Kwa habar ya Ismael kuwa muarabu Nakubaliana na Wewe.
Neno Mwebrania (Hebrew / ‘Ivri) linahusishwa na Eberi (Eber).
Mwanzo 10:21
“Na Shemu naye akazaliwa wana; naye ndiye baba wa wana wote wa Eberi…”
- ukoo ni: Nuhu → Shemu → Arpaksadi → Shela → Eberi → … → Ibrahimu → Isaka → Yakobo (Israeli)
jina Waebrania linahusishwa na uzao unaopita kwa Eberi, na baadaye kwa Yakobo (Israeli).
- Mungu alichagua Isaka kwa ajili ya AGANO
Mwanzo 17:19
“Nitalithibitisha agano langu kwake (Isaka) na uzao wake baada yake, liwe agano la milele.”
Mwanzo 21:12
“Kwa maana katika Isaka ndipo uzao wako utakapoitwa.”
- Ina maana Sio kila mwana wa Ibrahimu anakuwa uzao wa agano.
Isaka ndiye aliyeteuliwa kubeba agano la Mungu.
Yakobo (Israeli) ndipo taifa lilipoanza
Isaka alimzaa Yakobo, ambaye Mungu alimpa jina jipya Israeli.
Mwanzo 32:28
“Jina lako halitaitwa tena Yakobo, bali Israeli…”
- wana wa Yakobo = makabila 12
- Hapo ndipo taifa la Waisraeli (Waebrania) lilipoanza rasmi
Kwa ufupi Waebrania = uzao wa Isaka → Yakobo (Israeli)
- Jina linahusishwa na Eberi.
- Agano la Mungu lilipitia Isaka.
- Taifa lilijengwa kupitia Yakobo (Israeli).
Ishamel inawezena ndio alianzisha Uarabu.
Mwanzo 21:21
“Naye akakaa katika jangwa la Parani, mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.”
Mwanzo 25:13–18
“Hao ndio wana wa Ishmail… wakaishi kutoka Havila hata Shuri…”
Kufupisha Ishmail:
- Alikaa jangwani (Parani / Hijazi)
- Alioa Mmisri.
- Watoto wake waliishi Arabia.