Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

Juzi mida ya asubuhi mvua ilinyesha Dar na around saa tatu hivi ikapiga radi moja kubwa sana kwa wanaokaa pande za goba, mbezi,tegeta A,msumi,makabe etc. wataelewa ninachosema..radi ambayo ilipelekea umeme kukatika kwa dakika chache tu ila tayari ilikua imeshafanya uharibifu kwenye vifaa vya umeme nikiwemo mimi na majirani kadhaa tuliounguliwa TV. Binafsi natumiaga fridge guard kwenye TV lakini ngoma haikusaidia sababu haikua low voltage. Nimekaa Dar muda sijakutana na hali hii maana ilikua ni radi ya level ya zile konki za kanda ya kigoma, katavi na Rukwa. Nimetoka dukani kwa mangi mitaa ya huku nimekuta jamaa wengine nao wanaongelea kuunguliwa TV sababu ya ile radi. Kuna muhanga mwingine humu?
Na maeneo haya Uliyoyataja ndoyo yanaongoza kwa kuwa na Wanaume wengi WAPIGA MILUZI kwa sasa huko Jijini Dar es Salaam hivyo huenda Mwenyezi Mungu kaamua Kuwaadhibu Kimtindo.
 
Kipitishi kizuri cha umeme. KIZURI
Vipitisho vya umeme vinapangwa kulingana na ubora wake
Nkisema bora nnamaanisha uwezo wake wa kupitish umeme bila ya kuwa na upotevu wa umeme
Kwahyo hata km kitapoteza kwa asilimia 99 bado kinauwezo wa kupitisha ila sio kwa ubora kama gold,silver..,,au copper
 
Juzi mida ya asubuhi mvua ilinyesha Dar na around saa tatu hivi ikapiga radi moja kubwa sana kwa wanaokaa pande za goba, mbezi,tegeta A,msumi,makabe etc. wataelewa ninachosema..radi ambayo ilipelekea umeme kukatika kwa dakika chache tu ila tayari ilikua imeshafanya uharibifu kwenye vifaa vya umeme nikiwemo mimi na majirani kadhaa tuliounguliwa TV. Binafsi natumiaga fridge guard kwenye TV lakini ngoma haikusaidia sababu haikua low voltage. Nimekaa Dar muda sijakutana na hali hii maana ilikua ni radi ya level ya zile konki za kanda ya kigoma, katavi na Rukwa. Nimetoka dukani kwa mangi mitaa ya huku nimekuta jamaa wengine nao wanaongelea kuunguliwa TV sababu ya ile radi. Kuna muhanga mwingine humu?
Waha na Wakinga na Wasukuma wameongezeka Huko Dar kwenu ndio maana. Bila kusahau wafipa. Ndio wenye kupenda radi
 
Kwa hiyo ukikata kipande cha waya kwenye circuit ukapachika kipande cha tofali la kuchoma Watu watapata umeme? Kipitishi kizuri.
Vipitisho vya umeme vinapangwa kulingana na ubora wake
Nkisema bora nnamaanisha uwezo wake wa kupitish umeme bila ya kuwa na upotevu wa umeme
Kwahyo hata km kitapoteza kwa asilimia 99 bado kinauwezo wa kupitisha ila sio kwa ubora kama gold,silver..,,au copper
 
Nasikia radi za kigoma zikipiga zinaondoka na zizi zima la ng'ombe.
 
Endeleeni kuweka vi earthlod vya 6000!
Mkuu ata kama ameweka Earth rod ya 200k lakini haijafika kwenye switch socket na metal boxes zote ndani ya nyumba haitakuwa na msaada wowote.
Pia kuna wale mafundi wakati wa maintenance huwa wanazikata Earth wires ili kuzia Earth leakage inayosababisha RCB Kutrip so wanakupa Panadol na sio dawa yakumaliza tatizo
 
huku watu kujua madhara yake ni ngumu maana sio ukanda wa radi,ila nina uhakika wengi wameweka za magumashi, zikipiga radi kama za kanda ya ziwa hata kwa wiki nyumba nyingi yatatokea majanga kwenye vifaa vya umeme
oyaa ee., radi za kanda ya ziwa[emoji23] ni nomaa na nusu!
 
Kwa kawaida kama ilivyo kwa binadamu, umeme unataka kupita katika njia fupi na rahisi kupitika. Umeme hupita katika njia iliyo rahisi kwake kurudi ardhini. Njia pekee inayotumiwa na umeme kurudi ardhini bila madhara yote ni kupitia katika waya ambao kwa lugha ya kiingereza unaitwa Earth Wire na kisha Earth Rod. Mchakato mzima wa kukamilisha ufanyaji kazi wa huu mfumo unaitwa Grounding. Ikiwa kutatokea tatizo katika waya unaobeba umeme baada ya matumizi(neutral wire), au tatizo lolote la kiufundi ambalo litasababisha ongezeko la ghafla la umeme kutokana na radi kwa mfano, basi earth wire itaubeba umeme huu wa ziada kwenda ardhini. Kwa muunganiko huu wa earth wire na earth rod, ardhi inafikika kirahisi sana na umeme. Maana yake ni kwamba mfumo huu wa grounding una wajibu wa kumlinda mtumiaji wa umeme inapotokea tatizo la umeme.

Ikiwa radi ingepiga katika nyumba yako ingeweza kusababisha hatari katika mfumo wako wa umeme na madhara mengine
Lakini kama mfumo huo umeunganishwa ipasavyo na mfumo wa earth(Grounding) kiasi chote cha umeme wenye madhara kwa mtumiaji au vifaa vya umeme kitaishia ardhini badala ya kuunguza kila kitu kilichounganishwa katika umeme kwa wakati huo au kumdhuru binadamu.

Sote tunafahamu kwamba ardhi ni kipitisha umeme kizuri kwa asili yake. Na kama nilivyosema awali umeme unapenda kupita katika njia rahisi na fupi, kwa hivyo ku-ground mfumo wako wa umeme ni kuufanya umeme wenye madhara kwako kupata mahali pa kupita kwa urahisi badala ya kwenda ardhini kupitia mwili wako. Hivyo kwa kifupi kabisa, Earthing au Grounding ni kuunganisha vifaa vyako vinavyotumia umeme katika ardhi ya dunia kwa kutumia waya(Earth wire) na fimbo(Earth rod) mara nyingi ya shaba ambayo huzikwa katika ardhi yenye unyevu wa kutosha.
Zamani walikua wana weka kabomba kana pita hadi chini ya ardhi tulikua una viita vya kukinga radi ..now days nyumba nyingi hawana sijui ndo technology
 
Bado hiyo ni copper plated sio kama ile ya 80k na uthibitisho ni katika kuikunja,pure cooper hukunjika kirahisi.Kipindi cha nyuma hizo za 40k zilikuwa zinakunjika lakini sio sasa pia kuwa plated kunaweza kusifanye mvutano na sumaku kipimo kinachodanganya wengi.Bora hata iwe aluminium kuliko hiyo cooper plated.
 
Siku ukienda tena kununua earth rod nenda na sumaku ikiwa original huwa sumaku hainasi
Thanks for this tip mkuu. Ntafuatilia ili kama vp nibadilishe
 
Back
Top Bottom