Quran Al-An'am 6:7 - Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangeli sema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uchawi dhaahiri.
JE, NI QURANI YA AINA GANI ILITEREMSWA KWA SABABU KITABU CHA KARATASI HAKIKUTOKA KWA ALLAH??
Hapa allah anathibitisha kuwa Muhammad hawezi kusoma na kuandika.
👇
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
AL - A'RAAF - 158
"Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka"
Karibuni kwa mjadala japo najua uzi hautadumu huu ila ile ya
Covax inapeta tu.
Kazi kwenu mods😁😁😁
View attachment 3420905
Ngoja nikufundishe uelewe
Unavyoambiwa mtume hakusoma maana yake ni kwamba hakuna binadamu yoyote katika Duniani anaweza kujitokeza hadharani akasema Mimi ndio nilimfundisha mtume Muhammad kusoma na kuandika au sijui nilimfundisha hesebabu au sijui nilimfundisha physics binadamu huyo hayupo
Kuhusu manabii wengine kama walipita mashuleni na university hilo Sina ujuzi nalo labda wewe unaweza ukatusaidia Musa, Daudi na Yesu walisoma university gani na walimu wao walikuwa wanaitwa akina prophesor nani?
Ila mtume Muhammad hakufundishwa na binadamu yoyote na Allah alifanya hivyo kusudi Ili amfundishe mwenyewe
Malaika Jibril ndio alikuwa Mwalimu wa mtume Muhammad na Ili kuonyesha kuwa elimu ni muhimu Aya tano za kwanza za Quran aliyofunuliwa mtume Muhammad zilikuwa zinasisitiza kusoma
Quran 96:1
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
Quran 96:2
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
Quran 96:3
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
Quran 96:4
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
Quran 96:5
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
First time Malaika Jibril anakuja Kwa mtume alikuja na hizo aya na maana yake ni kwamba Jibril alikuja na maandishi ndio maana akawa anamwambia mtume asome
Mtume akasema Mimi siwezi kusoma akamshika kifuani na kumminya huku akimlazimisha asome
Kwanini aliminya alikuwa anamuomyesha kuwa kusoma sio hiyari Yani lazima asome
Na mwisho wa siku akaweza kuzisoma hizo aya 5 na malaika Jibril akaenda zake
Malaika Jibril akaendelea kuja na kufundisha mtume na akaambiwa mtume Muhammad asiwe na hofu kwani atasomeshwa na hato sahau
Quran 87:6
Tutakusomesha wala hutasahau,
Quran 87:7
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
Quran 87:8
Na tutakusahilishia yawe mepesi.
Sasa ngoja nikuonyeshe baadhi ya vitu alivyofundishwa mtume karine ya 7 alafu hao Wazungu wako ambao wewe ndio unaamini wanaelimu sana wakaja kukopi na kupest Kwa huyo ambaye mkiikaa huko makanisani mnadanganywa kuwa Muhammad alikuwa hajui kitu kumbe wao wanakopi na kupest kwakwe
Quran 21:30
Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?
Karine ya 7 mtume Muhammad anatufundisha kupitia Quran kuwa kuwa Mbingu na aridhi zilikuwa zimeambata Yani kilikuwa kitu kimoja Kisha Allah akaziachanisha Yani akaulipua huo muunganiko zikaachana
Karine ya 19 Wazungu wanakuja na idea ya Big bang theory wanapita mulemule alipopita mtume Muhammad kuwa Mbingu na aridhi zilikuwa kitu kimoja ukatokea mlipuko vikaachana hapa Wazungu wamemkopy mtume Muhammad
Hiyo Aya inamalizia kuwa viumbe hai vyote vimeumbwa Kwa maji
Karine ya 19 Baada ya Wazungu kugundua microscope na kufanya uchunguzi juu ya viumbe hai wakagundua kuwa viumbe hai ni mkusanyiko wa cell na 90% ya cell za viumbe hai ni maji
Acha niishie hapa mambo ni mengi maana hata hesabu za Algebra msingi wake ni Quran huyo Alijabili alisoma Aya za Quran zinazofundisha hesabu ndio na yeye akaafundisha hesabu maana katika Dunia hii Kuna hesabu za aina mbili tu hesabu za kirumi na hesabu za kiarabu ndio hizo algebra na ulimwengu wote wa kisayansi unaongozwa na hesabu za kiarabu
Nyinyi makafiri tukikuangalieni Huwa tunawaenea huruma jinsi mnavyodanganywa