Tetesi: R Kelly sasa ana Tsh 29,000 kwenye akaunti

Tetesi: R Kelly sasa ana Tsh 29,000 kwenye akaunti

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Chicago,USA.
Ukisikia ssiku ya kufa nyani miti yote uteleza ndio haya yanayomkuta mwanamuziki R Kelly.

Mwanamuziki huyo ambaye amepitia kipindi kigumu cha kukabiliwa na kesi ya unyanyasaji wa kingono amejikuta akibaki bila salio baada ya mdeni wake kukomba kiasi cha dola 154,527 za kimarekani zilizokuwa katika akaunti yake.

Imeelezwa kwamba aliyekuwa baba mwenye nyumba amabpo R Kelly alikuwa akiishi hapoalifungua madai mahakamani baada ya R Kelly kutolipia malimbikizo ya kodi ya nyumba hiyo.

Hukumu iliyotolewa mahakamani iliagiza mwanamuziki hiyo akatwe stahiki zake katika malipo ya kazi zake za muziki au zichukuliwe fedha zilizopo katika akaunti yake.

Pamoja na benki hiyo ya Wintrust kutoa pesa zote zilizopo kwenye akaunti ya R Kelly na kubakiza dola 13 ambazo ni sawa na Tsh 29,000 bado hazijafanikiwa kulipa deni lote.

Mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kali kama vile I BELIEVE,I CAN FLY,THE WORLD'S GREATEST na SOUND OF VICTORY anadaiwa dola 194,000 za pango la nyumba.

Mbali na kesi ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba pia amefunguliwa kesi na mzazi mwenzio kwa kushindwa kutoa pesa za matunzo ya mtoto.
 
Kweli wazungu washammaliza dah hapa anasuburi kufa msongo wa mawazo
 
Ali Kiba amsaidie tu R. Kelly kulipa kodi ya nyumba
 
Tatizo la mbele bana huna pa kuficha kitu.. Taarifa zako zote ziko kwenye system watu wanajua kila senti uliyo nayo na umeipataje. Ndio maana unakuta ishu kama za kodi lazma ukikwepa watakudaka tuu na mbaya zaidi wanazama kwenye akaunti wanakomba kila kitu hata uwe na akaunti 5 wanafyeka zotee. Yaani unaweza kulala tajiri kesho ukiingiza kadi kwenye ATM unaambiwa insufficient funds! Na kule ukipigika ndio basi tena hakuna kwa mjomba wala shangazi utapoenda kuchill ni mwendo wa homeless tu
 
Back
Top Bottom