Quran inawezaje kushindwa hesabu ndogo Kama hii?

Kama umetolewa mifano yote huko juu hujaelewa ni rahisi sana kuambiwa mtungi wa gesi ulijazwa kwa mdomo na ukaamini.
 
Sasa hao suni na Shia wanatumia muongozo gani kugawana urithi?
Wameboresha na kuirekebisha ule muongozo wa Quran ili isizidi 100%
Angalia hapa maboresho.
 

Attachments

  • inheritence.jpg
    181.2 KB · Views: 27
Kila mtu abaki na dini yake,
Hilo liko wazi mkuu.
Ila tunachotaka kusema kule kujisifu na kuponda vitabu vya wengine Kama vimebadilishwa huku wakijinasibu Kama Quran imeandikwa na Allah mbinguni Haina makosa yeyote na imekamilika.
Kama kweli Allah ndio muandishi anashindwaje hata kugawa asilimia tu kwa warithi?
 
Quran haisomwi kama gazeti lazima uchambuliwe na mtu aliyeisomea haijalishi unazungumza lugha ya kiarabu au ya kiswahili
Mkuu hata usome vipi uzuri namba hazidanganyi unaweza kucheza na maneno lakini sio namba zitakuumbua tu
Mke 1/8
Baba 1/6
Mama 1/6
Watoto wa kike wawili 2/3
 
Mkuu hata usome vipi uzuri namba hazidanganyi unaweza kucheza na maneno lakini sio namba zitakuumbua tu
Mke 1/8
Baba 1/6
Mama 1/6
Watoto wa kike wawili 2/3
Kwa hiyo majaji wote wa Mahakama hawajawahi kuyaona hayo makosa uje uyaone wewe?kwamba wewe una akili kuliko majaji wote?kama umechambuliwa kwa lugha ya kiswahili na bado huelewi,umeelekezwa mantiki ndogo tu huoni kisha mwenyewe unajiona Genius halafu ukitoka hapo unaenda kwa Mwamposa kisha anakwambia Mungu amenituma nije kwako mimi ni nabii wenu amesema toa hela kisha mnampa ananunua magari yake na mkewe kama yule wa kujaza gesi ya jiko kwa mdomo kisha wakitajirika wanawakejeli kwamba maskini walionichangia hela ni wajinga kama alivyofanya k8boko ya wachawi baada ya kurudi kwao Congo
 
Hiyo imekupoteza kidogo kwani kuna mtu imemuacha hapo lakini hongera kwa kuthubutu kutafuta elimu na mola akujaze mapenzi ya kusaka ukweli (haki)

Hawa watu wanaletaga mambo wakidhani wanaukomesha uislamu kumbe ndio wanaukuza bila kujua. Natoa elimu kwa ufupi sana kuhusu hili jambo na kwa mwenye akili ataelewa lakini kwa mwenye nia ovu na uislamu atabaki na ujinga wake

Kwanza kabisa waislamu wote tunakubaliana kwamba tunaongozwa na quran inayofafanuliwa na maneno ya mtume kisha maneno ya mtume yanafafanuliwa na maswahaba halafu maneno ya maswahaba yanafafanuliwa na wanazuoni wa zama hizo kisha wa zama zilizofuata hivyo hivyo mpaka wa zama hizi

Tukianza kwanza kabisa kuna aya inasema "...ALICHOKULETEENI MTUME KICHUKUENI NA ANACHOKUKATAZENI KIACHENI". Kisha tukienda kwenye sunna kuna hadithi inasema "...SHIKAMANENI NA YALE NILIYOKUACHIENI NA YALE WATAKAYOWALETEA MAKHALIFA WAONGOFU" (Nimenukuu kwa kujikita kwenye maana tu sijachukua nukuu halisi kutoka vyanzo vya quran na hadith)

Sasa kwa hoja kama hiyo kwanza ni kweli kabisa urithi upo kama alivyoandika lakini swali la msingi ni je ikitokea ikawa hesabu inaonesha kuzidi kwenye mgawanyo kuliko mali halisi yenyewe je tunafanyaje? Kwa taarifa yako ni kwamba wewe siyo wa kwanza kuishi hapa duniani wala wewe siyo peke yako umeona jambo hilo wala siyo wewe pekee unaejua hisabati sanaa

Scenario kama hii ilishatokea kipindi cha maswahaba wa mtume ambapo umar aligawa urithi kwa warithi akakuta denominator kwenye jumla inakuwa ndogo kuliko numerator. Kumbuka kuwa mafungu yote jumla yake inatakiwa isizidi kitu kizima yaani 1/1 au 100%. Kwa mfano kwenye mfano aliouleta utaona ukijumlisha zile sehemu zote unapata jumla ni 27/24

Umar alipokutana na scenario hii aliwaita wataalamu waliopo kwenye utawala wake (kina ibn abbas, ibn mas'ud, zayd, aliy nk) na baada ya kujadiliana wakatoka na suluhisho kwamba numerator ifanywe ndiyo denominator na hapo itakuwa kila fungu limepunguzwa kwa uwiano sahihi bila kuvuruga uhalisia wa mafungu ya urithi

Yaani itahama kutoka (3/24, 16/24, 4/24, 4/24) na kwenda kuwa (3/27, 16/27, 4/27, 4/27). Hii kitu ilishasolviwa kitambo tu ni basi watu wana nia zao za hovyo. Hisabati haidanganyi ni ishu ya calculations tu au HAMKUSOMA MADA YA UWIANO DARASA LA VI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…