Anzia kusoma Quran 7 : 155 - 157
Ila nakuwekea mstari mmoja ambao ndio una hoja yangu.
Quran inasema kuwa Mussa alimtabiria Mohamed kuwa ataandikwa katika Torati na Injili.
Je Mussa alijua kutakuwa na Injili?.
100% Mohamed kabun hiki kitabu kwa kutumia janja janja tu.
Kaunganisha unganisha visa na hadith za Kiyahudi na kuja na dini yake.
Eti wahyi. Wahyi? 😎😎😎😎
Maneno ya Mussa👇👇👇
Quran 7 : 157
"Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa"
Naomba utetezi
Jagina adriz Kazakh destroyer Covax gallow bird
Cc ndugu zangu katika imani
hamis77 Dumas the terrible Che mittoga Infropreneur
Kwanza hiyo Aya uliyoitoa hakuna sehemu inayosema kuwa Musa alisema Mtume Muhammad ataandikwa katika injili haya Maneno wewe sijui umeyapata wapi
MTUME MUHAMMAD NDANI YA BIBILIA
1) Kumbukumbu la Torati 18:18
Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Hapo Mungu anamwambia Musa kuwa atatoa Nabii miongoni mwa ndugu zao
Waisrael watoto Isaka
Warabu wa Saudi Arabia ni watoto wa Ishmael
Hivyo basi hawa ni ndugu
Nabii mfano wa Musa
Musa amezaliwa na baba na mama
Muhammad nae amezaliwa na baba na mama
Musa alipewa utume akiwa mtu mzima
Muhammad nae alipewa utume akiwa mtu mzima
Musa amepewa Taurati Ina amri , Sheria na hukumu
Muhammad amepewa Quran Ina amri, Sheria na hukumu
Musa alioa na kuzaa watoto
Muhammad nae alioa na kuzaa watoto
Musa amekufa na kuzikwa
Muhammad amekufa na kuzikwa
2) Kumbukumbu la Torati 33:2 Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani,
Mlima Sinai alipewa utume Nabii Musa
Mlima Seiri upo Juda alipewa utume Yesu
Mlima Parani upo Saudi Arabia amepewa utume mtume Muhammad ni
3) Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Mlima Parani upo Saudi Arabia
4)Isaya 21:13
Ufunuo juu ya Arabuni. Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala, Enyi misafara ya Wadedani.
Isaya 21:14
Waleteeni wenye kiu maji, Enyi wenyeji wa nchi ya Tema; Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
Dedani ni jina mototo wa Nabii Ishmael na Tema ni jina la mtoto wa Nabii Ishmael na Hadi Leo hi huo mji wa Tema upo Saudi Arabia
Hao wote ni manabii
Je wayahudi ambao walikuwa wasomi wa hayo maandiko wanasemaje?
Yohana 1:19
Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
Yohana 1:20
Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.
Yohana 1:21
Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
Wasomi wa kiyahudi waliposikia Kuna Nabii amekuja wakatuma watu wakamuuliza yeye ni nani
Yohana mbatizaji akasema yeye sio kristo
Wakamuuliza wewe ni Eliya akasema hapana
Wakamuuliza wewe unabii yule?
Yohana akasema La Mimi sio
Yohana mbatizaji anajulikana
Kristo anajulikana
Eliya anajulikana yeye alipaa walidhani labda amerudi
Huyo Nabii Yule ni nani? Ambaye wayahudi walikuwa wanajua kuwa atakuja?
Nyinyi wagalatia Wazungu wamekuingizeni chaka na Jahanam inakusubirini