Kifaa kinacholinda mfumo wako wa umeme dhidi ya Radi ni aina hizi mbili za circuit breaker
1. Residual Current Circuit Breaker (RCCB)
2. Residual Current Device (RCD)
Radi (lightning) inapopiga circuit breaker hizi hu trip (huzima mfumo wote wa umeme), hivi ndio inavyolinda sakiti yako.
Note; binafsi naikubali RCCB kampuni ya EUROTRIX.
Kazi ya earthing system ni;
1. Kumlinda mtu asipigwe na shock ya umeme.
Mfano. Waya wenye umeme (live wire) unapogusa bati la friji, maana ake mtu akigusa lile bati la friji atapigwa na shock ya umeme, badala yake sasa endapo mfumo wako ukiwa na earthing basi umeme wote uliovuja kwenye bati la friji hupelekwa chini ya ardhi, hivyo basi hata mtu akigusa lile bati hatapigwa na shock ya umeme kwa maana umeme tayari unaelekea chini.
2. Kulinda kifaa kisiungue dhidi ya umeme unaovuja.
Mfano. Kama umeme utavuja, yaani waya ukagusa bati la friji kama hujafanya earthing kwenye sakiti yako basi kuna uwezekano wa friji lako kuungua endapo waya mwingine wenye potential tofauti ukagusa bati hilo la friji, endapo utafanya earthing basi umeme wote hupelekwa chini na friji lako litabaki salama.
Note; Earthing system hailindi kifaa dhidi ya Radi (lightning)