Tetesi: R Kelly sasa ana Tsh 29,000 kwenye akaunti

Kwahiyo hata TID ana ela kuliko kells now..!?

Kadanganye vijiwe vya wavuta bangi
 
Imeelezwa...

Pamoja na benki hiyo ya Wintrust kutoa pesa zote zilizopo kwenye akaunti ya R Kelly na kubakiza dola 13 ambazo ni sawa na Tsh 29,000

Imeelezwa wapi?

Wacha kutulisha matango pori wewe!

Weka source inayosema R Kelly kabaki na dola 13 kwenye account.
 
Unakatwaje fedha kwenye account ambayo hujakubaliana na mtu uliyeingia mkataba naye kuhusu umiliki wa account isiyohusika? Nataka kujua tu maana hata kodi ya nyumba wanakata kwenye acc uliyoisajili kwa malipo
 
Japo siiamini hii habari but ujinga mwingine tunajitakia! Ina maana jamaa hakuwa kbs na nyumba yake binafsi? Wht abt other investiments apart from muziki???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma huku nacheka...eti ni mwendo wa homeless tu...hahahhhh
 
this guy wanafanya kila linalowezekana waDestroy his carrier & life. Inahitaji moyo wa chuma kuishi kama r kelly kwa kipindi hiki dah.

 
ina maana hajawahi kununua wala kujenga nyumba.

baasi mpuuzi. hata bidhaa zake hakua nazo, biashara? huu pia ni uzembe
Alikuwa na nyumba kubwa sana aliyojenga mwenyewe (sio ya kununua)
Aliijenga mwaka 1997 kwenye ardhi ya ukubwa wa 20,000 square foot na ilikuwa na vyumba 16 na bafu 4 na indoor pool
Iliuzwa mwishoni baada ya mkasa na kesi yake hiyo akashindwa kulipa mortgage
Kesi yake imekula hela nyingi sana
Ukiwa na hela unataka ujinasue kwa kesi hapo unashika lawyers wakubwa nao wanakupiga haswa mpaka wanakufilisi na kushinda kesi sio lazima


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Ungeweka na source ilikotoka maana nakumbuka alikuwa anazo kama $1m sasa naomba upunguze utoe za mishkaki, bajaj alizopanda yaani kila kitu isipokuwa za kuhonga maana hawezi tena anafuatiliwa
Zipunguzeeee weeee mpaka zifike hizo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Ulaya na America pagumu sana black hatupendw sana ukiwini ukiwa na gud life lazima wakutengenezee scenario matata sana wakufilisi hawapend kuona black ni zaid yao
 
U9f 0 aquarium ugh l

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyani Ngabu amuunganishie kibarua cha kubeba box...maana bora mkono uende kinywani

angekuwa bongo ningempa dili la kupandisha watalii mlima Kilimanjaro
 
nyumba kubwa sana aliyojenga mwenyewe (sio ya kununua)
Aliijenga mwaka 1997....

Iliuzwa mwishoni baada ya mkasa na kesi yake hiyo akashindwa kulipa mortgage


WACHA kutulisha matango pori wewe!

Mortgage inaingiaje kwenye nyumba ya kujenga mwenyewe?

Umesema mara tatu nyumba kajenga mwenyewe!

We vp we diaspora wewe? Jielimisheni mkiwa huko.
 
Ulaya na America pagumu sana black hatupendw sana ukiwini ukiwa na gud life lazima wakutengenezee scenario matata sana wakufilisi hawapend kuona black ni zaid yao
Sisi Waafrica tunapenda sana kutia huruma kwa upuuzii tunao ufanya tukidhani hamna anaetuona..... Mbona wakina Jay Z, Dr Dre etc hawana case za kijinga kama hizi? Huyu R.Kelly alibaki watoto wadogo... Tuacheni kusingizia wazungu kila kitu japo nao wana mapungufu yao...

Sisi hatutaki kuheshimu haki za watoto kabisa, ulaya huwezi kuhonga kijinga na case ikazimwa kama hapa bongo, Tanzania wabakaji wapo kibao na wanajulikana lakini sheria haiwafikii sababu ya hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…