Kuhusu mtafaruku kati ya Mayahudi na Wazayuni hili naunga mkono. Kama wiki moja nyuma niliona video kati ya Myahudi na Mzayuni wakizozana,kuhusi imani zao.Kuwatetea wayahudi Mkuu, wao wanafuata Torah, na Torah ni kitabu kitakatifu na wayahudi wengi wa ukweli
Lakini kuhusu kufata Taurati hili si kweli,sababu Mayahudi walibadili maandiko ya Taurati kimaana na kimuundi,ndiyo maana ukisoma katika vitabu vyao utaona kuna andiko ambalo nabii Musa anaelezea kifo chake hali ya kuwa yuko hai,jambo ambalo haliwezekani huku wakidai ya kuwa ameandika hayo nabii Musa.
Almuhimu Talmudi ndiyo kitabu chao Mayahudi wenyewe na ndiyo wanakifata. Uzayuni ni chama kilichoanzishwa kati ya karne ya 20 au 21.