakupaswa
kutumia njia hii ya kufanya
mashambulio kwani miongoni mwa
waliofariki walikuwemo pia watu
wema wasio na hatia yoyote.Tukubali
njia aliyotumia haikuwa sahihi na hivyo
anahesabika kama ni muuaji na
anapaswa ashtakiwe kwa kosa hilo.”
Austin akakatishwa na muhudumu
aliyegonga kengele ya mlangoni
.Austina akaenda kuufungua na
muhudumu alitaka kufahamu kila
mmoja angependa kutumia kitu gani
katika mlo wa asubuhi.
“kweli hapa tumefika katika
himaya ya kifalme.Sijawahi
kuhudumiwa na wahudumu
wachangamfu na wenye adabu kubwa
kama hawa” akasema Austin halafu
akaelekea bafuni kuoga.Akiwa bafuni
mlango ukafunguliwa akaingia
Amarachi.Bila aibu akaliachia taulo
likaanguka chini akabaki mtupu na
kuyaamsha upya mashetani ya
Austin.Ikulu kukakasirika ghafla.
“This is the good way to start a
day” akasema Amarachi na kumfuata
Austin akaikamata ikulu kwa mikono
yake laini akaanza kuichezea na kuzidi
kuipandisha hasira.Austin hakupoteza
muda akaanzisha mtanange wa asubuhi
humo humo bafuni.Ilikuwa ni asubuhi
njema sana kwao.Baada ya kipute kile
cha kuanzia siku kumalizika wakaoga
pamoja
“Ni heri nikakosa kila kitu lakini si
kumkosa Austin.This man is my
world.Nadhani nilipangiwa nipitie
mateso makali na baadae nije nianze
maisha ya furaha na kusahau magumu
yote niliyopitia na Austin ndiye furaha
yangu.Huyu pekee ndiye anayeweza
kunisahaulisha machungu yote
niliyopitia.I’ll figt for him.Nitapambana
na yeyote hadi nihakikishe nimepata
nafasi ndaniya moyo wake.Upatapo
bahati ya kumpata mwanaume kama
huyu usikubali akakuponyoka na
ndivyo nitakavyofanya” akawaza
Amarachi wakati wakioga
Kisha oga wakaenda kuungana na
akina Yasmin kwa ajili ya chakula cha
asubuhi
“Wote mmeamka salama? Austin
akawauliza akina Yasmin
“Tuko salama.” Akajibu Yasmin.
Walipata kifungua kinywa na
baada ya kumaliza Austin akasema
“Yasmin suala lenu
linashughulikiwa.Tayari rais David
Zumo amekubali kuwasaidia na kama
mnavyofahamu huyu ni mtu tajiri sana
na nchi nyingi zinamuheshimu kwa
hiyo ni rahisi kwake kupata mahala
ambako mnaweza kwenda kuishi na
kuanza maisha yenu mapya.Pindi
mambo yakikaa tayari nitakujulisha ila
naendelea kusisitiza kwamba uwe na
uhakika kwamba hati ile ipo na si
kunidanganya.Kwa juhudi zote hizi
tunazozifanya halafu nigundue kwamba
ulikuwa unanidanganya nakuapia
nitakuteketeza wewe na familia yako
bila huruma” akasema Austin huku
Maria na Boaz wakimtazama kwa woga
“Usiwe na hofu Austin.Ninafahamu
nini maana ya makubaliano na katu
siwezi kukudanganya katika jambo
kubwa kama hili.Uwe na amani na
endelea kukamlisha mambo .Kila kitu
kikiwa tayari nitakuelekeza mahala
hati ilipo” akasema Yasmin na Austin
akainuka
“Austin ninaweza kuzungumza
nawe kwa dakika chache? Akauliza
Boaz na Austin akakubali wakasogea
karibu na bwawa la kuogelea.
