Saturday May 01 2021
In summary
Waliofariki ni Jafari Amiri (12) mwanafunzi wa darasa la nne na Hamidu Amiri (9) mwanafunzi wa darasa tatu.Handeni. Watoto wawili wa familia moja wakazi wa kata ya Malezi wilayani Handeni Mkoa wa Tanga wamefariki baada ya kupigwa na radi.
Diwani wa Malezi, Shabani Kitombo leo Jumamosi Mei Mosi, 2021 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo jioni wakati watoto hao wakiwa nyumbani kwao.
“Wakiwa ndani radi iliwapiga na kufariki dunia hapohapo kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema watoto walikuwa nyumbani kwao wakati mvua inanyesha na punde ilipiga radi ambayo imesababisha vifo vyao,” amesema.