Rafiki Yangu above 30 Hana Nguo za Heshima, Kabati Lake Limejaa Jeans!

Tafuta tu pesa nyingi uache kuwaza vitu vidogo nguo yyte inaweza kua ya heshima au sio ya heshima

Kuna suluari ya kitambaa ila fupi na inabana miguu na matako hiyo siyo nguo ya heshima ila kuna jeans pana na inafit vizuri mwilina na inaruhusu mwili kupumua hiyo ni nguo ya heshima

Mm nazan nguo ya heshima ni ile inayofuata vigezo na mashart haijalishi ni jean au sulual ya kitambaa

Kuna vijana tunakutana nao humu mitaani amevaa suluari ya kitambaa adi unashangaa surual fupi imebana miguu na matako
 
Kwanza tuangalie unaweza vaa jeans kali na tshirt ukatupia koti la suti zuri na ukapendeza pia na wala hujavunja heshima. Na unaweza vaa hizo unaita suti suruali mlegezo au imebana mpaka sehemu za siri zinaonekana na ukawa umevunja hiyo heshima. Pia kuvaa jeans siyo vazi lisilo la heshima hata kidogo. Ni vazi kama mavazi mengine na siyo kila mtu anapenda vaa suti. Ingekuwa anaenda interview ningemshauri kuvaa labda shati na kadet au suruali ya kitambaa lakini harusi maana yake ameamua jiachia ili akafurahie. Au ulitaka amzidi bwana harusi ? Wengi tumekuwa na kasumba ya kuona jeans ni nguo za kihuni au zisizo na heshima. Wapo watu wa hovyo kabisa wanavaa suti na wapo wenye heshima zao na pesa zao wanavaa jeans.Mimi binafsi huwa kuna wakati napiga jeans safi nzuri na shati yangu na koti lasuti na nikifika sehemu napewa heshima kama kawaida.Je unajuaje mwenzio maisha yake ni ya field zaidi tofauti na wewe labda ambaye kutwa upo kwenye vikao au kwenye AC? Maisha tunatofautiana shughuli zetu za kiuchumi huwezi mlazimisha mtu awe na suti hali kazi yake kila siku ni ya field kubangaiza.Au ulitaka awe na suti kabatini awe anategea harusi? je kama mwaka ukiisha hakuna mwaliko? Sikubaliani kabisa na kuwa jeans ni vazi la kihuni au lisilo la heshima.
 
Mimi nina miaka 70 kabati langu limejaa kaptula na vinjunga, hapo vipi?
 
We vaa za babu zako ZILE za ngozi muache jamaa avae zisizo na heshima
 
Mm hata vikao tu navaa jeans, nimejikaza Sana nimevaa kadeti ya grey au dark blue, ukinitegemea Mimi Eti ndio niwe second man mpiga suti Kali basi umechemka maybe iwe kwenye kikao serious cha dili lakini hivi visherehe sijui mitoko ya Kufurahi na wabongo wenzangu hapana kabisa, binafsi sipendi macho mengi...Simshauri mtu anitegemee kwenye hizo ishu. Nakumbuka nikiwa Bwana mdogo tulipanga kutoka na Mzee, ikabidi Mzee aniangalie weee akahisi huyu dogo hayupo serious na mitoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…