“Austin my son” akasema Boaz na
Austin akamkatisha
“Don’t call me your son” akasema
Austin kwa ukali
“Sawa Austin hata kama ukikataa
nisikuite hivyo lakini kwangu utabaki
kuwa mwanangu kwani nimepata
nafasi ya kuishi nawe na kukulea kama
mwanangu.Tuachane na hayo nataka
kuzungumza nawe jambo dogo la
muhimu” akasema Boaz na kumtazama
Austin kwa makini halafu akaendelea
“Nafahamu mimi na wewe kwa
sasa hatuna mahusiano mazuri.Kama
binadamu ninakiri nimekukosea sana
na haya yote yanayonikuta sasa hivi
ninayastahili.Kwa muda ulionifunga
katika kile chumba nimejitafakari sana
kuhusu maisha yangu na nimegundua
namna nilivyokuwa naenenda katika
njia mbaya.Nimewakosea watu wengi si
wewe peke yako lakini kwa niaba yao
wote nataka nikuombe samahani
wewe.Nafahamu ni vigumu kwako
kunisamehe lakini nakuhakikishia
kabisa kwamba toka ndani ya moyo
wangu nimeyajutia makosa
yangu.Ninashukuru kwa kunipa tena
nafasi nyingine kuanza maisha
mapya.Sikuwa nimetegemea kabisa
kama ningeipata nafasi hii.Endapo
tutafanikiwa katika mpango huu na
tukaenda nchi za mbali nataka nibadili
maisha yangu na kuishi maisha ya
kawaida na ya halali kwa hiyo
nimefanya maamuzi.” Akanyamaza
kidogo na kuendelea
“Nataka uuze mali zangu zote na
fedha itakayopatikana tutaigawa katika
mafungu matatu.Moja lako,lingine
langu na lingine ni kwa ajili ya mdogo
wako.Nilimpotezea dira na mwelekeo
kwa hiyo nataka kuyabadili maisha
yake.Nataka awe na maisha mazuri.Ni
hilo tu ninalotaka kukueleza” Akasema
Boaz
“Boaz ninashukuru umenisaidia
sana na nimefika hapa nilipo kwa
msaada wako.Siwezi kulisahau hilo na
ndiyo maana nimekupa nafasi nyingine
japokuwa uwezo wa kukupoteza kabisa
nilikuwa nao.Hata hivyo ahsante kwa
hilo uliloliamua lakini kama utauza
mali zako ni kwa ajili yako na familia
yako.Mimi na mdogo wangu hatuhitaji
hata senti moja kutoka katika mali
zako.We need honest money and not
drug money.Nenda ukautumie utajiri
wako kuanzisha biashara za halali na
uishi maisha ya halali” akasema Austin
“Austin nakuomba tafadhali jipe
muda na ulitafakari suala hili,usifanye
maamuzi kwa haraka.Hili ni jambo
lenye manufaa makubwa kwako.Nina
mali nyingi na endapo zitauzwa zote
pesa itakayopatikana ni nyingi sana na
utaweza kuishi maisha mazuri wewe na
mdogo wako.Nataka niwasaidie na wala
sina lengo baya nanyi” akasema Boaz
“Boaz nimekwisha kuambia
kwamba mimi na mdogo wangu
hatuhitaji pesa zako.Bado nina nguvu
za kufanya kazi na nitafanya kazi kwa
bidii nitapata pesa za kutuwezesha
mimi na mdogo wangu kuishi maisha
mazuri.” Akasema Austin na kuondoka
akamfuata Amarachi aliyekuwa
amekaa katika kiti pembeni ya bwawa
la kuogelea
“Alikuwa anasemaje Boaz?
Akauliza
“ he’s crazy.Anataka kuuza mali
zake zote halafu atugawie nusu ya
fedha mimi na mdogo wangu Linda”
“Umemkubalia? Amarachi
akauliza
“Hapana.Siwezi kukubali fedha
yake haramu yenye laana,inayotokana
kuuza dawa za kulevya.Bado nina
nguvu na nitapambana kuhakikisha
ninapata mali za kuniwezesha mimi na
mdogo wangu kuishi maisha mazuri”
akasema Austin.
