Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

Mkuu Rudi shule, hujajua kazi ya earthing system bado, kama hujui kitu bora unyamaze kuliko kutoa elimu ya uongo.

Hoja kwa hoja, tuepuke kashfa kiongozi wangu, tuko hapa kujifunza. Hebu mkosoe huyu kiongozi kwa hoja ili na Mimi nielimike kupitia Hilo.

Kifaa kinacholinda mfumo wako wa umeme dhidi ya Radi ni aina hizi mbili za circuit breaker
1. Residual Current Circuit Breaker (RCCB)
2. Residual Current Device (RCD)
Radi (lightning) inapopiga circuit breaker hizi hu trip (huzima mfumo wote wa umeme), hivi ndio inavyolinda sakiti yako.
Note; binafsi naikubali RCCB kampuni ya EUROTRIX.

Kazi ya earthing system ni;

1. Kumlinda mtu asipigwe na shock ya umeme.
Mfano. Waya wenye umeme (live wire) unapogusa bati la friji, maana ake mtu akigusa lile bati la friji atapigwa na shock ya umeme, badala yake sasa endapo mfumo wako ukiwa na earthing basi umeme wote uliovuja kwenye bati la friji hupelekwa chini ya ardhi, hivyo basi hata mtu akigusa lile bati hatapigwa na shock ya umeme kwa maana umeme tayari unaelekea chini.

2. Kulinda kifaa kisiungue dhidi ya umeme unaovuja.
Mfano. Kama umeme utavuja, yaani waya ukagusa bati la friji kama hujafanya earthing kwenye sakiti yako basi kuna uwezekano wa friji lako kuungua endapo waya mwingine wenye potential tofauti ukagusa bati hilo la friji, endapo utafanya earthing basi umeme wote hupelekwa chini na friji lako litabaki salama.

Note; Earthing system hailindi kifaa dhidi ya Radi (lightning)

Mkuu uko sahihi 100
Ila kuna some additional unatakiwa kuzijua pia

Umeme wa radi ni kama maji yaliyomwagwa aridhini
Hayana uelekeo
Umeme una kiwango chake kikizidi ndipo cct breaker inafyatuka
Ikiwa haitafyatuka itaunguza vitu
Ikiwa mfumo wa earth uko sawa umeme huo utaenda aridhini pengine bila ya kuzima cct au bila ya kuunguza vitu
Thus baadhi ya nyumba watu hu link ma paa yao na mfumo wa earth

Uko sahihi Mkuu
Kama manguli mmekubaliana mimi pimbi ni nani hata niwakatalie?
 
Huko radi nyingi ni za kiutamaduni, mnatengeneza radi zenu wenyewe.
Mzee baba mimi sio kwetu huku, nipo kikazi na ndio mvua za masika za kwanza hizi tangia nihamie pande hizi. Alafu hizo Imani ifikie kipindi tuachane nazo kwa kipindi hiki cha advanced technology. Kwa wanaelewa kwanini radi zinapiga maeneo flani duniani topographically hatushangai mikoa iliyopitiwa na bonde la ufa kuwa na lightening and thunder storms zenze nguvu.
 
mbebishana kwa hoja nipenda comment ja jamaa aliyesema kinachopitisha umeme kweny. udongo ni ule uyevu uyevu
Mkuu kunakitu kinaitwa vipitisho rasmi
Na visivyo rasmi

Ieleweke ya kua vyote ni vipitisho ila vinazidiana uwezo wake

Mti ni kipitisho
Waya ni kipirisho
Maji ni kipitisho
Ila tu vinginge ni rasmi vingine sio rasmi
Uwezo,ubora ndio vinaamua kipi kikae wapi

Aridhi ni kipitisho ila sio rasmi sio bora ila kinapitisha
 
Pumba kama pumba
Screenshot_20240526_075054_Gallery.jpg
 
Udongo

Umesema Udongo ni kipitishi kizuri cha umeme. Ukitumia tofali za kuchoma kama nyaya za umeme,taa itawaka?

Mfano ukaunganisha betri mbili na tofali moja la kuchoma kisha glopu ukakamilisha circuit,glopu itawaka? Circuit yenye glopu,waya,betri mbili. Ukaamua ufanye tofali kama betri la tatu. Umeme utapita na glopu kuwaka?
Nemecheka sana aisee, kweli walimu wa shule za msingi wanatakiwa waipwe kuliko wale wa sekondari. Ushaambiwa udongo bado unaleta hoja za tofali la kuchoma. We kwa akili yako tofali la kuchoma na udongo ni sawa?
 
Daah umenikumbusha kipindi kimoja 2020-2021 nili ishi katavi wilaya ya mlele
Aisee huko Kuna radi nibalaaaa
Mvua kidogotu radi Zina miminika kama upepo...!!
 
Nemecheka sana aisee, kweli walimu wa shule za msingi wanatakiwa waipwe kuliko wale wa sekondari. Ushaambiwa udongo bado unaleta hoja za tofali la kuchoma. We kwa akili yako tofali la kuchoma na udongo ni sawa?
Content. Udongo unawezakuwa ktk maumbo mbalimbali ikiwemo tofali kama hutaki tofali la kuchoma basi tofali Hilo Hilo kabla halijachomwa.
Bado linaundwa kwa udongo.
 
Content. Udongo unawezakuwa ktk maumbo mbalimbali ikiwemo tofali kama hutaki tofali la kuchoma basi tofali Hilo Hilo kabla halijachomwa.
Bado linaundwa kwa udongo.
Kwa hiyo nikisema niweke mbegu za alizeti kwenye chakula badala ya mafuta ya alizeti nakuwa niko sawa tu au sio. si zote ni alizeti. Nenda shule ujifunze kubadilika kwa states za vitu,

We unajua maji yanapitisha umeme, lakini kuna namna maji ukiyafanya hayapitishi umeme.

Au kwa kuwa umesema tofali ya kuchoma ni udongo, tuichukue tuchanganye na simenti tupate tofali ya block, unaonaje hapo.
 
Afu mwingine anaweka ya 6000😂😂
Kwa nini mnahangaika kigezo cha bei badala ya kutumia kigezo cha ''inayofaa kwa kazi hiyo''. Je, mtu akiuziwa hiyo ya 6000 kwa 100,000 itafaa? Mimi nadhani tungehimiza kuwa tutumie mafundi wenye ujuzi na wanaoaminika kuliko kigezo cha bei.
 
Back
Top Bottom