DAR ES SALAAM - TANZANIA
Hali ya mzee maboko baba yake
Irene iliendelea vyema.Marcelo
alikesha macho usiku mzima
kuhakikisha kwamba hali yake
inaimarika na hadi ilipofika asubuhi
hali yake ilikuwa nzuri.
“Marcelo ninaondoka na Mukasha
kuna sehemu tunakwenda kwa hiyo
utasimamia kila kitu hapa.Hakuna mtu
yeyote kutoka wala kuingia humu
ndani” akasema Job
“Sawa Job lakini baadae
nitalazimika kutoka kidogo kwenda
hospitali kuchukua baadhi ya dawa na
kulirudisha lile gari la wagonjwa
nililoondoka nalo siku ile kwani
linahitajika hospitali. Vile vile ninataka
nikafanye mpango ili ikiwezekana mzee
huyu apelekwe nje ya nchi haraka kwa
gharama za hospitali yangu kwani kwa
hali yake anahitaji huduma kwa haraka
sana” akasema Marcelo
“Ok fanya hivyo.Mimi sifahamu
nitarejea saa ngapi ila ikitokea nikipata
tatizo nitakutaarifu” akasema Job kisha
akaongozana na Mukasha wakaelekea
garini
“ Nahitaji kuonana na Irene”
akasema Mukasha
“Hapana huwezi kuonana naye
kwa sasa,amepumzika” akasema
Job.Wakaingia garini na kumkabidhi
Mukasha mkoba uliojaa pesa.
“milioni kumi na tano ziko humo.”
Akasema Job
“Tutakapofika kwa Abdul,utabaki
ndani ya gari na nitakutambulisha
kama dereva wangu.Usithubutu kutoka
ndani ya gari” akasema Mukasha.
Job akachukua kisanduku Fulani
kidogo akakifungua na kutoa kidude
kidogo na kumtaka Mukasha akiweke
sikioni.
“Hiki ni kifaa kwa ajili ya
mawasiliano kati uangu nawe.Nitasikia
kila utakachokiongea kwa hiyo
usijaribu kufanya ujinga wowote na
wala usithubutu kukitoa sikioni”
akasema Job wakaondoka
Walikaribia kufika katika jumba
la kifahari analoishi Abdul Chizo
ambaye ni mtu wa karibu sana na dogo
Bill.
“Nyumbani kwake ni pale kwenye
lile jumba la rangi ya bluu bahari”
akasema Mukasha.Jumba la Abdul
lilikuwa juu ya kilima kidogo na toka
ukiwa mbali uliweza kuuona uzuri
wake.
“Watu hawa wanaishi maisha
mazuri kama wako peponi.Yote hii kwa
sababu ya biashara ya dawa za
kulevya.Maisha haya ndiyo
yaliyomshawishi mke wangu Mona
kuniacha na kuolewa na wauza
madawa.Sijui nitamfanya nini siku
nikionana naye uso kwa uso” akawaza
Job
Walikaribia kufika getini
wakakutana na taa ikawamulika
“Hiyo taa ni kifaa cha kukagua
magari na kutambua kama gari lako
limembeba mlipuko au kama kuna
hatari yoyote na kutoa taarifa.Ulinzi wa
hapa ni mkali sana” akasema
Mukasha.Walisimamishwa getini na
walinzi wawili wenye silaha .Mukasha
akajitambulisha na wakaombwa
wasubiri ,Abdul akapigiwa simu na
baada ya muda wakaruhusiwa kuingia
ndani.Walielekezwa sehemu ya
kuegesha na Mukasha akashuka akiwa
na ule mkoba wenye fedha Job akabaki
ndani ya gari
“Ee Mungu nisaidie niweze kupata
taarifa zitakazonisaidia kumpata
mwanangu” akaomba Job
Mukasha akaongozwa ndani na
kutakiwa asubiri katika sebule ndogo
yenye samani za kuvutia.Ilichukua
dakika kumi kwa Abdul
kuwasili.Alikuwa amevaa kaptura na
fulana nyepesi na alionekana kutoka
katika mazoezi.Abdu alikuwa ni mrefu
mwenye umbo lililojaa
“Mzee Mukasha.Shikamoo mzee
wangu”
“Marahaba Abdu.habari yako?
“Habari yangu nzuri.Nimestushwa
kwa ujio wako wa ghafla asubuhi hii.Ni
muda refu sana umepita toka ulipokuja
hapa kwangu.Halafu nilisikia ulipatwa
na matatizo.Vipi maendeleo yako?
akasema Abdul
“Kwa sasa ninaendelea vyema na
jeraha la sikioni nililolipata linaendelea
kupona.Baada ya kupata nafuu
nimeona nije kumsalimia kijana wangu
mara moja’
“Karibu sana”akasema Abdul
“Abdul nafahamu una shughuli
nyingi kwa hiyo sitaki kuchukua muda
mrefu.Nimekuja kwa mambo
mawili.Kwanza kabisa ningependa
ufahamu kuwa kwa sasa mimi niko
mafichoni.Nimeingia katika mgogoro
mkubwa na rais Ernest.Ni mgogoro
binafsi kwa hiyo ninafanya mambo
yangu kwa kujificha ficha wakati
nikishughulikia taratibu za kwenda nje
ya nchi na kutulia uko.Hili si jambo
kubwa sana kwani liko ndani ya uwezo
wangu kulimaliza ila siku nikija kwako
kukuomba msaada tafadhali usiache
kunisaidia.Jambo la pili nimesikia
taarifa za kuhusu Bill ila bado
sijaamini.je ni kweli Bill kafariki?
“Ni kweli Bill kafariki.Naye
alikuwemo katika ile hoteli
iliyolipuliwa.Mimi na yeye kuna mahala
tulitakiwa kwenda lakini tukaahirisha
kwani alitakiwa kuonana na rais katika
hoteli ile.Akiwa pale hotelini alinipigia
simu tukaongea akanifahamisha
kwamba bado anamsubiri rais na
baadae ukatokea mlipuko.Nilikwenda
kuthibitisha kama kweli ni yeye na
ndipo nilipoanza kusambaza taarifa
kwa watu mbali mbali utanisamehe
kwa kutokufikishia taarifa kwani
mambo yalikuwa mengi na sikuweza
kuwataarifu watu wote.Kwa kuwa
mwili wake umeharibika sana
tumeamua kwamba hatutaweza
kuuweka kwa muda mrefu kwa hiyo
leo atazikwa.Taratibu zote
zimeandaliwa na shuguli za kuuaga
mwili wa marehemu zitafanyika
katikaule uwanja wa mpira ulio karibu
na nyumbani kwake ambao
aliutengeneza kwa gharama zake”
Akasema Bill
“Nimesikitika sana.Bill alikuwa ni
kijana jasiri mno na mpambanaji
mkubwa kama ulivyo wewe.Pole sana
Abdul” akasema Mukasha huku sura
yake ikionyesha simanzi kubwa
“Ahsante sana mzee” akasema
Abdul.
‘By the way unaweza
kumkumbuka mwanamke mmoja Bill
aliwahi kuwa naye Yule mweupe mrefu
ana nywele ndefu nimemsahau jina”
“Monalisa? Akauliza Abdul
“Exactly !! Monalisa.Yuko wapi
sasa hivi? Sijamuona naye kwa muda
mrefu”
“Monalisa kwa sasa anaishi
Arusha.Yule hakuwa mtu wa Bill bali
alitumwa na Don ila yeye na Bill
walikuwa watu wa karibu sana na mara
nyingi walikuwa wakiwasiliana.Tayari
nimekwishamjulisha kuhusu msiba huu
toka jana na amesema kwamba leo saa
nne asubuhi atakuja na ndege ili
kushiriki mazishi.Mona mambo yake ni
mazuri sana siku hizi.Si Mona Yule
aliyekuwa akiishi na yule bwana wake
aliyepata kichaa.Alikuwa anamchakaza
bure.Hivi sasa wewe mwenyewe
ukimuona utampotea.Atakuwepo
msibani leo kama utapata nafasi ya
kuja utamuona” akasema Abdul.
“Abdul nataka nikuulize
swali.Umewahi kumuona Don? Who is
he? Tumekuwa katika mtandao huu
kwa muda mrefu mara zote tumekuwa
tukimsikia” akasema Mukasha
“Don sijawahi kumuona hata mimi
ninamsikia tu.Hii ilikuwa ni siri kubwa
ya Bill na amekufa nayo.Sijui kama
kuna mtu mwingine atakayemfahamu
huyo Don ni nani”akasema Abdul
“Abdul naomba nisiendelee
kuchukua muda mrefu,nina jambo la
mwisho lililonileta hapa
kwako.Nimeishiwa mzigo hivyo
nimekuja kutafuta kama una kiasi
chochote unisaidie.Nataka mzigo wa
milioni kumi na tato tu” akasema
Mukasha
“Oh Mukasha mbona umekuja kwa
wakati mbaya sana.Kwa hivi sasa mzigo
umekuwa adimu mno kutokana na hali
kubadilika ghafla.Nimemaliza kabisa na
sina akiba.Ninategemea kupokea mzigo
wiki ijayo na nikipokea nitakujulisha”
Akasema Abdul
Mukasha hakuwa na cha kufanya
tena hapo nyumbani kwa Abdul
wakaagana akarejea katika gari
alimokuwamo Job wakaondoka.
“Natumai umesikia mazungumzo
yangu na Abdul.Pesa zako zote hizi
hapa zimesalimika ” akasema Mukasha
“Abdul hakuweza kukutilia shaka
yoyote? Akauliza Job
“ Hapana ni vijana wangu wale
nimekua nao katika mtandao wetu kwa
miaka mingi kwa hiyo hana shaka
yoyote na mimi.Nadhani sasa kazi yako
nimeifanya vizuri na umekwisha
fahamu kila kitu.Mkeo anaishi Arusha
na huyo mtu anayeitwa Don ndiye yuko
naye.Leo hii atakuja kwa ajili ya
mazishi ya Bill na endapo kutakuwa na
uwezekano basi utaonana naye”
akasema Mukasha
“Mukasha mimi ni mtu jasiri lakini
leo nimeumizwa sana.Nilimpatia Mona
kila alichokuwa anakihitaji.Nilimpa
maisha mazuri lakini bado hakuridhika
na akataka maisha ya starehe
zaidi.Kinachoniumzia zaidi kama
alitaka maisha yale ya starehe
angeenda yeye pekee kuliko kuondoka
na mwanangu.Sijawahi kumuona
mwanangu wa pekee kwa miaka
kadhaa sasa.Lazima nimtafute Mona na
anieleze alipo mwanangu.Sina shida na
yeye ila ninachokitaka ni mwanangu
tu” akasema Job
“Job mimi kazi yangu uliyotaka
nikusaidie imekwisha na kilichobaki ni
upande wako.Ninahitaji na mimi
unitekelezee mambo yangu kama
tulivyokubaliana”
“Usihofu Mukasha.Twende
tukaichukue familia yako na
tutaipeleka nyumbani kwangu .Akina
Austin watakaporejea basi tutaangalia
namna ya kufanya kuwaondoa hapa
nchini.Nimezungumza na Austin
asubuhi ya leo na amekubali
kukusaidia lakini endapo utatusaidia
kupata taarufa za muhimu kuhusu
Ernest kwani wewe umekuwa ni
mshirika wake wa karibu sana”
akasema Job
“Msihofu kuhusu hilo mimi
nitawasaidia na kwa pamoja
tutafanikiwa kumuondoa Ernest kwani
mimi na yeye kwa sasa ni maadui
wakubwa” akasema Mukasha
Walikwenda hadi katika nyumba
walimokuwa wakiishi familia ya
Mukasha wakawachukua na kuelekea
moja kwa moja nyumbani kwa Job.